Zingatia haya unapokuwa ugenini

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
227
333
Unajua kuwa unaweza kuwa mgeni ambaye wenyeji hutamani aondoke haraka kwa sababu mbalimbali ikiwemo kukuchoka?

Hali hii inaweza kukutokea wewe au mtu mwingine yeyote anaposafiri kwenda ugenini iwe kwa ndugu au rafiki.

Inatokea wenyeji kuanza kuuliza kwa njia za mkato ili wajue unaondoka lini kurudi ulikotoka.

Si hivyo tu inaweza kutokea wewe mgeni ukayachukia mazingira ya ugenini hata kama wenyeji wanakuhitaji uendelee kubaki.

Hii inaweza kutokana na jinsi unavyojisikia unapokuwa mazingira ya ugenini, pamoja na mtazamo wako kwa wenyeji.

Fahamu mambo machache ya kufanya na yale unayopaswa kuyaepuka unapokuwa ugenini.

Kwanza kabisa, wakati wote tambua na ukumbuke kuwa mahali ulipo sio nyumbani kwako au kwenu, hivyo zingatia kuwa kuna namna uhuru wako wa kufanya mambo unapungua.

Kama ukiwa nyumbani kwenu una tabia ya kuchagua vyakula basi jitahidi kupunguza masharti ili wenyeji wasije kukuona mgeni mwenye madoido.

Kama wewe ni mwanaume hili ni muhimu sana kwako kwa sababu wanaume hawahusiki sana jikoni, ukiwa na masharti mengi kuhusu vyakula wapishi watatamani uondoke haraka ili wapunguze mzigo wa kupika.

Sambamba na hilo usijiweke mtegoni kwa kujinyima kula kwa kuhofia kuwa upo ugenini kula kadri ya uwezo wako ili usije ishi kwa kukosa amani kutokana na njaa.

Jambo lingine ni kuwa mwepesi wa kusoma mazingira kabla hujafanya jambo, wahenga wanasema ukiwa ugenini usifue nguo ya ndani kama hujui wapi pa kuianika isije kukupa tabu.

Ukiwa ugenini watoto wenyeji hufurahia ujio wako, utataniwa, utachukizwa kiasi cha kupandwa kwenye mabega. Kuwa mwenye busara uwakataze wasikuzoee kupitiliza watakudhalilisha na usitamani kuendelea kubaki ugenini.

Hata hivyo mgeni usijivike kiremba cha mbwa mkali ukakaripia watoto mpaka wakahofia uwepo wako uhuru wao ukawa mashakani basi utachukiwa na watatamani uondoke.

Usiwe mtu wa kukaa kama bango la barabani, usiyesemeshwa na mtu wala kubadilika.
Ucheshi iwe sehemu ya maisha yako ya ugenini wenyeji watakupenda na kukuona kama mtu uliyekuja kuwapa furaha na fikra mpya.

Hata hivyo ucheshi wako, uchunge kwenye kila unachokiongea mbele yao usiwe mtu wa kuongea hata yasiyoeleweka kama vile umbea itakuharibia.

Kama wewe ni mwanaume jitahidi unaposafiri kuelekea eneo la mbali ugenini, uwe na nauli ya kurudia mfukoni ili pindi utakapoona mambo hayaendi sawa uage na kuondoka pasipo kusubiri utafutiwe nauli na wenyeji.

Na kila unaposafiri na kufika ugenini zingatia kuwa ugeni ni siku mbili au tatu, baada ya hapo kubali kuwa sehemu ya maisha ya wenyeji, fanya kazi kama wao ili kuwapunguzia mzigo wa majukumu ya kukuhudumia.

Mwisho ili uwe mgeni mwenye thamani ondoka wakati ambao wenyeji wanatamani uendelee kuwepo usisubiri kuondoka wakati ambao wamekuchoka.

Peter Mwaihola
Photo_1706277066165.jpg
 
Peter MwaiholaView attachment 2883613

Angalizo zuri kwa wazurulaji
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom