Fanya haya kuongeza thamani ya ibada yako katika mikusanyiko ya kiroho

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,587
15,373
1: Ingia kwenye ibada ukiwa na ajenda. Usiende kwa sababu watu huwa wanaenda. Jitahidi uwe na hoja na ajenda siriasi ukizopanga kuwasilisha kwa Mungu wako.

2: Usipende kukaa nyuma au mwisho. Ili kuwa mzingativu jitahidi ukae kuanzia siti za katikati kuelekea mbele kwa mnenaji. Usiulize nyuma atakaa nani? Watakaa wanaopenda.

3: Usiende ibadani bila kitu cha kutoa. Ibada bila sadaka haijakamilika. Mungu anasema usiende mikono mitupu. Sadaka sio mchango. Sadaka lazima uinuize na kuitamkia unachotaka ikufanyie.

4: Linda kusudi la kuwa hapo. Ibadani huwa kuna mawakala wa ibirisi wanaojijua na wengine wanatumika bila kujua. Hawa ni wale wasiotulia muda wote wanazunguka, wanaongelesha watu, wanavaa kujionyesha, Wanakosoa watoa neno, wanavuruga usikuvu. Ibada yenye fujo na ukosefu wa utulivu ni ishara ya uwepo wa nguvu za giza ibadani. Usiziunge mkono. Focus.

Ni hayo tu.

Sabato njema.
 
Chief umenena hasa.
Kuna kitu hapo huwa nakipa nafasi kutokana na Roho wa Mungu anavyoniongoza.

Hapo mwisho umesema Sabato Njema siyo?.
 
hiyo namba 2.
Mungu hana Mipaka..hata ukikaa nje. ata kubariki tu
Msingi wa hoja sio mahala unapokaa, ni utulivu na usikivu. Katika nyumba nyingi za sala wanaopenda kukaa nje au nyuma wengi sio wote huwa wanaajenda zao, pia hakuna usikivu, pia ni rahisi kuwa distracted.

Ndio maana ibadani ni kuwahi ili uchague mahala ambapo lengo la kwenda ibadani utalilinda hadi lifaulu.
 
Uko sahihi .watu tunaabudu kimazoea sana, ibada znafanana na sherehe za harusi
Kuna watu ni majasiri kufanya ujinga mbele za Mungu ibadani kuliko hata ukweni.

Lazima uingie ibadani ukiwa unajua utakutana na watu waliopinda. Ukiwaendekeza wanakutoa katika uwepo.
 
1: Ingia kwenye ibada ukiwa na ajenda. Usiende kwa sababu watu huwa wanaenda. Jitahidi uwe na hoja na ajenda siriasi ukizopanga kuwasilisha kwa Mungu wako.

2: Usipende kukaa nyuma au mwisho. Ili kuwa mzingativu jitahidi ukae kuanzia siti za katikati kuelekea mbele kwa mnenaji. Usiulize nyuma atakaa nani? Watakaa wanaopenda.

3: Usiende ibadani bila kitu cha kutoa. Ibada bila sadaka haijakamilika. Mungu anasema usiende mikono mitupu. Sadaka sio mchango. Sadaka lazima uinuize na kuitamkia unachotaka ikufanyie.

4: Linda kusudi la kuwa hapo. Ibadani huwa kuna mawakala wa ibirisi wanaojijua na wengine wanatumika bila kujua. Hawa ni wale wasiotulia muda wote wanazunguka, wanaongelesha watu, wanavaa kujionyesha, Wanakosoa watoa neno, wanavuruga usikuvu. Ibada yenye fujo na ukosefu wa utulivu ni ishara ya uwepo wa nguvu za giza ibadani. Usiziunge mkono. Focus.

Ni hayo tu.

Sabato njema.
Amen
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom