Ukabila, Ukanda na Udini ni kete ya mwisho ya CHADEMA?

Ukabila, Ukanda na Udini ni kete ya mwisho ya CHADEMA?

Mkuu;
Hii hoja iko juu ya uwezo wako kifikra, jaribu kuwa msomaji tu au tafuta hoja ambazo ziko chini ya uwezo wako.

Siwezi kushangaa kama utaendelea kuweka hapa pumba zako kwa sababu hujui kama uwezo wako kifikra ni mdogo!

Samahani kama nitakukwaza kwa sababu ukweli ni mchungu!
Hoja kwa hoja. Usipojibu hoja zake kwa hoja, basi huna hoja wewe.
 
Kwahiyo unataka kusema hakuna mambo yaliyobadilika tubakitu kuaminiaelezo ya jaji Warioba na tume yake?
Tufanye matokeo ya tume hiyo kwa Tanzania yetu pendwa yawe ndio MSAHAFU na BIBLIA?

Wewe hujaona kama Polepole alishabadilika na kuona ukuu wa wilaya unafaa?Tafakari na urekebishe mada yako mambo yanabadilika kutokana na nyakati,mazingira,mahitaji ya jamii
Mkuu,
Kama mambo yangekuwa yamebadilika ninaamini UKUTA wa CHADEMA usingeyeyuka kwa haraka kiasi hicho.
 
Madai ya viongozi wakuu wa CHADEMA ya kudai Rais Magufuli ni mkabila na anapendelea watu wa kanda ya Ziwa na Wakristo yananikumbusha mwaka 2008 wakati wa kampeni kati ya Barack Obama na Hillary Clinton wakiwania nafasi ya kuteuliwa kuwa wagombea Urais kwa tiketi ya chama cha Democratic.

Wakati akiongea na wananchi wa eneno la Pennsylvania, Obama alinukuliwa akisema, ’’Clinton is throwing kitchen sink at me, that may make for good headlines and good television, but it doesn't make for good government’’.

Baada ya Hillary Clinton na timu yake kugundua wameshindwa kumdondosha Obama kwa kutumia hoja za uongozi na uchumi walianza kueneza kuwa Obama sio Mzaliwa wa Marekani na pia ni Mwislam kwa hivyo hana uzalendo na atawapendelea zaidi Waislam.

Mbinu ya Hillary Clinton yenya dhana ya ‘’throwing kitchen sink’’ haikuzaa matunda na matokeo yake Barack Obama aliteuliwa na chama kuwa mgombea Urais wa Marekani na hatimaye kuwa Rais wa Marekani.

Neno la msingi hapa ni ‘’Throwing kitchen sink’’.

Throwing kitchen sink kwa maana ya kiswahili cha kawaida ni kutumia mbinu chafu ili umshinde mpinzani wako baada ya kugundua kuwa umeshindwa kumshinda kwa kutumia mbinu zingine ulizodhani utamshinda.

Baada ya CHADEMA kuiuza silaha yenye hoja ya Ufisadi kwa CCM mwishoni mwa mwaka 2015 na kujikuta hawana silaha nyingine muhimu ya kisiasa, waliamua kuanza kutengeneza silaha nyingine yenye hoja za ‘’Udikteta Uchwara’’.

CHADEMA walianza kwa kupiga kelele wakisema Rais Magufuli ni ‘’Dikteta Uchwara’’na wakaanzisha operesheni walioita Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania(UKUTA) lakini wananchi wengi waliwapuuza.

Kupuuzwa katika Hoja ya Dikteta Uchwara baada ya kupiga kelele kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu kwa sasa wamekuja na silaha yenye hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini.

Hii hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini ni sawa na ‘’throwing kitchen sink’’ wakitegemea kumwangamiza kisiasa Rais Magufuli.

Mtu anayefahamu mazingira ya Tanzania atakuwa alijua mapema kuwa hoja ya ‘’Dikteta Uchwara’’ isingefanikiwa nchini kwa sababu haina soko.

Ieleweke kuwa wakati akiwasilisha takwimu za ukusanji wa maoni ya wananchi kuhusu mapendekezo ya Katiba Mpya, Jaji Warioba alibainisha kuwa katika jumla ya maoni 772,211 yaliyotolewa na wananchi 351,664 yanayohusu maeneo 47 ya kiuchumi, kisiasa na kijamii yaliyochukua nafasi tano za juu ni haya yafuatayo;
1) Haki za Binadamu(uhuru wa kuabudu na mahusiano ya ndoa),
2)Muungano (muundo na hadhi ya washirika)
3)Huduma za Jamii(Elimu na Afya),
4) Rasilimali za Taifa(Ardhi, Maliasili na Mazingira) na,
5)Vyombo vya utoaji haki(Mahakama ya kadhi na Utendaji wa Mahakama)


Suala la Utawala wa Sheria(Udikteta) linalopigiwa kelele na CHADEMA lilichukua nafasi ya tatu kutoka mwisho kati ya maeneo 47 likiwa na jumla ya maoni 43 pekee.

Ukitaka kusoma takwimu, GONGA LINK>>Jukwaa la Katiba Tanzania

Kwa mantiki hii hoja ya Udikteta Uchwara ilikosa soko kabla hata CHADEMA hawajaanza kuuza kwa wananchi.

Ukichunguza utagundua kuwa Rais Magufuli kwa sasa anapambana na vipaumbele hivyo vitano (Mimba za utotoni, Elimu, Afya, Ardhi, Maliasili na Mazingira) kama vilivyotolewa na wananchi kwenye Tume ya Jaji Warioba,

Kama ni suala la Udikteta, Mwl. Nyerere alikuwa Dikteta kweli kweli kwa sababu alifuta mfumo wa vyama vingi na Katiba haikuwa na sehemu inayohusu Tamko la Haki za Binadamu huku kila aliyejaribu kumkosoa aliishia kizuizini au kukimbia nchi. Wananchi walilazimishwa kukubali kuwa zinazodumu ni fikra pekee za Mwenyekiti wa CCM/Rais wa Tanzania.

Pamoja na Udikteta wa kweli kweli, Utawala wa Mwl. Nyerere mpaka sasa ni nembo inayong’aa Tanzania na kama ukitaka kupotea katika ulingo wa kisiasa nchini, mshambulie Mwl. Nyerere. Hii inaonyesha kuwa suala la Udikteta sio tatizo kuu nchini na ndio maana wanaopiga kelele kuhusu Udikteta hawapati ushirikiano kutoka kwa wananchi wengi.

Kushindwa vibaya kwa silaha ya Udikteta Uchwara kumewafanya CHADEMA waje na silaha ya Ukabila, Ukanda na Udini kabla ya kuanza harakati za kudai Katiba Mpya au Tume ‘’huru ya Uchaguzi’’.

CHADEMA wanafahamu hawawezi kuanza kudai Katiba Mpya au Tume ''huru ya uchaguzi'' kabla hawajamdhoofisha kisiasa Rais Magufuli na kama hawatamdhoofisha kisiasa hawatapata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi na taasisi zenye sauti kubwa nchini.

Kadri siku zinavyokwenda ndivyo ambavyo muda unakuwa sio rafiki katika harakati zao za kumdhoofisha Rais Magufuli. Ndio maana wameibuka na dhana ya ’'Throwing kitchen sink’’ kama alivyofanya Hillary Clinton kwa Baraka Obama mwaka 2008.

Sikushangaa sana kusikia tamko la Edward Lowassa na Tundu Lissu kuhusu Udini, Ukabila na Ukanda, These people are brassy and racing against time!

Hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini ni hoja ambayo ni ngumu sana nchini na yenye kuhitaji uangalifu mkubwa(delicate business) na kama ukifanya bila uangalifu mkubwa unaweza kujikuta unapoteza hata kile ulichonacho.

Vijana wa CCM walijaribu kidogo kuitumia silaha ya Ukabila kwa CHADEMA wakajikuta wanapoteza majimbo ya Kilimanjaro na Arusha. Wazee ndani ya CCM wakawapiga stop kuiuza.

Kama hukufanikiwa kusoma mjadala kuhusu Dhana ya Udini, Ukabila na Ukanda wa CHADEMA unaweza kupata hapa;
GONGA LINK>>Dhana ya Udini, Ukabila na Ukanda wa CHADEMA

CHADEMA wakaitumia silaha ya Udini kwa Rais Kikwete kwenye Uchaguzi Mkuu 2010 wakajikuta wanawapoteza Waislam wengi.
Kwa maelezo zaidi kuhusu udini wa Rais Kikweye;
GONGA LINK>>Kikwete: Waliochochea Ukabila ndio wanachochea Udini leo

Sielewi CHADEMA wamejiandaa kiasi gani kuhusu hii hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini wa Rais Magufuli na kama wakishindwa kuiuza kwa wananchi wengi, hata kile kidogo walichonacho kama mtaji wa kisiasa wanaweza kujikuta wanapoteza hasa ikichukuliwa kuwa CCM ni wazoefu kwenye masuala ya propaganda za kisiasa.
chadema wamekuwa wafa maji hawaishi kutapatapa magufuli kawanyosha wameishiwa hoja
 
Kwa hiyo kuwa ndugu wa Magu ndio hana haki ya kufanya kazi serikalini au tatizo ni nini hapa ?
Makamu wa Rais- Zenji
Waziri Mkuu - Lindi
Spika - Dodoma
Naibu Spika- Mbeya
Mawaziri wandamizi
Lukuvi- Iringa
Mwakyembe- Mbeya
Mhagama- Ruvuma
Simbachawene- Dodoma
Makamba- Tanga
Ummy mwalimu- Tanga
Mpango - Kigoma
Ndalichako- Kigoma
Muhongo- alikuwa kutoka Mara
Nape - alikuwa kutoka Lindi
Kabudi - ???

Huo upendeleo upo wapi hapo ?
Wewe ng'ang'ana na hiyo orodha ukifikiri utaweza kuitumia kufifisha hoja ya Lissu. Tafuta clip ya pc ya Lissu uisikilize upyandio ulete tena utetezi wako!
 
Mkuu,
Kama mambo yangekuwa yamebadilika ninaamini UKUTA wa CHADEMA usingeyeyuka kwa haraka kiasi hicho.
UKUTA wa Chadema haukuyeyuka kwa sababu unayojaribu kuonyesha hapa. Inajulikana ni viongozi wa dini na watu wengine wenye hekima na busara katika nchi hii waliingilia kati. Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) na taasisi zingine za dini walianzisha mazungumzo yenye lengo la kuondoa wingu lililosababisha kuitishwa kwa UKUTA. Ingawa inajulikana pia kwamba upande ule mwingine "ulipuuza" na ushiriki wao katika mazungumzo yale yaliyoratibiwa na CCT ulikuwa ukisuasua, lakini lakini kutokana na ushauri wa viongozi wa dini na watu wenye busara na hekima, UKAWA na Chadema waliamua kuahirisha UKUTA.

Kwenye andishi lako umerejea taarifa ya Tume ya Warioba kuonyesha kuwa wakati watu wakihojiwa juu ya mapendekezo ya Katiba Mpya suala la 'utawala wa sheria' halikuwa kipaumbele chao. Umetumia hiyo kuhitimisha kwamba hata sasa 'udikiteta uchwara' sio tatizo kwa watanzania walio wengi. Kwamba unamanisha wananchi hawaioni tofauti ya hali ya 'utawala bora' ilivyokuwa wakati Tume ya Warioba ilipokuwa ikikusanya maoni na ilivyo sasa?
 
Hivi ni uongo kweli alichosema TL au na kiukweli mpaka sasa kuna ukabila au hakuna ukabila kwenye gvt yetu, taifa letu linapita katika kipindi kibaya sana maana tumepata vyongozi wanaochukulia nchi kama sehemu ya mtaji wa maisha yao na wakiamini kuwa wao ndyo waumini wa nchi hii tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo kuwa ndugu wa Magu ndio hana haki ya kufanya kazi serikalini au tatizo ni nini hapa ?
Makamu wa Rais- Zenji
Waziri Mkuu - Lindi
Spika - Dodoma
Naibu Spika- Mbeya
Mawaziri wandamizi
Lukuvi- Iringa
Mwakyembe- Mbeya
Mhagama- Ruvuma
Simbachawene- Dodoma
Makamba- Tanga
Ummy mwalimu- Tanga
Mpango - Kigoma
Ndalichako- Kigoma
Muhongo- alikuwa kutoka Mara
Nape - alikuwa kutoka Lindi
Kabudi - ???

Huo upendeleo upo wapi hapo ?
Mkuu unataka kutuaminisha hakuna mwananchi kutoka mikoa ya Kilimanjaro au Arusha anaeweza kuteuliwa kwenye mojawapo ya nafasi nyeti?
 
Mkuu unataka kutuaminisha hakuna mwananchi kutoka mikoa ya Kilimanjaro au Arusha anaeweza kuteuliwa kwenye mojawapo ya nafasi nyeti?
Kama wabunge wengi wa Klm na Arusha wanatoka upinzani ulitaka wachaguliwe vipi, unatambau kuwa Klm ndio ilikuwa na mawaziri wengi kipindi cha JK, unatambau Klm na Arusha ndio wanaongoza kwa kutoa mawaziri wakuu na mawaziri wa fedha, mbona wilaya moja ya Monduli imeshatoa mawaziri wakuu wawili ila hakuna tatizo kwa hilo.

Nyie watu mnafikiria kikabila sana, ndio maana mnafikiria kila mtu anawaza hivyo. Nitajie hata mbunge mmoja tu wa CCM kutoka Klm au Arusha mwenye hadhi ya uwaziri na ametoswa.
BTW, Maghembe na Kairuki pia ni wa Klm hao.
 
Mkuu;
Hii hoja iko juu ya uwezo wako kifikra, jaribu kuwa msomaji tu au tafuta hoja ambazo ziko chini ya uwezo wako.

Siwezi kushangaa kama utaendelea kuweka hapa pumba zako kwa sababu hujui kama uwezo wako kifikra ni mdogo!

Samahani kama nitakukwaza kwa sababu ukweli ni mchungu!

We no mjinga tu ukielimishwa utaelimika ila bado mjinga
 
Hoja huwa hazitolewi kutafuta soko Mara zote hoja nzito huwa hazina soko , Kwa mfano hoja ya Escrow haikuwa na soko leo ni sifa kwahiyo hii uliyoandika inaweza kuwa sifa ya wengine baadaye! Na wakati huo utasema kama unavyosema ya ufisadi ambayo wakati huo haikuwa na soko na hata wananchi wakuchagua wenye hoja hiyo!
 
CCM v/s CHADEMA.

Watu wanaona yanayoendelea acheni kutumia nguvu kubwa kujisafisha.
 
msemajiUkweli.Umeleta hoja za uhakika lakina watu wanaleta vioja.
Unachosema ni kweli hoja ya ukabila udini na ukanda kwa Tanzania ya Leo haina maana Tanzania ambayo ina mchanganyiko wa mabila dini na kanda haiwezi kuwa na mashiko kwa watanzania.Miaka ya 2010 ccm walikuwa na hoja kama hizo dhidi ya cdm lakini haikuweza kuzaa matunda sidhani kama cdm wataiweza.mytake cdm kwa hoja hii watafeli tena vibaya sana

great thinker

 
Back
Top Bottom