Msaada wa kisheria tafadhali.

Voldemort

Member
Jul 4, 2019
15
41
Wasalaam ndugu zangu, iko hivi

Nilipata Kazi taasisi moja hapa Dar nikiwa mkoani mwanzoni mwa mwezi huu wa 12. Kutokana na kutokuwa na ndugu ambaye ningeweza kufikia kwake ilibidi nitafute chumba Kwa akili ya makazi.

Nilipata chumba na nikalipia Kodi ya miezi 6 na kupewa mkataba na mwenye nyumba. Niliporipoti kazini nikakuta walishatuandalia appartments za kukaa ambazo zimeshalipiwa na taasisi yenyewe.

Nilipogundua hilo nikaamua kupitia mkataba ule wa kupangisha chumba na kubaini Kuna kifungu kinachokataza kumrithisha mpangaji mwingine bila idhini ya mwenye nyumba. Hivyo nikaamua kumfata mwenye nyumba na kumuelezea Hali halisi na kumwomba anirudishie kodi ya miezi mitano akate ya mwezi mmoja.

Nilipomweleza akakubali ila akasema kuwa pesa kashaitumia labda atafute mpangaji wa kunireplace na akishalipa Kodi basi atanirudishia. Tukakubaliana na kuandikishana na nikamkabidhi chumba ili atafute mpangaji mwingine baada ya week 1 anirudishie Hela.

Muda ulipowadia nikamtafuta akanijibu kuwa bado hajapata mpangaji mwingine. Kesho yake nikaamua kupitia hapo ili nitafute dalali aweze kutusaidia kupata mpangaji mwingine. Nilipofika pale nikakuta ashapangisha mtu mwingine na baada ya kuulizia nikaambiwa alimpangisha siku ile ile nilipotoka. Nikampigia simu akapokea akasema kuwa hiyo siyo shida yake Kwa sababu mimi ndiye niliyevunja mkataba na kuanzia siku hiyo akaacha kupokea simu zangu.

Nikaamua kwenda serikali ya mtaa Kwa mwenyekiti nikamueleza Hali halisi. Mwenyekiti akampigia simu lakini hakupokea hivyo akaniandikia barua ya kwenda polisi.

Nilipofika polisi akapigiwa simu na Askari Zaidi ya mara 10 lakini hakupokea hivyo nikaambiwa niende mahakamani nikafungue shauri

Naenda kujua, kulingana na scenario hapo juu shauri litakuwa la madai au utapeli? Then vipi kuhusu gharama za kufungua shauri hazitokuwa kubwa Sana??

Naombeni msaada wa kisheria ndugu zangu.
 
Mhonge polisi nenda nae hapo akampe vitisho atakulipa tu
 
Hiyo itakuwa ni madai na huko ndo patakuwa kipengele kulipwa. Wewe fanya mbinu ongea na askari hapo mmoja mwambie nikilipwa hiyo hela utachukua kiasi kadhaaa.
 
Hizo mnaziita madai watu wamefungwa kwa kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.

BTW: Ndo kwanza umeajiriwa halafu uwe na ratiba ya kushinda mahakamani,haitaathiri ajira yako mpya?
 
Huo muda unaopoteza na hela utakazopoteza kwenda mahakamani bora Ungeenda hata Kulimaa maana nakuhakikishia HUTAAMBULIA HATA 100...!! Wenye nyumba wa bongo huwa wana njaa kali asilimi 95 ndo maana hata masharti yao ya kiwakii.. Mimi niliacha laki 3 mahali ungesee sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom