UKAWA kusambaratika kabla ya Oktoba

UKAWA kusambaratika kabla ya Oktoba

Ukawa ni sumu ya kuiondoa madarakani serikali ya wachovu ccm.
Mchovu ni wewe usiyejua unafanya nini unapelekeshwa na watu wasio na msaada kwako. Kaa kimya vinginevyo subiri sheria ya mitandao itakayokusindikiza keko au isanga
 
Ukawa ni sumu ya kuiondoa madarakani serikali ya wachovu ccm.

Kama umetambua ukawa ni sumu! Watanzania sumu haionjwi. Tusithubutu kuonja sumu ya ukawa. Haifai kwa jamii. UKAWA NI SUMU HATARI KWA USTAWI WA TANZANIA.
 
Mkuu tabia ya kuingia jikoni kuanza kupekuwa masufuria ya matango na mboga zikiwa bado motoni, si nzuri. Waache wapishi wamalize kazi yao, wakiwa tayari,, utaalikwa mezani kula.

Kuwahi kupata ama kuchelewa kupata kuna athari gani ikiwa bado UKAWa wako ndani ya muda? Deadline ya tume ingekuwa imefungwa, ulikuwa na haki ya kuhoji.

Kama vile ccm wanavyohangaika kutafuta wadhamini na maigizo ya kuwapa watu fedha ili wajitokeze kwa wingi kwneye hizo show, waache UKAWA nao wafanye michakato yao.

Mchakato ukikamilika, utapewa jina. Usilazimishe wafuate utashi wako wakati wana taratibu na vipaumbele vyao. Walianzisha ukawa bila mchango wala ridhaa yako, hawahitaji mwongozo wako juu ya kuimarisha na kuhitimisha makubaliano yao.

Na wewe kwa kuwa huna ITIKADI YA UKAWA, huwezi kuwa mzani mzuri wa kupima mafanikio ya UKAWA. Vinginevyo unataka kulazimisha uongozi kwenye kitengo usichokijua kwa kuwa tu unataka kuongoza lakin mwisho wake ni uharibifu.

Mbona hujasifia accomplishments walizokwishafanya kwenye mgawanyo wa majimbo? Unakimbilia kupiga ramli kwa majimbo 12 yaliyosalia bila kukumbuka mgawanyo wa majimbo ni mchakato pia?

UKAWA wako makini. Hawafanyi kazi kwa kubahatisha au bora liende. Waachie wenyewe, muda ukifika watatoa taarifa.

CCm imegawanyika vipande visivyohesabika. Hujawasikia UKAWA wakiingilia kutoa mwongozo nini ccm wafanye katika hali hiyo. Vivyo hivyo UKAWA hawahitaji mwongozo kutoka CCm namna wataendesha mmipango yao.

Kaka kama kusoma huwezi basi omba usaidiwe hoja ilitolewa na mmoja wa wafuasi wa UKAWA naona unamshambulia mleta uzi betta ungeanza na source wa taarifa....ukiona jamaa toka ndani ya umoja wa ukawa anaongea jua kuna jambo....inasemekana kuna mvutano mkubwa sana ndani ya umoja wao na kuna bomu linakaribia kupasuka hakik hakuna atakayepona....oooh ukawa oooh ts all over me nasubiri kusikia tu nini kitatokea...Napongeza upande wa pili kwa kuamua kujitokeza kunadi kile walichonacho ili tuwapime with what they have...UKAWA wao wanaendelea kulumbana...
 
Wewe Kinjikitile unahangaishwa na majimbo 12 wakati bunge lijalo ni wabunge zaidi ya 600, hiyo haiwezi kuwa sababu ya watu kushindwa kuafikiana, hata wakisema ngoja haya majimbo kila mmoja awe kivyake ila huku tulikokubaliana iwe hivyo bado ni turufu ya maana kwao na sidhani kama itawapunguzia nguvu kama wakipenda kubaki na nguvu zao. Wengi tuna mihemko ya kisiasa na agenda za kiitikadi, ila hatima ya Tanzania itakayoleta maendeleo kwa wananchi wake wala si UKAWA au CCM au chama kimoja wapo, ila mifumo inayoweza kulindwa pale mshika usukani anapojisahau na kuona kama ni yeye peke yake anaweza kuwa dereva...lazima wawepo wengine wakumwambia katika hili lazima ubadili gear uweze kupanda mlima. Hivyo upinzani mimara ni maendeleo pia ya nchi yetu, upinzani dhaifu ni liache liende ndani ya yeyeote atakayekuwa amekabidhiwa mamlaka ya kutawala. Ukiangalia mkakati ya reli ya Kenya toka Mombasa hadi Kampala, Kigali, Bujumbura na Kisangani unatuondoa kwenye SOUTHERN CORRIDOH yaani Zambia, DRC maana Musumbiji na Zimbabwe wanapumulia mitaji ya SA, sisi tutakuwa na nguvu tu endapo tutakuwa na uchumi wa kwenda kote kaskazini kwenye East DRC na kusini Zambia na Lubumbashi. Masoko madogo madogo kama Rwanda na Burundi (volume ya watu milioni kama 15 twaweza kugawana wa wakenya halafu Uganda nayo tukagawana na Kenya na tukapata Southern Sudan kabla haijaingiliwa na wengine). Tusipokuwa na upinzani imara hatufiki kokote maana siasa zetu ni za kibinafsi mno na hii inaligharimu taifa kwa masuala ya maendeleo hasa kwa vijaji vijavyo maana kizazi chetu kitakuwa cha kuishia kunywa maji haya haya machafu na umeme usiokuwa na uhakika. Tuimarishe CCM ndiyo, tuimarishe pia na upinzani ili dereva yeyote aweze kushtuliwa anavyotupeleka vibaya na akasikia kwa nguvu ya kura za wabunge wasioweza kufanya maamzi wao pekee yao kama tulivyo kwa sasa hapa Tz.

Mkuu kama wameshindwa kuwa waaminifu na wanapigania majimbo 12 itakuaje tukiwakabidhi nchi si watacheza kiduku hao!!!tusipoteze muda ukiwa mwaminifu kwenye jambo dogo unakua mwaminifu pia kwenye jambo kubwa hicho ndo kipimo cha UKAWA na wamekiweka wenyewe juzi tu kusininwametwangana mpaka wakapasuana na sasa hivi wanapigana huko , na ndo sera yao wao ni kupigana tu kwani ni mara ngapi hata wabunge wao umewasikia wakisema tutazichapa tu??.tena wengine wanajiita wasomi na wataalam wa sheria wanaamini katika ngumi? Uaminifu katika hilo ni mdogo na ubinafsi unatawala sana mfano tu ni Zanzibar CUF wametoa jimbo 1 tu teh teh teh teh
 
Uwezo wako wa kufikiria ndo umeishia hapo.

Kijana emma uwezo wako wewe wa kufikiri mbona hatuuoni unaishia kuandika vitu visivyo na maana be an intellectual otherwise utakuwa unajiaibisha humu sioni huyo source kaja na fact kaeleza hali halisi sasa wewe ndugu yangu ckuelewi wakati hata kwenye secretariat ya ukawa haupo....kikubwa ni kushadadia yale unayopendezwa nayo paipo kuangalia the otherside.....wacha wataalam wachambue waeleze kile kilichopo halafu wewe tulia pembeni
 
Mkuu kama wameshindwa kuwa waaminifu na wanapigania majimbo 12 itakuaje tukiwakabidhi nchi si watacheza kiduku hao!!!tusipoteze muda ukiwa mwaminifu kwenye jambo dogo unakua mwaminifu pia kwenye jambo kubwa hicho ndo kipimo cha UKAWA na wamekiweka wenyewe juzi tu kusininwametwangana mpaka wakapasuana na sasa hivi wanapigana huko , na ndo sera yao wao ni kupigana tu kwani ni mara ngapi hata wabunge wao umewasikia wakisema tutazichapa tu??.tena wengine wanajiita wasomi na wataalam wa sheria wanaamini katika ngumi? Uaminifu katika hilo ni mdogo na ubinafsi unatawala sana mfano tu ni Zanzibar CUF wametoa jimbo 1 tu teh teh teh teh
Sidhani kama ni sahihi kusema wameshindwa kuaminiana katika majimbo kumi na mawili na hivo ni kama nchi nzima. Hata ndani ya chama tawala kuna kutoelewana na nadhani huu ni uhalisia si wa siasa tu bali wa maisha ya binadamu. Ugomvi wa siku nyingi wa kambi za wagombea urais ni dalili na kielelezo tosha kuwa siasa wakati mwingine kuna kutokukubaliana katika mtizano na hivyo mnakubali kutokukubaliana katika hilo. Kauli za kupigana tusizitumie sana maana nadhani si upinzani tu, tusisahau maneno ya Lusinde Arumeru na tukadhani ni vema kurekodi mambo maovu toka upande mmoja. Pili kauli za wapigwe tu sidhani kama zinatofauti na nitapigana maana kuamuru kupiga ni kwa kuwa una wa kuamuru kama huna utasema nitapambana mwenyewe. Mimi si mshabiki wa UKAWA wala CCM ila ni mchambuzi wa wanasiasa wetu na kuona jinsi tunavyoweza kulifikisha taifa letu bado na sema changa ukilinganisha na dola za kuanzia enzi za akina Aristotle na sisi tulipo, hivyo cha kutusaidia ni kutoa tathmini ya kweli ya kinachoendelea hata kama anayekifanya ni mzazi wako unayempenda sana. Ukiona baba yako kalewa na anaendesha gari halafu ukamshangilia ili aongeze spidi, ama humpendi baba yako ama wewe mwenyewe haumo ndani ya gari kama umo ndani ya gari basi ni ile kitu inaitwa 'mission to suicide'. Tukosoe na tujenge tanzania yetu, wakifanya vema wape haki yao wakiboronga aliyeko pembeni ndo anaweza kufanya tathmini ya kweli mara nyingi
 
Umetumwa wewe mende msaliti, ndo nyie mlotajwa hapo, ukubwa wa pua sio uwingi wa kamasi wewe! Ukubwa wa chadema isiwe kigezo kuwa na njaa na uchu kiasi kuwanyima wenzenu majimbo.
CUF ajalazimishwa Kujiunga na Ukawa Kama anaona Hawezi kujiunga na Ukawa ATOKE- lakini ninachoua mimi hizi chochoko zinatengenezwa na CCM pamoja na Mtoa Maada Jay- milionea. Wenyewe CUF wametulia Wanasubiri Ushindi wa Nguvu kutoka UKAWA
 
Kwa hiyo wabunge wa ccm na mawaziri kwenye mikutano hutumia magari ya baba yako?

Acha kurukaruka hiyo namba KUB ni gari la CHADEMA? Si kapewa na Serikali ya CCM?nyie mnasema nini unaruka na kukanyaga afu mnaburuzwa eti kuna upinzani!
 
Sidhani kama ni sahihi kusema wameshindwa kuaminiana katika majimbo kumi na mawili na hivo ni kama nchi nzima. Hata ndani ya chama tawala kuna kutoelewana na nadhani huu ni uhalisia si wa siasa tu bali wa maisha ya binadamu. Ugomvi wa siku nyingi wa kambi za wagombea urais ni dalili na kielelezo tosha kuwa siasa wakati mwingine kuna kutokukubaliana katika mtizano na hivyo mnakubali kutokukubaliana katika hilo. Kauli za kupigana tusizitumie sana maana nadhani si upinzani tu, tusisahau maneno ya Lusinde Arumeru na tukadhani ni vema kurekodi mambo maovu toka upande mmoja. Pili kauli za wapigwe tu sidhani kama zinatofauti na nitapigana maana kuamuru kupiga ni kwa kuwa una wa kuamuru kama huna utasema nitapambana mwenyewe. Mimi si mshabiki wa UKAWA wala CCM ila ni mchambuzi wa wanasiasa wetu na kuona jinsi tunavyoweza kulifikisha taifa letu bado na sema changa ukilinganisha na dola za kuanzia enzi za akina Aristotle na sisi tulipo, hivyo cha kutusaidia ni kutoa tathmini ya kweli ya kinachoendelea hata kama anayekifanya ni mzazi wako unayempenda sana. Ukiona baba yako kalewa na anaendesha gari halafu ukamshangilia ili aongeze spidi, ama humpendi baba yako ama wewe mwenyewe haumo ndani ya gari kama umo ndani ya gari basi ni ile kitu inaitwa 'mission to suicide'. Tukosoe na tujenge tanzania yetu, wakifanya vema wape haki yao wakiboronga aliyeko pembeni ndo anaweza kufanya tathmini ya kweli mara nyingi

Wewe sio UKAWA ni mchambuzi wa siasa, siasa zipi hizo acha usanii?
 
Na mtasubiri sana magamba mwaka huu ndo mwisho wenu
 
CDM wamejivika umungu mtu hawana lolote TEAM WAZALENDO
 
CDM wamejivika umungu mtu hawana lolote TEAM WAZALENDO
Umeona eeenh! Jamaa hao ni sheedah, vurugu, uongo na mambo ya ugaidi Chadema wanaongoza. Wana kazi ngumu mwezi October mwaka huu, maana hawatapata kuingia pale Ikulu.
 
Huyu atakuwa ametumwa na ACT-Wasaliti si bure!
Hivi ACT BADO Wanafanya mikutano kwa kasi ile ile. maana nimepenyezewa upenuni ni kwamba hela imekata, wale ambao walikuwa wanawapa hela saizi nao wako Busy na kutafuta wadhamini. Mtegemea cha nduguye hakika hufa maskini! Kama kweli wao ni Wazalendo waendelee na kampeni hata kwa kutumia Baiskeli au guta!
 
Na wewe sio bure lazima utakuwa umetumwa tuu maana unavyowatetea hao maboss wako wa Ukawa, hahahaha!
 
Umeona eeenh! Jamaa hao ni sheedah, vurugu, uongo na mambo ya ugaidi Chadema wanaongoza. Wana kazi ngumu mwezi October mwaka huu, maana hawatapata kuingia pale Ikulu.
ID 3 vp unabadili mwelekeo? Mmawia
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom