Ukabila, Ukanda na Udini ni kete ya mwisho ya CHADEMA?

Siasa za ukanda/ukabila ukishazileta hadharani moja kwa moja tunaamin hutupendi na ulikusudia kutuattack tutakuchukia upende usipende!!..
At certain times kila mtu anapenda kupewa kipaumbele hiyo ni human nature!..
Tunamsubiri Lissu kanda ya ziwa aje tueleza alimaanisha nini kwenye kauli zake!!..
Akienda Kanda ya ziwa atawaambia wananchi wasimchague Rais Magufuli kwa sababu anapendelea watu wa kanda ya ziwa!

Mtasubiri na ninaamini akienda kanda ya ziwa atakuwa na porojo zingine!
 
Chama chochote kinapokosa hoja huwa inakimbilia Udini na Ukabila. Chadema sasa ndio imekuwa kimbilio cha mafisadi na kuna mwelekeo wa wanatumika kujaribu kuharibu legacy ya Rais Magufuli.
Ninakubaliana na angalizo lako.

Sifahamu wamejiandaa kiasi gani ili kuhakikisha wanamdhoofisha Rais Magufuli kwa kutumia kigezo hiki!
 
Madai ya viongozi wakuu wa CHADEMA ya kudai Rais Magufuli ni mkabila na anapendelea watu wa kanda ya Ziwa na Wakristo yananikumbusha mwaka 2008 wakati wa kampeni kati ya Barack Obama na Hillary Clinton wakiwania nafasi ya kuteuliwa kuwa wagombea Urais kwa tiketi ya chama cha Democratic.

Wakati akiongea na wananchi wa eneno la Pennsylvania, Obama alinukuliwa akisema, ’’Clinton is throwing kitchen sink at me, that may make for good headlines and good television, but it doesn't make for good government’’.

Baada ya Hillary Clinton na timu yake kugundua wameshindwa kumdondosha Obama kwa kutumia hoja za uongozi na uchumi walianza kueneza kuwa Obama sio Mzaliwa wa Marekani na pia ni Mwislam kwa hivyo hana uzalendo na atawapendelea zaidi Waislam.

Mbinu ya Hillary Clinton yenya dhana ya ‘’throwing kitchen sink’’ haikuzaa matunda na matokeo yake Barack Obama aliteuliwa na chama kuwa mgombea Urais wa Marekani na hatimaye kuwa Rais wa Marekani.

Neno la msingi hapa ni ‘’Throwing kitchen sink’’.

Throwing kitchen sink kwa maana ya kiswahili cha kawaida ni kutumia mbinu chafu ili umshinde mpinzani wako baada ya kugundua kuwa umeshindwa kumshinda kwa kutumia mbinu zingine ulizodhani utamshinda.

Baada ya CHADEMA kuiuza silaha yenye hoja ya Ufisadi kwa CCM mwishoni mwa mwaka 2015 na kujikuta hawana silaha nyingine muhimu ya kisiasa, waliamua kuanza kutengeneza silaha nyingine yenye hoja za ‘’Udikteta Uchwara’’.

CHADEMA walianza kwa kupiga kelele wakisema Rais Magufuli ni ‘’Dikteta Uchwara’’na wakaanzisha operesheni walioita Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania(UKUTA) lakini wananchi wengi waliwapuuza.

Kupuuzwa katika Hoja ya Dikteta Uchwara baada ya kupiga kelele kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu kwa sasa wamekuja na silaha yenye hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini.

Hii hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini ni sawa na ‘’throwing kitchen sink’’ wakitegemea kumwangamiza kisiasa Rais Magufuli.

Mtu anayefahamu mazingira ya Tanzania atakuwa alijua mapema kuwa hoja ya ‘’Dikteta Uchwara’’ isingefanikiwa nchini kwa sababu haina soko.

Ieleweke kuwa wakati akiwasilisha takwimu za ukusanji wa maoni ya wananchi kuhusu mapendekezo ya Katiba Mpya, Jaji Warioba alibainisha kuwa katika jumla ya maoni 772,211 yaliyotolewa na wananchi 351,664 yanayohusu maeneo 47 ya kiuchumi, kisiasa na kijamii yaliyochukua nafasi tano za juu ni haya yafuatayo;
1) Haki za Binadamu(uhuru wa kuabudu na mahusiano ya ndoa),
2)Muungano (muundo na hadhi ya washirika)
3)Huduma za Jamii(Elimu na Afya),
4) Rasilimali za Taifa(Ardhi, Maliasili na Mazingira) na,
5)Vyombo vya utoaji haki(Mahakama ya kadhi na Utendaji wa Mahakama)


Suala la Utawala wa Sheria(Udikteta) linalopigiwa kelele na CHADEMA lilichukua nafasi ya tatu kutoka mwisho kati ya maeneo 47 likiwa na jumla ya maoni 43 pekee.

Ukitaka kusoma takwimu, GONGA LINK>>Jukwaa la Katiba Tanzania

Kwa mantiki hii hoja ya Udikteta Uchwara ilikosa soko kabla hata CHADEMA hawajaanza kuuza kwa wananchi.

Ukichunguza utagundua kuwa Rais Magufuli kwa sasa anapambana na vipaumbele hivyo vitano (Mimba za utotoni, Elimu, Afya, Ardhi, Maliasili na Mazingira) kama vilivyotolewa na wananchi kwenye Tume ya Jaji Warioba,

Kama ni suala la Udikteta, Mwl. Nyerere alikuwa Dikteta kweli kweli kwa sababu alifuta mfumo wa vyama vingi na Katiba haikuwa na sehemu inayohusu Tamko la Haki za Binadamu huku kila aliyejaribu kumkosoa aliishia kizuizini au kukimbia nchi. Wananchi walilazimishwa kukubali kuwa zinazodumu ni fikra pekee za Mwenyekiti wa CCM/Rais wa Tanzania.

Pamoja na Udikteta wa kweli kweli, Utawala wa Mwl. Nyerere mpaka sasa ni nembo inayong’aa Tanzania na kama ukitaka kupotea katika ulingo wa kisiasa nchini, mshambulie Mwl. Nyerere. Hii inaonyesha kuwa suala la Udikteta sio tatizo kuu nchini na ndio maana wanaopiga kelele kuhusu Udikteta hawapati ushirikiano kutoka kwa wananchi wengi.

Kushindwa vibaya kwa silaha ya Udikteta Uchwara kumewafanya CHADEMA waje na silaha ya Ukabila, Ukanda na Udini kabla ya kuanza harakati za kudai Katiba Mpya au Tume ‘’huru ya Uchaguzi’’.

CHADEMA wanafahamu hawawezi kuanza kudai Katiba Mpya au Tume ''huru ya uchaguzi'' kabla hawajamdhoofisha kisiasa Rais Magufuli na kama hawatamdhoofisha kisiasa hawatapata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi na taasisi zenye sauti kubwa nchini.

Kadri siku zinavyokwenda ndivyo ambavyo muda unakuwa sio rafiki katika harakati zao za kumdhoofisha Rais Magufuli. Ndio maana wameibuka na dhana ya ’'Throwing kitchen sink’’ kama alivyofanya Hillary Clinton kwa Baraka Obama mwaka 2008.

Sikushangaa sana kusikia tamko la Edward Lowassa na Tundu Lissu kuhusu Udini, Ukabila na Ukanda, These people are brassy and racing against time!

Hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini ni hoja ambayo ni ngumu sana nchini na yenye kuhitaji uangalifu mkubwa(delicate business) na kama ukifanya bila uangalifu mkubwa unaweza kujikuta unapoteza hata kile ulichonacho.

Vijana wa CCM walijaribu kidogo kuitumia silaha ya Ukabila kwa CHADEMA wakajikuta wanapoteza majimbo ya Kilimanjaro na Arusha. Wazee ndani ya CCM wakawapiga stop kuiuza.

Kama hukufanikiwa kusoma mjadala kuhusu Dhana ya Udini, Ukabila na Ukanda wa CHADEMA unaweza kupata hapa;
GONGA LINK>>Dhana ya Udini, Ukabila na Ukanda wa CHADEMA

CHADEMA wakaitumia silaha ya Udini kwa Rais Kikwete kwenye Uchaguzi Mkuu 2010 wakajikuta wanawapoteza Waislam wengi.
Kwa maelezo zaidi kuhusu udini wa Rais Kikweye;
GONGA LINK>>Kikwete: Waliochochea Ukabila ndio wanachochea Udini leo

Sielewi CHADEMA wamejiandaa kiasi gani kuhusu hii hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini wa Rais Magufuli na kama wakishindwa kuiuza kwa wananchi wengi, hata kile kidogo walichonacho kama mtaji wa kisiasa wanaweza kujikuta wanapoteza hasa ikichukuliwa kuwa CCM ni wazoefu kwenye masuala ya mikakati na propaganda za kisiasa.
Nijuavyo mie,Cdm ishakufa tyar kisiasa. Haswa inapomuachia Lissu awe msemaji mkuu wa Chama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeongea ujinga mwingi ili kujaza sever tu. Hivi ni chama gani kilichokuwa kinawaambia Watanzania kwamba Chadema ni chama cha wachaga na watu wa kaskazini? Siamini kama umesahau hilo.
Unasemaje Wananchi waliwapuuza Chadema na hoja yao ya UKUTA ikiwa serikali yetu iliingilia kati kwa gharama kubwa kuwaandaa polisi kote nchi huku msemo wa sijaribiwi ukianza kusikika? Siamini kama umesahau hili.
Kama hoja ya dikteta uchwara imepuuzwa na Watanzania, kwa nini Lissu yupo mahabusu leo? Kwa nini tusimpe nafasi Wananchi wampuuze kweli? Hofu ya watawala inatoka wapi ikiwa Wananchi wameipuuza?
Mpaka sasa Mheshimiwa Rais anajitahidi kufanya kazi ya kujiangamiza kisiasa baada ya kujiangamiza kijamii.. Huwezi kupambana na watu uliowafunga kamba na miguu, ukawawekea kitambaa cheusi machoni huku ukiwafungia ndani kisha ukajipa uhakika kuwa unakubalika.
Hii ni hulka ya viongozi waoga pekee.
Kiongozi makini na anayejiamni huwapa wenzake nafasi ya kusikilizwa kisha Wananchi huachwa waamue wenyewe... Anachokifanya sasa ni kuuza udhaifu wake kwa Wananchi, huku wengi wao wakitamani waliozuiwa waseme kwa niaba ya wengi.
Tunaweza kulikataa hili lkn kamwe hatuwezi kulificha!
Huko tuendako CCM tutakuwa na wakati mgumu sana wa kujibu hoja za Watanzania waliozibwa midomo leo!
 
Duh, mara umekuwa CCM na kuwakana makamanda wenzako? Chezeya CCM weye.
Wapiga makofi kwenye mikutano huwa hamjifichi!
Nakushauri utumie ubongo wako vizuri.
Nipo huru kifikra. Mie sio sawa na wale waliokuwa wapenyeza vi memo bungeni ili tumbili aseme... Waoga wa kupoteza mkate wao! Leo ndio wanajifanya wakali, huku wakichagua wa kuwabwekea!
 
Wapiga makofi kwenye mikutano huwa hamjifichi!
Nakushauri utumie ubongo wako vizuri.
Nipo huru kifikra. Mie sio sawa na wale waliokuwa wapenyeza vi memo bungeni ili tumbili aseme... Waoga wa kupoteza mkate wao! Leo ndio wanajifanya wakali, huku wakichagua wa kuwabwekea!
Ha ha ha, endelea kujidanganya. Sina tatizo na hilo.
 
Kama huna hoja si unyamaze.Mleta mada kaja na vielelezo na mifano kwa kila hoja unakuja na maigizo mliyoyazowea.Hayawezi kuwashawishi wapiga kura malalamiko yenu,jenga hoja kupinga hoja.
Hoja wakati nyie mnakumbatia mabinamu na wajomba kuongoza
 
Malumumba bana, mapovu yanawatoka bila kujua wanataka nini. Hapo zungumzeni saaaana lkn msikimbie siku tukiliamsha dude.

Usimuone Kobe katulia ndani ya gome lake ana lake jambo. Wanachadema msiwasikilize mafufuzela wanaotumwa kutuchokoza. Wanataka kutuchokoza tutoe vichwa nje watukate shingo.

Tutulize dude siku tukiliamusha na hadi ikulu.
 
Malumumba bana, mapovu yanawatoka bila kujua wanataka nini. Hapo zungumzeni saaaana lkn msikimbie siku tukiliamsha dude.

Usimuone Kobe katulia ndani ya gome lake ana lake jambo. Wanachadema msiwasikilize mafufuzela wanaotumwa kutuchokoza. Wanataka kutuchokoza tutoe vichwa nje watukate shingo.

Tutulize dude siku tukiliamusha na hadi ikulu.
 
Malumumba bana, mapovu yanawatoka bila kujua wanataka nini. Hapo zungumzeni saaaana lkn msikimbie siku tukiliamsha dude.

Usimuone Kobe katulia ndani ya gome lake ana lake jambo. Wanachadema msiwasikilize mafufuzela wanaotumwa kutuchokoza. Wanataka kutuchokoza tutoe vichwa nje watukate shingo.

Tutulize dude siku tukiliamusha na hadi ikulu.
Umetumia haki yako ya kikatiba kuandika pumba!
 
Umenena Kiongozi.

Na ndio maana Kipindi cha Uchaguzi uliopita Mwaka Elfu mbili na Kumi na tano (2015), humu Kelele zilikuwa nyingi sana lakini baada ya Matokeo palikuwa Kimya sana, ilichukua takribani kama Wiki Tatu hivi Wadau kuanza kurudi na kuanza kuchangia Mada mbali mbali.

Ukweli ni kwamba Mitandaoni kuna wapiga Kelele, lakini inapokuja kwenye Utendaji/Utekelezaji ogopa sana wale Watu ambao hawasikiki
Mkuu;
Mitandao huwa inadanganya wengi sana!

Siasa ni zaidi ya kupiga kelele kwenye mitandao.

Ninakuhakikisha kama itaendelea kuwa kama ilivyo kwa sasa, vyama vya upinzani vitapoteza majimbo mengi sana kwenye uchaguzi 2020.
 
Yan huyu mtoa mada sijui anayejiita Hashtag# MSEMA UWONGO [HASHTAG]#lingekuwa[/HASHTAG] n grup la watsup wanajamvi tungeshamwambia Group Admin akutoe kwa hoja zako za nguvu ya soda kama hizi

Sent using Jamii Forums mobile app
Siwezi kushangaa kusikia wewe ni kati ya wale wanataka uhuru wa ''kujieleza'' lakini cha kushangaza hutaki wengine wajieleze.
 
Back
Top Bottom