Ukabila, Ukanda na Udini ni kete ya mwisho ya CHADEMA?

Hivi hadi akina Mwita Waitara-MARA, John Heche-MARA, Ezekiel Wenje-MARA, Laurence Masha-MWANZA na nk. wanakubaliana na Tindu Lisu kuwa kanda yao inapendelewa?
 
Zama kwenye hoja ya LISU na lisu kataja teuzi za kikanda kwa majina,ungetusaidia kwa kuonyesha kuwa waliotajwa na LISU sio wa kanda ya ziwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe umetuliza akili ukaona Lissu kaja na hoja ya ukweli ambayo haiwezi kujibika?
Kama ni hivyo basi wewe bado sana. Katika kujenga hoja kwa tafiti za kisomi au kisayansi huwezi kuchukua sample space chache kutoka eneo moja au mawili ukaitumia kutoa jibu la jumla kwa eneo kubwa au maeneo tofauti mengi ukaja kufanya majumuisho kwamba maeneo haya eneo zima ukijumlisha ndio mambo/jambo lipo hivi.
Mfano: Huwezi kuchukua sample space kwa ajili ya kupima HIV kwa wagonjwa sita(6) toka mikoa 6 tofauti kwa mtindo wa mtu mmoja kila mkoa. Kisha ukapata 50% ya hao ni HIV +ve ukasema 50% ya watanzania ni waathirika wa HIV. Lissu amechukua taasisi chache sana akachagua mtu mmoja au wawili tena wa juu sio taasisi nzima kisha katoa hitimisho ajira za upendeleo kwa ukanda. Angalia baraza la mawaziri utapata picha hakuna ukanda. Angeendelea kutuwekea TISS, BOT, PCCB, TRA, Magereza, Uhamiaji, Tume ya kudhibiti Madawa ya Kulevya, TPA(Bandari), TPDC, AG, CAG, TBS, TIC, TIB, Wakuu wa wilaya na mikoa, Wakurugenzi wa wilaya, TCRA, Zimamoto, Social Funds zote na mamlaka inayo zisimamia, Secritariate ya Ajira, na taasisi zingine kibao zinazo pata viongozi wake kupitia teuzi za Raisi au mawaziri husika ambao mnasema kila kitu mawaziri wanapokea amri toka kwake. Orodha ya baraza la mawaziri ipo humu wadau wameshaiweka isome vizuri.
 
Najiuliza tu kwa ujinga wangu, kama viongozi wa CHADEMA kutoka mikoa ya kanda ya ziwa (Mara, Mwanza, Geita, Kagera, Shinyanga na Simiyu) wanaafiki kauli ya Tindu Lisu kwamba makabila yao yanapendelewa na Raisi Magufuli
 
Makamu wa Rais - Zenje
Mkuu - Lindi
Spika - Dodoma
Naibu Spika - Mbeya
Mawaziri wandamizi ;
Lukuvi - Iringa
Mwakyembe - Mbeya
Simbachaweni - Dodoma
Makamba - Tanga
Ummy Mwalimu - Tanga
Maghembe - Kilimanjaro
Kairuki - Kilimanjaro
Mpango - Kigoma
Ndalichako - Kigoma
Mwigulu - Singidag
Mbarawa - Zenji
Kabudi - Dodoma
Nape - alikuwa Lindi
Muhongo - Mara
Mahiga - Iringa
Lwenge - Iringa
Mhagama - Ruvuma
Mwinyi - Zenji

Huu ukabila na ukanda upo wapi hapo, Lissu atavuna tu chuki anayopanda 2020
Bado hujakamilisha hesabu mkuu,hii inji haina viongozi hao tu,weka teuzi zote alizofanya mkuu wa kanda ndo tuchambue vizuri
 
Wewe umetuliza akili ukaona Lissu kaja na hoja ya ukweli ambayo haiwezi kujibika?
Kama ni hivyo basi wewe bado sana. Katika kujenga hoja kwa tafiti za kisomi au kisayansi huwezi kuchukua sample space chache kutoka eneo moja au mawili ukaitumia kutoa jibu la jumla kwa eneo kubwa au maeneo tofauti mengi ukaja kufanya majumuisho kwamba maeneo haya eneo zima ukijumlisha ndio mambo/jambo lipo hivi.
Mfano: Huwezi kuchukua sample space kwa ajili ya kupima HIV kwa wagonjwa sita(6) toka mikoa 6 tofauti kwa mtindo wa mtu mmoja kila mkoa. Kisha ukapata 50% ya hao ni HIV +ve ukasema 50% ya watanzania ni waathirika wa HIV. Lissu amechukua taasisi chache sana akachagua mtu mmoja au wawili tena wa juu sio taasisi nzima kisha katoa hitimisho ajira za upendeleo kwa ukanda. Angalia baraza la mawaziri utapata picha hakuna ukanda. Angeendelea kutuwekea TISS, BOT, PCCB, TRA, Magereza, Uhamiaji, Tume ya kudhibiti Madawa ya Kulevya, TPA(Bandari), TPDC, AG, CAG, TBS, TIC, TIB, Wakuu wa wilaya na mikoa, Wakurugenzi wa wilaya, TCRA, Zimamoto, Social Funds zote na mamlaka inayo zisimamia, Secritariate ya Ajira, na taasisi zingine kibao zinazo pata viongozi wake kupitia teuzi za Raisi au mawaziri husika ambao mnasema kila kitu mawaziri wanapokea amri toka kwake. Orodha ya baraza la mawaziri ipo humu wadau wameshaiweka isome vizuri.

Mkuu hakuna shaka kuwa huyu sisonje ni mkabila,wewe baki na kumtetea ila siye tunasema ni mkabila na mdini
 
Mkuu hakuna shaka kuwa huyu sisonje ni mkabila,wewe baki na kumtetea ila siye tunasema ni mkabila na mdini

Makamu wa Rais - Zenje
Mkuu - Lindi
Spika - Dodoma
Naibu Spika - Mbeya
Mawaziri wandamizi ;
Lukuvi - Iringa
Mwakyembe - Mbeya
Simbachaweni - Dodoma
Makamba - Tanga
Ummy Mwalimu - Tanga
Maghembe - Kilimanjaro
Kairuki - Kilimanjaro
Mpango - Kigoma
Ndalichako - Kigoma
Mwigulu - Singidag
Mbarawa - Zenji
Kabudi - Dodoma
Nape - alikuwa Lindi
Muhongo - Mara
Mahiga - Iringa
Lwenge - Iringa
Mhagama - Ruvuma
Mwinyi - Zenji

Huu ukabila na ukanda upo wapi hapo, Lissu atavuna tu chuki anayopanda 2020
 
Makamu wa Rais - Zenje
Waziri Mkuu - Lindi
Spika - Dodoma
Naibu Spika - Mbeya
Mawaziri wandamizi ;
Lukuvi - Iringa
Mwakyembe - Mbeya
Simbachaweni - Dodoma
Makamba - Tanga
Ummy Mwalimu - Tanga
Maghembe - Kilimanjaro
Kairuki - Kilimanjaro
Mpango - Kigoma
Ndalichako - Kigoma
Mwigulu - Singidag
Mbarawa - Zenji
Kabudi - ???
Nape - alikuwa Lindi
Muhongo - Mara
Mahiga - Iringa
Lwenge - Iringa
Mhagama - Ruvuma
Mwinyi - Zenji

Huu ukabila na ukanda upo wapi hapo, Lissu atavuna tu chuki anayopanda 2020
kwa hoja dhaifu kama hii unadhani inatabadiri uhalisia??
 
Madai ya viongozi wakuu wa CHADEMA ya kudai Rais Magufuli ni mkabila na anapendelea watu wa kanda ya Ziwa na Wakristo yananikumbusha mwaka 2008 wakati wa kampeni kati ya Barack Obama na Hillary Clinton wakiwania nafasi ya kuteuliwa kuwa wagombea Urais kwa tiketi ya chama cha Democratic.

Wakati akiongea na wananchi wa eneno la Pennsylvania, Obama alinukuliwa akisema, ’’Clinton is throwing kitchen sink at me, that may make for good headlines and good television, but it doesn't make for good government’’.

Baada ya Hillary Clinton na timu yake kugundua wameshindwa kumdondosha Obama kwa kutumia hoja za uongozi na uchumi walianza kueneza kuwa Obama sio Mzaliwa wa Marekani na pia ni Mwislam kwa hivyo hana uzalendo na atawapendelea zaidi Waislam.

Mbinu ya Hillary Clinton yenya dhana ya ‘’throwing kitchen sink’’ haikuzaa matunda na matokeo yake Barack Obama aliteuliwa na chama kuwa mgombea Urais wa Marekani na hatimaye kuwa Rais wa Marekani.

Neno la msingi hapa ni ‘’Throwing kitchen sink’’.

Throwing kitchen sink kwa maana ya kiswahili cha kawaida ni kutumia mbinu chafu ili umshinde mpinzani wako baada ya kugundua kuwa umeshindwa kumshinda kwa kutumia mbinu zingine ulizodhani utamshinda.

Baada ya CHADEMA kuiuza silaha yenye hoja ya Ufisadi kwa CCM mwishoni mwa mwaka 2015 na kujikuta hawana silaha nyingine muhimu ya kisiasa, waliamua kuanza kutengeneza silaha nyingine yenye hoja za ‘’Udikteta Uchwara’’.

CHADEMA walianza kwa kupiga kelele wakisema Rais Magufuli ni ‘’Dikteta Uchwara’’na wakaanzisha operesheni walioita Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania(UKUTA) lakini wananchi wengi waliwapuuza.

Kupuuzwa katika Hoja ya Dikteta Uchwara baada ya kupiga kelele kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu kwa sasa wamekuja na silaha yenye hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini.

Hii hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini ni sawa na ‘’throwing kitchen sink’’ wakitegemea kumwangamiza kisiasa Rais Magufuli.

Mtu anayefahamu mazingira ya Tanzania atakuwa alijua mapema kuwa hoja ya ‘’Dikteta Uchwara’’ isingefanikiwa nchini kwa sababu haina soko.

Ieleweke kuwa wakati akiwasilisha takwimu za ukusanji wa maoni ya wananchi kuhusu mapendekezo ya Katiba Mpya, Jaji Warioba alibainisha kuwa katika jumla ya maoni 772,211 yaliyotolewa na wananchi 351,664 yanayohusu maeneo 47 ya kiuchumi, kisiasa na kijamii yaliyochukua nafasi tano za juu ni haya yafuatayo;
1) Haki za Binadamu(uhuru wa kuabudu na mahusiano ya ndoa),
2)Muungano (muundo na hadhi ya washirika)
3)Huduma za Jamii(Elimu na Afya),
4) Rasilimali za Taifa(Ardhi, Maliasili na Mazingira) na,
5)Vyombo vya utoaji haki(Mahakama ya kadhi na Utendaji wa Mahakama)


Suala la Utawala wa Sheria(Udikteta) linalopigiwa kelele na CHADEMA lilichukua nafasi ya tatu kutoka mwisho kati ya maeneo 47 likiwa na jumla ya maoni 43 pekee.

Ukitaka kusoma takwimu, GONGA LINK>>Jukwaa la Katiba Tanzania

Kwa mantiki hii hoja ya Udikteta Uchwara ilikosa soko kabla hata CHADEMA hawajaanza kuuza kwa wananchi.

Ukichunguza utagundua kuwa Rais Magufuli kwa sasa anapambana na vipaumbele hivyo vitano (Mimba za utotoni, Elimu, Afya, Ardhi, Maliasili na Mazingira) kama vilivyotolewa na wananchi kwenye Tume ya Jaji Warioba,

Kama ni suala la Udikteta, Mwl. Nyerere alikuwa Dikteta kweli kweli kwa sababu alifuta mfumo wa vyama vingi na Katiba haikuwa na sehemu inayohusu Tamko la Haki za Binadamu huku kila aliyejaribu kumkosoa aliishia kizuizini au kukimbia nchi. Wananchi walilazimishwa kukubali kuwa zinazodumu ni fikra pekee za Mwenyekiti wa CCM/Rais wa Tanzania.

Pamoja na Udikteta wa kweli kweli, Utawala wa Mwl. Nyerere mpaka sasa ni nembo inayong’aa Tanzania na kama ukitaka kupotea katika ulingo wa kisiasa nchini, mshambulie Mwl. Nyerere. Hii inaonyesha kuwa suala la Udikteta sio tatizo kuu nchini na ndio maana wanaopiga kelele kuhusu Udikteta hawapati ushirikiano kutoka kwa wananchi wengi.

Kushindwa vibaya kwa silaha ya Udikteta Uchwara kumewafanya CHADEMA waje na silaha ya Ukabila, Ukanda na Udini kabla ya kuanza harakati za kudai Katiba Mpya au Tume ‘’huru ya Uchaguzi’’.

CHADEMA wanafahamu hawawezi kuanza kudai Katiba Mpya au Tume ''huru ya uchaguzi'' kabla hawajamdhoofisha kisiasa Rais Magufuli na kama hawatamdhoofisha kisiasa hawatapata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi na taasisi zenye sauti kubwa nchini.

Kadri siku zinavyokwenda ndivyo ambavyo muda unakuwa sio rafiki katika harakati zao za kumdhoofisha Rais Magufuli. Ndio maana wameibuka na dhana ya ’'Throwing kitchen sink’’ kama alivyofanya Hillary Clinton kwa Baraka Obama mwaka 2008.

Sikushangaa sana kusikia tamko la Edward Lowassa na Tundu Lissu kuhusu Udini, Ukabila na Ukanda, These people are brassy and racing against time!

Hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini ni hoja ambayo ni ngumu sana nchini na yenye kuhitaji uangalifu mkubwa(delicate business) na kama ukifanya bila uangalifu mkubwa unaweza kujikuta unapoteza hata kile ulichonacho.

Vijana wa CCM walijaribu kidogo kuitumia silaha ya Ukabila kwa CHADEMA wakajikuta wanapoteza majimbo ya Kilimanjaro na Arusha. Wazee ndani ya CCM wakawapiga stop kuiuza.

Kama hukufanikiwa kusoma mjadala kuhusu Dhana ya Udini, Ukabila na Ukanda wa CHADEMA unaweza kupata hapa;
GONGA LINK>>Dhana ya Udini, Ukabila na Ukanda wa CHADEMA

CHADEMA wakaitumia silaha ya Udini kwa Rais Kikwete kwenye Uchaguzi Mkuu 2010 wakajikuta wanawapoteza Waislam wengi.
Kwa maelezo zaidi kuhusu udini wa Rais Kikweye;
GONGA LINK>>Kikwete: Waliochochea Ukabila ndio wanachochea Udini leo

Sielewi CHADEMA wamejiandaa kiasi gani kuhusu hii hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini wa Rais Magufuli na kama wakishindwa kuiuza kwa wananchi wengi, hata kile kidogo walichonacho kama mtaji wa kisiasa wanaweza kujikuta wanapoteza hasa ikichukuliwa kuwa CCM ni wazoefu kwenye masuala ya mikakati na propaganda za kisiasa.
Umeandika kuwa hoja ya udikiteta uchwara haipo, watu wanapokuuliza kuuliza kuhusu makatazo na kamatakamata za kisiasa zinazoendelea unasema hii siyo sehemu yake! Lakini ili kurahisisha mada ungeweka madai yako wazi kwa mifano halisi badala ya mifano ya Marekani iliyochukua nafasi kubwa. Mwisho kuwa mvumilivu bila kutumia ukali na hasira kwani kwa kufanya hivyo inaonesha kuwa huipendi Chadema, sasa kama nihivyo wewe ni bora ungewaachia wenyewe nawe ukaendelea na yako.
 
We mpuuzi mmesahau nyie ndo mnaosema cdm chama cha kikabila na kikanda Leo mmpe practice ukanda na ukabila mnaelezwa ukweli mnatumia mapoliccm
741ae2c1bc1f77d06243a7cb959bd105.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa hoja dhaifu kama hii unadhani inatabadiri uhalisia??
Makamu wa Rais - Zenje
Mkuu - Lindi
Spika - Dodoma
Naibu Spika - Mbeya
Mawaziri wandamizi ;
Lukuvi - Iringa
Mwakyembe - Mbeya
Simbachaweni - Dodoma
Makamba - Tanga
Ummy Mwalimu - Tanga
Maghembe - Kilimanjaro
Kairuki - Kilimanjaro
Mpango - Kigoma
Ndalichako - Kigoma
Mwigulu - Singidag
Mbarawa - Zenji
Kabudi - Dodoma
Nape - alikuwa Lindi
Muhongo - Mara
Mahiga - Iringa
Lwenge - Iringa
Mhagama - Ruvuma
Mwinyi - Zenji

Huu ukabila na ukanda upo wapi hapo, Lissu atavuna tu chuki anayopanda 2020
 
Back
Top Bottom