..Kuelekea uchaguzi mkuu 2015, swali hili huwa najiuliza sana... Muunganiko wa vyama hivi vitatu vya upinzani nchini Tanzania (CHADEMA, CUF, na NCCR-MAGEUZI) mwezi October watamsimamisha nani kuwa mgombea? Tukitazama kiundani tunaona kila chama kina mwanachama ambaye ni imani yangu anatamani nafasi hii ya Urais..
Angalia CUF kuna mchumi Prof. Ibrahim Lipumba ambaye amekuwa mgombea kwa miaka 15 sasa, CHADEMA kuna Dr. Slaa ambaye kagombea mara moja tu lakini ushawishi alionao kwa wananchi ni mkubwa hasa kupitia kuibua kwake kashfa mbalimbali kubwa nchini za ufisadi na kutoka NCCR- MAGEUZI kuna Joseph Mbatia ambaye nae ana uwezo mkubwa wa kuibua hoja, kuijadili na kuitetea hasa kwenye maswala ya Elimu na Uchumi wa Nchi.. Sasa swali langu liko palepale, NI NANI ATAGOMBEA URAIS KUPITIA MUUNGANIKO HUU? Naomba kuwasilisha.