Lipumba Mwenyekiti mpya wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD)

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) huku makamu wake akiwa ni mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, Haji Ambar Khamis.

Uchaguzi huo umefanyika leo Jumatatu Julai 3, 2023 katika mkutano mkuu wa TCD uliokuwa na ajenda mbalimbali ikiwemo ya uchaguzi wa mwenyekiti mpya ambapo wajumbe kutoka vyama vya Chadema, ACT Wazalendo, CUF, CCM, NCCR Mageuzi na CHAUMMA walishiriki.

Profesa Lipumba amepokea kijiti kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana.

Viongozi hao watatumikia uongozi wa TCD kwa kipindi cha mwaka mmoja, kwa mujibu wa Katiba ya TCD.

Akizungumza baada ya kuchaguliwa, Profesa Lipumba amesema vipaumbele vyake katika mwaka mmoja wa uenyekiti wake ni kuongeza ushirikiano na maridhiano ndani ya vyama vya siasa, kujenga asasi za kidemokrasia na mchakato wa kupata katiba.
 
Lipumba na ule mdomo wake unaocheza kama wa mamba aonapo windo soon akitupiwa kamnofu atawavuruga wenzie.
 
Back
Top Bottom