UKAWA Wapigwa Bao la Kisigino

UKAWA Wapigwa Bao la Kisigino

Huyu naye awe katibu wa UKAWA? Kanisa limemshinda, familia imemshinda, chama kimemshinda na sasa UKAWA utamshinda
Nashangaa kazi ni kuegemewa na watu kama picha inavyoonesha hasa ndiyo kazi anayoiweza haya mengine anajichanganya halafu anawachanganya na wenzake,utakumbuka ukawa nje ya bunge sijui kaipotezea wapi.
 
Kwanza kabisa nikupe pole sana kwa kuwadanganya wananchi kwamba ukawa walichukua posho zote na hapo hapo unasema walirudi tena kuchukua posho sasa unajichanganya mwenyewe.kama walichukua posho zote walikuja kufanya nini tena bungeni?

Swala la kuzuia mikutano yao hilo liko wazi kwamba ukawa wako sahihi kwa kile wanachokisimamia ndio maana ccm inaogopa na kulitumia vibaya jeshi la police wakizani watanzania ni vibofu kumbe mlango wa nyuma mnajimaliza wenyewe pole pole.

Kumbuka kwa sasa kila mtu anafanya maombi maoni ya tume yapite ya serikali tatu.wewe kwa ushabiki unafanya kinyume na maombi hayo adhabu yako utaipata hapahapa duniani wala hilo halina ubishi.

Sasa nakwambia mlivyowazuia ukawa ndo mnawapa nguvu zaidi kujipanga huku wakisubiri sherehe za muungano zipite wamjibu rais kwa hoja juu ya maoni ya tume.hamtaweza kuzuia huu mchakato labda dunia ife.

Tarehe 30 April ni kesho kutwa tu.mikutano itafanyika na hoja kama zilivyotolewa na warioba zitatolewa hivyo basi usione kama wamenyamazishwa bali sauti kuu itatokea na wananchi tumeamua tutawachangia pesa ili mchakato ufike maeneo yote nchi nzima.

Mwisho nawapongeza ukawa kwa kusimamia maoni ya wananchi na kutoka nje ya bunge ili kutokuwa sehemu ya interahamwe ambao kazi yao ni kupora pesa za walipa kodi kwa kisingizio cha kuandika katiba mpya wakati wanaandika katiba ya ccm.

Mungu mbariki warioba, wabariki ukawa, msamehe Lizaboni kwa kuwa anatetea ufisadi alio nao asiumbuke, ibariki Tanzania.

mkuu, kuhusu posho, hakuna mahala nimesema kuwa wamechukua posho. Isipokuwa nimesema kuwa kuna taarifa zilizagaa kuwa walichukua posho. Kwa vile zimetangazwa kupitia vyombo vya habari, ni wazi kuwa watanzania wengi wamezosikia na wamewalaani kwa kitendo hicho.

Kuhusu mikutano ya UKAWA kuzuiwa, ni dhahiri kuwa CCM imetumia silaha ilizonazo kwa manufaa ya taifa. Hata wakifanya mikutano hiyo, haitakuwa na matarajio waliyokuwa nayo awali. Kumbuka kuzuiwa kwa UKAWA hakujawapa nguvu hata kidogo na badala yake wamehemewa ile mbaya
 
Usiwe mtumwa kiasi hicho. Komba kasema nini bungeni! Bulembo kasema nini bungeni! Ni kelele tupu hakuna hoja.kila mtu atahukumiwa kwa matendo yake.ccm leo haipo kesho chama kingine chukua hatua.
Lisu alisema nini bungeni,mbowe alisema nini,Jusa alisema nini na Lipumba alisema nini acha bangi zako sote tunafuatilia bunge mambo yako ya kibavicha sitaki.
 
Lengo la ukawa walitaka kuchukua pesa bila kufanya kazi tena walitaka kuchukua mara mbili mwigulu kawastukia sasa wanahangaika kama ndege juu ya mti uhuni huu tulijua utakuwa na mwisho ,mwisho wenyewe ndiyo huu watakoma.

Siku zote ukikosa hoja ni vizuri ukabuni mpango mkakati mpya kuliko kupotosha.ukawa hawana njaa ni wazarendo kwelikweli kitendo cha kuacha posho na kurudi kwa wananchi ni uzalendo wa aina yake tuwapongeze.sasa mnazusha tu.hayo yote yatakwisha.
 
Pole sana ndugu. Wewe kama unaita pumba, Watanzania wengi wanaziamini na hakika kila kona mitaani wananchi wanawalaani vibaya sana hawa UKAWA

Ambaye anaalaani takwimu zilizowasilishwa na tume, wanaodhihaki tume, yenye wajumbe kama warioba, salimu, kabudi, baregu na wengine wengi,
atakuwa mwendawazimu!
 
Nashangaa kazi ni kuegemewa na watu kama picha inavyoonesha hasa ndiyo kazi anayoiweza haya mengine anajichanganya halafu anawachanganya na wenzake,utakumbuka ukawa nje ya bunge sijui kaipotezea wapi.
Hakika ndani ya UKAWA, kuna wachanganyaji wengi kweli
 
Nashangaa kazi ni kuegemewa na watu kama picha inavyoonesha hasa ndiyo kazi anayoiweza haya mengine anajichanganya halafu anawachanganya na wenzake,utakumbuka ukawa nje ya bunge sijui kaipotezea wapi.

Simiyu kuna maafa, nenda kawasaidie jamaa zako!
 
Ambaye anaalaani takwimu zilizowasilishwa na tume, wanaodhihaki tume, yenye wajumbe kama warioba, salimu, kabudi, baregu na wengine wengi,
atakuwa mwendawazimu!
Walaaniwe wale wote wenye dhamira ya kuliangamiza taifa hili. Ahsante Mungu kwa kuwafumbua macho wabunge wa CCM kupitia mwenyekiti wake Rais JK
 
Mh! Tunachotaka AMANI, UPENDO, USHIRIKIANO UNAFUU WA MAISHA, HUDUMA BORA ZA AFYA, UMEME , MAJI SAFI , MIUNDO MBINU e.t.c
 
Walaaniwe wale wote wenye dhamira ya kuliangamiza taifa hili. Ahsante Mungu kwa kuwafumbua macho wabunge wa CCM kupitia mwenyekiti wake Rais JK

Wanaopindua takwimu ndo wataliangamiza taifa hili! Maana masikio yao wameziba na pamba, hawasikii!
 
ukawa watoto deko. Hakuna sababu inayozui bkt kutokuweza kupiga kura ya maamuzi hata kama ukawa hawapo. We ngoja bkt liendele agosti uone kama kura hazitapigwa. Hayo matumaini ya ukawa et hakuna kura bila wao hz ndoto macho

Sidhani kama unajua uliloliandika,hata CCM wanajua kuwa Upande wa pili wa Zanzibar ambao CUF ndiyo wanawabunge pekee hawawezi pata 2/3 ya kura na hapa kinachotakiwa ni marithiano tu,vinginevyo ninakuhakikishia hakuna Katiba hapo.

Pili hata hao wajumbe wa CCM toka Zanzibar wanatudanganya tu,kwao huko hawautaki aslani huo Muungano na wanawategema zaidi hao CUF na ninauhakika wanakifurahia sana kilichotokea sababu wanajua dhahiri hawataki Muungano.

Wajumbe hawa wa CCM wakiwa Zanzibar hawautaki huo muungano iweje leo wautake?Au sababu ya posho?Kama ni mtu wa Bara,ni bora ukaelewa mapema,wa bara ndiyo tuliokwenye matatizo hapa,hawa wanatudanganya tu.Ni bora wangesema ukweli kila kitu kikatatuliwa katika kweli kuliko hivi ilivyo.Hakuna kitu hapo kaka yangu.
 
Hadi tutakapoanza kuchinjana hadharani ndipo CCM watakapojua si kila jambo ni la kulazimishia matakwa yao.

Hivi hawa CCM mbona wangeweza kuwashawishi wananchi kwa kutumia akili ya kawaida kabisa hata bila kuhonga na kugombana na mtu?
Wao wanashikilia dola na kila rasilimali ya nchi na wana balozi nyingi huko nje-ikimaanisha wana-connections kibao za kuturidhisha japo nusu ya matakwa yetu wananchi...lakini walivyo wajinga,wanataka kutumia nguvu na ujeuri...wapuuzi kabisa.

Watakacholazimisha kukiandika kama katiba,hakika kitasababisha bendera yetu kuja kuwa na rangi nyekundu.

I don't hate politics but i hate stupid political parties like CCM.
 
nenda lumumba ukachukue buku 7 uende ukalale
Wadau, amani iwe kwenu.

Mtakumbuka kuwa tarehe 17 Aprili 2014, Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wanaojiita kwa jina la UKAWA, walitoka Bungeni Mjini Dodoma wakati wa mjadala wa Rasimu ya Katiba katika sura ya Kwanza na ya Sita kwa madai kuwa wamechoshwa na CCM kutumia uwingi wao kushinikiza muundo wa serikali mbili na kuhamasisha makundi ya kijamii wakiwemo waumini kususia muundo wa muungano wa serikali tatu. Wakati wanatoka, walisema kuwa wanaenda kuishtaki CCM kwa wananchi.

Wadau, wakati UKAWA wanapanga kwenda kuishtaki CCM kwa wananchi, CCM tayari ipo kwa wananchi ikiwaeleza bayana wananchi sababu za chama kupendekeza muundo wa muungano wa serikali mbili huku ikipinga kwa nguvu muungano wa serikali tatu. Tumemuona Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana akifanya ziara za kichama huko Kigoma na mikoa ya kanda ya Ziwa. Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) umeratibu na kuendesha matembezi ya bodaboda katika mikoa kadhaa nchini na ujumbe katika matembezi hayo ni kuuenzi muungano ulioasisiwa na Hayati Mwalimu Nyerere na Abeid Aman Karume. Katika ziara zote hizo, wananchi wameonekana kuelewa na kuwashangaa wale wanaotaka kuvuruga amani na utulivu wa nchi yetu.

Wadau, UKAWA walipoondoka Bungeni, walitarajia kuwa, Bunge hilo litavunjwa kutokana na wao kutokuwepo. Matarajio yao ni kuwa, Bunge likiahirishwa, azma yao ya kukwamisha mchakato huo yatakuwa yametimia. Hata hivyo, haikuwa hivyo. Wabunge waliobaki wengi wao wakiwa ni wa CCM wanaendelea na mjadala na kwa takriban wiki mbili sasa, CCM wamepata muda wa kutosha wa kusema yale yaliyo dhihiri huku wananchi wengi wakisikiliza kupitia Runinga, Radio na kusoma kupitia mitandao ya kijamii ukiwemo mtandao huu pendwa wa JF. Hakika wabunge wengi waliopata nafasi ya kuongea wamemwaga nondo za uhakika zilizowashawishi wananchi huku wakiendeleza vijembe vile vile vilivyowakimbiza UKAWA. Nina hakika kuwa wanavipata vijembe hivyo huko huko waliko. Hakika kwa hili, UKAWA wamepigwa bao la kisigino na wananchi wanaendelea kuwalaani katika kona zote za nchi.

Wadau, wakati UKAWA wanaondoka, zilisikika taarifa kuwa wamechukua posho zote na kujongomea. Hakika kashfa hii imewachafua sana na hawatakuja kusafishika katu. Watanzania wana hasira nao sana na hakika wasitarajie kuungwa mkono na wananchi wengi. Ingawa jitihada zimefanyika za kuwasafisha na kashfa hiyo kupitia Gazeti la Mwananchi, ukweli ni kwamba wananchi wengi wameamini kuwa wabunge hao wamechukua posho na kutokomea. Hilo ni doa kuu ambalo haliwezi kuondolewa kwa Omo wala Aerial.

Wadau, wakati UKAWA wanaondoka, walitarajia kuwa wataanzisha maandamano na mikutano nchi nzima kuanzia siku ya pili baada ya kuondoka kwao. Hata hivyo, walipigwa stop hadi tarehe 30 Aprili ndipo watakapoanza kufanya mikutano ya hadhara na si maandamano tena. Tunajua kuwa wakati huo Bunge Maalum litakuwa limesitishwa na wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi watakuwa wanajiandaa na vikao vya Bunge la Bajeti. Hawa UKAWA wataendelea vipi kuwa na mshikamano ilhali wabunge watakuwa busy na bunge la bajeti? Hakika hili ni bao jingine la kisigino. Kwa sasa wamekalishwa chini kama bondia aliyepigwa na mpinzani wake huku akihema asijue la kufanya. Wakati wao wataanza mikutano ya katiba, wananchi watakuwa wameshahamishia mawazo yao kwenye Bunge la Bajeti huku wakisubiri kwa hamu kusikia ni nini serikali itafanya juu yao. Hakika kati ya bajeti na Katiba, ni wazi kuwa suala la bajeti ndilo hugusa maisha ya wananchi moja kwa moja na hivyo ni vigumu kwa UKAWA kupata watu wa kuwaunga mkono.

Wadau, wakati UKAWA wanaondoka, walitarajia kuwa wataungwa Mkono na wabunge wengi wa kundi la 201. Hata hivyo siku moja tu baada ya kuondoka kwao, baadhi ya wabunge ambao waliondoka pamoja nao akiwemo Mwalimu Ezekiel Oluoch, walirejea Bungeni huku wakiwakana na kuwananga UKAWA. Hakika hili ni pigo jingine. Imekuwa ni fedheha kwao na sasa wamekuwa mabubu kwa vile hawana avenue ya kusemea.

Wadau, baada tu ya UKAWA kuondoka, kuna shirika moja limejifanya kuendesha utafiti ili kujua mtizamo wa wananchi juu ya mijadala bungeni. Eti katika utafiti huo, kwamba Wazanzibari wengi wanaunga mkono muundo wa serikali tatu kama ilivyo kwa bara. Mbaya zaidi, wakamuita mzee Warioba ili atetee hoja hiyo. Hakika hii ni fedheha kubwa na imedhihirisha ni kwa namna gani UKAWA wametepeta. Badala ya kumuacha mzee wa watu augulie madongo anayopewa bungeni, wao wanazidi kumdhalilisha. Mbaya zaidi, Warioba akajifanya kukemea lugha zinazotolewa bungeni asi if yeye ni Presidaa.

Wadau, Mwenyekiti wa CCM ambaye ndiye Rais wa Nchi anatarajia kuwa mgeni rasmi wakati wa sherehe za Mei Mosi yaani siku moja tu baada ya UKAWA kuanza mikutano yao. Ingawa suala la katiba si moja ya ajenda ya sherehe hizo, ni wazi kuwa Mheshimiwa Rais anatumia
]
 
Mkuu, sidhani kama umesoma na kuelewa. Hata hivyo, suala la muundo upi wa muungano unafaa haliwezi kupatiwa ufumbuzi humu JF. Mjadala kwa sasa upo ndani ya bunge maalum. Kitendo cha UKAWA kuondoka Dodoma ni wazi kuwa wamejinyima fursa ya kutoa hoja za kutosha juu ya mfumo wanaoupendekeza

Kama kiongozi aliyetegemewa kutokuegemea upande wowote amesaliti wadhifa wake sidhani kama mjadala ungeendelea.Alichokosea na anachoendelea kufanya Sitta ni kufumbia macho matusi,ubaguzi,kashfa,dharau ,mipasho ambayo imeleta mgawanyika ndani ya bunge hilo.

Haiwezekani anasimama mjumbe wa upinzani akiongea lugha isiyofaa waliowengi wanapewa nafasi ya kuomba mwongozo au taarifa na mjumbe kuombwa afute kauli yake,lakini ona upande wa pili wa wajumbe ambao ni CCM wametoa kejeli,matusi,dharau na hata kufikia mahali kujigawa kwa ukabila na ukanda,na Sitta hakuliona hilo pamoja na kuomba muongozo na taarifa,je kulikuwa na uhalali gani?

Kwanini hakukemea?Tuliokuwa tunaangalia hilo Bunge hatukuwa tunaangalia kwa minajili ya huyu kundi gani lakini imetufanya tumuone Sitta ndiyo kikwazo kikubwa kwenye kuapta mijadala yenye hoja zenye mantiki na tija kwa Taifa.

Juzi,Paul Makondo amewatukana wajumbe walio nje ya ukumbi kwa kuwaita watoto wa shetani,Sitta amemuomba tu futa kauli na alivyokataa basi kosa limeisha,kwanini asiende mbali na kumtoa nje au kumpeleka kwa Kamati ya nidhamu?

Kwanza Kamati hiyo inawajumbe wote waCCM unadhani itaweza kumwadabisha Makonda?Lizboni kuwa fair tetea haki popote ulipo hata kama unayemtetea mnatofautiana kwenye itikadi.

Kwa kweli ukiniuliza nani ameliharibu bunge hili maalum,kwa moyo mmoja nitakujibu Sitta na Makamu wake Suluhu,huo ndiyo ukweli wameshindwa kuliendesha Bunge kwa ufanisi bila kujali vyama watokako.

Haitupendezi wale tunaopenda haki itawale kokote bila kujali unitikadi gani au kabila utokalo.Ndivyo nilivyo,labda wa aina yangu tupo wachache lakini ndvyo ninavyofikiri.

Hata leo badala ya wajumbe kujadili hoja iliyopo mezani wanajadili watu waliotoka nje.
 
Siri: UVCCM Inampango Wakuchoma tena Makanisa kama Ukawa watafanya mikutano Zanzibar.

Ndugu Wazalendo wa Zanzibar na Wale wa Tanganyika/Tanzania Bara ambao wanaipendelea Nchi yetu hii impya ya Tanzania kuwa na Umoja, amani, Utulivu na Muungano wenye Muundo wa Serikali 3 ambao utaondoa kero na manunguniko. Napenda kuwajuilisha kwamba nimepata habari kutoka kwa Sheha mmoja wa CCM ambae mimi ni jamaa yangu wa damu.
Amesema UVCCM wameanshaandaa Kufanya fujo visiwani ili Wa Wadis-rupt (wawaharibie) UKAWA pindipo kama watafanya Mikutano Zanzibar. Hoja hiyo inaaminika kuwa ni mpango mwengine kabamba wakutaka Kumshinikiza Maalim Seif na Ugaidi katika Chama chake CUF. HIvo Ile hoja ya LUKUVI kusema kwamba wanaogopa Serikali ya Kiislamu inaweza kujengwa zaidi hapo pindipo Makanisa mengine yatachomwa Visiwani..
Tunatakiwa tuichukue habari hii in a Serious matter niko mbioni kuipata barua waliojiandaa CCM na nitaiweka hapa kama itawezekana..
Nawasilisha Ujumbe.
 
Nasubiri kura hiyo kesho tuone mwisho wa vijembe na matusi yote tuliyoyasikia kwa kipindi chote tangu UKAWA walipotoka
 
Kama kiongozi aliyetegemewa kutokuegemea upande wowote amesaliti wadhifa wake sidhani kama mjadala ungeendelea.Alichokosea na anachoendelea kufanya Sitta ni kufumbia macho matusi,ubaguzi,kashfa,dharau ,mipasho ambayo imeleta mgawanyika ndani ya bunge hilo.

Haiwezekani anasimama mjumbe wa upinzani akiongea lugha isiyofaa waliowengi wanapewa nafasi ya kuomba mwongozo au taarifa na mjumbe kuombwa afute kauli yake,lakini ona upande wa pili wa wajumbe ambao ni CCM wametoa kejeli,matusi,dharau na hata kufikia mahali kujigawa kwa ukabila na ukanda,na Sitta hakuliona hilo pamoja na kuomba muongozo na taarifa,je kulikuwa na uhalali gani?

Kwanini hakukemea?Tuliokuwa tunaangalia hilo Bunge hatukuwa tunaangalia kwa minajili ya huyu kundi gani lakini imetufanya tumuone Sitta ndiyo kikwazo kikubwa kwenye kuapta mijadala yenye hoja zenye mantiki na tija kwa Taifa.

Juzi,Paul Makondo amewatukana wajumbe walio nje ya ukumbi kwa kuwaita watoto wa shetani,Sitta amemuomba tu futa kauli na alivyokataa basi kosa limeisha,kwanini asiende mbali na kumtoa nje au kumpeleka kwa Kamati ya nidhamu?

Kwanza Kamati hiyo inawajumbe wote waCCM unadhani itaweza kumwadabisha Makonda?Lizboni kuwa fair tetea haki popote ulipo hata kama unayemtetea mnatofautiana kwenye itikadi.

Kwa kweli ukiniuliza nani ameliharibu bunge hili maalum,kwa moyo mmoja nitakujibu Sitta na Makamu wake Suluhu,huo ndiyo ukweli wameshindwa kuliendesha Bunge kwa ufanisi bila kujali vyama watokako.

Haitupendezi wale tunaopenda haki itawale kokote bila kujali unitikadi gani au kabila utokalo.Ndivyo nilivyo,labda wa aina yangu tupo wachache lakini ndvyo ninavyofikiri.

Hata leo badala ya wajumbe kujadili hoja iliyopo mezani wanajadili watu waliotoka nje.
Tetty, porojo nyiiiingiiiii point sifuri
 
Nasubiri kura hiyo kesho tuone mwisho wa vijembe na matusi yote tuliyoyasikia kwa kipindi chote tangu UKAWA walipotoka
Mkuu, kura haitapigwa kesho. Itapigwa mwezi wa Nane
 
Back
Top Bottom