UKAWA katiba sio turufu kwenu

msumeno

JF-Expert Member
Aug 3, 2009
2,827
1,729
Ukawa nionavyo mimi kwa uelewa wangu finyu...swala la katiba sio turufu inayoweza kuwafikisha ikulu..watanzania si kama wakenya..ingekuwa wakenya hata haya maadamano yalogeuka kama zile ngoma zetu za uswahilini za vigodoro au vile vigoma vya uruguayi yangekua na msisimko mkubwa na for sure watawala wangesalimu amri tu kwa nguvu ya umma. Lakini wengi wetu hata ile katiba tu ya kwanza hatuijui na wengine hata rangi ya cover tu hatulijui wacha kilichomo sasa katika mazingira haya kuwambia watu wakabiliane na police sio rahisi. Ingekua vyema kwanza mkatuelewesha maana ya katiba na athari zake kwa maisha yetu..maana nimewasikia wengine wakisema hata bila ya katiba naishi. Ukiangalia sana unaona kuwa ukawa wangekaa bungeni na kufanya upinzani wa kweli bungeni kwa hoja zenye kashiko wananchi wangewaelewa na popularity ingeogezeka sana kinyume na hivi sasa. Kibaya zaidi wakati wao wakiendelea na maandamano ya vigodoro ccm wao wanalamba vichwa vijijini. Hivi ukawa mmeshindwa kuliona hili?
 
Teh teh, eti ccm wanalamba vichwa vijijini. Duh. Mkuu vijijini ni ngome ya ccm muda mrefu ingawa hakuna maji, barabara wala umeme!
 
Tanzania inabadilika na watu wanabadilika sana, ninauhakika likiboreshwa daftari la wapiga kura na ukawa wasimamie kura vizuri ccm wanaondoka mchana kweupe...hata wakilazimisha urais ila wabunge 60% itakuwa ukawa na hapo ccm indirectly inaondoka..lkn kama BUNGENI wamebaki wenyewe na kura hazija timia je huku kwa wanachi sijui itakuwaje..?
 
Kwa taarifa yako ukawa kutoka imekuwa vizuri sana ili baadae wakiingia madarakani wawe na uwezo wa kuandika katiba ya wananchi, vinginevyo mngejifanya wote walikuwepo wakati wa kutunga katiba hata kama hawakukubaliana nayo.
 
Kwa taarifa yako ukawa kutoka imekuwa vizuri sana ili baadae wakiingia madarakani wawe na uwezo wa kuandika katiba ya wananchi, vinginevyo mngejifanya wote walikuwepo wakati wa kutunga katiba hata kama hawakukubaliana nayo.

Hapo mkuu Tindo tumekusoma, hapo ukawa wamecheza haswa!
 
maandamano yamedoda,
na haya maandamano yatawapunguzia UKAWA wafuasi wao badala ya kuwaongezea. take it or not
 
badala yake wameandamana polisi tena bila kibali na bango lisemalo hatutaki katiba ya ccm
 
Back
Top Bottom