UKAWA Wapigwa Bao la Kisigino

UKAWA Wapigwa Bao la Kisigino

I hate mjadala wa UKAWA. Kama CCM wameshinda vita wamalizie basi kutengeneza katiba. UKAWA unawahusu nini? Non sense kupoteza nguvu ya akili kutafuta majibu ya kuwaelewesha watu wanaojipendekeza CCM kwa maslahi.
 
Haujui jinsi gani JK amepata pigo kubwa na haujui jinsi gani anashauriwa asitishe bunge hili kwa ajili ya hatua ya UKAWA. Ungesubiri usikie hotuba yake ya jumamosi kwanza, hotuba ambayo maandaliz yake ni pamoja na kuwadhibiti ukawa wasimtangulie kwa hoja mbele ya umma.


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
We have a long way to go, yaani magamba n' supporters hufikiria posho na vijembe, shame.
 
Haujui jinsi gani JK amepata pigo kubwa na haujui jinsi gani anashauriwa asitishe bunge hili kwa ajili ya hatua ya UKAWA. Ungesubiri usikie hotuba yake ya jumamosi kwanza, hotuba ambayo maandaliz yake ni pamoja na kuwadhibiti ukawa wasimtangulie kwa hoja mbele ya umma.


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Mkuu, JK yupo smart sana. Amesubiri vikao vya bunge vimemalizika ndo anataka kuongea. Hakika nampenda sana Rais wangu
 
I hate mjadala wa UKAWA. Kama CCM wameshinda vita wamalizie basi kutengeneza katiba. UKAWA unawahusu nini? Non sense kupoteza nguvu ya akili kutafuta majibu ya kuwaelewesha watu wanaojipendekeza CCM kwa maslahi.
Mkuu, UKAWA ni mawakala wa shetani wanaostahili kulaaniwa na kukemewa kwa nguvu zote
 
Mkuu, UKAWA ni mawakala wa shetani wanaostahili kulaaniwa na kukemewa kwa nguvu zote
If you are self contained achana nao endeleeni na shughuli zenu! In this Era hakuna kitu cha laana wala nini, hatuwezi kusogea mbele if we wait for miracles za laana za kimaslahi.
 
If you are self contained achana nao endeleeni na shughuli zenu! In this Era hakuna kitu cha laana wala nini, hatuwezi kusogea mbele if we wait for miracles za laana za kimaslahi.
Mkuu, hizo hekaya unamuimbia nani?
 
Mkuu, hizo hekaya unamuimbia nani?

Bila shaka ni wewe uliyetumwa ndani ya uzi huu. Unahitaji kuelewa kitu kimoja kuwa kama lengo la CCM limetimia, is not Bad watunge katiba na sio kupoteza muda kujadili UKAWA. Sasa unaposema Hekaya namuimbia nani sijakuelewa kama wewe umejitoa nje ya mawazo yako.
 
Unafikiri wangeacha kuendelea na vikao? Halafu 300000 wangezipata wapi? Ukawa kama wataweka maslahi ya posho mbele kama walivyoweka mainterahamwe watakuwa wamefeli! Kama kuna wajumbe wa bunge la katiba kutoka Ukawa wanatamani walipwe 300000 nao watakuwa ni mafisadi walewale! Ukombozi ni kujitoa mhanga!
Mkuu posho walizokomba ni mpaka tarehe 30-04-2014.Baada ya kuchukuwa chao wakasepa,upo hapo.
 
Hayo ni mawazo yako Mkuu na huko ni kushindwa kulikopindukia

Unalipwa kwa uchochezi ewe kiumbe, rudi shule ili ujue tofauti kati ya 1+1 na kuunganisha(mfano mbao mbili zikiunganishwa pamoja huwa ubao mmoja si 2).KASOME
 
Mwanakijiji,
Unadhani hawa watu wameteuliwa kwa sifa gani walizonazo? Mimi nadhani udini.

1.Omar Ramadhan Mapuri (China)
2.Adadi Rajabu (Zimbabwe)
3.Mwanaidi Sinare Maajar (London-Uingereza)
4.Ahamada Ngemera (Berlin-Ujerumani)
5.Hussein Said Khatib (Muscat-Oman)

Pointless story not interested
 
ujue thelusi mbili inapelea kwa hesabu ndogo sana,na hapo hujaweka wale 201,na bahati mbaya wenje akawambia wamehongwa wali na soda,unadhani wataelemea wapi?.pia kuna wapinzani wamebaki mle mjengoni kama mrema,hamad etc.

Lolote laweza kutokea hiyo kesho.

Thelusi mbili ya Zanzibar haipatikani na akuna ibara yoyote inaweza kupitishwa bila marithiano ya pande zote
 
...umeandika mashairi mengi pumba tupu....Mnaposhabikia mambo muwe na uelewa wa kutosha Mtaumbuka bure ...
Soma miongozo ya bunge kanuni name sheria ndipo ulete mada pole
Naipenda Tanganyika
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Mtakumbuka kuwa tarehe 17 Aprili 2014, Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wanaojiita kwa jina la UKAWA, walitoka Bungeni Mjini Dodoma wakati wa mjadala wa Rasimu ya Katiba katika sura ya Kwanza na ya Sita kwa madai kuwa wamechoshwa na CCM kutumia uwingi wao kushinikiza muundo wa serikali mbili na kuhamasisha makundi ya kijamii wakiwemo waumini kususia muundo wa muungano wa serikali tatu. Wakati wanatoka, walisema kuwa wanaenda kuishtaki CCM kwa wananchi.

Wadau, wakati UKAWA wanapanga kwenda kuishtaki CCM kwa wananchi, CCM tayari ipo kwa wananchi ikiwaeleza bayana wananchi sababu za chama kupendekeza muundo wa muungano wa serikali mbili huku ikipinga kwa nguvu muungano wa serikali tatu. Tumemuona Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana akifanya ziara za kichama huko Kigoma na mikoa ya kanda ya Ziwa. Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) umeratibu na kuendesha matembezi ya bodaboda katika mikoa kadhaa nchini na ujumbe katika matembezi hayo ni kuuenzi muungano ulioasisiwa na Hayati Mwalimu Nyerere na Abeid Aman Karume. Katika ziara zote hizo, wananchi wameonekana kuelewa na kuwashangaa wale wanaotaka kuvuruga amani na utulivu wa nchi yetu.

Wadau, UKAWA walipoondoka Bungeni, walitarajia kuwa, Bunge hilo litavunjwa kutokana na wao kutokuwepo. Matarajio yao ni kuwa, Bunge likiahirishwa, azma yao ya kukwamisha mchakato huo yatakuwa yametimia. Hata hivyo, haikuwa hivyo. Wabunge waliobaki wengi wao wakiwa ni wa CCM wanaendelea na mjadala na kwa takriban wiki mbili sasa, CCM wamepata muda wa kutosha wa kusema yale yaliyo dhihiri huku wananchi wengi wakisikiliza kupitia Runinga, Radio na kusoma kupitia mitandao ya kijamii ukiwemo mtandao huu pendwa wa JF. Hakika wabunge wengi waliopata nafasi ya kuongea wamemwaga nondo za uhakika zilizowashawishi wananchi huku wakiendeleza vijembe vile vile vilivyowakimbiza UKAWA. Nina hakika kuwa wanavipata vijembe hivyo huko huko waliko. Hakika kwa hili, UKAWA wamepigwa bao la kisigino na wananchi wanaendelea kuwalaani katika kona zote za nchi.

Wadau, wakati UKAWA wanaondoka, zilisikika taarifa kuwa wamechukua posho zote na kujongomea. Hakika kashfa hii imewachafua sana na hawatakuja kusafishika katu. Watanzania wana hasira nao sana na hakika wasitarajie kuungwa mkono na wananchi wengi. Ingawa jitihada zimefanyika za kuwasafisha na kashfa hiyo kupitia Gazeti la Mwananchi, ukweli ni kwamba wananchi wengi wameamini kuwa wabunge hao wamechukua posho na kutokomea. Hilo ni doa kuu ambalo haliwezi kuondolewa kwa Omo wala Aerial.

Wadau, wakati UKAWA wanaondoka, walitarajia kuwa wataanzisha maandamano na mikutano nchi nzima kuanzia siku ya pili baada ya kuondoka kwao. Hata hivyo, walipigwa stop hadi tarehe 30 Aprili ndipo watakapoanza kufanya mikutano ya hadhara na si maandamano tena. Tunajua kuwa wakati huo Bunge Maalum litakuwa limesitishwa na wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi watakuwa wanajiandaa na vikao vya Bunge la Bajeti. Hawa UKAWA wataendelea vipi kuwa na mshikamano ilhali wabunge watakuwa busy na bunge la bajeti? Hakika hili ni bao jingine la kisigino. Kwa sasa wamekalishwa chini kama bondia aliyepigwa na mpinzani wake huku akihema asijue la kufanya. Wakati wao wataanza mikutano ya katiba, wananchi watakuwa wameshahamishia mawazo yao kwenye Bunge la Bajeti huku wakisubiri kwa hamu kusikia ni nini serikali itafanya juu yao. Hakika kati ya bajeti na Katiba, ni wazi kuwa suala la bajeti ndilo hugusa maisha ya wananchi moja kwa moja na hivyo ni vigumu kwa UKAWA kupata watu wa kuwaunga mkono.

Wadau, wakati UKAWA wanaondoka, walitarajia kuwa wataungwa Mkono na wabunge wengi wa kundi la 201. Hata hivyo siku moja tu baada ya kuondoka kwao, baadhi ya wabunge ambao waliondoka pamoja nao akiwemo Mwalimu Ezekiel Oluoch, walirejea Bungeni huku wakiwakana na kuwananga UKAWA. Hakika hili ni pigo jingine. Imekuwa ni fedheha kwao na sasa wamekuwa mabubu kwa vile hawana avenue ya kusemea.

Wadau, baada tu ya UKAWA kuondoka, kuna shirika moja limejifanya kuendesha utafiti ili kujua mtizamo wa wananchi juu ya mijadala bungeni. Eti katika utafiti huo, kwamba Wazanzibari wengi wanaunga mkono muundo wa serikali tatu kama ilivyo kwa bara. Mbaya zaidi, wakamuita mzee Warioba ili atetee hoja hiyo. Hakika hii ni fedheha kubwa na imedhihirisha ni kwa namna gani UKAWA wametepeta. Badala ya kumuacha mzee wa watu augulie madongo anayopewa bungeni, wao wanazidi kumdhalilisha. Mbaya zaidi, Warioba akajifanya kukemea lugha zinazotolewa bungeni asi if yeye ni Presidaa.

Wadau, Mwenyekiti wa CCM ambaye ndiye Rais wa Nchi anatarajia kuwa mgeni rasmi wakati wa sherehe za Mei Mosi yaani siku moja tu baada ya UKAWA kuanza mikutano yao. Ingawa suala la katiba si moja ya ajenda ya sherehe hizo, ni wazi kuwa Mheshimiwa Rais anatumia japo muda kidogo kuelezea juu ya mchakato huo. Hakika nitamshangaa sana kama hatagusia hilo. Katika hotuma hiyo, ni wazi kuwa Rais Kikwete atasimamia msimamo wake ule ule alioutoa Bungeni tarehe 21 Machi 2014 wakati akilizindua bunge maalum. Hotuba hiyo ya JK itazidi kuwatokomeza kabisa UKAWA na kwa vile wananchi wengi watasikiliza hotuba hiyo, ni wazi kuwa hata UKAWA watazunguka nchi nzima, hawatabadili fikra za wananchi. Hili ni pigo jingine kwa UKAWA.

Wadau, yapo mengi ila kwa hayo niliyoyasema, ni wazi kuwa UKAWA wamelikoroga na lazima walinywe. Hakika wamepigwa bao la kisigino huku wakibaki hawana cha kufanya.


kinachosikitisha ni jinsi vijana mnavyofurahia ukandamizaji wa demokrasia na kutumika kwa polisi kisiasa.karma is a bi***
 
Chabruma amekusikia. Mbumbumbu angekushughulisha muda huu?
Mimi wa kushughulishwa na Kibwengo kama wewe mtega nyoka kutoka Mpitimbi Songea aka mchumia tumbo wa UVCCM!!?...na hapa kinachokusumbua ni njaa tu na si kitu kingine. Unatia aibu sana Chabruma
 
Back
Top Bottom