UKAWA Wapigwa Bao la Kisigino

UKAWA Wapigwa Bao la Kisigino

Wadau, amani iwe kwenu.

Mtakumbuka kuwa tarehe 17 Aprili 2014, Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wanaojiita kwa jina la UKAWA, walitoka Bungeni Mjini Dodoma wakati wa mjadala wa Rasimu ya Katiba katika sura ya Kwanza na ya Sita kwa madai kuwa wamechoshwa na CCM kutumia uwingi wao kushinikiza muundo wa serikali mbili na kuhamasisha makundi ya kijamii wakiwemo waumini kususia muundo wa muungano wa serikali tatu. Wakati wanatoka, walisema kuwa wanaenda kuishtaki CCM kwa wananchi.

Wadau, wakati UKAWA wanapanga kwenda kuishtaki CCM kwa wananchi, CCM tayari ipo kwa wananchi ikiwaeleza bayana wananchi sababu za chama kupendekeza muundo wa muungano wa serikali mbili huku ikipinga kwa nguvu muungano wa serikali tatu. Tumemuona Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana akifanya ziara za kichama huko Kigoma na mikoa ya kanda ya Ziwa. Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) umeratibu na kuendesha matembezi ya bodaboda katika mikoa kadhaa nchini na ujumbe katika matembezi hayo ni kuuenzi muungano ulioasisiwa na Hayati Mwalimu Nyerere na Abeid Aman Karume. Katika ziara zote hizo, wananchi wameonekana kuelewa na kuwashangaa wale wanaotaka kuvuruga amani na utulivu wa nchi yetu.

Wadau, UKAWA walipoondoka Bungeni, walitarajia kuwa, Bunge hilo litavunjwa kutokana na wao kutokuwepo. Matarajio yao ni kuwa, Bunge likiahirishwa, azma yao ya kukwamisha mchakato huo yatakuwa yametimia. Hata hivyo, haikuwa hivyo. Wabunge waliobaki wengi wao wakiwa ni wa CCM wanaendelea na mjadala na kwa takriban wiki mbili sasa, CCM wamepata muda wa kutosha wa kusema yale yaliyo dhihiri huku wananchi wengi wakisikiliza kupitia Runinga, Radio na kusoma kupitia mitandao ya kijamii ukiwemo mtandao huu pendwa wa JF. Hakika wabunge wengi waliopata nafasi ya kuongea wamemwaga nondo za uhakika zilizowashawishi wananchi huku wakiendeleza vijembe vile vile vilivyowakimbiza UKAWA. Nina hakika kuwa wanavipata vijembe hivyo huko huko waliko. Hakika kwa hili, UKAWA wamepigwa bao la kisigino na wananchi wanaendelea kuwalaani katika kona zote za nchi.

Wadau, wakati UKAWA wanaondoka, zilisikika taarifa kuwa wamechukua posho zote na kujongomea. Hakika kashfa hii imewachafua sana na hawatakuja kusafishika katu. Watanzania wana hasira nao sana na hakika wasitarajie kuungwa mkono na wananchi wengi. Ingawa jitihada zimefanyika za kuwasafisha na kashfa hiyo kupitia Gazeti la Mwananchi, ukweli ni kwamba wananchi wengi wameamini kuwa wabunge hao wamechukua posho na kutokomea. Hilo ni doa kuu ambalo haliwezi kuondolewa kwa Omo wala Aerial.

Wadau, wakati UKAWA wanaondoka, walitarajia kuwa wataanzisha maandamano na mikutano nchi nzima kuanzia siku ya pili baada ya kuondoka kwao. Hata hivyo, walipigwa stop hadi tarehe 30 Aprili ndipo watakapoanza kufanya mikutano ya hadhara na si maandamano tena. Tunajua kuwa wakati huo Bunge Maalum litakuwa limesitishwa na wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi watakuwa wanajiandaa na vikao vya Bunge la Bajeti. Hawa UKAWA wataendelea vipi kuwa na mshikamano ilhali wabunge watakuwa busy na bunge la bajeti? Hakika hili ni bao jingine la kisigino. Kwa sasa wamekalishwa chini kama bondia aliyepigwa na mpinzani wake huku akihema asijue la kufanya. Wakati wao wataanza mikutano ya katiba, wananchi watakuwa wameshahamishia mawazo yao kwenye Bunge la Bajeti huku wakisubiri kwa hamu kusikia ni nini serikali itafanya juu yao. Hakika kati ya bajeti na Katiba, ni wazi kuwa suala la bajeti ndilo hugusa maisha ya wananchi moja kwa moja na hivyo ni vigumu kwa UKAWA kupata watu wa kuwaunga mkono.

Wadau, wakati UKAWA wanaondoka, walitarajia kuwa wataungwa Mkono na wabunge wengi wa kundi la 201. Hata hivyo siku moja tu baada ya kuondoka kwao, baadhi ya wabunge ambao waliondoka pamoja nao akiwemo Mwalimu Ezekiel Oluoch, walirejea Bungeni huku wakiwakana na kuwananga UKAWA. Hakika hili ni pigo jingine. Imekuwa ni fedheha kwao na sasa wamekuwa mabubu kwa vile hawana avenue ya kusemea.

Wadau, baada tu ya UKAWA kuondoka, kuna shirika moja limejifanya kuendesha utafiti ili kujua mtizamo wa wananchi juu ya mijadala bungeni. Eti katika utafiti huo, kwamba Wazanzibari wengi wanaunga mkono muundo wa serikali tatu kama ilivyo kwa bara. Mbaya zaidi, wakamuita mzee Warioba ili atetee hoja hiyo. Hakika hii ni fedheha kubwa na imedhihirisha ni kwa namna gani UKAWA wametepeta. Badala ya kumuacha mzee wa watu augulie madongo anayopewa bungeni, wao wanazidi kumdhalilisha. Mbaya zaidi, Warioba akajifanya kukemea lugha zinazotolewa bungeni asi if yeye ni Presidaa.

Wadau, Mwenyekiti wa CCM ambaye ndiye Rais wa Nchi anatarajia kuwa mgeni rasmi wakati wa sherehe za Mei Mosi yaani siku moja tu baada ya UKAWA kuanza mikutano yao. Ingawa suala la katiba si moja ya ajenda ya sherehe hizo, ni wazi kuwa Mheshimiwa Rais anatumia japo muda kidogo kuelezea juu ya mchakato huo. Hakika nitamshangaa sana kama hatagusia hilo. Katika hotuma hiyo, ni wazi kuwa Rais Kikwete atasimamia msimamo wake ule ule alioutoa Bungeni tarehe 21 Machi 2014 wakati akilizindua bunge maalum. Hotuba hiyo ya JK itazidi kuwatokomeza kabisa UKAWA na kwa vile wananchi wengi watasikiliza hotuba hiyo, ni wazi kuwa hata UKAWA watazunguka nchi nzima, hawatabadili fikra za wananchi. Hili ni pigo jingine kwa UKAWA.

Wadau, yapo mengi ila kwa hayo niliyoyasema, ni wazi kuwa UKAWA wamelikoroga na lazima walinywe. Hakika wamepigwa bao la kisigino huku wakibaki hawana cha kufanya.
Kapige mswaki domo lako linanuka mataputapu
 
Ukiwa MZALENDO huwezi kufurahia kilichotokea.Kususia mchakato huu si jambo jema kwa jamii yetu,na ukumbuke waliobungeni hawawezi kufanya chochote kwenye rasimu hiyo hata kupiga kura hawawezi.Ni vyema ukalijua hilo.

Kweli kabisa... Wengi hatujafurahia
Hembu mweleze ukweli...
 
Tetty, porojo nyiiiingiiiii point sifuri

Kwa muonekano wako na siwezi kukulazimisha kuona nimeongea sense,ila wale wanaotukana,kutoa mipasho na kuongelea watu huko Bungeni ndiyo wanye point.Na ukifikiri Watanzania wa leo ni wale wa mwaka 47,wa zidumu fikra za mwenyekiti.Pole sana.
 
Kweli kabisa... Wengi hatujafurahia
Hembu mweleze ukweli...

Hawezi kuelewa ni sawa na sikio la kufa.Pili kumbuka tumeshagawanyika tayari na ndiyo ilikuwa makusudi yao,wakidhani wanachokifanya kinatija kwa taifa.
 
Hawezi kuelewa ni sawa na sikio la kufa.Pili kumbuka tumeshagawanyika tayari na ndiyo ilikuwa makusudi yao,wakidhani wanachokifanya kinatija kwa taifa.

Weee acha tyuuu Katka kutugawanya wamefanikiwa ndugu.... Wala hata sio kidogo..
 
Ni lazima wawalaani kwa vile ni mawakala wa Shetani. Ni maadui wa taifa hili na nitawashangaa sana wabunge wasipowasema vibaya hawa UKAWA

Nisalimie ile ID ya Chabruma....sijapata kuona mngoni -------- na mbumbumbu kama wewe.
 
:scared::scared::scared::scared::scared::scared::scared::scared::scared::scared::scared::scared::scared::scared::scared::scared::scared::scared::scared::scared:
 
Wamerudi mmoja mmoja, bado wale vimbelembele, wanaona gere!
 
Habari hii si ya kupuuzwa hata kidogo! naomba vyombo vya dola vifuatilie hata kama ni uongo tu! inaweza kupuuzwa, halafu baadae ikatokea! itakuwa ni majanga! hivi kweli yote ni rasimu ya Tume ya Warioba au kuna agenda ya siri?
 
Mh! sizani kama upo sawa kifikra..jitazame upya.Kama ni mchumia tumbo basi sawa.
 
Mh! sizani kama upo sawa kifikra..jitazame upya.Kama ni mchumia tumbo basi sawa.
Mkuu, nipo sana tena kupita maelezo. Mie si kama Tundu Lissu ambaye anafikia hatua ya kumtukana hayati Bana wa Taifa
 
Wamerudi mmoja mmoja, bado wale vimbelembele, wanaona gere!
Mkuu, akina Jussa na Lissu wanahitaji kurudi ila kwa laana waliyopata kutokana na kumtusi baba wa taifa wamebaki wanajutia upuuzi wao
 
Hoja dhaifu hutolewa na akili dhaifu zinazoongozwa na Rais dhaifu!!!!
 
Back
Top Bottom