Ukabila, Ukanda na Udini ni kete ya mwisho ya CHADEMA?

Ukabila, Ukanda na Udini ni kete ya mwisho ya CHADEMA?

Madai ya viongozi wakuu wa CHADEMA ya kudai Rais Magufuli ni mkabila na anapendelea watu wa kanda ya Ziwa na Wakristo yananikumbusha mwaka 2008 wakati wa kampeni kati ya Barack Obama na Hillary Clinton wakiwania nafasi ya kuteuliwa kuwa wagombea Urais kwa tiketi ya chama cha Democratic.

Wakati akiongea na wananchi wa eneno la Pennsylvania, Obama alinukuliwa akisema, ’’Clinton is throwing kitchen sink at me, that may make for good headlines and good television, but it doesn't make for good government’’.

Baada ya Hillary Clinton na timu yake kugundua wameshindwa kumdondosha Obama kwa kutumia hoja za uongozi na uchumi walianza kueneza kuwa Obama sio Mzaliwa wa Marekani na pia ni Mwislam kwa hivyo hana uzalendo na atawapendelea zaidi Waislam.

Mbinu ya Hillary Clinton yenya dhana ya ‘’throwing kitchen sink’’ haikuzaa matunda na matokeo yake Barack Obama aliteuliwa na chama kuwa mgombea Urais wa Marekani na hatimaye kuwa Rais wa Marekani.

Neno la msingi hapa ni ‘’Throwing kitchen sink’’.

Throwing kitchen sink kwa maana ya kiswahili cha kawaida ni kutumia mbinu chafu ili umshinde mpinzani wako baada ya kugundua kuwa umeshindwa kumshinda kwa kutumia mbinu zingine ulizodhani utamshinda.

Baada ya CHADEMA kuiuza silaha yenye hoja ya Ufisadi kwa CCM mwishoni mwa mwaka 2015 na kujikuta hawana silaha nyingine muhimu ya kisiasa, waliamua kuanza kutengeneza silaha nyingine yenye hoja za ‘’Udikteta Uchwara’’.

CHADEMA walianza kwa kupiga kelele wakisema Rais Magufuli ni ‘’Dikteta Uchwara’’na wakaanzisha operesheni walioita Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania(UKUTA) lakini wananchi wengi waliwapuuza.

Kupuuzwa katika Hoja ya Dikteta Uchwara baada ya kupiga kelele kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu kwa sasa wamekuja na silaha yenye hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini.

Hii hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini ni sawa na ‘’throwing kitchen sink’’ wakitegemea kumwangamiza kisiasa Rais Magufuli.

Mtu anayefahamu mazingira ya Tanzania atakuwa alijua mapema kuwa hoja ya ‘’Dikteta Uchwara’’ isingefanikiwa nchini kwa sababu haina soko.

Ieleweke kuwa wakati akiwasilisha takwimu za ukusanji wa maoni ya wananchi kuhusu mapendekezo ya Katiba Mpya, Jaji Warioba alibainisha kuwa katika jumla ya maoni 772,211 yaliyotolewa na wananchi 351,664 yanayohusu maeneo 47 ya kiuchumi, kisiasa na kijamii yaliyochukua nafasi tano za juu ni haya yafuatayo;
1) Haki za Binadamu(uhuru wa kuabudu na mahusiano ya ndoa),
2)Muungano (muundo na hadhi ya washirika)
3)Huduma za Jamii(Elimu na Afya),
4) Rasilimali za Taifa(Ardhi, Maliasili na Mazingira) na,
5)Vyombo vya utoaji haki(Mahakama ya kadhi na Utendaji wa Mahakama)


Suala la Utawala wa Sheria(Udikteta) linalopigiwa kelele na CHADEMA lilichukua nafasi ya tatu kutoka mwisho kati ya maeneo 47 likiwa na jumla ya maoni 43 pekee.

Ukitaka kusoma takwimu, GONGA LINK>>Jukwaa la Katiba Tanzania

Kwa mantiki hii hoja ya Udikteta Uchwara ilikosa soko kabla hata CHADEMA hawajaanza kuuza kwa wananchi.

Ukichunguza utagundua kuwa Rais Magufuli kwa sasa anapambana na vipaumbele hivyo vitano (Mimba za utotoni, Elimu, Afya, Ardhi, Maliasili na Mazingira) kama vilivyotolewa na wananchi kwenye Tume ya Jaji Warioba,

Kama ni suala la Udikteta, Mwl. Nyerere alikuwa Dikteta kweli kweli kwa sababu alifuta mfumo wa vyama vingi na Katiba haikuwa na sehemu inayohusu Tamko la Haki za Binadamu huku kila aliyejaribu kumkosoa aliishia kizuizini au kukimbia nchi. Wananchi walilazimishwa kukubali kuwa zinazodumu ni fikra pekee za Mwenyekiti wa CCM/Rais wa Tanzania.

Pamoja na Udikteta wa kweli kweli, Utawala wa Mwl. Nyerere mpaka sasa ni nembo inayong’aa Tanzania na kama ukitaka kupotea katika ulingo wa kisiasa nchini, mshambulie Mwl. Nyerere. Hii inaonyesha kuwa suala la Udikteta sio tatizo kuu nchini na ndio maana wanaopiga kelele kuhusu Udikteta hawapati ushirikiano kutoka kwa wananchi wengi.

Kushindwa vibaya kwa silaha ya Udikteta Uchwara kumewafanya CHADEMA waje na silaha ya Ukabila, Ukanda na Udini kabla ya kuanza harakati za kudai Katiba Mpya au Tume ‘’huru ya Uchaguzi’’.

CHADEMA wanafahamu hawawezi kuanza kudai Katiba Mpya au Tume ''huru ya uchaguzi'' kabla hawajamdhoofisha kisiasa Rais Magufuli na kama hawatamdhoofisha kisiasa hawatapata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi na taasisi zenye sauti kubwa nchini.

Kadri siku zinavyokwenda ndivyo ambavyo muda unakuwa sio rafiki katika harakati zao za kumdhoofisha Rais Magufuli. Ndio maana wameibuka na dhana ya ’'Throwing kitchen sink’’ kama alivyofanya Hillary Clinton kwa Baraka Obama mwaka 2008.

Sikushangaa sana kusikia tamko la Edward Lowassa na Tundu Lissu kuhusu Udini, Ukabila na Ukanda, These people are brassy and racing against time!

Hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini ni hoja ambayo ni ngumu sana nchini na yenye kuhitaji uangalifu mkubwa(delicate business) na kama ukifanya bila uangalifu mkubwa unaweza kujikuta unapoteza hata kile ulichonacho.

Vijana wa CCM walijaribu kidogo kuitumia silaha ya Ukabila kwa CHADEMA wakajikuta wanapoteza majimbo ya Kilimanjaro na Arusha. Wazee ndani ya CCM wakawapiga stop kuiuza.

Kama hukufanikiwa kusoma mjadala kuhusu Dhana ya Udini, Ukabila na Ukanda wa CHADEMA unaweza kupata hapa;
GONGA LINK>>Dhana ya Udini, Ukabila na Ukanda wa CHADEMA

CHADEMA wakaitumia silaha ya Udini kwa Rais Kikwete kwenye Uchaguzi Mkuu 2010 wakajikuta wanawapoteza Waislam wengi.
Kwa maelezo zaidi kuhusu udini wa Rais Kikweye;
GONGA LINK>>Kikwete: Waliochochea Ukabila ndio wanachochea Udini leo

Sielewi CHADEMA wamejiandaa kiasi gani kuhusu hii hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini wa Rais Magufuli na kama wakishindwa kuiuza kwa wananchi wengi, hata kile kidogo walichonacho kama mtaji wa kisiasa wanaweza kujikuta wanapoteza hasa ikichukuliwa kuwa CCM ni wazoefu kwenye masuala ya mikakati na propaganda za kisiasa.
Wamejirudishia tu,wao ni wa kaskazini pia. Hata to ni mkasikazini hawafai kutuongoza ni mafisadi. Mfano orodha ya waescrow. Waepa.
 
Ccm mmebaki kutafuta wapi tuwakamate cdm. Cdm ni chama kubwa hawakamatiki kirahisi hivyo. Tapatapeni tu mwishowe mtaishia dambo.
 
Mkuu sijui kama umesoma vizuri. Huyu jamaa kakili ktk bandiko vijana wa CCM walikuwa wa kwanza kuanza jaribio la kutumia kete ya ukanda na ukabila wakazuiwa na wazee wa CCM. Soma kabla hujakosoa au kutukana km ulivyofanya. Mtu mwerevu hukubali makosa na kujifunza kwa wenzie asiyoyajua. Mleta mada ameeleta hoja ya msaada sana kwa CDM na Lissu iwapo tu wewe ni mwerevu, kwa maana ameleta na ushahi( literature review) jinsi wao CCM walivyotumia mbinu hii chafu na wakafeli. Na mimi naafikiana nae kwa maana wakati huo nami nilikuwa shabiki damu wa CDM na tulipambana sana mitandaoni kuwagalagaza CCM na hoja ya ukabila na ukanda tena pia walijaribu kutumia nao ketebya udini(ukatoliki) wa Dr.Slaa. Hayaadini kwa wanachadema wenye akili na wale wote free minded!

Huyo ni aina ya wanaJf wengi ambao wao husoma heading tu na kuanza kuandika pumba!
 
CHADEMA ni Chama cha Upinzani hakijawahi kushika dola/nchi. Wana angalia walioshika Nchi wanatawalaje? Teuzi zao za Uongozi zinabalance Diversity ya Watanzania? ( Umri, kabila, jinsia)? Vyama vya Upinzani TZ si Cdm tu: kuna Cuf, UDP, tlp, ACT Wazalendo, Hashim Rungwe, Nccr mageuzi, Nld. Mbona mmewasahau inasakamwa Cdm tu ambayo haina Serikali?

Uongozi upi unaosema kwa sababu hata kwenye vyama vya siasa kuna viongozi.
 
Mkuu MsemajiUkweli, naona watu wanajaribu kukujibu bila kuusoma walaka wako wote....
Mihemko ya kisiasa itatufanya tushindwe kujadil vzr

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu,
Usiwe na wasi wasi hao hata kwa mijeledi wataelewa tu hoja.

Kuna wengine wameelewa vizuri ila kwa sababu hawana hoja mbadala ndio maana wanakuja na vioja.

Hawawezi kupambana na ukweli na kushinda.
 
We mpuuzi mmesahau nyie ndo mnaosema cdm chama cha kikabila na kikanda Leo mmpe practice ukanda na ukabila mnaelezwa ukweli mnatumia mapoliccm

Kama huna hoja si unyamaze.Mleta mada kaja na vielelezo na mifano kwa kila hoja unakuja na maigizo mliyoyazowea.Hayawezi kuwashawishi wapiga kura malalamiko yenu,jenga hoja kupinga hoja.
 
Mada yako ni nzur ila ungeshaur nini kifanyike.Je n kweli kua serikal ya Magufuli haina ukanda ndani yake..Je unavyosema ukanda haupo Tz.Mfn n ktk Teuz za Rais alizofanya...Sijaona akizingatia balance ya Ukanda..Huenda Magu anataka atoe shukrani zake za uchaguz kwa kupata kura nying kanda ya ziwa..Ili 2020 apate cha kujinad aje awambie na ndio maana niliwapa IGP,na ndio maana nilimteua AG,na ndio maana niliwapa Naib Jaj Mkuu,Na ndio maana nilimteua Mkuu WA Majesh hapa,orodha n ndefu sana..Ya wateule kutoka kanda...

Mmeishiwa majibu.Pro.Maghembe anatoka kanda ipi,Dr.Mwandosya ni wa wapi,Waziri Mkuu Majaliwa anatokea wapi,Januari Makamba? Dr.Kigwangala? Pro.Kabudi? Dr.Ndalichako? nitamaliza ukurasa.Mnataka ampe nani mridhike? Kazi yenu kulalamika,mkikosa cha kusema mnasingizia jua,mmekuwa mbaazi nyie?

Kikwete mlimwita mdini,dhaifu,asiyetulia nchini leo ni "role model wenu'' mmesahau maatusi yote ya hovyo tuliyompa.Ridhiwani alikuwa "punching bag" ya matusi yetu,leo kama vile hayupo.Alikuwa Mbunge na bado ni Mbunge,baba yake katoka salama Ikulu matusi yote yamekwisha.Mnatafuta pa kumtukana JPM hampaoni mwazua hoja zile zile mfu.Hana huruma za Jakaya na hasubiri mbwe mbwe.Kwa mtindo huu wa malalamika daima mtaimba wimbo wa kuibiwa kura.
 
Madai ya viongozi wakuu wa CHADEMA ya kudai Rais Magufuli ni mkabila na anapendelea watu wa kanda ya Ziwa na Wakristo yananikumbusha mwaka 2008 wakati wa kampeni kati ya Barack Obama na Hillary Clinton wakiwania nafasi ya kuteuliwa kuwa wagombea Urais kwa tiketi ya chama cha Democratic.

Wakati akiongea na wananchi wa eneno la Pennsylvania, Obama alinukuliwa akisema, ’’Clinton is throwing kitchen sink at me, that may make for good headlines and good television, but it doesn't make for good government’’.

Baada ya Hillary Clinton na timu yake kugundua wameshindwa kumdondosha Obama kwa kutumia hoja za uongozi na uchumi walianza kueneza kuwa Obama sio Mzaliwa wa Marekani na pia ni Mwislam kwa hivyo hana uzalendo na atawapendelea zaidi Waislam.

Mbinu ya Hillary Clinton yenya dhana ya ‘’throwing kitchen sink’’ haikuzaa matunda na matokeo yake Barack Obama aliteuliwa na chama kuwa mgombea Urais wa Marekani na hatimaye kuwa Rais wa Marekani.

Kufananisha mwenendo wa siasa za Marekani na mwenendo wa siasa zetu, bila kuzingatia tofauti zilizopo, siyo sahihi, na kwa hiyo conclusions haziwezi kuwa sahihi. Hillary na Obama walikuwa na uwanja sawa kwa maana kwamba kila mmoja alikuwa na uhuru wa kuchagua strategy ya kutumia. tunaambiwa Obama alitumia nguvu ya Internet kwa mafanikio makubwa, wakati mama Hillary alitegemea zaidi mbinu za kizamani, na pia mumewe Bill, ambaye naye alishakuwa "old school" pamoja na sifa nyingi za "best campaigner". Kule hakuna polisi kukamata upande mmoja. Katika nchi za Afrika, kama ambavyo hata Job Ndugai aliwahi kukiri, kuwa mpinzani ni shida. utasumbuliwa, mara umekamatwa, mara umepigwa virungu, nk. hapa kwetu, ni kama mchezo wa ngumi ambapo mmoja amefungwa mikono yake na kufungwa kitambaa usoni. halafu huyo mwingine ndiyo pia Refa!

Neno la msingi hapa ni ‘’Throwing kitchen sink’’.

Throwing kitchen sink kwa maana ya kiswahili cha kawaida ni kutumia mbinu chafu ili umshinde mpinzani wako baada ya kugundua kuwa umeshindwa kumshinda kwa kutumia mbinu zingine ulizodhani utamshinda.

Hapa najiuliza, hivi ni nani hasa anaye-throw kitchen sink? Hivi CCM inapoamua kwamba CHADEMA hawawezi kufanya mikutano, kwanza ilianza ya hadhara, baadaye ikaonekana hapana, kataza hata hiyo ya ndani, wakati CCM inafanya yote bila shida yoyote. hiyo mbona ni zaidi ya kitchen sink? mimi nadhani hiyo ni TOILET SINK! Kumbuka sheria ya vyama vya siasa inaruhusu vyama vifanye kazi zake. Nakumbuka Jaji Manento, wakati huo akiwa mkuu wa tume ya haki za binadamu na utawala bora, wakati wa tukio la Mwangosi kule Iringa. Polisi ilipiga marufuku mikutano ya CHADEMA kwa kisingizio kwamba kuna zoezi la sensa linaendelea. Mwanzo CHADEMA walitii. baadaye siku za sensa zilipoongezwa kwa maana kwamba wale ambao hawajajiandikisha ndio waende, CHADEMA wakaendelea na ratiba yao, kwa kufanya mkutano wa ndani. hilo likawa nongwa, wakapigwa mabomu humo humo ukumbini. Jaji Manento aliikemea Polisi kwa kuvunja sheria ya Takwimu, ambayo inasema wazi kwamba shughuli zote za taasisi mbalimbali, serikali na watu binafsi zitaendelea kama kawaida wakati wa zoezi la sensa. hapo utaona kwamba CCM inapata sapoti ya polisi katika mchezo wa kuvutana kamba na upinzani.

Baada ya CHADEMA kuiuza silaha yenye hoja ya Ufisadi kwa CCM mwishoni mwa mwaka 2015 na kujikuta hawana silaha nyingine muhimu ya kisiasa, waliamua kuanza kutengeneza silaha nyingine yenye hoja za ‘’Udikteta Uchwara’’.
Hapa labda niseme tu kwamba wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2015, hoja kuu ilikuwa ni MABADILIKO. Hii ndiyo hoja iliyokuwa inawagusa wananchi. kwamba nchi ilikuwa na uchafu mwingi kutokana na utendaji mbovu wa serikali ya CCM, hilo halikuwa siri. na mojawapo ya uchafu ilikuwa ni ufisadi. lakini walichotaka watanzania ni ufumbuzi wa matatizo yote haya, na hapo ndipo MABADILIKO ilipoingia. CCM walilitambua hilo na ndio maana WALIIBA hoja hii na wakaanza kuimba wimbo wa MABADILIKO SAHIHI, na pia KUGUSHI kauli mbiu ya M4C kwamba ni MAGUFULI FOR CHANGE. hii inadhihirisha uchovu wa CCM kiasi kwamba hawawezi hata kuja na hoja au kauli mbiu. kweli CCM CHOKA MBAYA.

CHADEMA walianza kwa kupiga kelele wakisema Rais Magufuli ni ‘’Dikteta Uchwara’’na wakaanzisha operesheni walioita Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania(UKUTA) lakini wananchi wengi waliwapuuza.

Kwanza ijulikane kwamba ni kweli kwamba Magufuli ni Dikteta, kwa maana kwamba anajiona kwamba yeye ndiyo sheria, ana "absolute power". Tumeshuhudia akitoa kauli tata nyingi tu, mfano hii ya kuagiza kwamba hakuna mtoto wa kike mjamzito ambaye atarudi katika shule za serikali, kinyume hata na Manifesto ya CCM.

Pili, ili tujue kwamba wananchi walipuuza UKUTA, ilitakiwa serikali isiwatishe watu. watu waachwe waamue wenyewe kama wataunga mkono UKUTA au la. lakini ndio kwanza tulishuhudia mazoezi ya kijeshi nchi nzima haijawahi kutokea. Hapo JPM alitoa vitisho vikali sana, kwamba "sijaribiwi" , "wasisubiri mwezi ujao, waandamane hata kesho, waone cha mtema kuni".

Ilikuwa ni hekima tu iliyotumika, kwamba badala ya kuachia serikali ya CCM ichinje watu wake yenyewe (= uwendawazimu), bora kuepusha maafa. CCM, chini ya Dikteta Magu, iliuwa tayari kuendesha mauaji ya halaiki (Mass Murder). Hivi kama CHADEMA wangetumia haki yao ya kikatiba, wakaandamana, na Magu kwa kutaka kuonesha kwamba hajaribiwi, akafanya hayo mauaji, hii nchi ndio ingekuwa bora zaidi? haina tofauti na yule mjomba aliyembaka binti yule mpaka akafa. ni unyama wa hali ya juu sana. Wapinzani wanatakiwa kupongezwa kwa hili. ni sawa na kusema ukipigana na mwendawazimu, watu hawatajua nani mwendawazimu kati yenu.

Kupuuzwa katika Hoja ya Dikteta Uchwara baada ya kupiga kelele kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu kwa sasa wamekuja na silaha yenye hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini.

Hoja ya Dikteta Uchwara bado inanguvu sana, maana kama ingekuwa imepuuzwa, Tundu Lissu asingeng'ang'aniwa na Polisi, mpaka wanagombea "mkojo" wa Lissu. yaani wanaume wazima mnahaha kama mbwa mwenye njaa, kisa mtu mmoja tu anawasotesha. mnakuna vichwa jinsi ya kumdhiti.



Ukichunguza utagundua kuwa Rais Magufuli kwa sasa anapambana na vipaumbele hivyo vitano (Mimba za utotoni, Elimu, Afya, Ardhi, Maliasili na Mazingira) kama vilivyotolewa na wananchi kwenye Tume ya Jaji Warioba,
Mbinu ya JPM kupambana na "mimba za utotoni" ndiyo kupiga marufuku watoto wenye mimba kurudi shuleni? kwa JPM hiyo ni mbinu haswa!!

Kama ni suala la Udikteta, Mwl. Nyerere alikuwa Dikteta kweli kweli kwa sababu alifuta mfumo wa vyama vingi na Katiba haikuwa na sehemu inayohusu Tamko la Haki za Binadamu huku kila aliyejaribu kumkosoa aliishia kizuizini au kukimbia nchi. Wananchi walilazimishwa kukubali kuwa zinazodumu ni fikra pekee za Mwenyekiti wa CCM/Rais wa Tanzania.

Pamoja na Udikteta wa kweli kweli, Utawala wa Mwl. Nyerere mpaka sasa ni nembo inayong’aa Tanzania na kama ukitaka kupotea katika ulingo wa kisiasa nchini, mshambulie Mwl. Nyerere. Hii inaonyesha kuwa suala la Udikteta sio tatizo kuu nchini na ndio maana wanaopiga kelele kuhusu Udikteta hawapati ushirikiano kutoka kwa wananchi wengi.

Nyerere alikuwa anajenga taifa kutoka chini kabisa. Kumbuka wakoloni ndio waliounda Tanganyika, kwa mfumo wa koloni. hatukuwa taifa kabla ya ukoloni. kwa hiyo kazi ya kuunda taifa ilikuwa kubwa na muhimu. hata hivyo kuna sehemu Nyerere alikosea pia. na yeye mwenyewe anakiri hayo. lakini tofauti kubwa ya Magu na Nyerere ni kwenye vision, focus. Nyerere alipoona matatizo ya baada ya uhuru, alianzisha harakati za kuandaa visheni ya taifa jipya. likazaliwa Azimio la Arusha. Nyerere aliweka mfumo. hakuwa mtu wa kutoa maamuzi tu kutoka kichwani. maamuzi kama ya kuhamia Dodoma kwa kasi, na mengine mengi, hayapo kwenye mfumo. anaamua yeye kama yeye. basi. alipoanza kutekeleza Elimu Bure, alianza Januari mara baada ya kuapishwa Novemba. hapa kuwa na bajeti ya hilo, lakini akaanzisha tu.

Wananchi wana njaa, anapiga marufuku watu wasiseme wana njaa, waseme wameshiba. Nyerere hakufanya vituko kama hivyo.

Kushindwa vibaya kwa silaha ya Udikteta Uchwara kumewafanya CHADEMA waje na silaha ya Ukabila, Ukanda na Udini kabla ya kuanza harakati za kudai Katiba Mpya au Tume ‘’huru ya Uchaguzi’’.

CHADEMA wanafahamu hawawezi kuanza kudai Katiba Mpya au Tume ''huru ya uchaguzi'' kabla hawajamdhoofisha kisiasa Rais Magufuli na kama hawatamdhoofisha kisiasa hawatapata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi na taasisi zenye sauti kubwa nchini.

Kadri siku zinavyokwenda ndivyo ambavyo muda unakuwa sio rafiki katika harakati zao za kumdhoofisha Rais Magufuli. Ndio maana wameibuka na dhana ya ’'Throwing kitchen sink’’ kama alivyofanya Hillary Clinton kwa Baraka Obama mwaka 2008.
Magu atajimaliza mwenyewe. Ni kweli anafanya mengi mazuri, lakini kuna maovu anayofanya ambayo yanaweza baadaye kufuta mazuri yake. mfano namna anavyoshughulika na uchumi, na kusababisha watu wa chini kuwa na maisha magumu sana. sioni kwa vipi atabadili upepo wa hali ngumu, maana sioni uwekezaji katika kilimo, na uzalishaji kwa ujumla. Sera ya viwanda ni kelele tupu. siyo kwa kiwango kama tunavyojinasibu. Nyerere hakutangaza kujenga nchi ya viwanda, lakini angalia alijenga viwanda vingapi?

Hayo ya ukabila na ukanda kama yangekuwa siyo kweli, serikali ingetoa kauli tu na kumpuuza Tundu Lissu. lakini wapi! message sent and delivered, unaona watu wanahaha na mkojo wa Lissu.
 
Ccm ni waasisi wa sias za ukabila walianza at kafu ni waislama, wakaja cdm ni wakriato na wakanda ,aiasa hizi zitatumaliza tutakuwa kama sudan kusi
Bila mwafaka wa kitaifa kizazi cha nne frm now kitasoma no_
 
MsemajiUkweli kwa mada yako nakuunga mkono!!...
Chadema haina sera imebaki kutumia madhaifu ya mtu binafsi kujitangaza na hata ukiangalia saa hivi wamebaki kutupiana vijiti tu akianza Lissu anakuja Mdee mara Lowassa.
Ila chadema ya kipindi kile mbeya akigonga sugu, arusha anagonga lema, kati yupo Lissu, ujiji anakua Zito, Dr. Slaa anapita safisha kila sehemu yani full raha!!!..
Kipindi hicho nipo chuo mwana M4C haswa!..
Damn i miss the old moments!..
Mkuu,

Hii ndio CHADEMA mpya!
 
Back
Top Bottom