Ukabila, Ukanda na Udini ni kete ya mwisho ya CHADEMA?

Madai ya viongozi wakuu wa CHADEMA ya kudai Rais Magufuli ni mkabila na anapendelea watu wa kanda ya Ziwa na Wakristo yananikumbusha mwaka 2008 wakati wa kampeni kati ya Barack Obama na Hillary Clinton wakiwania nafasi ya kuteuliwa kuwa wagombea Urais kwa tiketi ya chama cha Democratic.

Wakati akiongea na wananchi wa eneno la Pennsylvania, Obama alinukuliwa akisema, ’’Clinton is throwing kitchen sink at me, that may make for good headlines and good television, but it doesn't make for good government’’.

Baada ya Hillary Clinton na timu yake kugundua wameshindwa kumdondosha Obama kwa kutumia hoja za uongozi na uchumi walianza kueneza kuwa Obama sio Mzaliwa wa Marekani na pia ni Mwislam kwa hivyo hana uzalendo na atawapendelea zaidi Waislam.

Mbinu ya Hillary Clinton yenya dhana ya ‘’throwing kitchen sink’’ haikuzaa matunda na matokeo yake Barack Obama aliteuliwa na chama kuwa mgombea Urais wa Marekani na hatimaye kuwa Rais wa Marekani.

Neno la msingi hapa ni ‘’Throwing kitchen sink’’.

Throwing kitchen sink kwa maana ya kiswahili cha kawaida ni kutumia mbinu chafu ili umshinde mpinzani wako baada ya kugundua kuwa umeshindwa kumshinda kwa kutumia mbinu zingine ulizodhani utamshinda.

Baada ya CHADEMA kuiuza silaha yenye hoja ya Ufisadi kwa CCM mwishoni mwa mwaka 2015 na kujikuta hawana silaha nyingine muhimu ya kisiasa, waliamua kuanza kutengeneza silaha nyingine yenye hoja za ‘’Udikteta Uchwara’’.

CHADEMA walianza kwa kupiga kelele wakisema Rais Magufuli ni ‘’Dikteta Uchwara’’na wakaanzisha operesheni walioita Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania(UKUTA) lakini wananchi wengi waliwapuuza.

Kupuuzwa katika Hoja ya Dikteta Uchwara baada ya kupiga kelele kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu kwa sasa wamekuja na silaha yenye hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini.

Hii hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini ni sawa na ‘’throwing kitchen sink’’ wakitegemea kumwangamiza kisiasa Rais Magufuli.

Mtu anayefahamu mazingira ya Tanzania atakuwa alijua mapema kuwa hoja ya ‘’Dikteta Uchwara’’ isingefanikiwa nchini kwa sababu haina soko.

Ieleweke kuwa wakati akiwasilisha takwimu za ukusanji wa maoni ya wananchi kuhusu mapendekezo ya Katiba Mpya, Jaji Warioba alibainisha kuwa katika jumla ya maoni 772,211 yaliyotolewa na wananchi 351,664 yanayohusu maeneo 47 ya kiuchumi, kisiasa na kijamii yaliyochukua nafasi tano za juu ni haya yafuatayo;
1) Haki za Binadamu(uhuru wa kuabudu na mahusiano ya ndoa),
2)Muungano (muundo na hadhi ya washirika)
3)Huduma za Jamii(Elimu na Afya),
4) Rasilimali za Taifa(Ardhi, Maliasili na Mazingira) na,
5)Vyombo vya utoaji haki(Mahakama ya kadhi na Utendaji wa Mahakama)

Suala la Utawala wa Sheria(Udikteta) linalopigiwa kelele na CHADEMA lilichukua nafasi ya tatu kutoka mwisho kati ya maeneo 47 likiwa na jumla ya maoni 43 pekee.

Ukitaka kusoma takwimu, GONGA LINK>>Jukwaa la Katiba Tanzania

Kwa mantiki hii hoja ya Udikteta Uchwara ilikosa soko kabla hata CHADEMA hawajaanza kuuza kwa wananchi.

Ukichunguza utagundua kuwa Rais Magufuli kwa sasa anapambana na vipaumbele hivyo vitano (Mimba za utotoni, Elimu, Afya, Ardhi, Maliasili na Mazingira) kama vilivyotolewa na wananchi kwenye Tume ya Jaji Warioba,

Kama ni suala la Udikteta, Mwl. Nyerere alikuwa Dikteta kweli kweli kwa sababu alifuta mfumo wa vyama vingi na Katiba haikuwa na sehemu inayohusu Tamko la Haki za Binadamu huku kila aliyejaribu kumkosoa aliishia kizuizini au kukimbia nchi. Wananchi walilazimishwa kukubali kuwa zinazodumu ni fikra pekee za Mwenyekiti wa CCM/Rais wa Tanzania.

Pamoja na Udikteta wa kweli kweli, Utawala wa Mwl. Nyerere mpaka sasa ni nembo inayong’aa Tanzania na kama ukitaka kupotea katika ulingo wa kisiasa nchini, mshambulie Mwl. Nyerere. Hii inaonyesha kuwa suala la Udikteta sio tatizo kuu nchini na ndio maana wanaopiga kelele kuhusu Udikteta hawapati ushirikiano kutoka kwa wananchi wengi.

Kushindwa vibaya kwa silaha ya Udikteta Uchwara kumewafanya CHADEMA waje na silaha ya Ukabila, Ukanda na Udini kabla ya kuanza harakati za kudai Katiba Mpya au Tume ‘’huru ya Uchaguzi’’.

CHADEMA wanafahamu hawawezi kuanza kudai Katiba Mpya au Tume ''huru ya uchaguzi'' kabla hawajamdhoofisha kisiasa Rais Magufuli na kama hawatamdhoofisha kisiasa hawatapata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi na taasisi zenye sauti kubwa nchini.

Kadri siku zinavyokwenda ndivyo ambavyo muda unakuwa sio rafiki katika harakati zao za kumdhoofisha Rais Magufuli. Ndio maana wameibuka na dhana ya ’'Throwing kitchen sink’’ kama alivyofanya Hillary Clinton kwa Baraka Obama mwaka 2008.

Sikushangaa sana kusikia tamko la Edward Lowassa na Tundu Lissu kuhusu Udini, Ukabila na Ukanda, These people are brassy and racing against time!

Hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini ni hoja ambayo ni ngumu sana nchini na yenye kuhitaji uangalifu mkubwa(delicate business) na kama ukifanya bila uangalifu mkubwa unaweza kujikuta unapoteza hata kile ulichonacho.

Vijana wa CCM walijaribu kidogo kuitumia silaha ya Ukabila kwa CHADEMA wakajikuta wanapoteza majimbo ya Kilimanjaro na Arusha. Wazee ndani ya CCM wakawapiga stop kuiuza.

Kama hukufanikiwa kusoma mjadala kuhusu Dhana ya Udini, Ukabila na Ukanda wa CHADEMA unaweza kupata hapa;
GONGA LINK>>Dhana ya Udini, Ukabila na Ukanda wa CHADEMA

CHADEMA wakaitumia silaha ya Udini kwa Rais Kikwete kwenye Uchaguzi Mkuu 2010 wakajikuta wanawapoteza Waislam wengi.
Kwa maelezo zaidi kuhusu udini wa Rais Kikweye;
GONGA LINK>>Kikwete: Waliochochea Ukabila ndio wanachochea Udini leo

Sielewi CHADEMA wamejiandaa kiasi gani kuhusu hii hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini wa Rais Magufuli na kama wakishindwa kuiuza kwa wananchi wengi, hata kile kidogo walichonacho kama mtaji wa kisiasa wanaweza kujikuta wanapoteza hasa ikichukuliwa kuwa CCM ni wazoefu kwenye masuala ya mikakati na propaganda za kisiasa.

What is denial in psychology?

Primitive Defense Mechanisms. Denial.
Denial is the refusal to accept reality or fact, acting as if a painful event, thought or feeling did not exist. It is considered one of the most primitive of the defense mechanisms because it is characteristic of early childhood development.
 
Unaweza ukawa unawaza kile ambacho kiko karibu na ubongo wako watanadi wapi ikiwa kila unalosema kuhusu magu unaitwa mchochezi haha mnajitetea kweli siasa mpaka 2020 hapo ndio unahisi watawambia watu au punguza mawazo hayo watu hata wangeamua wanavyoona inafaa bado hawataki hata ingekuwa kwa folen bado ccm mmejimilikisha nchi kwa polisi na wanajeshi umesahau oparation ukuta mkawaomba wanajeshi waanze kufagia barabarani , ile wananchi waliweza kuipokea kama uchaguzi mnagiza bunduki na mbomu ndo mjue kuwa mnalazimisha ushindi ambao mpaka leo ni siri yenu wenyewe kuwa nani anashinda kwa sababu safu za wahesabu kura yote inaandaliwa na rais wa ccm

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UKUTA wa Chadema haukuyeyuka kwa sababu unayojaribu kuonyesha hapa. Inajulikana ni viongozi wa dini na watu wengine wenye hekima na busara katika nchi hii waliingilia kati. Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) na taasisi zingine za dini walianzisha mazungumzo yenye lengo la kuondoa wingu lililosababisha kuitishwa kwa UKUTA. Ingawa inajulikana pia kwamba upande ule mwingine "ulipuuza" na ushiriki wao katika mazungumzo yale yaliyoratibiwa na CCT ulikuwa ukisuasua, lakini lakini kutokana na ushauri wa viongozi wa dini na watu wenye busara na hekima, UKAWA na Chadema waliamua kuahirisha UKUTA.

Kwenye andishi lako umerejea taarifa ya Tume ya Warioba kuonyesha kuwa wakati watu wakihojiwa juu ya mapendekezo ya Katiba Mpya suala la 'utawala wa sheria' halikuwa kipaumbele chao. Umetumia hiyo kuhitimisha kwamba hata sasa 'udikiteta uchwara' sio tatizo kwa watanzania walio wengi. Kwamba unamanisha wananchi hawaioni tofauti ya hali ya 'utawala bora' ilivyokuwa wakati Tume ya Warioba ilipokuwa ikikusanya maoni na ilivyo sasa?
Tunaweza kukubali kutokubaliana!

Naomba uniambia, hayo mazungumzo ya taasisi za dini yalifanyika wapi katika ukumbi gani?

Nini matokeo ya mazungumzo yao na yalitolewa wapi?
 
741ae2c1bc1f77d06243a7cb959bd105.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app

We una akili sana maan umeweza kutuwekea vithibitisho vya wanachama wawili ndani ya cdm wenye mahusiano,ila hukuweza kuweka wa ccm wewe kweli ni kanjanjA mjanja
 
Tunaweza kukubali kutokubaliana!

Naomba uniambia, hayo mazungumzo ya taasisi za dini yalifanyika wapi katika ukumbi gani?

Nini matokeo ya mazungumzo yao na yalitolewa wapi?
Ukipata muda wa kupitia kwa makini tovuti ya Christian Council of Tanzania (CCT) utakuta kuna mambo yanahusiana na hilo ingawa unaweza usikutane na neno UKAWA haraka.
 
msemajiUkweli.Umeleta hoja za uhakika lakina watu wanaleta vioja.
Unachosema ni kweli hoja ya ukabila udini na ukanda kwa Tanzania ya Leo haina maana Tanzania ambayo ina mchanganyiko wa mabila dini na kanda haiwezi kuwa na mashiko kwa watanzania.Miaka ya 2010 ccm walikuwa na hoja kama hizo dhidi ya cdm lakini haikuweza kuzaa matunda sidhani kama cdm wataiweza.mytake cdm kwa hoja hii watafeli tena vibaya sana

great thinker
Tusubiri muda ndio utatoa ukweli kuhusu hii hoja ya CHADEMA.

Sifahamu wamejiandaa kwa kiwango gani katika kuitetea hoja yao.
 
Mkuu, mimi nadhani CDM wana mfumo wa ubongo ambao upo tofauti na binadamu wengine. Vinginevyo wasingethubutu kuileta hoja hii kwa wananchi ikizingatiwa kuwa mwl. Nyerere aliipigia kelele sana enzi za uhai wake.
Mbaya zaidi ni kwamba, hiyo habari ya UDIKTETA, UDINI, UKABILA na UKANDA wanaiona na kuihisi CDM pekee yao. Watu wengine huku mitaani hawana habari hata kidogo na wanaendelea na shughuli zao kama jana na leo.
Kwa mtazamo wangu ni kwamba hoja hii waliyoianzisha ni sawa kabisa na kuchukua sumu ukilenga kumuulia adui yako halafu adui yako huyo anakugeuzia kibao anakunywesha mwenyewe.
Kwa mantiki hiyo utakuwa umejiua wewe mwenyewe.
BILA SHAKA HOJA ITAWAMALIZA WAO WENYEWE.

Sent using Jamii Forums mobile app

Ndio maana nimesema hii ni silaha ya mwisho kwa Rais Magufuli.

Kama wanajitambua na wangekuwa na silaha zingine wangezitumia.

Siamini kama hawajui athari za kutumia hii silaha kwa Tanzania.
 
MsemajiUkweli
Unaamuni kweli Magu katika teuzi zake haangalii udini?
Nipatie teuzi gani aliyowahi kufanya tangu akiwa waziri mpaka rais watu wa dini ile wakafika hata 10%
Hoja ya elimu ni mfu na haina mashiko
Wangekuwa wanaandika kwenye CV imani za dini zao ningekupatia idadi yao.

Kama wewe unafahamu unaweza kutoa hiyo idadi!
 
Kama Chadema silaha hao ni ukabila, basi wajibiwe hoja kwa hoja, siyo kutumia Jeshi la Polisi kuua hoja. Nilitegemea Rais Magufuli na chama chake wajibu hoja zinazoibuliwa hata kama zinaonekana za kijinga.
Umetoa mfano wa Obama alipopigwa dongo na Clinton, lakini umejijibu mwenyewe kuwa alizijibu kwa hoja.
Lakini tunaona hapa Rais wetu hataki uhuru wa maoni, watu wamkosoe. Hataki vyama vya siasa vufanye kazi kama mikutano ya hadhara, na hata ya Ndani, ila yeye na chama chake wafanye tu. Demokrasia iko wapi hapo?
Afadhali Nyerere alifuta vyama vingi mwaka 1965, sasa huyu kuvifuta hataki lakini anavizuia kufanya kazi wakati vipo kisheria.
Huu ni udhaifu mkubwa kiuongozi

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio kila hoja zinatakiwa kupata majibu.

Hoja za kipumbavu haziwezi kupata majibu kutoka kwa watu wanaojitambua kiakili na kifikra.
 
28 Reactions
Reply
Back
Top Bottom