Elections 2015 UKAWA kusimamisha mgombea Urais 2015

Jamani ni mawazo yangu tu , wadau kama kuna mtu anaweza kushawishi hii move itokee
naamini kutakuwa na uwezekano mkubwa wa kukifanya chama cha mapinduzi kuwa chama pinzani 2015
 
Mzee warioba hata asipogombea yeye, anaweza pia kusaidia mchakato wa kumpata mgombea makini kupitia ukawa ushawishi wake bado lulu
 
Jamani ni mawazo yangu tu , wadau kama kuna mtu anaweza kushawishi hii move itokee
naamini kutakuwa na uwezekano mkubwa wa kukifanya chama cha mapinduzi kuwa chama pinzani 2015

Aondoke hata leo , CCM hawana haja na wanachama kama wakina Warioba. Siku akisema anarudisha kadi mie natangaza siku hiyo ntasheherekea na itakuwa sikukuu.
 
Jamani ni mawazo yangu tu , wadau kama kuna mtu anaweza kushawishi hii move itokee
naamini kutakuwa na uwezekano mkubwa wa kukifanya chama cha mapinduzi kuwa chama pinzani 2015
Hata asipogombea warioba mwakani bado ccm kitabaki kuwa chama pinzani kwani ukawa inatisha
 
Kuna vigezo ambavyo nimeviona kuwa katika jumuiya inayounda ukawa na kugundua kuwa kuna vigezo vifuatavyo kati ya wale viongozi wanne nani anafaa kugombea urahisi:

1- Lipumba ana experience ya muda mrefu katika siasa za nchi hii kuliko wote wale
2- Anaongoza kwa shule, Lipumba ni Professor tena wa uchumi na ukizingatia tatizo tulokuwa nalo Tanzania ni uchumi
3- Akipewa Lipumba itakuwa njia nzuri ya kupata kura nyingi Zanzibar ambao kwa mtazamo wangu viongozi wengine wowote hawana ubavu wa kushindana na CCM Zanzibar
4- Lipumba ni kiongozi mzalendo ambaye hajawai kuwa na kasha yoyote ukilinganisha na viongozi wengine.
 
Nafikiri jumuiya za kimataifa zitawapeni support kwa kuwa Lipumba ni mchumi anayekubalika kimataifa, na wana imani naye sana akichukua nchi ataipeleka mbali kiuchumi
 
Sifa nyingine ni hii hapa. Lipumba hajawahi kushinda uchaguzi wowote toka kuzaliwa kwake.
 
hakika wewe hustahili Wala haufai kuwa katika umoja WA UKAWA .

UKAWA tulishakubaliana yeyote atakaesimamishwa ni halali kwetu. usitupangie kutoka lumumba kapambaneni NA matikiti maji yenu akina WASSIRA NA wenzie
 
kwahiyo wewe bila slaa huelewi somo?
 
Freedom of expression.....hongera kw akujitendea haki mengine tuachia wana ukawa.
 
Wewe usituaribie na njaa yako ya kichwani. sisi tutamweka binadamu mwenye sifa na mvuto kwa wananchi. atakayetupenda sote bila itikadi ya aina yoyote. mwenye kusimamia uchumi wa nchi na mali za watanzania kama zakwake. anayekuza kipato cha kila mtanzania kama watoto wake. Mwenye kujali ELIMU na kuthamini wafanyakazi wake kama wale wa ikulu na TRA. Mwalimu awe yule aliyepata FIRST CLASS darasani. Mwenye undugu kwa kila mtanzania na sio mtandao. Mwenye kula, kunywa na kuvaa chakwetu.... nk. HIVYO HAO WENYE KULAZIMISHA MAJINA YAO HAWAFAI NA HAWANA SIFA. JINA LA RAIS MJAYE BADO. ILA YUPO. MUNGU NI MWEMA KILIO CHETU AMEKISIKIA
 
Kuna vigezo ambavyo nimeviona kuwa katika jumuiya inayounda ukawa na kugundua kuwa kuna vigezo vifuatavyo kati ya wale viongozi wanne nani anafaa kugombea urahisi:

1- Lipumba ana experience ya muda mrefu katika siasa za nchi hii kuliko wote wale
2- Anaongoza kwa shule, Lipumba ni Professor tena wa uchumi na ukizingatia tatizo tulokuwa nalo Tanzania ni uchumi
3- Akipewa Lipumba itakuwa njia nzuri ya kupata kura nyingi Zanzibar ambao kwa mtazamo wangu viongozi wengine wowote hawana ubavu wa kushindana na CCM Zanzibar
4- Lipumba ni kiongozi mzalendo ambaye hajawai kuwa na kasha yoyote ukilinganisha na viongozi wengine.

UKAWA hawajaungana ili kugawana vyeo bali wameungana kwa mambo ya msingi kabisa. Si vizuri kuanza kuwachanganya wananchi vichwa bali tunatakiwa kujenga misingi ya kuelekea ukombozi wa kweli ambapo kila mwananchi ana mchango na madaraka yake. Tuachane na urais wa kiimla
 
Watu wengi wamekuiwa waikjiuliza kuhusu nani aweza kuwa mgombea urais kupitia muungano wa ukawa.kwa maoni yangu, hili sio swali gumu kuliko lile la nani atasimama kwa niaba ya ukawa katika viti vya udiwani na ubunge.

kwa maoni yangu na wengine wanaofatilia siasa za tanzania, swala la mgombea urais kupitia ukawa lipo wazi kabisa kwamba mgombea atakayeweza kukidhi vigezo hivi hapa chini ndiye hasa atakayeweza kuiwakilisha ukawa.na sio vinginenvyo;

1. RUZUKU YA CHAMA HUSIKA.
Kwakuwa ukawa sio chama, ila ni taasisi inayoundwa na vyama na kwa kuwa uchagui mkuu kwa ujumla ni gharama kubwa sana, ni wazi chama kilicho na ruzuku kubwa ndicho kinaweza kutoa mgombea urais labda itokee ukawa wapewe fedha z kusimamisha mgombea urais toka nje ya ruzuku ya vyama husika.kwa maneno mengine, ni kuangalia tuu kati ya chadema, cuf na nccr-mageuzi ni chama kipi kina ruzuku kubwa zaid.

2.
UHAI WA CHAMA
Ni wazi kuwa ili ukawa wawezeekushuinda uchaguzi katika ngazi ya urais kama zilivyo ngazi za ubunge na madiwani ni lazima iweke mgombea anayetoka katika chama chenye uhai zaidi.hii ni kwasababu chama chenye uhai kina wapenz na wafuas wengi zaidi.jambo la kujiuliza ni kuwa kati ya vyama vinavyounda ukawa, ni chama kipi chenye uhai zaidi?.

(japo tunaweza kutofautiana katika vigezo vya uhai wa chama).kwa maoni yangu, uhai wa chama waweza kupimwa kwa kuangalia mikutano na shughuli za kisiasa zilizofanywa na chama husika katika kipindi cha kutoka 2010 hadi sasa.kama chama husika sio hai kisiasa, sio rahisi kutoa mgombea anayeuzika kwa watu.

3. MTANDAO WA CHAMA
Kadhalika, ni lazima mgombea husika atokkwenye chama chenye mtandao nchi nzima.hii itasaidia kuratibu shughuli za kampeni na ufuatiliaji wa kura za mgombea husika.chama husika lazima kiwe na mtandao imara na unaofanya kazi a kiuongozi nchi nzima au angalau semehmu kubwa ya nchi ili kweli kiweze kurahisisha kazi ya mgombea urais

4. UMAARUFU WA MGOMBEA HUSIKA.
Bila kujali vigezo vingine kama umri na elimu, mgombea wa urais kupitia ukawa ni lazima awe na mvuto na umaarufu kwa wapiga kura kuliko wagombea wengine wanaoweza kutoka ndani ya ukawa.

Hii ni kwasaabu siasa zetu bado hazijaama kutoka katika umaarufu wa mtu binafsi na kwenda katika sera ake na mipango ya chama husika.
kwa maoni yangu,mgombea urais kutoka ukawa atapatikana[pamja na vigezo vingine vyovyote kupitia vigezo hivyo hapo. Nawasilisha
 
Back
Top Bottom