Ukabila, Ukanda na Udini ni kete ya mwisho ya CHADEMA?

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,172
23,975
Madai ya viongozi wakuu wa CHADEMA ya kudai Rais Magufuli ni mkabila na anapendelea watu wa kanda ya Ziwa na Wakristo yananikumbusha mwaka 2008 wakati wa kampeni kati ya Barack Obama na Hillary Clinton wakiwania nafasi ya kuteuliwa kuwa wagombea Urais kwa tiketi ya chama cha Democratic.

Wakati akiongea na wananchi wa eneno la Pennsylvania, Obama alinukuliwa akisema, ’’Clinton is throwing kitchen sink at me, that may make for good headlines and good television, but it doesn't make for good government’’.

Baada ya Hillary Clinton na timu yake kugundua wameshindwa kumdondosha Obama kwa kutumia hoja za uongozi na uchumi walianza kueneza kuwa Obama sio Mzaliwa wa Marekani na pia ni Mwislam kwa hivyo hana uzalendo na atawapendelea zaidi Waislam.

Mbinu ya Hillary Clinton yenya dhana ya ‘’throwing kitchen sink’’ haikuzaa matunda na matokeo yake Barack Obama aliteuliwa na chama kuwa mgombea Urais wa Marekani na hatimaye kuwa Rais wa Marekani.

Neno la msingi hapa ni ‘’Throwing kitchen sink’’.

Throwing kitchen sink kwa maana ya kiswahili cha kawaida ni kutumia mbinu chafu ili umshinde mpinzani wako baada ya kugundua kuwa umeshindwa kumshinda kwa kutumia mbinu zingine ulizodhani utamshinda.

Baada ya CHADEMA kuiuza silaha yenye hoja ya Ufisadi kwa CCM mwishoni mwa mwaka 2015 na kujikuta hawana silaha nyingine muhimu ya kisiasa, waliamua kuanza kutengeneza silaha nyingine yenye hoja za ‘’Udikteta Uchwara’’.

CHADEMA walianza kwa kupiga kelele wakisema Rais Magufuli ni ‘’Dikteta Uchwara’’na wakaanzisha operesheni walioita Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania(UKUTA) lakini wananchi wengi waliwapuuza.

Kupuuzwa katika Hoja ya Dikteta Uchwara baada ya kupiga kelele kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu kwa sasa wamekuja na silaha yenye hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini.

Hii hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini ni sawa na ‘’throwing kitchen sink’’ wakitegemea kumwangamiza kisiasa Rais Magufuli.

Mtu anayefahamu mazingira ya Tanzania atakuwa alijua mapema kuwa hoja ya ‘’Dikteta Uchwara’’ isingefanikiwa nchini kwa sababu haina soko.

Ieleweke kuwa wakati akiwasilisha takwimu za ukusanji wa maoni ya wananchi kuhusu mapendekezo ya Katiba Mpya, Jaji Warioba alibainisha kuwa katika jumla ya maoni 772,211 yaliyotolewa na wananchi 351,664 yanayohusu maeneo 47 ya kiuchumi, kisiasa na kijamii yaliyochukua nafasi tano za juu ni haya yafuatayo;
1) Haki za Binadamu(uhuru wa kuabudu na mahusiano ya ndoa),
2)Muungano (muundo na hadhi ya washirika)
3)Huduma za Jamii(Elimu na Afya),
4) Rasilimali za Taifa(Ardhi, Maliasili na Mazingira) na,
5)Vyombo vya utoaji haki(Mahakama ya kadhi na Utendaji wa Mahakama)

Suala la Utawala wa Sheria(Udikteta) linalopigiwa kelele na CHADEMA lilichukua nafasi ya tatu kutoka mwisho kati ya maeneo 47 likiwa na jumla ya maoni 43 pekee.

Ukitaka kusoma takwimu, GONGA LINK>>Jukwaa la Katiba Tanzania

Kwa mantiki hii hoja ya Udikteta Uchwara ilikosa soko kabla hata CHADEMA hawajaanza kuuza kwa wananchi.

Ukichunguza utagundua kuwa Rais Magufuli kwa sasa anapambana na vipaumbele hivyo vitano (Mimba za utotoni, Elimu, Afya, Ardhi, Maliasili na Mazingira) kama vilivyotolewa na wananchi kwenye Tume ya Jaji Warioba,

Kama ni suala la Udikteta, Mwl. Nyerere alikuwa Dikteta kweli kweli kwa sababu alifuta mfumo wa vyama vingi na Katiba haikuwa na sehemu inayohusu Tamko la Haki za Binadamu huku kila aliyejaribu kumkosoa aliishia kizuizini au kukimbia nchi. Wananchi walilazimishwa kukubali kuwa zinazodumu ni fikra pekee za Mwenyekiti wa CCM/Rais wa Tanzania.

Pamoja na Udikteta wa kweli kweli, Utawala wa Mwl. Nyerere mpaka sasa ni nembo inayong’aa Tanzania na kama ukitaka kupotea katika ulingo wa kisiasa nchini, mshambulie Mwl. Nyerere. Hii inaonyesha kuwa suala la Udikteta sio tatizo kuu nchini na ndio maana wanaopiga kelele kuhusu Udikteta hawapati ushirikiano kutoka kwa wananchi wengi.

Kushindwa vibaya kwa silaha ya Udikteta Uchwara kumewafanya CHADEMA waje na silaha ya Ukabila, Ukanda na Udini kabla ya kuanza harakati za kudai Katiba Mpya au Tume ‘’huru ya Uchaguzi’’.

CHADEMA wanafahamu hawawezi kuanza kudai Katiba Mpya au Tume ''huru ya uchaguzi'' kabla hawajamdhoofisha kisiasa Rais Magufuli na kama hawatamdhoofisha kisiasa hawatapata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi na taasisi zenye sauti kubwa nchini.

Kadri siku zinavyokwenda ndivyo ambavyo muda unakuwa sio rafiki katika harakati zao za kumdhoofisha Rais Magufuli. Ndio maana wameibuka na dhana ya ’'Throwing kitchen sink’’ kama alivyofanya Hillary Clinton kwa Baraka Obama mwaka 2008.

Sikushangaa sana kusikia tamko la Edward Lowassa na Tundu Lissu kuhusu Udini, Ukabila na Ukanda, These people are brassy and racing against time!

Hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini ni hoja ambayo ni ngumu sana nchini na yenye kuhitaji uangalifu mkubwa(delicate business) na kama ukifanya bila uangalifu mkubwa unaweza kujikuta unapoteza hata kile ulichonacho.

Vijana wa CCM walijaribu kidogo kuitumia silaha ya Ukabila kwa CHADEMA wakajikuta wanapoteza majimbo ya Kilimanjaro na Arusha. Wazee ndani ya CCM wakawapiga stop kuiuza.

Kama hukufanikiwa kusoma mjadala kuhusu Dhana ya Udini, Ukabila na Ukanda wa CHADEMA unaweza kupata hapa;
GONGA LINK>>Dhana ya Udini, Ukabila na Ukanda wa CHADEMA

CHADEMA wakaitumia silaha ya Udini kwa Rais Kikwete kwenye Uchaguzi Mkuu 2010 wakajikuta wanawapoteza Waislam wengi.
Kwa maelezo zaidi kuhusu udini wa Rais Kikweye;
GONGA LINK>>Kikwete: Waliochochea Ukabila ndio wanachochea Udini leo

Sielewi CHADEMA wamejiandaa kiasi gani kuhusu hii hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini wa Rais Magufuli na kama wakishindwa kuiuza kwa wananchi wengi, hata kile kidogo walichonacho kama mtaji wa kisiasa wanaweza kujikuta wanapoteza hasa ikichukuliwa kuwa CCM ni wazoefu kwenye masuala ya mikakati na propaganda za kisiasa.
 
Madai ya viongozi wakuu wa CHADEMA ya kudai Rais Magufuli ni mkabila na anapendelea watu wa kanda ya Ziwa na Wakristo yananikumbusha mwaka 2008 wakati wa kampeni kati ya Barack Obama na Hillary Clinton wakiwania nafasi ya kuteuliwa kuwa wagombea Urais kwa tiketi ya chama cha Democratic.

Wakati akiongea na wananchi wa eneno la Pennsylvania, Obama alinukuliwa akisema, ’’Clinton is throwing kitchen sink at me, that may make for good headlines and good television, but it doesn't make for good government’’.

Baada ya Hillary Clinton na timu yake kugundua wameshindwa kumdondosha Obama kwa kutumia hoja za uongozi na uchumi walianza kueneza kuwa Obama sio Mzaliwa wa Marekani na pia ni Mwislam kwa hivyo hana uzalendo na atawapendelea zaidi Waislam.

Mbinu ya Hillary Clinton yenya dhana ya ‘’throwing kitchen sink’’ haikuzaa matunda na matokeo yake Barack Obama aliteuliwa na chama kuwa mgombea Urais wa Marekani na hatimaye kuwa Rais wa Marekani.

Neno la msingi hapa ni ‘’Throwing kitchen sink’’.

Throwing kitchen sink kwa maana ya kiswahili cha kawaida ni kutumia mbinu chafu ili umshinde mpinzani wako baada ya kugundua kuwa umeshindwa kumshinda kwa kutumia mbinu zingine ulizodhani utamshinda.

Baada ya CHADEMA kuiuza silaha yenye hoja ya Ufisadi kwa CCM mwishoni mwa mwaka 2015 na kujikuta hawana silaha nyingine muhimu ya kisiasa, waliamua kuanza kutengeneza silaha nyingine yenye hoja za ‘’Udikteta Uchwara’’.

CHADEMA walianza kwa kupiga kelele wakisema Rais Magufuli ni ‘’Dikteta Uchwara’’na wakaanzisha operesheni walioita Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania(UKUTA) lakini wananchi wengi waliwapuuza.

Kupuuzwa katika Hoja ya Dikteta Uchwara baada ya kupiga kelele kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu kwa sasa wamekuja na silaha yenye hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini.

Hii hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini ni sawa na ‘’throwing kitchen sink’’ wakitegemea kumwangamiza kisiasa Rais Magufuli.

Mtu anayefahamu mazingira ya Tanzania atakuwa alijua mapema kuwa hoja ya ‘’Dikteta Uchwara’’ haitafanikiwa nchini kwa sababu haina soko.

Ieleweke kuwa wakati akiwasilisha takwimu za ukusanji wa maoni ya wananchi kuhusu mapendekezo ya Katiba Mpya, Jaji Warioba alibainisha kuwa katika jumla ya maoni 772,211 yaliyotolewa na wananchi 351,664 yanayohusu maeneo 47 ya kiuchumi, kisiasa na kijamii yaliyochukua nafasi tano za juu ni haya yafuatayo;
1) Haki za Binadamu(uhuru wa kuabudu na mahusiano ya ndoa),
2)Muungano (muundo na hadhi ya washirika)
3)Huduma za Jamii(Elimu na Afya),
4) Rasilimali za Taifa(Ardhi, Maliasili na Mazingira) na,
5)Vyombo vya utoaji haki(Mahakama ya kadhi na Utendaji wa Mahakama)

Suala la Utawala wa Sheria(Udikteta) linalopigiwa kelele na CHADEMA lilichukua nafasi ya tatu kutoka mwisho kati ya maeneo 47 likiwa na jumla ya maoni 43 pekee.

Ukitaka kusoma takwimu, GONGA LINK>>Jukwaa la Katiba Tanzania

Kwa mantiki hii hoja ya Udikteta Uchwara ilikosa soko kabla hata CHADEMA hawajaanza kuuza kwa wananchi.

Kama ni suala la Udikteta, Mwl. Nyerere alikuwa Dikteta kweli kweli kwa sababu alifuta mfumo wa vyama vingi na Katiba haikuwa na sehemu inayohusu Tamko la Haki za Binadamu huku kila aliyejaribu kumkosoa aliishia kizuizini au kukimbia nchi. Wananchi walilazimishwa kukubali kuwa zinazodumu ni fikra pekee za Mwenyekiti wa CCM/Rais wa Tanzania.

Pamoja na Udikteta wa kweli kweli, Utawala wa Mwl. Nyerere mpaka sasa ni nembo inayong’aa Tanzania na kama ukitaka kupotea katika ulingo wa kisiasa nchini, mshambulie Mwl. Nyerere. Hii inaonyesha kuwa suala la Udikteta sio tatizo kuu nchini na ndio maana wanaopiga kelele kuhusu Udikteta hawapati ushirikiano kutoka kwa wananchi wengi.

Kushindwa vibaya kwa silaha ya Udikteta Uchwara kumewafanya CHADEMA waje na silaha ya Ukabila, Ukanda na Udini kabla ya kuanza harakati za kudai Katiba Mpya au Tume ‘’huru ya Uchaguzi’’.

CHADEMA wanafahamu hawawezi kuanza kudai Katiba Mpya au Tume ''huru ya uchaguzi'' kabla hawajamdhoofisha kisiasa Rais Magufuli na kama hawatamdhoofisha kisiasa hawatapata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi na taasisi zenye sauti kubwa nchini.

Kadri siku zinavyokwenda ndivyo ambavyo muda unakuwa sio rafiki katika harakati zao za kumdhoofisha Rais Magufuli. Ndio maana wameibuka na dhana ya ’'Throwing kitchen sink’’ kama alivyofanya Hillary Clinton kwa Baraka Obama mwaka 2008.

Sikushangaa sana kusikia tamko la Edward Lowassa na Tundu Lissu kuhusu Udini, Ukabila na Ukanda, These people are brassy and racing against time!

Hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini ni hoja ambayo ni ngumu sana nchini na yenye kuhitaji uangalifu mkubwa(delicate business) na kama ukifanya bila uangalifu mkubwa unaweza kujikuta unapoteza hata kile ulichonacho.

Vijana wa CCM walijaribu kidogo kuitumia silaha ya Ukabila kwa CHADEMA wakajikuta wanapoteza majimbo ya Kilimanjaro na Arusha. Wazee ndani ya CCM wakawapiga stop kuiuza.

CHADEMA wakaitumia silaha ya Udini kwa Rais Kikwete kwenye Uchaguzi Mkuu 2010 wakajikuta wanawapoteza Waislam wengi.

Sielewi CHADEMA wamejiandaa kiasi gani kuhusu hii hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini wa Rais Magufuli na kama wakishindwa kuiuza kwa wananchi wengi, hata kile kidogo walichonacho kama mtaji wa kisiasa wanaweza kujikuta wanapoteza.
We mpuuzi mmesahau nyie ndo mnaosema cdm chama cha kikabila na kikanda Leo mmpe practice ukanda na ukabila mnaelezwa ukweli mnatumia mapoliccm
 
Mkuu;
Hii hoja iko juu ya uwezo wako kifikra, jaribu kuwa msomaji tu au tafuta hoja ambazo ziko chini ya uwezo wako.

Siwezi kushangaa kama utaendelea kuweka hapa pumba zako kwa sababu hujui kama uwezo wako kifikra ni mdogo!

Samahani kama nitakukwaza kwa sababu ukweli ni mchungu!
 
Ccm ni wanafiki sana na wabaguzi, kampeni zote mmetumia swala la ukabila na udini leo limesemwa na upinzani ndo mnajua athari zake. Wajinga sana nyie
 
Hapa kuna hoja au ni rubbish ya mchumia njaa wa lumumba?
 
Ccm ni wanafiki sana na wabaguzi, kampeni zote mmetumia swala la ukabila na udini leo limesemwa na upinzani ndo mnajua athari zake. Wajinga sana nyie
Mkuu;
Tatizo lako umesoma kichwa cha mada na kumwaga pumba! Kwa pumba hizi ulizomwaga sitegemei kama una uwezo wa kusoma mada yote na kuelewa vizuri.

Kusema fulani mjinga bila wewe kujua ujinga wako ni kuonyesha jinsi usivyojitambua!
 
CDM wameshindwa hata kujifunza makosa ya CCM, CCM walijaribu kufanya propaganda ya aina hii, matokeo yake 2015 Arusha na Klm karibu yote ilienda CDM. Vivyo hivyo ndivyo itatokea kwa CCM, hao wote wanaopigwa propaganda sasa watajiona ni sehemu ya CCM na wataipiginia CCM haswaa.
 
Mada yako ni nzur ila ungeshaur nini kifanyike.Je n kweli kua serikal ya Magufuli haina ukanda ndani yake..Je unavyosema ukanda haupo Tz.Mfn n ktk Teuz za Rais alizofanya...Sijaona akizingatia balance ya Ukanda..Huenda Magu anataka atoe shukrani zake za uchaguz kwa kupata kura nying kanda ya ziwa..Ili 2020 apate cha kujinad aje awambie na ndio maana niliwapa IGP,na ndio maana nilimteua AG,na ndio maana niliwapa Naib Jaj Mkuu,Na ndio maana nilimteua Mkuu WA Majesh hapa,orodha n ndefu sana..Ya wateule kutoka kanda...
 
Kwahiyo unataka kusema hakuna mambo yaliyobadilika tubakitu kuaminiaelezo ya jaji Warioba na tume yake?
Tufanye matokeo ya tume hiyo kwa Tanzania yetu pendwa yawe ndio MSAHAFU na BIBLIA?

Wewe hujaona kama Polepole alishabadilika na kuona ukuu wa wilaya unafaa?Tafakari na urekebishe mada yako mambo yanabadilika kutokana na nyakati,mazingira,mahitaji ya jamii
 
Madai ya viongozi wakuu wa CHADEMA ya kudai Rais Magufuli ni mkabila na anapendelea watu wa kanda ya Ziwa na Wakristo yananikumbusha mwaka 2008 wakati wa kampeni kati ya Barack Obama na Hillary Clinton wakiwania nafasi ya kuteuliwa kuwa wagombea Urais kwa tiketi ya chama cha Democratic.

Wakati akiongea na wananchi wa eneno la Pennsylvania, Obama alinukuliwa akisema, ’’Clinton is throwing kitchen sink at me, that may make for good headlines and good television, but it doesn't make for good government’’.

Baada ya Hillary Clinton na timu yake kugundua wameshindwa kumdondosha Obama kwa kutumia hoja za uongozi na uchumi walianza kueneza kuwa Obama sio Mzaliwa wa Marekani na pia ni Mwislam kwa hivyo hana uzalendo na atawapendelea zaidi Waislam.

Mbinu ya Hillary Clinton yenya dhana ya ‘’throwing kitchen sink’’ haikuzaa matunda na matokeo yake Barack Obama aliteuliwa na chama kuwa mgombea Urais wa Marekani na hatimaye kuwa Rais wa Marekani.

Neno la msingi hapa ni ‘’Throwing kitchen sink’’.

Throwing kitchen sink kwa maana ya kiswahili cha kawaida ni kutumia mbinu chafu ili umshinde mpinzani wako baada ya kugundua kuwa umeshindwa kumshinda kwa kutumia mbinu zingine ulizodhani utamshinda.

Baada ya CHADEMA kuiuza silaha yenye hoja ya Ufisadi kwa CCM mwishoni mwa mwaka 2015 na kujikuta hawana silaha nyingine muhimu ya kisiasa, waliamua kuanza kutengeneza silaha nyingine yenye hoja za ‘’Udikteta Uchwara’’.

CHADEMA walianza kwa kupiga kelele wakisema Rais Magufuli ni ‘’Dikteta Uchwara’’na wakaanzisha operesheni walioita Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania(UKUTA) lakini wananchi wengi waliwapuuza.

Kupuuzwa katika Hoja ya Dikteta Uchwara baada ya kupiga kelele kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu kwa sasa wamekuja na silaha yenye hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini.

Hii hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini ni sawa na ‘’throwing kitchen sink’’ wakitegemea kumwangamiza kisiasa Rais Magufuli.

Mtu anayefahamu mazingira ya Tanzania atakuwa alijua mapema kuwa hoja ya ‘’Dikteta Uchwara’’ haitafanikiwa nchini kwa sababu haina soko.

Ieleweke kuwa wakati akiwasilisha takwimu za ukusanji wa maoni ya wananchi kuhusu mapendekezo ya Katiba Mpya, Jaji Warioba alibainisha kuwa katika jumla ya maoni 772,211 yaliyotolewa na wananchi 351,664 yanayohusu maeneo 47 ya kiuchumi, kisiasa na kijamii yaliyochukua nafasi tano za juu ni haya yafuatayo;
1) Haki za Binadamu(uhuru wa kuabudu na mahusiano ya ndoa),
2)Muungano (muundo na hadhi ya washirika)
3)Huduma za Jamii(Elimu na Afya),
4) Rasilimali za Taifa(Ardhi, Maliasili na Mazingira) na,
5)Vyombo vya utoaji haki(Mahakama ya kadhi na Utendaji wa Mahakama)

Suala la Utawala wa Sheria(Udikteta) linalopigiwa kelele na CHADEMA lilichukua nafasi ya tatu kutoka mwisho kati ya maeneo 47 likiwa na jumla ya maoni 43 pekee.

Ukitaka kusoma takwimu, GONGA LINK>>Jukwaa la Katiba Tanzania

Kwa mantiki hii hoja ya Udikteta Uchwara ilikosa soko kabla hata CHADEMA hawajaanza kuuza kwa wananchi.

Kama ni suala la Udikteta, Mwl. Nyerere alikuwa Dikteta kweli kweli kwa sababu alifuta mfumo wa vyama vingi na Katiba haikuwa na sehemu inayohusu Tamko la Haki za Binadamu huku kila aliyejaribu kumkosoa aliishia kizuizini au kukimbia nchi. Wananchi walilazimishwa kukubali kuwa zinazodumu ni fikra pekee za Mwenyekiti wa CCM/Rais wa Tanzania.

Pamoja na Udikteta wa kweli kweli, Utawala wa Mwl. Nyerere mpaka sasa ni nembo inayong’aa Tanzania na kama ukitaka kupotea katika ulingo wa kisiasa nchini, mshambulie Mwl. Nyerere. Hii inaonyesha kuwa suala la Udikteta sio tatizo kuu nchini na ndio maana wanaopiga kelele kuhusu Udikteta hawapati ushirikiano kutoka kwa wananchi wengi.

Kushindwa vibaya kwa silaha ya Udikteta Uchwara kumewafanya CHADEMA waje na silaha ya Ukabila, Ukanda na Udini kabla ya kuanza harakati za kudai Katiba Mpya au Tume ‘’huru ya Uchaguzi’’.

CHADEMA wanafahamu hawawezi kuanza kudai Katiba Mpya au Tume ''huru ya uchaguzi'' kabla hawajamdhoofisha kisiasa Rais Magufuli na kama hawatamdhoofisha kisiasa hawatapata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi na taasisi zenye sauti kubwa nchini.

Kadri siku zinavyokwenda ndivyo ambavyo muda unakuwa sio rafiki katika harakati zao za kumdhoofisha Rais Magufuli. Ndio maana wameibuka na dhana ya ’'Throwing kitchen sink’’ kama alivyofanya Hillary Clinton kwa Baraka Obama mwaka 2008.

Sikushangaa sana kusikia tamko la Edward Lowassa na Tundu Lissu kuhusu Udini, Ukabila na Ukanda, These people are brassy and racing against time!

Hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini ni hoja ambayo ni ngumu sana nchini na yenye kuhitaji uangalifu mkubwa(delicate business) na kama ukifanya bila uangalifu mkubwa unaweza kujikuta unapoteza hata kile ulichonacho.

Vijana wa CCM walijaribu kidogo kuitumia silaha ya Ukabila kwa CHADEMA wakajikuta wanapoteza majimbo ya Kilimanjaro na Arusha. Wazee ndani ya CCM wakawapiga stop kuiuza.

CHADEMA wakaitumia silaha ya Udini kwa Rais Kikwete kwenye Uchaguzi Mkuu 2010 wakajikuta wanawapoteza Waislam wengi.

Sielewi CHADEMA wamejiandaa kiasi gani kuhusu hii hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini wa Rais Magufuli na kama wakishindwa kuiuza kwa wananchi wengi, hata kile kidogo walichonacho kama mtaji wa kisiasa wanaweza kujikuta wanapoteza.
Lots of nonsense n seemingly beneficiary of dictator uchwara n nepotism

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu;
Hii hoja iko juu ya uwezo wako kifikra, jaribu kuwa msomaji tu au tafuta hoja ambazo ziko chini ya uwezo wako.

Siwezi kushangaa kama utaendelea kuweka hapa pumba zako kwa sababu hujui kama uwezo wako kifikra ni mdogo!

Samahani kama nitakukwaza kwa sababu ukweli ni mchungu!
hakuna cha juu wala nini .kwani watanzania hatuoni mnavyowakamata wapinzani hovyo na kuwatia ndani huku ccm mkiendelea na mikutano ya kisiasa? mbona hili hujalizugumzia?
 
Huu ni uwanja wa majadiliano na kwa msingi huu, hata wewe unaweza kujadili kwa kuleta thread myingine.
 
Hoja jadidi za namna hii ama tuseme wachangiaji "viona mbali" kama ninavyokuita mtoa mada, mkae kama timu ili kupambana na hoja za kichumia tumbo zinazotolewa na hawa "makinda" wanaofundishwa kuruka kabla hawajaota mbawa.
Imekuwa ukisema popote kuhusu Rais Magufuli, wao wanakimbilia kutaja ccm.
Je ni kweli mambo anayofanya Magufuli sasa hivi ni ya "mafisi" wa ccm?
Je Magufuli ana mafungamano na kulea kwa njia ya kuwatetea mibaka uchumi ya ccm?
Tujadili maendeleo ayafanyayo kuliko kuja na hoja za udini karne ya 21.
 
usikwepe swali nakuuliza viongozi wa upinzani kukamatwa wanapofanya mikutano ya ndani huku wa ccm wakiendelea unaona ni sawa? hii ndio demokrasia ?
Nimekuambia hii sio mada yake na unaweza kuanzisha mada hiyo mpya na nikachangia!

Inawezekana umesoma heading pekee halafu ukatoa komenti!
 
Back
Top Bottom