UKAWA Wapigwa Bao la Kisigino

UKAWA Wapigwa Bao la Kisigino

nimekuambia toka jana,haya mambo yanafuata ratiba,kesho ndo ilitakiwa kura ipigwe.swali ni je,kura itapigwa kesho ama la?
watapiga kura kwa sheria ipi? labda kama watapiga kura kupitisha serikali3 kama zilivyo kwenye rasimu maana hawana uwezo wa kubadili kifungu chochote kwa mujibu wa sheria.
 
Mh!Pole wale watanzania wa jana si wa leo na kamwe hawezi kuwa wa kesho.Ni bahati mbaya umekubali kudanganywa na wajume wa CCM toka Zanzibar kuwa wanapenda Muungano uendelee,lakini wakiwa kwenye Bunge la wawakilishi ni hao hao wanaokataa kuwepo kwa muungano,na si hilo tu hata uwepo wa Watanzania bara kuwepo Zanzibar,kufanya kazi au biashara.Ni mara ngapi biashara za Wadanganyika wenzaki zinachomwa moto si sababu ya biashara kuwa haramu la,bali sababu ya wanakotoka.

Cha msingi ningeona unaongea jema kama ungewaeleza wajumbe hawa waeleze ukweli ili tuapte suluhisho la kudumu.Kuna wengine ni wapenzi wa serikali mbili lakini lenye suluhisho la kudumu na marithiano ya pande zote mbili.Kwa kutudanganya watanzania hakutasaidia Muungano kamwe.Mnaweza kutumia nguvu kuwalazimisha muungano muutakao,lakini sidhani kama kutakuwa na usalama huko tuendako.

Wazee walisema ni rahisi kumlazimisha Punda kwenda kisimani,lakini si rahisi kumlazimisha kunywa maji.
 
"Kipofu hamuongozi kipofu mwenziwe" Ukawa wote wamekutana vipofu watupu.
 
ukiwa mzalendo huwezi kufurahia kilichotokea.kususia mchakato huu si jambo jema kwa jamii yetu,na ukumbuke waliobungeni hawawezi kufanya chochote kwenye rasimu hiyo hata kupiga kura hawawezi.ni vyema ukalijua hilo.

ukawa watoto deko. Hakuna sababu inayozui bkt kutokuweza kupiga kura ya maamuzi hata kama ukawa hawapo. We ngoja bkt liendele agosti uone kama kura hazitapigwa. Hayo matumaini ya ukawa et hakuna kura bila wao hz ndoto macho
 
Huna hata uelewa wa kitu unachosema. Kama --------- basi utakuwa hufanyi hata tafiti ndogo zisizohitaji fedha na akili yako imedumaa.
 
watapiga kura kwa sheria ipi? Labda kama watapiga kura kupitisha serikali3 kama zilivyo kwenye rasimu maana hawana uwezo wa kubadili kifungu chochote kwa mujibu wa sheria.

kura zitapigwa agosti sio kesho mkuu. Pia kasome pia vizuri sheria ya kunda bkt ,utajua kama bkt inauwezo wa kubadili rasimu au la. Ukawa ndo walichemka hapo wakakubali kwenda ikulu kupata uji na jk. Kwa ufupi sheria inaruhusu kutoa na kuweka jambo jipya.
 
Hahahahahahaaaaaaaaaaaaa,du kuwa kichaa sio lazima kuokota makopo na kulala majalalani,
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Mtakumbuka kuwa tarehe 17 Aprili 2014, Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wanaojiita kwa jina la UKAWA, walitoka Bungeni Mjini Dodoma wakati wa mjadala wa Rasimu ya Katiba katika sura ya Kwanza na ya Sita kwa madai kuwa wamechoshwa na CCM kutumia uwingi wao kushinikiza muundo wa serikali mbili na kuhamasisha makundi ya kijamii wakiwemo waumini kususia muundo wa muungano wa serikali tatu. Wakati wanatoka, walisema kuwa wanaenda kuishtaki CCM kwa wananchi.

Wadau, wakati UKAWA wanapanga kwenda kuishtaki CCM kwa wananchi, CCM tayari ipo kwa wananchi ikiwaeleza bayana wananchi sababu za chama kupendekeza muundo wa muungano wa serikali mbili huku ikipinga kwa nguvu muungano wa serikali tatu. Tumemuona Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana akifanya ziara za kichama huko Kigoma na mikoa ya kanda ya Ziwa. Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) umeratibu na kuendesha matembezi ya bodaboda katika mikoa kadhaa nchini na ujumbe katika matembezi hayo ni kuuenzi muungano ulioasisiwa na Hayati Mwalimu Nyerere na Abeid Aman Karume. Katika ziara zote hizo, wananchi wameonekana kuelewa na kuwashangaa wale wanaotaka kuvuruga amani na utulivu wa nchi yetu.

Wadau, UKAWA walipoondoka Bungeni, walitarajia kuwa, Bunge hilo litavunjwa kutokana na wao kutokuwepo. Matarajio yao ni kuwa, Bunge likiahirishwa, azma yao ya kukwamisha mchakato huo yatakuwa yametimia. Hata hivyo, haikuwa hivyo. Wabunge waliobaki wengi wao wakiwa ni wa CCM wanaendelea na mjadala na kwa takriban wiki mbili sasa, CCM wamepata muda wa kutosha wa kusema yale yaliyo dhihiri huku wananchi wengi wakisikiliza kupitia Runinga, Radio na kusoma kupitia mitandao ya kijamii ukiwemo mtandao huu pendwa wa JF. Hakika wabunge wengi waliopata nafasi ya kuongea wamemwaga nondo za uhakika zilizowashawishi wananchi huku wakiendeleza vijembe vile vile vilivyowakimbiza UKAWA. Nina hakika kuwa wanavipata vijembe hivyo huko huko waliko. Hakika kwa hili, UKAWA wamepigwa bao la kisigino na wananchi wanaendelea kuwalaani katika kona zote za nchi.

Wadau, wakati UKAWA wanaondoka, zilisikika taarifa kuwa wamechukua posho zote na kujongomea. Hakika kashfa hii imewachafua sana na hawatakuja kusafishika katu. Watanzania wana hasira nao sana na hakika wasitarajie kuungwa mkono na wananchi wengi. Ingawa jitihada zimefanyika za kuwasafisha na kashfa hiyo kupitia Gazeti la Mwananchi, ukweli ni kwamba wananchi wengi wameamini kuwa wabunge hao wamechukua posho na kutokomea. Hilo ni doa kuu ambalo haliwezi kuondolewa kwa Omo wala Aerial.

Wadau, wakati UKAWA wanaondoka, walitarajia kuwa wataanzisha maandamano na mikutano nchi nzima kuanzia siku ya pili baada ya kuondoka kwao. Hata hivyo, walipigwa stop hadi tarehe 30 Aprili ndipo watakapoanza kufanya mikutano ya hadhara na si maandamano tena. Tunajua kuwa wakati huo Bunge Maalum litakuwa limesitishwa na wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi watakuwa wanajiandaa na vikao vya Bunge la Bajeti. Hawa UKAWA wataendelea vipi kuwa na mshikamano ilhali wabunge watakuwa busy na bunge la bajeti? Hakika hili ni bao jingine la kisigino. Kwa sasa wamekalishwa chini kama bondia aliyepigwa na mpinzani wake huku akihema asijue la kufanya. Wakati wao wataanza mikutano ya katiba, wananchi watakuwa wameshahamishia mawazo yao kwenye Bunge la Bajeti huku wakisubiri kwa hamu kusikia ni nini serikali itafanya juu yao. Hakika kati ya bajeti na Katiba, ni wazi kuwa suala la bajeti ndilo hugusa maisha ya wananchi moja kwa moja na hivyo ni vigumu kwa UKAWA kupata watu wa kuwaunga mkono.

Wadau, wakati UKAWA wanaondoka, walitarajia kuwa wataungwa Mkono na wabunge wengi wa kundi la 201. Hata hivyo siku moja tu baada ya kuondoka kwao, baadhi ya wabunge ambao waliondoka pamoja nao akiwemo Mwalimu Ezekiel Oluoch, walirejea Bungeni huku wakiwakana na kuwananga UKAWA. Hakika hili ni pigo jingine. Imekuwa ni fedheha kwao na sasa wamekuwa mabubu kwa vile hawana avenue ya kusemea.

Wadau, baada tu ya UKAWA kuondoka, kuna shirika moja limejifanya kuendesha utafiti ili kujua mtizamo wa wananchi juu ya mijadala bungeni. Eti katika utafiti huo, kwamba Wazanzibari wengi wanaunga mkono muundo wa serikali tatu kama ilivyo kwa bara. Mbaya zaidi, wakamuita mzee Warioba ili atetee hoja hiyo. Hakika hii ni fedheha kubwa na imedhihirisha ni kwa namna gani UKAWA wametepeta. Badala ya kumuacha mzee wa watu augulie madongo anayopewa bungeni, wao wanazidi kumdhalilisha. Mbaya zaidi, Warioba akajifanya kukemea lugha zinazotolewa bungeni asi if yeye ni Presidaa.

Wadau, Mwenyekiti wa CCM ambaye ndiye Rais wa Nchi anatarajia kuwa mgeni rasmi wakati wa sherehe za Mei Mosi yaani siku moja tu baada ya UKAWA kuanza mikutano yao. Ingawa suala la katiba si moja ya ajenda ya sherehe hizo, ni wazi kuwa Mheshimiwa Rais anatumia japo muda kidogo kuelezea juu ya mchakato huo. Hakika nitamshangaa sana kama hatagusia hilo. Katika hotuma hiyo, ni wazi kuwa Rais Kikwete atasimamia msimamo wake ule ule alioutoa Bungeni tarehe 21 Machi 2014 wakati akilizindua bunge maalum. Hotuba hiyo ya JK itazidi kuwatokomeza kabisa UKAWA na kwa vile wananchi wengi watasikiliza hotuba hiyo, ni wazi kuwa hata UKAWA watazunguka nchi nzima, hawatabadili fikra za wananchi. Hili ni pigo jingine kwa UKAWA.

Wadau, yapo mengi ila kwa hayo niliyoyasema, ni wazi kuwa UKAWA wamelikoroga na lazima walinywe. Hakika wamepigwa bao la kisigino huku wakibaki hawana cha kufanya.

Wewe ni mbumbumbu kweli,hakuna nondo wala gogo vinavyoongelewa na hao ccm,wote wanaongea pumba tu tena za kukaririshwa na mabwana zao,na wanachoongea ni kilekile,na kwakuwa ni ma mbumbumbu yamekalia kujadili wa tu badala ya hiyo rasimu,si waseme basi hiyo serikali 2wanayotaka itatatuaje kero za muungano,hawawezi maana tangu muungano hizi kero zipo tu,jk akasema hizo kero zinazungumzika,kivipi? Ikiwa tangu enzi na enzi kero zipo tu?au walikuwa hajui kuzizungumza sasa hivi ndiyo wamejuwa?mburula nyinyi!
 
Mh!Pole wale watanzania wa jana si wa leo na kamwe hawezi kuwa wa kesho.Ni bahati mbaya umekubali kudanganywa na wajume wa CCM toka Zanzibar kuwa wanapenda Muungano uendelee,lakini wakiwa kwenye Bunge la wawakilishi ni hao hao wanaokataa kuwepo kwa muungano,na si hilo tu hata uwepo wa Watanzania bara kuwepo Zanzibar,kufanya kazi au biashara.Ni mara ngapi biashara za Wadanganyika wenzaki zinachomwa moto si sababu ya biashara kuwa haramu la,bali sababu ya wanakotoka.

Cha msingi ningeona unaongea jema kama ungewaeleza wajumbe hawa waeleze ukweli ili tuapte suluhisho la kudumu.Kuna wengine ni wapenzi wa serikali mbili lakini lenye suluhisho la kudumu na marithiano ya pande zote mbili.Kwa kutudanganya watanzania hakutasaidia Muungano kamwe.Mnaweza kutumia nguvu kuwalazimisha muungano muutakao,lakini sidhani kama kutakuwa na usalama huko tuendako.

Wazee walisema ni rahisi kumlazimisha Punda kwenda kisimani,lakini si rahisi kumlazimisha kunywa maji.
Mkuu, sidhani kama umesoma na kuelewa. Hata hivyo, suala la muundo upi wa muungano unafaa haliwezi kupatiwa ufumbuzi humu JF. Mjadala kwa sasa upo ndani ya bunge maalum. Kitendo cha UKAWA kuondoka Dodoma ni wazi kuwa wamejinyima fursa ya kutoa hoja za kutosha juu ya mfumo wanaoupendekeza
 
Pole sana ndugu. Hakika uzi huu si level yako

mpododo unakuwasha sio bure! Ukawa wametoka bungeni kwanini waliobaki bungeni wanawazungumzia walio nje? watunge katiba wawaache waliosusia,
 
Back
Top Bottom