Mabalozi Wapya - Utamaduni wa kuzungusha viongozi!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,731
40,836
Bila ya shaka hadi sasa mtakuwa mmeshapata habari kuwa Mhe. Kikwete ameteua mabalozi wapya. Wengi wao ni wapya na wengine ni wa zamani. Wengine haina hata mantiki sijui kwa nini wamepewa ubalozi!! Baadhi ya uteuzi huo.

Mhe. Ramadhani O. Mapuri - Balozi mpya China....

Kamanda Adadi Rajabu - Balozi Mpya Harare Zimbabwe!!

Balozi Kibelloh - Atolewa Uingereza na kwenda Paris

Balozi Daraja wa US..??????????????????
 
Nimesoma huo uitwao, "uteuzi", ambao kwangu miye naita ku recycle walewale waliokuwepo sikuzote!!....Yaani sioni hata aliyeteuliwa, bali naona waliobadilishiwa kazi zao tu, toka kituo kimoja cha kazi kwenda kingine.
 
Mwanakijiji,
Unadhani hawa watu wameteuliwa kwa sifa gani walizonazo? Mimi nadhani udini.

1.Omar Ramadhan Mapuri (China)
2.Adadi Rajabu (Zimbabwe)
3.Mwanaidi Sinare Maajar (London-Uingereza)
4.Ahamada Ngemera (Berlin-Ujerumani)
5.Hussein Said Khatib (Muscat-Oman)
 
:lol: :lol: :lol: :lol:

Guys, lets be serious, tukianza kunyosheana vidole hatutafika kokote. Kilicho muhimu ni kujenga misingi imara ya kuimarisha UCHUMI wetu kwa faida ya wote.
Labda tuwajadili hao walioteuliwa kama uwezo wanao au lah. na akiteua wakwere sijui ndio tutasemaje!!!. Na huo uteuzi je ni yeye JK kateua au kapelekewa na Bi mdogo Asha ili aidhinishe uteuzi na hapo mtasemaje? anyway my point is tuangalie uwezo wa walioteuliwa na si kabila wala dini
 
Wanabodi
Samahanini kama comment zangu zenye sura ya udini zimeleta mtafuruku lakini nilikuwa nimemuuliza mwanakijiji na yeye najua anajua ni kwa nini nimemuuliza hivyo.
Kuhusu watu walioteuliwa sidhani kama kuna mjadala hapo, sidhani kama kuna mtu yeyote hapo ambaye ana hadhi ya kuwa balozi, nadhani watu watakaosikitika zaidi ni wale vijana pala foreign ambao walikuwa wanamatumaini kuwa sasa nafasi za ubalozi wataanza kupewa mabalozi wa kweli lakini kumbe mfumo ni ule ule wanasiasa, mapolisi, wanajeshi ndiyo wataoendelea kuwa mabalozi.
Ogah
IGP ni mkwere na watu hawakuongelea hilo.
 
Wanabodi,

Ni muhimu kwa watu kuacha uoga na kuwa free to express their opinions regardless kwamba wataoffend kikundi fulani cha watu, suala la udini katika uchaguzi wa hawa mabalozi ni jambo ambalo hata mimi nilifikiria na wala sioni aibu kusema hivyo !

Tuache unafiki wa kuogopa kulizungumzia hilo , Dini hapa imeplay part yake kwa mtazamo wangu . Katika nchi ambayo imekuwa made 50% wakristo na 50 % waislamu haya ni mambo muhimu ya kuangalia wakati wa kuchagua viongozi kumake sure kwamba tunakuwa na equal representation

Masuala ya dini yapo jamani tuache unafiki let's be realistic .
 
Jamani wanabodi tuache maneno ya udini na ukabila. Mimi naweza kuwa mkristo mzuri sana, tena wa damu!!!!!!!!! Lakini haininyimi usingizi hata kama majina hayo yote yatakuwa mnayoyashukia nyie kuwa ni waislamu au nani. Hata safu zote ziwe waislamu au wakristo, mie kitakacho nipunguzia usingizi kama hawatafanya kazi zao zinavyotakiwa. They should do the right thing!
Labda tunge jadili jinsi gani mtu kama mapuri ambaye aliamrisha jeshi lipige wananch amepewa hiyo post! Je wako qualified??
 
Interested Observer ,

The problem is you are too theoretical , Kusema kwamba hata kama viongozi wote wakiwa ni wa dini fulani aitakunyima usingizi ...huo ni uongo na unafiki mkubwa !

Ni jambo la kushangaza sana kuchagua mabalozi watano wote wawe wa dini moja , Watu wa Rwanda walikuwa na mentality kama zako interested observer ndio maana walifika pale walipofika .

Tuacheni huu unafiki wa kuogopa kuongelea ishu fulani as if ni taboo wakati tukiwa majumbani kwetu tunazingumzia !
 
Tukisemea tu udini au mnafikiri ndio ataacha!!!!, no way hawezi, na huo si ufumbuzi wa suala zima. Tuseme kuhusu QUALIY ili siku zijazo JK awe makini ktk teuzi zake. kuna mtu kama mapuri anajulikana ni mropokaji na anaplekwa nchi ambayo tunahitaji mtu very smart kwenye mambo ya kiuchumi pia, etc etc
 
Ogah ,

Mimi sikupata bahati ya kuyaona hayo madai ya waislamu juu ya mkapa , ila ningefurahi sana kama ungeyapost hapa . Lakini nadhani ishu ya kujoin vyuo vya elimu ya juu tanzania iko very straight forward na wala aijali dini ,, inategemea grade ulizopata ukiwa kidato cha sita na kozi unayotaka kujoin !

Najua suala hili watu hawataki kuzungumzia lakini ni very sensitive na kuna kila sababu ya kuzungumzia haya mambo before it is too late ! Hivi Jk mwenyewe atajisikieje siku hiyo atakapokuwa akiwaapisha hao mabalozi watano na kila mmoja akiapa kutumia kitabu kimoja tuu cha dini ?

Ndio maana mwanzoni kabisa nimesema ni lazima tunapotoa mawazo yetu hapa ni muhimu kutokuwa too theoretical.
 
Hilo la udini kama akiamua kuliweka mbele litamrudi tu na ATALIJUTIA BAADAYE. Ila labda hilo halitumii kwa sasa bali uwezo wa mtu. Lakini cha ajabu NA KIBAYA hapa ni huyo balozi wa UK kuhamishiwa Paris. Huyu balozi amelalamikiwa sana na watu mbali sasa kuliko JK?. Hii siyo recycling kuhusu akina Adadi Mapuri nk?

AU HUYO BALOZI WA UK NI MCHAPA KAZI SANA ILA LBDA TU ANA TABIA YA KUDHARAU WATU WA CHINI? LAKINI NI MCHAPA KAZI WA KAZI ZA SERIKALI?

LBDA KIBURI CHA UONGOZI KINAANZA KUONGEZEKA , THEN KAMA ITAKUWA HIVYO BASI TUTEGEMEE HATA MABADILIKO YA KATIBA ILI ATAWALE ZAIDI.
 
Nilijua jambo kama hili linaweza kutokea. Lazima mkae na kujiuliza ni kwa nini watu wameanza kuongelea udini? Sababu kubwa ni kwamba wameshindwa kujua ni vigezo gani ametumia kuwateua aliowateua, je wale vijana pale foreign wengi wao wakiwa wa dini hiyo hiyo hawawezi kazi kama vipuri, mapuri jina lolote mnalomwita? Mimi sina matatizo sana na udini kwani watu wengi najua wana majina ya dini fulani ila siyo waumini wazuri wa dini hizo. Hata kama alitaka kuongeza idadi ya waislamu kwenye utumishi wa umma please wako wengi wenye uwezo siyo Adadi au Mapuri. Pia baada ya kusoma post zenu ilibidi nilichunguze baraza la mawaziri, nimegundua kwenye wizara muhimu (key) uwiano ni 1:6. Hebu chunguzeni nje, fedha, mipango, ulinzi, ndani, na usalama wa raia. Kama mtoa hoja mmoja alivyosema tuangalie utendani wao wa kazi, good, wengi wao hatuoni wanafanya nini. Watu wanakosa sababu zilizowaweka pale ndiyo maana wanaanza kuhoji na kubuni sababu nyingine.
Uteuzi wa Makamba ni usaliti kwa wananchi na kuendelea kujilinda, Makamba ni kiongozi wa serikali hawezi kuuliza swali lolote bungeni ni sawa na kujiuliza mwenyewe au waziri kumuuliza waziri mwenzake, nadhani lingekuwa jambo la busara kumteua mtu ambaye atawakilisha wananchi siyo serikali bungeni. Ila kutokana na mabadiliko yaliyotokea naona kuna mabadiliko anataka kufanya kwenye Chama, kuna mtu anataka amuingize kwenye nafasi ya mapuri ili aiandae nafasi ya EL, na Makamba nahisi amepewa ubunge kwa ajiri ya kazi za chama ndani ya bunge.
 
Wanabodi
Kigezo cha maana katika nafasi ya uongozi ni uwezo. Hiyo ni dhana: lakini hali halisi mara nyingi kuna mchanganyiko wa vigezo, vingine vikiwa wazi, na vingine mpaka vichokonolewe na wanaoona mbali.

Mimi sikufikiria suala la udini. Ila tatizo langu ni uwezo. Mtu kama Mapuri kupelekwa China. JK must be joking! China is an emerging superpower with a multitude of trade and business opportunities. Huko kuna changamoto nyingi zaidi kuliko kuwa balozi wa nchi kama Malawi au Zimbabwe. Uwezo wa Mapuri na Zombe una tofauti gani?

Is JK showing his true colours at last?
 
Hii inaitwa Strategy.

With Mapuri kwenda China, CCM inaongeza nguvu zake za ushirikiano na nchi ya Kijamaa.

Adadi kwenda Zimbabwe ni big security move, Zimbabwe ni delicate sasa hivi na ki-usalama ni vizuri kupeleka mwana usalama.

UK- sijui Mama Maajaar ambaye ni wakili role yake ni vipi labda ni kumpa mwanamke wa kwanza nafasi kubwa ya kiubalozi na pia "kuangalia mikataba"? No clue of her appointment on political or technical merits

Hao wengine perhaps ni career diplomats and they fit their places.

Udini? Tushaanza visingizio tena!
 
sam said:
Wanabodi
Samahanini kama comment zangu zenye sura ya udini zimeleta mtafuruku lakini nilikuwa nimemuuliza mwanakijiji na yeye najua anajua ni kwa nini nimemuuliza hivyo.
Kuhusu watu walioteuliwa sidhani kama kuna mjadala hapo, sidhani kama kuna mtu yeyote hapo ambaye ana hadhi ya kuwa balozi, nadhani watu watakaosikitika zaidi ni wale vijana pala foreign ambao walikuwa wanamatumaini kuwa sasa nafasi za ubalozi wataanza kupewa mabalozi wa kweli lakini kumbe mfumo ni ule ule wanasiasa, mapolisi, wanajeshi ndiyo wataoendelea kuwa mabalozi.
Ogah
IGP ni mkwere na watu hawakuongelea hilo.

Balozi is a political post and does not need anyone to be a career diplomat, it needs someone who can talk the president talks and directives. Other officers on the embassy, need to be technocrats=career diplomats to ensure that the purpose of having our station in certain country is strategically and effective.

Ndio maana Military, education & culturals affairs and economical attachees lazima wawe na wezo wa kidiplomasia !
 
Rufiji said:
Wanabodi,

Ni muhimu kwa watu kuacha uoga na kuwa free to express their opinions regardless kwamba wataoffend kikundi fulani cha watu, suala la udini katika uchaguzi wa hawa mabalozi ni jambo ambalo hata mimi nilifikiria na wala sioni aibu kusema hivyo !

Tuache unafiki wa kuogopa kulizungumzia hilo , Dini hapa imeplay part yake kwa mtazamo wangu . Katika nchi ambayo imekuwa made 50% wakristo na 50 % waislamu haya ni mambo muhimu ya kuangalia wakati wa kuchagua viongozi kumake sure kwamba tunakuwa na equal representation

Masuala ya dini yapo jamani tuache unafiki let's be realistic .

Rufiji,

What is the point of having a balance government based on religion if it is not effective? why fear that if one group is majority then they have an advantage?

Bottom line we are repeating the same nonsense by bitching about religion the same way it done after independence and continued in the past 3 administrations.

It is time to move one and think progressivelly and ask if these apointees can deliver! The foundation of our success is based on efficiency and effectivenes of those who are empowered to run things and not political or religious affiliation.
 
sam said:
Nilijua jambo kama hili linaweza kutokea. Lazima mkae na kujiuliza ni kwa nini watu wameanza kuongelea udini? Sababu kubwa ni kwamba wameshindwa kujua ni vigezo gani ametumia kuwateua aliowateua, je wale vijana pale foreign wengi wao wakiwa wa dini hiyo hiyo hawawezi kazi kama vipuri, mapuri jina lolote mnalomwita? Mimi sina matatizo sana na udini kwani watu wengi najua wana majina ya dini fulani ila siyo waumini wazuri wa dini hizo. Hata kama alitaka kuongeza idadi ya waislamu kwenye utumishi wa umma please wako wengi wenye uwezo siyo Adadi au Mapuri. Pia baada ya kusoma post zenu ilibidi nilichunguze baraza la mawaziri, nimegundua kwenye wizara muhimu (key) uwiano ni 1:6. Hebu chunguzeni nje, fedha, mipango, ulinzi, ndani, na usalama wa raia. Kama mtoa hoja mmoja alivyosema tuangalie utendani wao wa kazi, good, wengi wao hatuoni wanafanya nini. Watu wanakosa sababu zilizowaweka pale ndiyo maana wanaanza kuhoji na kubuni sababu nyingine.
Uteuzi wa Makamba ni usaliti kwa wananchi na kuendelea kujilinda, Makamba ni kiongozi wa serikali hawezi kuuliza swali lolote bungeni ni sawa na kujiuliza mwenyewe au waziri kumuuliza waziri mwenzake, nadhani lingekuwa jambo la busara kumteua mtu ambaye atawakilisha wananchi siyo serikali bungeni. Ila kutokana na mabadiliko yaliyotokea naona kuna mabadiliko anataka kufanya kwenye Chama, kuna mtu anataka amuingize kwenye nafasi ya mapuri ili aiandae nafasi ya EL, na Makamba nahisi amepewa ubunge kwa ajiri ya kazi za chama ndani ya bunge.

Mwamba ngoma huvutia kwake.

I am not defending Kikwete, but the truth of matter is that, all political appointments are based on personal relationship and loyalty. It is an added value if a political appointee is a technocrat and specialist of the field.

The only area that I believe we should have serious concerns is on Technocrats. Makatibu wakuu, wakurugenzi wa mikoa, wilaya, halmashauri, wizara and all sort of technical stuff that creates a structure and backbone of institution.

Waziri, Balozi, Mkuu wa Mkoa, Mbunge wa kuteuliwa could be anybody, as long as they side with the person that appointed them and spearhead the vision of Raisi.

He needs to have people who will work for his agenda in addition to Chama's agenda and country agenda.

Agenda ya Kikwete is his, not Tanzania, we have entrusted him by his visiion and Agenda, we do not have right to interfere. We can questions his moves as we should, and if we are not satisfied, there is a process to remove him and his administration from the trust we have handed him.

As of now, sitishiki na uteuzi wa kidini, my worry is efficiency and effectivenes.

If we were to lean on Udini, let ask ourselves who was running the country when we sold everything to wawekezaji and all shitty contracts and agreements we have signed for the next 20 years.

It was Ben, Emmanuel (ole Naiko), John (Rubambe) Andrew, Mary and Frederick!
 
Good to have you back Rev.

Nakubaliana na hoja yako, kimsingi huko ndio kwa kuanzia, turekebishe tulikokosea, na ikibidi kuwafikisha mahakani waliotuingiza mkenge., Hawa akina 'vipuri" walioteuliwa, nawaasa wafanye kazi zao kwa juhudi wakishirikiana vema na technocrats waliopo kwenye hizo balozi zao, wasilete uungu mtu, wasikilize hoja za waTZ waishio huko na ikibidi kuzipatia ufumbuzi/kufanyia kazi, kwani si matatizo pekee yanayopelekwa balozi, kuna hadi proposals za miradi ya kiuchumi ndani ya nchi hizo, balozi zetu zitusaidie ktk kuhakikisha nasi tunawekeza nchi za watu.
 
Sam na wengineo,
Hivi hawa mabolozi wanasaidia nini community ya kiislaam huko walikochaguliwa?
Jamani hawa mabolozi wetu wote toka Mwinyi hadi Mkapa na leo hii JK wapo huko kama wawakilishi wa CCM na sera zao. Tanzania imepata mikopo na misaada kibao toka Uingereza, Germany na Marekani kulingana na wizi unaokubalika. Wametunza vizuri account na hisa na wazee wao hawapo huko kuwakilisha mkristu wala muislaam na wala hawajiali kama kuna watanzania nje ama hakuna.
Huyo Karume alipochaguliwa watu walitukana kwa lugha yzao,matusi mazito lakini kulingana na navyosikia ndiye alitokea kuwa bolozi bora kuliko wengi bila kujali dini, kabila wala rangi yake..Hakubagua mtu. Leo hii hana nafasi ktk balozi na kulingana na habari nazozisikia hakupendwa na baadhi ya watu ambao walitaka maslahi yao mbele.
 
Back
Top Bottom