UKAWA waeleza sababu za kuzomea Bungeni

UKAWA waeleza sababu za kuzomea Bungeni

RUCCI

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2011
Posts
1,702
Reaction score
1,716
Wabunge wa Ukawa wameelezea sababu zilizowafanya kuchukua uamuzi wa kupiga kelele baada ya Rais wa Zanzibar, Dkt Ali Mohamed Shein kuingia Bungeni hali iliyopelekea kutolewa nje ya Bunge hilo.

Mbunge wa jimbo la Hai ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa Ukawa, Freeman Mbowe alieleza kuwa walishindwa kuvumilia kuona ujio wa Dkt Shein akiingia Bungeni hapo pamoja na msheshimiwa Pandu Kificho ambaye alidai hivi sasa sio Spika wa Baraza la Wawakilishi kwa kuwa Baraza hilo lilikwisha vunjwa.

Tumeshangaa kuona Pandu Kificho anaingia kama Spika wa Baraza la Wawakilishi wakati Baraza limeshavunjwa, tulishangaa kuona Dkt Shein anaingia kama Rais wa Zanzibar wakati huo kipindi chake cha kukaa madarakani miaka mitano kimekwisha kikatiba, alisema Mbowe.

Naye mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu alisisitiza kuwa wataendelea kuonesha msimamo wao huku akimlalamikia Spika wa Bunge hilo kuwa anaendesha Bunge kibabe.

Leo hii askari wenye uniform, mae-FFU askari wa fujo wameingia ndani ya ukumbi wa Bunge. Sasa kwa wasiofahamu, ukumbi wa Bunge katika nchi kama za kwetu na nchi zinazofuata utaratibu kama wa kwetu, ukumbi wa Bunge huwa haingii mtu yoyote asiyekuwa Mbunge. Ndio maana ili Makamo wa rais na wale wakubwawakubwa tuliokuwa tunawapigia kelele? waingie, ilibidi tutengue kanuni ili kuwaruhusu waingie, alisema Tundu Lissu.

Mwenyekiti wa wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF), Juma Hamad Omary alimtaja Maalim Seif Sharif Hamad kuwa kiongozi anayepaswa kuigwa kwa kuwa aliwahi kukubali kushindwa mara kadhaa licha ya mapungufu kuonekana na kwamba hata alipokuwa Makamu wa Kwanza wa rais na kisha wawakilishi wa CCM kukataa asuhudhurie kwenye sherehe za kufunga Baraza la Wawakilishi, aliamua kutohudhuria.

Chanzo: Dar 24
 
Hi ndiyo Afrika viongozi au vyama vinang'ang'ania madaraka kwa mbinu mbalimbali wakisingizia demokrasia. Hongera JK, Mkapa na Mwinyi kukubali kuondoka madarakani muda ulipofikia tamati kikatiba; wangeweza kubadilisha katiba. Udhaifu uliopo ni vyama kufikiri vitatawala milele.
 
CCM wameamua kuitawala nchi hii kiubabe sana. Hata pale wanapojua kuwa wanaikanyaga katiba walio apa nayo, bado wanafanya vivyo mchana peupe kwa kujifanya ati hawaoni shida yeyote kwa sababu vyombo vyote vya dola wameviweka mfukoni.
Sawa, lakini, angalieni mnapovuka mipaka zaidi. Naunga mkono UKAWA kutoka nje ya ukumbi. Spika, endelea kuvunja kanuni mlizoziweka
 
Nimeshangaa sana spika kusoma riot act kama platoon commander.Disperse Mara ya kwanza disperse mara ya pili disperse mara ya tatu! Bila ya ustaarabu wa UKAWA bila shaka tungeshuhudia blood sport bungeni hapo jana.
 
Mi nafikiri wangekuwa hawaonekani kwenye tv basi wasingefanya vile.
 
Ndugai kafanya la maana kuwaondoa malofa ukumbini! Mpumbavu ni mpumbavu tuuu! Mi ukawa wamenikera pamoja na kwa niliwapankura yangu. They are morons!
 
Vipi aligusia kitendo cha maalim kujitangaza mshindi kabla tume haijamaliza kutangaza matokeo?
 
kwanini walitoka wangesubiri hao ffu ujumbe wao ungepata coverage yakutosha vilio vyao vingesikika kila kona ya dunia.
 
Ukawa ni majuha tu,haya huyo sefu kapata huo urais?urais haupatikani kwa kugonga meza.
 
Bado haijaeleweka,kuzomea zomea ni ulimbukeni na haitoi taswira ya watu civillised,afterall sio mara ya kwanza na ndio sababu tendo lenyewe la kuzomea wala halikuwa na punch kwa wananchi kwani waliona hakuna jipya na kwamba UKAWA NI ILE ILE.nilikuwa nimekaa na mwanangu wa miaka minne wa chekechea akawa ananiambia "baba waone wale wanafanya kama sisi shuleni" NIMEMNUKUU.
 
Ujumbe umefika na dunia imesikia, hilo tendo la kutoka nje wakati raisi anahutubia lina maana kubwa sana kisiasa, wasioelewa watalichukulia kiurahisi, na ndio maana Spika amesema ni jambo la kuudhi, mgogoro wa Zanzibar wapaswa utafutiwe ufumbuzi mapema
 
Makofuli aonyeshe uungwana kwa vitendo,yeye kama rais anajua matokeo halisi ya zanzibar,kama anataka kuwa kipenzi cha watu aanze na kumtambua maalim seif kama rais,aache kishabikia chama cha mapinduzi.isije ikawa HAPASTORY TU,HAKUNA KAZI#
 
Back
Top Bottom