Mohamedex121
JF-Expert Member
- Jan 27, 2022
- 1,734
- 3,310
Wanawake hata wakiwa wacha Mungu namna gani wanashindwa kukubali rukhsa moja iliyotolewa na Allah aliyetukuka, nayo ni mume kuoa mke wa pili. Allah Aliyetukuka kwa hekma yake ametoa ruhusa hii pale aliposema:
"Basi oeni mnaowapenda katika wanawake wawili, au watatu au wanne, na mkiogopa kuwa hamuwezi kufanya uadilifu, basi oeni mmoja tu' (Qur'an 4:3).
Kitu muhimu cha mke kufanya ni kumsaidia mumewe kuchagua mke mwenye dini na maadili ya Kiislamu. Usiwe ndio sababu ya kuharibu uhusiano na wewe na kumpelekea kufanya zinaa kwa ajili yako kuifanya hali yake kuwa ngumu katika suala hilo.
Kisheria mume hahitaji idhini au ruhusa ya mke katika kuoa mke mwengine. La kufanya ni kumsaidia aweze kutimiza haki zako na za mke mpya na wala usiwe ndio sababu ya uhasama na kutolewa talaka.
Ukimruhusu mumeo kuoa mke qa pili utapata faida zifuatazo:
(1) Utapata thawabu kwa kumzuia mumeo na zinaa.
(2) Mumeo atazidi kukupenda na kukuthamini, kinyume na utakapomfanyia matatizo huenda akachukizwa na wewe na huenda apoteze mapenzi yote kwako.
(3) Utakuwa miongoni kwa waumini wanaopokea na kukubali sheria za dini. Utapata thawabu za kuwa na subra kwa jambo zito kama hili.
(4) Utakuwa mfano mzuri kwa wanawake wengine na utapata thawabu kwa kila mwanamke atakaekuiga mfano wako kwa kukubali waume zao kuongeza mke
Allah awatangulie hili dada zangu muwe wenye kuridhia kwa moyo msafi, Amin.