Uke wenza (najua wanawake mtachukia hili)

Uke wenza (najua wanawake mtachukia hili)

Tusaidiane kutokomeza uesherati na uzinzi kwa kukaribishana katika ndoa

Mtu ukiwa msherati hata ukioa kumi bado unachafua nje tu, hiyo ni tabia ya mtu na wala haihusiani na idadi ya wake zako.
Oa mke mmoja mpendane wawili na utayafurahia maisha, hili la kuleta ligi baina ya wanawake kwenye ndoa wanaishia kurogana na maupuzi mengine ya hovyo hayawezekani kwenye karne ya leo, labda enzi hizo za hao mitume maana maisha yalikua rahisi, hakukua na changamoto hizi za kisasa.
Hata waarabu wenye dini yao siku hizi wamekomaa kwenye ndoa za mke mmoja, waafrika tu ndio wameng'ang'ania kisa tamaa.
 
Mi uke wenza SI utaki...kuishi wmenyewe sishindwi...
Sio mbaya....akitaka kuoa mwingine...aniachoe nyumba na watoto....Sina tatizo..
Tuta co parenting....ila sishei dudu kwa kujua
Unakufuru ujue
 
Wanawake hata wakiwa wacha Mungu namna gani wanashindwa kukubali rukhsa moja iliyotolewa na Allah aliyetukuka, nayo ni mume kuoa mke wa pili. Allah Aliyetukuka kwa hekma yake ametoa ruhusa hii pale aliposema:

"Basi oeni mnaowapenda katika wanawake wawili, au watatu au wanne, na mkiogopa kuwa hamuwezi kufanya uadilifu, basi oeni mmoja tu' (Qur'an 4:3).

Kitu muhimu cha mke kufanya ni kumsaidia mumewe kuchagua mke mwenye dini na maadili ya Kiislamu. Usiwe ndio sababu ya kuharibu uhusiano na wewe na kumpelekea kufanya zinaa kwa ajili yako kuifanya hali yake kuwa ngumu katika suala hilo.

Kisheria mume hahitaji idhini au ruhusa ya mke katika kuoa mke mwengine. La kufanya ni kumsaidia aweze kutimiza haki zako na za mke mpya na wala usiwe ndio sababu ya uhasama na kutolewa talaka.

Ukimruhusu mumeo kuoa mke qa pili utapata faida zifuatazo:

(1) Utapata thawabu kwa kumzuia mumeo na zinaa.

(2) Mumeo atazidi kukupenda na kukuthamini, kinyume na utakapomfanyia matatizo huenda akachukizwa na wewe na huenda apoteze mapenzi yote kwako.

(3) Utakuwa miongoni kwa waumini wanaopokea na kukubali sheria za dini. Utapata thawabu za kuwa na subra kwa jambo zito kama hili.

(4) Utakuwa mfano mzuri kwa wanawake wengine na utapata thawabu kwa kila mwanamke atakaekuiga mfano wako kwa kukubali waume zao kuongeza mke

Allah awatangulie hili dada zangu muwe wenye kuridhia kwa moyo msafi, Amin.

View attachment 2796730
Kwangu mm kuongeza mke kutaendana na umri atleast 45 ila miaka 30 una wawili watatu kwa zama zetu ina ukakasi kidogo japokuwa sio katazo
 
[QUOTE="Loading failed, post: 48274531, member: 727
Je, utaondoaje dhana ya mke mkubwa na mke mdogo kwa mujibu wa kuzingatia tendo la ndoa, ni vipi basi utazingatia dhana hii kuondoa mtazamo wa mke mkubwa na mdogo ukizingatia yule wa kwanza kumuingia ndiye wa kwanza na ndiye atakaye kua mke mkubwa kwa wa mwisho kumuingilia ambaye atakua mdogo?
Kama wote nimeona siku Moja huwezi epuka Kwamba mmoja ndio atakuwa wa kwanza kuingiliwa lakini point na Lengo langu si kuoa mmoja Kisha baada ya miaka au miezi au siku baada uoe mwingine , basi yule wa kwanza hujiweka status ya mi-mke mkubwa.
Pia unaweza kuwadanganya ila ukweli unaujua.Kumdanganya mmke Kwa kuepuka Shari au kuongeza mapenzi hakuna tatizo.[/QUOTE]Ukimaliza kudanganya tubu na ibaki siri yako
 
Kwanini iwe nyumba na si mke
Waislam wanatambua mke wa pili na hata wa tatu; Dini nyingine hazitambui mke zaidi ya mmoja na hii ndio inachangia ongezeko la watoto wasiokuwa na baba mijini
Kuna Research ilifanywa Kenya Ikaonesha hivi;
Jiji la Mombasa na ukanda wa pwani ambako Waislam ni kama 90% watoto wa mitaani hawapo au niseme ni wachache sana ILA Nairobi na majiji mengine yasiyokuwa na Waislamu wengi, watoto wa mitaani, single mother, na nyumba ndogo ni MAFURIKO...
 
Kikawaida ndoa ya mke zaidi ya mmoja ni ngumu sana, moyo huwa unapenda mwanamke mmoja tu, ila kwa wanawake wengine ni kutamani na kukidhi matakwa ya kingono tu. Kingine nchi za kiarabu nyingi wanaamini kwa mke mmoja tu but kwa huku kwetu africa kuoa mke zaidi ya mmoja ni hatar sana utalishwa limbwata(uchafu) na kila mwanamke mwisho wa siku utakuwa mweu, kingine kuoa wake 4 sio kwamba huwezi kuwa na michepuko.
 
Mi uke wenza SI utaki...kuishi wmenyewe sishindwi...
Sio mbaya....akitaka kuoa mwingine...aniachoe nyumba na watoto....Sina tatizo..
Tuta co parenting....ila sishei dudu kwa kujua
😂😂
 
Sheria za ugandamizi yaani nihenyeke na wewe ugali dagaa mara tulale njaa tuunge unge weeee siku umepata tuuu ati ukaongeze mwanamke.....jengine kuhudumia mke mmoja matatizo Bado linaongeza mke..... Mwanaume ungejisikiaje mkeo aolewe na wanaume wawili? Mnagonga wawili shimo Moja we utajisikiaje?unadhani mwanamke naye Hana moyo? Haumiii au Hana hisia?
 
Kwahiyo unamlaumu Mungu alieziumba mbingu na dunia? Inamaana wewe ni mjuzi kumzidi yeye?
 
Kikawaida ndoa ya mke zaidi ya mmoja ni ngumu sana, moyo huwa unapenda mwanamke mmoja tu, ila kwa wanawake wengine ni kutamani na kukidhi matakwa ya kingono tu. Kingine nchi za kiarabu nyingi wanaamini kwa mke mmoja tu but kwa huku kwetu africa kuoa mke zaidi ya mmoja ni hatar sana utalishwa limbwata(uchafu) na kila mwanamke mwisho wa siku utakuwa mweu, kingine kuoa wake 4 sio kwamba huwezi kuwa na michepuko.
Mungu ndie aliesema hivyo sasa sijui wewe ujuaji umeutoa wapi
 
Back
Top Bottom