UKAWA waitisha kikao cha dharura

UKAWA waitisha kikao cha dharura

Hali ni tete kama ndo hivo, wanainchi watazidi kuwa na imani na CCM, upinzani ndio basi.
pumba kweli ww.mwka huu mtakuja na kila usanii.tunakula CCM tunalala UKAWA.Raha sana mwaka huu.
 
Babu Duni leo alikuwa viwanja vya Barafu Mburahati na Jumapili atakuwa mkoa wa Manyara Katesh Hanang.
Una lingine la kuzusha!?

Tehtehteh babu Duniiiii... Mburahati anafanyaje sasa, anasaga mahindi au... Anyways kama yeye alikuwa Mburahati basi nikutaarifu tu kuwa wenzake nccr mageuzi walikuwa star tv na vilio tele... Tehtehteh mibavicha bana... Hivi bado tu hamjui kuwa mshauzwa?? Poleni sana.
 
Kufuatia hali kuwa tete ndani ya kambi ya UKAWA, viongozi wa vyama vinavyounda umoja huo wanatarajia kukutana kwa dharura kesho kujadili mwenendo wa umoja wao.

Taarifa za ndani ya UKAWA zinasema Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe ambaye yupo nchini Marekani atalazimika kurudi haraka nchini na inaelezwa huenda akaingia usiku huu au mapema kesho kwaajili ya kikao hicho cha dharura ambacho kitaamua hatma ya umoja huo.

Mbali na Mbowe, timu yote ya kampeni za mgombea urais na mgombea mwenyewe pamoja na mgombea mwenza wanatarajia kusitisha kampeni na kurudi Dar es Salaam kwa siku ya kesho hadi watakapopata mwafaka wa masuala yanayobishaniwa ndani ya umoja huo.

Taarifa zinasema, kumekuwa na malalamiko kutoka kwa viongozi wa CUF kulalamikia kutotimizwa kwa makubaliano yaliyofikiwa wakati wanaungana na kupjnga jinsi Chadema wanavyoendesha umoja huo hadi kufikia hatua ya mgombea mwenza wa Chadema Juma Duni kutangaza kujitoa kwenye chama hicho na inaelezwa kikao hicho kitatumika kumuomba asijitoe.

CUF wanalalamikia UKAWA kuendeshwa na mtu mmoja ambaye ni Mbowe badala ya kuendeshwa kama taasisi na amekuwa akichukua maamuzi bila kushirikisha wengine.

"UKAWA ni Mbowe na yeye ndo anaendesha mambo anavyotaka kwa maslahi yake na mkwewe mzee Mtei. Huu ni uhuni ambao tulikuwa tunausikia tu ila leo tunajionea baada ya kuingia ndani" alisema kiongozi mmoja wa CUF ambaye alisisitiza kama Mbowe lengo lake lilikuwa ni kuua CUF amefanikiwa ila dhambi hiyo itamtafuna na watahakikisha Chadema haibaki salama.
 
Tanzania ya Magufuli itakuwa ya ujinga na ukapuku uliokithiri.
 
Lowasa ni mtu hatari sana yaani CCM wanahangaika sana
 
IT masaki, mbona picha za mama hamuweki? Mnakiuka maagizo ya wakubwa.
 
Hotuba ya Lusinde bungeni alifananisha ukawa ni kama kuweka mayai mengi ndani ya kapu moja akitokea mtu mwenye shabaha akalipiga lile kapu ndo kwisha habari yake
Na je alijiuliza itakuwaje kama akikosekana mtu mwenye shabaha? Hapa duniani wapo watu walioumbwa kuona vitu negative tu...Lakini nikupe pole kama unaona kuna kitu cha kuchukua toka kwa Lusinde.
 
mgogoro gani?acheni kuamini kila taarifa za humu

..mkuu kuna binadamu humu hawazipi akili zao nafasi kbs kufikiria, yani wakigeuzwa kulia wanageuka, wakirudishwa kushoto wanageuka, ili mradi wapo wapo tu.Gamba limekaa lumumba limetunga story mnaamini kirahisi tu!
 
Robethin nyinyi mliotawala nchi hii zaidi ya miaka hamsini hamna uchu wa madaraka??
MaCCM oneni hata aibu basi, Uchaguzi ni kidemokrasia atakaye shinda ndiye Raisi!!
 
Last edited by a moderator:
yaani wewe unadhani Dhalula ndiyo sahihi na siyo dharura, LMAO,Sasa sijui kilaza nani aliyeandika Dharura au aliyedhani Dharula ndiyo sahihi?wenye kujua kiswahili wanisaidie.

..umemuelewa vzr au umekurupuka!
 
habari zenu za lumumba pelekeni lunumba huko.
Ndio maana tunawangoa october 25, uwezu wa kufikiri umeishia hapo.
Mtaota sana ndoto za mchana .
 
Duh!! Ila magamba wana mbinu za kishamba kweli!!! wameona hii nayo ni mbinu kali sana kuwarubuni wana mabadiliko. Kama mwendo wenyewe ndo huu mkitoka tu baaasi kurudi madarakani itakuwa ndoto,, mmezoea kupeana vyeo bila kujali uwezo wa mtu kwasababu tu ya jina la baba. Lowasa atashinda kwa ulainiìii maana anapambana na matope badala ya ubongo.
 
Back
Top Bottom