UKAWA haya lazima yajadiliwe

UKAWA haya lazima yajadiliwe

Sio wote wenye uwezo wa kuzifikia hizo Chanel, mapenzi kwenye chama yasikufanye uwe Kipofu kwa mapungufu yake.

Watu maumivu yalianza kwenye ujio wa ajabu ajabu wa Lowassa, wengi waligumia kwa ndani, wachache tulijitokeza kupinga tukaitwa kila majina mabaya.

Tatizo la Chadema ni kuwa wanaopigania Chama ni wengine na wanaokuja kufaidika ni wengine!

Na ndo maana wanasema chadema ni ya Mbowe na mkwewe na kama hujui ndo ujue, nyie wote mnapoteza muda wenu bure wenye neema wapo.
 
CHADEMA hatujifaidishi

Tunagawana majukumu

Pole sana mkuu....Tangu lini wewe umekuwa chadema?

Kwa hiyo hayo majukumu wengine ni wa kupigania chama tu, wengine ni wa kupewa viti maalum tu.

Watu wameanza kutambua na kuhoji mienendo ya Chama, wengi wanaona madudu ya Chadema hadharani.

Safari hii mtakosa hata wa kumwita msaliti maana kama ni usaliti Mbowe ndio msaliti namba moja kwa kukipoteza Mwelekeo chama.
 
Kila kitu mnachukulia upuuzi, inawezakana uwezo wa kupambanua na kuchukua constructive critisicim ni sifuri aka mnaenda kidikteta.

Na kwa nini unataka hili lizungumzwe 'kupitia chanel' wakati humu ndipo mlipofanya kampeni? Something fishy!
Hahaha humu wanataka kuwe kunajadiliwa ya ccm na ACT tu ya Chadema kwenye Chanel, hawa jamaa wa ajabu sana!
 
Kila kitu mnachukulia upuuzi, inawezakana uwezo wa kupambanua na kuchukua constructive critisicim ni sifuri aka mnaenda kidikteta.

Na kwa nini unataka hili lizungumzwe 'kupitia chanel' wakati humu ndipo mlipofanya kampeni? Something fishy!

Ulimuona kiongoz yyt wa Chadema alikuja kufanya Kampeni? hebu tuwekee link nasisi tujue
 
Majibu huwezi Kupata HAPA mkuu....Kuna sehemu na channel za kupata majibu na SIO JF

Kwa taarifa yako kwa muda mrefu tumeijadili Chadema kwa uwazi na viongozi wake kuja kujibu hoja hapa akiwemo Dr Slaa . Mtandao huu umeijenga sana Chadema pengine kuliko unavyofahamu kupitia mijadala yenye afya kama hii. Acheni ushabiki uliojaa upofu hadi hutamani kusikia mkikosolewa. Hakuna swali gumu hapa maana naona mnajifunza kujibu ki CCM siku hizi ....
 
Kwa hiyo hayo majukumu wengine ni wa kupigania chama tu, wengine ni wa kupewa viti maalum tu.

Watu wameanza kutambua na kuhoji mienendo ya Chama, wengi wanaona madudu ya Chadema hadharani.

Safari hii mtakosa hata wa kumwita msaliti maana kama ni usaliti Mbowe ndio msaliti namba moja kwa kukipoteza Mwelekeo chama.

Ukikosolewa maana yake unayo impact

Umewahi kusikia UDP inakosolewa? Do u knw why?

CHADEMA kitaendelea kukua hatua kwa hatua kama kilivyonesha tangu mwaka 1992.

Wengi tunakipigania chama....spirit yetu sio kulipana ..au kulipana fadhila

Tutaendelea kupambana kukikuza chama chetu.

Kama chama kimepoteza mwelekeo.....ya nn kukijadili....mjadili vyenye muelekeo.....Guys stop your sheit here
 
Kila kitu mnachukulia upuuzi, inawezakana uwezo wa kupambanua na kuchukua constructive critisicim ni sifuri aka mnaenda kidikteta.

Na kwa nini unataka hili lizungumzwe 'kupitia chanel' wakati humu ndipo mlipofanya kampeni? Something fishy!

You guys need to Grow up.....Hii sio Ofisi ya CHADEMA

Nendeni Ufipa mtapata majibu

Upuuzi niliusema was in respect to coment alyotoa muhusika
 
Freeland

Sawa endeleeni kupigania chama "chenu"
 
Last edited by a moderator:
Na ndo maana wanasema chadema ni ya Mbowe na mkwewe na kama hujui ndo ujue, nyie wote mnapoteza muda wenu bure wenye neema wapo.

Mkuu .....hahahahahahah.....humu Jukwaani tuko kitambo sana ...tangu mwaka 2006....Tunajuana kwa Rangi

Huyo idawa hajawahi kuwa CHADEMA

sasa sisi wana CHADEMA tuko comfortable....Nyie CCM kinawauma nini?
 
Last edited by a moderator:
Hi Ukawa ndio kitu gani? Maana kama hakuna defition labda ni mkusanyiko wa watafutaji
 
The Boss

sioni kitufe cha like brodah!
ila tukumbuke kwamba nia ya UKAWA ilikuwa ni kumpata rais kwenye huu uchaguzi uliopita so baada ya kumkosa UKAWA hauna nguvu tena.
twende mbele CDM ilijisahau sana ikajikita kwenye kumpata rais hadi imejikuta imepokoknywa majimbo na kubaki na idadi ndogo ya wabunge this time tumeiona CUF ikifanya mazuri zaid kwangu naipongeza sana CUF. NCCR nayo imebaki na MBATIA tu.

tukirudi kwenye viti maalum watu wameyarudia yale yale waliyokuawa wakiyasema juu ya CCM kwamba viti maalum wanapeana kiurafiki/kiundugu. sasa jiulize hawa UKAWA wao huwa wanahubiri nini na kutenda nini?
 
Last edited by a moderator:
The Boss

Kwanza ungehoji vipi mtu ahamie kwenye chama siku hiyo hiyo au wiki hiyo hiyo au mwezi huo huo na awe mgombea Urais, ina maana wengine wote wa kabla yake "wapumbavu"?

Ukipata jibu ya hilo, hayo mengine wala hayatakuumiza kichwa.

Ukawa mtihani....ila kweli kitu kitu kina muda...helicopter imeruka...Rais wa awamu ya tano ...Hapa Kazi tunaye na ameshaanza kujenga Tanzania iliyokuwa inabomoka...bado mtu anafikiria ukawa nao wapo!!!
 
The Boss

Kwanza ungehoji vipi mtu ahamie kwenye chama siku hiyo hiyo au wiki hiyo hiyo au mwezi huo huo na awe mgombea Urais, ina maana wengine wote wa kabla yake "wapumbavu"?

Ukipata jibu ya hilo, hayo mengine wala hayatakuumiza kichwa.

mwali wala usipate shida kabisa,
Huko nyuma tulizoea kuona mabandiko lukuki yakijadili mwenendo mzima wa upatikanaji wa wabunge wa viti maalum wa CCM, wana CDM walizoea kutusi na kuzodoa kwa kauli tata na chungu mno. kiasi kwamba unaona kabisa ni kudhalialishwa.
This time CCM wamejitahd sana kuweka wazi taratibu zao za kuwapata viti maalum na kila mtu alijionea hakuna aliyeonewa na kama wapo basi hoja zao zilishighulikiwa ipasavyo.

sasa leo hii wale waliokuwa wazodoaji na awatusi ndo kimewageukiwa, hawataki kuwa wawazi, wamepeana kindugu/kirafiki, watu wanalalamika kila uchwao na wao wako kimya.

azma yao ya kumpata rais iliposhindwa haya mengine ni kama vile hayawahusu.

upinzani kwa nchi hii utachukua muda sana kuweza kujismamia katika misingi imara na ya haki.
 
Freeland
FL brodah!
usilewe ushabiki.
CDM imekuwa ama imeanza kudidimia this time?
bunge lililopita CDM ndio ilikwa na viti vingi vya ubunge na hadi kiongozi wa kambi ya upinzani alitoka CDM.
this year CDM ilijikita katika kumtafuta rais ikasahau wabunge kbs, matokeo yake tumeona CUF ikiibuka kidedea na kuwa na viti vingi ililinganishwa na CDM. CUF walijikita zaid katika kukuza chama, na kuhakikisha wanapata idadi kubwa ya wabunge ingawa pia walikuwa anamnadi rais wa umoja
kwenye bunge hili kiongozi wa kambi ya upinzani atatoka CUF ili halina ubish na usishangae kabisa coming election kwa upofu wenu CDM ikajikuta pabaya zaid
 
Last edited by a moderator:
The Boss

Wewe usijisumbue upinzani nchi hii bado saaaana; ni ule wa kuganga njaa tu hata Lowassa keshagundua ameingia chaka usishangae kesho na keshokutwa ukaliona kundi lote likitimkia walikotoka mbona Nkumba aliligundua hili mapema? yani jamaa wako disorganised ile mbaya sijui kiongozi gani makini atakuwa tayari kukabidhi nchi kwa genge la ovyo ovyo namna hii
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin

Tunaoangalia mambo positively CHADEMA imepanda

Sijui unatumia takwimu gani kuhusu huo Uongozi wa kambi rasmi

So far kwa idadi ya wabunge CHADEMA inaongoza ikifuatiwa na CUF

Sikatai kuna majimbo tumepoteza, lakini pia tumepata mengi.

Kinachnikera ni watu kudhani eti CHADEMA imefail,....Nooooo

Kwa mazingira ya kisiasa na katiba ya Tanzania....CHADEMA dd a wonderful Job
 
Last edited by a moderator:
Mkuu .....hahahahahahah.....humu Jukwaani tuko kitambo sana ...tangu mwaka 2006....Tunajuana kwa Rangi

Huyo idawa hajawahi kuwa CHADEMA

sasa sisi wana CHADEMA tuko comfortable....Nyie CCM kinawauma nini?
Ni udhaifu kuamini kila Mwanachadema lazima atetee madudu ya Chadema.

Demokrasia ni pamoja na kukubali kukosolewa.

Ukaribisho wa Lowassa umewakatisha tamaa makamanda wengi sana na wengi wamekaa pembeni, hilo wala hulioni.

Kuna viongozi wamejiuzulu huko sumbawanga kwa sababu ya figisufigisu kwenye viti maalum hilo wala hulioni.

Mbeya wametoa malalamiko rasmi kuhusu hivyo hivyo viti maalum hilo wala hulioni.

Unakaa unajifariji eti chama kitaendelea kukua hivyo, huku unaona wazi nyufa Zikijionyesha.

Hoja ya ufisadi ndio hiyo mmeitelekeza, Maana ndio iliyokijenga na kukipa umaarufu Chadema.

Hayo yote hamyaoni sababu mnaamini na kumchukulia Mbowe kama malaika.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom