Ukabila, Ukanda na Udini ni kete ya mwisho ya CHADEMA?

Ukabila, Ukanda na Udini ni kete ya mwisho ya CHADEMA?

Hoja jadidi za namna hii ama tuseme wachangiaji "viona mbali" kama ninavyokuita mtoa mada, mkae kama timu ili kupambana na hoja za kichumia tumbo zinazotolewa na hawa "makinda" wanaofundishwa kuruka kabla hawajaota mbawa.
Imekuwa ukisema popote kuhusu Rais Magufuli, wao wanakimbilia kutaja ccm.
Je ni kweli mambo anayofanya Magufuli sasa hivi ni ya "mafisi" wa ccm?
Je Magufuli ana mafungamano na kulea kwa njia ya kuwatetea mibaka uchumi ya ccm?
Tujadili maendeleo ayafanyayo kuliko kuja na hoja za udini karne ya 21.
Ninashukuru kwa angalizo lako.
 
Upumbavu wa Tundu Lissu utawagharimu kura nyingi sana hao CHADEMA.

Jamaa anawa alieanate watu wa kanda ya ziwa.

Natabiri kanda ya ziwa itampa ushindi mkubwa sana Magufuli na CCM yake kwenye uchaguzi ujao.
 
Una hasira nae kweli kweli lisu, naona kila post unamuita mpumbavu- sijui yy anakuchukuliaje
 
Upumbavu wa Tundu Lissu utawagharimu kura nyingi sana hao CHADEMA.

Jamaa anawa alieanate watu wa kanda ya ziwa.

Natabiri kanda ya ziwa itampa ushindi mkubwa sana Magufuli na CCM yake kwenye uchaguzi ujao.
Ninakubaliana na angalizo lako.

Kumbuka pia bila kupata kura nyingi kutoka kanda ya ziwa huwezi kuingia Ikulu lakini vile vile kuna idadi kubwa sana ya watu kutoka kanda ya ziwa ambao wako katika maeneo mbali mbali nchini.

Kama nilivyosema, suala la ukabila, ukanda na udini nchini linatakiwa lifanywe kwa uangalifu mkubwa hasa na wanasiasa wanaotegemea kazi zao kwa kupitia sanduku la kura.
 
Kumbuka pia bila kupata kura nyingi kutoka kanda ya ziwa huwezi kuingia Ikulu lakini vile vile kuna idadi kubwa sana ya watu kutoka kanda ya ziwa ambao wako katika maeneo mbali mbali nchini.

Sana tu aisee.

Kwa mfano Dar kuna Wasukuma na Wahaya kibao tu.

Lissu kakosea sana kuihusisha hiyo kanda nzima na huo upendeleo ambao haupo.

Watu wa kanda ya ziwa wakiamua kufanya kweli CHADEMA itakufa kabisa.
 
Mkuu, mimi nadhani CDM wana mfumo wa ubongo ambao upo tofauti na binadamu wengine. Vinginevyo wasingethubutu kuileta hoja hii kwa wananchi ikizingatiwa kuwa mwl. Nyerere aliipigia kelele sana enzi za uhai wake.
Mbaya zaidi ni kwamba, hiyo habari ya UDIKTETA, UDINI, UKABILA na UKANDA wanaiona na kuihisi CDM pekee yao. Watu wengine huku mitaani hawana habari hata kidogo na wanaendelea na shughuli zao kama jana na leo.
Kwa mtazamo wangu ni kwamba hoja hii waliyoianzisha ni sawa kabisa na kuchukua sumu ukilenga kumuulia adui yako halafu adui yako huyo anakugeuzia kibao anakunywesha mwenyewe.
Kwa mantiki hiyo utakuwa umejiua wewe mwenyewe.
BILA SHAKA HOJA ITAWAMALIZA WAO WENYEWE.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sana tu aisee.

Kwa mfano Dar kuna Wasukuma na Wahaya kibao tu.

Lissu kakosea sana kuihusisha hiyo kanda nzima na huo upendeleo ambao haupo.

Watu wa kanda ya ziwa wakiamua kufanya kweli CHADEMA itakufa kabisa.
Mbaya zaidi anapambana na CCM ambao ni wazoefu kwenye mikakati na propaganda.

Kwa sasa CCM wameamua kukaa kimya kwa sababu wanafahamu vizuri kuwa huu sio muda wake wa kujibu kwenye vyombo vya habari lakini wanachofanya kwa sasa ni kujibu kimya kimya kwa wananchi wa maeneo hayo.
 
MsemajiUkweli
Unaamuni kweli Magu katika teuzi zake haangalii udini?
Nipatie teuzi gani aliyowahi kufanya tangu akiwa waziri mpaka rais watu wa dini ile wakafika hata 10%
Hoja ya elimu ni mfu na haina mashiko
 
Madai ya viongozi wakuu wa CHADEMA ya kudai Rais Magufuli ni mkabila na anapendelea watu wa kanda ya Ziwa na Wakristo yananikumbusha mwaka 2008 wakati wa kampeni kati ya Barack Obama na Hillary Clinton wakiwania nafasi ya kuteuliwa kuwa wagombea Urais kwa tiketi ya chama cha Democratic.

Wakati akiongea na wananchi wa eneno la Pennsylvania, Obama alinukuliwa akisema, ’’Clinton is throwing kitchen sink at me, that may make for good headlines and good television, but it doesn't make for good government’’.

Baada ya Hillary Clinton na timu yake kugundua wameshindwa kumdondosha Obama kwa kutumia hoja za uongozi na uchumi walianza kueneza kuwa Obama sio Mzaliwa wa Marekani na pia ni Mwislam kwa hivyo hana uzalendo na atawapendelea zaidi Waislam.

Mbinu ya Hillary Clinton yenya dhana ya ‘’throwing kitchen sink’’ haikuzaa matunda na matokeo yake Barack Obama aliteuliwa na chama kuwa mgombea Urais wa Marekani na hatimaye kuwa Rais wa Marekani.

Neno la msingi hapa ni ‘’Throwing kitchen sink’’.

Throwing kitchen sink kwa maana ya kiswahili cha kawaida ni kutumia mbinu chafu ili umshinde mpinzani wako baada ya kugundua kuwa umeshindwa kumshinda kwa kutumia mbinu zingine ulizodhani utamshinda.

Baada ya CHADEMA kuiuza silaha yenye hoja ya Ufisadi kwa CCM mwishoni mwa mwaka 2015 na kujikuta hawana silaha nyingine muhimu ya kisiasa, waliamua kuanza kutengeneza silaha nyingine yenye hoja za ‘’Udikteta Uchwara’’.

CHADEMA walianza kwa kupiga kelele wakisema Rais Magufuli ni ‘’Dikteta Uchwara’’na wakaanzisha operesheni walioita Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania(UKUTA) lakini wananchi wengi waliwapuuza.

Kupuuzwa katika Hoja ya Dikteta Uchwara baada ya kupiga kelele kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu kwa sasa wamekuja na silaha yenye hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini.

Hii hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini ni sawa na ‘’throwing kitchen sink’’ wakitegemea kumwangamiza kisiasa Rais Magufuli.

Mtu anayefahamu mazingira ya Tanzania atakuwa alijua mapema kuwa hoja ya ‘’Dikteta Uchwara’’ isingefanikiwa nchini kwa sababu haina soko.

Ieleweke kuwa wakati akiwasilisha takwimu za ukusanji wa maoni ya wananchi kuhusu mapendekezo ya Katiba Mpya, Jaji Warioba alibainisha kuwa katika jumla ya maoni 772,211 yaliyotolewa na wananchi 351,664 yanayohusu maeneo 47 ya kiuchumi, kisiasa na kijamii yaliyochukua nafasi tano za juu ni haya yafuatayo;
1) Haki za Binadamu(uhuru wa kuabudu na mahusiano ya ndoa),
2)Muungano (muundo na hadhi ya washirika)
3)Huduma za Jamii(Elimu na Afya),
4) Rasilimali za Taifa(Ardhi, Maliasili na Mazingira) na,
5)Vyombo vya utoaji haki(Mahakama ya kadhi na Utendaji wa Mahakama)

Suala la Utawala wa Sheria(Udikteta) linalopigiwa kelele na CHADEMA lilichukua nafasi ya tatu kutoka mwisho kati ya maeneo 47 likiwa na jumla ya maoni 43 pekee.

Ukitaka kusoma takwimu, GONGA LINK>>Jukwaa la Katiba Tanzania

Kwa mantiki hii hoja ya Udikteta Uchwara ilikosa soko kabla hata CHADEMA hawajaanza kuuza kwa wananchi.

Ukichunguza utagundua kuwa Rais Magufuli kwa sasa anapambana na vipaumbele hivyo vitano (Mimba za utotoni, Elimu, Afya, Ardhi, Maliasili na Mazingira) kama vilivyotolewa na wananchi kwenye Tume ya Jaji Warioba,

Kama ni suala la Udikteta, Mwl. Nyerere alikuwa Dikteta kweli kweli kwa sababu alifuta mfumo wa vyama vingi na Katiba haikuwa na sehemu inayohusu Tamko la Haki za Binadamu huku kila aliyejaribu kumkosoa aliishia kizuizini au kukimbia nchi. Wananchi walilazimishwa kukubali kuwa zinazodumu ni fikra pekee za Mwenyekiti wa CCM/Rais wa Tanzania.

Pamoja na Udikteta wa kweli kweli, Utawala wa Mwl. Nyerere mpaka sasa ni nembo inayong’aa Tanzania na kama ukitaka kupotea katika ulingo wa kisiasa nchini, mshambulie Mwl. Nyerere. Hii inaonyesha kuwa suala la Udikteta sio tatizo kuu nchini na ndio maana wanaopiga kelele kuhusu Udikteta hawapati ushirikiano kutoka kwa wananchi wengi.

Kushindwa vibaya kwa silaha ya Udikteta Uchwara kumewafanya CHADEMA waje na silaha ya Ukabila, Ukanda na Udini kabla ya kuanza harakati za kudai Katiba Mpya au Tume ‘’huru ya Uchaguzi’’.

CHADEMA wanafahamu hawawezi kuanza kudai Katiba Mpya au Tume ''huru ya uchaguzi'' kabla hawajamdhoofisha kisiasa Rais Magufuli na kama hawatamdhoofisha kisiasa hawatapata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi na taasisi zenye sauti kubwa nchini.

Kadri siku zinavyokwenda ndivyo ambavyo muda unakuwa sio rafiki katika harakati zao za kumdhoofisha Rais Magufuli. Ndio maana wameibuka na dhana ya ’'Throwing kitchen sink’’ kama alivyofanya Hillary Clinton kwa Baraka Obama mwaka 2008.

Sikushangaa sana kusikia tamko la Edward Lowassa na Tundu Lissu kuhusu Udini, Ukabila na Ukanda, These people are brassy and racing against time!

Hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini ni hoja ambayo ni ngumu sana nchini na yenye kuhitaji uangalifu mkubwa(delicate business) na kama ukifanya bila uangalifu mkubwa unaweza kujikuta unapoteza hata kile ulichonacho.

Vijana wa CCM walijaribu kidogo kuitumia silaha ya Ukabila kwa CHADEMA wakajikuta wanapoteza majimbo ya Kilimanjaro na Arusha. Wazee ndani ya CCM wakawapiga stop kuiuza.

Kama hukufanikiwa kusoma mjadala kuhusu Dhana ya Udini, Ukabila na Ukanda wa CHADEMA unaweza kupata hapa;
GONGA LINK>>Dhana ya Udini, Ukabila na Ukanda wa CHADEMA

CHADEMA wakaitumia silaha ya Udini kwa Rais Kikwete kwenye Uchaguzi Mkuu 2010 wakajikuta wanawapoteza Waislam wengi.
Kwa maelezo zaidi kuhusu udini wa Rais Kikweye;
GONGA LINK>>Kikwete: Waliochochea Ukabila ndio wanachochea Udini leo

Sielewi CHADEMA wamejiandaa kiasi gani kuhusu hii hoja ya Ukabila, Ukanda na Udini wa Rais Magufuli na kama wakishindwa kuiuza kwa wananchi wengi, hata kile kidogo walichonacho kama mtaji wa kisiasa wanaweza kujikuta wanapoteza hasa ikichukuliwa kuwa CCM ni wazoefu kwenye masuala ya propaganda za kisiasa.
Kama Chadema silaha hao ni ukabila, basi wajibiwe hoja kwa hoja, siyo kutumia Jeshi la Polisi kuua hoja. Nilitegemea Rais Magufuli na chama chake wajibu hoja zinazoibuliwa hata kama zinaonekana za kijinga.
Umetoa mfano wa Obama alipopigwa dongo na Clinton, lakini umejijibu mwenyewe kuwa alizijibu kwa hoja.
Lakini tunaona hapa Rais wetu hataki uhuru wa maoni, watu wamkosoe. Hataki vyama vya siasa vufanye kazi kama mikutano ya hadhara, na hata ya Ndani, ila yeye na chama chake wafanye tu. Demokrasia iko wapi hapo?
Afadhali Nyerere alifuta vyama vingi mwaka 1965, sasa huyu kuvifuta hataki lakini anavizuia kufanya kazi wakati vipo kisheria.
Huu ni udhaifu mkubwa kiuongozi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwanini hampendi ukweli ..!!mnacho sema nyie ndio kiwesheria kweli ndio taifa linaongozwa kwa namna hiyo
 
Mbaya zaidi anapambana na CCM ambao ni wazoefu kwenye mikakati na propaganda.

Kwa sasa CCM wameamua kukaa kimya kwa sababu wanafahamu vizuri kuwa huu sio muda wake wa kujibu kwenye vyombo vya habari lakini wanachofanya kwa sasa ni kujibu kimya kimya kwa wananchi wa maeneo hayo.

Wafuasi wa Lissu humu washaanza kumpigia debe awe mpeperusha bendera wa chama chao 2020.

Sasa, kama kweli wanaamini hiyo hoja ya ukanda na ukabila ina mashiko basi na waifanye iwe ndo ajenda yao kuu kwenye huo uchaguzi.

Waiweke juu na mwanzoni kabisa kwenye election manifesto yao ya 2020 halafu tuone matokeo yake.

Hahahaaa.
 
Kama Chadema silaha hao ni ukabila, basi wajibiwe hoja kwa hoja, siyo kutumia Jeshi la Polisi kuua hoja. Nilitegemea Rais Magufuli na chama chake wajibu hoja zinazoibuliwa hata kama zinaonekana za kijinga.
Umetoa mfano wa Obama alipopigwa dongo na Clinton, lakini umejijibu mwenyewe kuwa alizijibu kwa hoja.
Lakini tunaona hapa Rais wetu hataki uhuru wa maoni, watu wamkosoe. Hataki vyama vya siasa vufanye kazi kama mikutano ya hadhara, na hata ya Ndani, ila yeye na chama chake wafanye tu. Demokrasia iko wapi hapo?
Afadhali Nyerere alifuta vyama vingi mwaka 1965, sasa huyu kuvifuta hataki lakini anavizuia kufanya kazi wakati vipo kisheria.
Huu ni udhaifu mkubwa kiuongozi

Sent using Jamii Forums mobile app
Makamu wa Rais - Zenje
Waziri Mkuu - Lindi
Spika - Dodoma
Naibu Spika - Mbeya
Mawaziri wandamizi ;
Lukuvi - Iringa
Mwakyembe - Mbeya
Simbachaweni - Dodoma
Makamba - Tanga
Ummy Mwalimu - Tanga
Maghembe - Kilimanjaro
Kairuki - Kilimanjaro
Mpango - Kigoma
Ndalichako - Kigoma
Mwigulu - Singidag
Mbarawa - Zenji
Kabudi - ???
Nape - alikuwa Lindi
Muhongo - Mara
Mahiga - Iringa
Lwenge - Iringa
Mhagama - Ruvuma
Mwinyi - Zenji

Huu ukabila na ukanda upo wapi hapo, Lissu atavuna tu chuki anayopanda 2020
 
kwanini hampendi ukweli ..!!mnacho sema nyie ndio kiwesheria kweli ndio taifa linaongozwa kwa namna hiyo
Makamu wa Rais - Zenje
Waziri Mkuu - Lindi
Spika - Dodoma
Naibu Spika - Mbeya
Mawaziri wandamizi ;
Lukuvi - Iringa
Mwakyembe - Mbeya
Simbachaweni - Dodoma
Makamba - Tanga
Ummy Mwalimu - Tanga
Maghembe - Kilimanjaro
Kairuki - Kilimanjaro
Mpango - Kigoma
Ndalichako - Kigoma
Mwigulu - Singidag
Mbarawa - Zenji
Kabudi - ???
Nape - alikuwa Lindi
Muhongo - Mara
Mahiga - Iringa
Lwenge - Iringa
Mhagama - Ruvuma
Mwinyi - Zenji

Huu ukabila na ukanda upo wapi hapo, Lissu atavuna tu chuki anayopanda 2020
 
Wafuasi wa Lissu humu washaanza kumpigia debe awe mpeperusha bendera wa chama chao 2020.

Sasa, kama kweli wanaamini hiyo hoja ya ukanda na ukabila ina mashiko basi na waifanye iwe ndo ajenda yao kuu kwenye huo uchaguzi.

Waiweke juu na mwanzoni kabisa kwenye election manifesto yao ya 2020 halafu tuone matokeo yake.

Hahahaaa.
Tanzania ni zaidi ya siasa za kwenye mitandao. Hawa wanaomshangilia kwenye mitandao ni sehemu ndogo sana ya wapiga kura nchini.

Hakuna atakayepambana na Lowassa ndani ya CHADEMA ili awe mgombea kwa tiketi ya CHADEMA.

Viongozi wote wakuu wa CHADEMA wamekua wafungua mlango wa gari la Lowassa ili ashuke au apande, watapata wapi uwezo wa kumpiga stop nafasi ya kugombea Urais.

Ninakuhakikishia kama Tundu Lissu atagombea hii silaha ya ukabila, ukanda na udini itamdhoofisha sana ikitumiwa na CCM ambao wana uzoefu kwenye propaganda.

Sifahamu CHADEMA wamejipanga vipi lakini ninachojua Tundu Lissu amewapa CCM silaha ya kuiangamiza CHADEMA.
 
Makamu wa Rais - Zenje
Waziri Mkuu - Lindi
Spika - Dodoma
Naibu Spika - Mbeya
Mawaziri wandamizi ;
Lukuvi - Iringa
Mwakyembe - Mbeya
Simbachaweni - Dodoma
Makamba - Tanga
Ummy Mwalimu - Tanga
Maghembe - Kilimanjaro
Kairuki - Kilimanjaro
Mpango - Kigoma
Ndalichako - Kigoma
Mwigulu - Singidag
Mbarawa - Zenji
Kabudi - ???
Nape - alikuwa Lindi
Muhongo - Mara
Mahiga - Iringa
Lwenge - Iringa
Mhagama - Ruvuma
Mwinyi - Zenji

Huu ukabila na ukanda upo wapi hapo, Lissu atavuna tu chuki anayopanda 2020
Msizunguke mbuyu, hao hawakutajwa na Lissu. Jibuni hoja kwa waliotajwa kama ni uongo uwekwe mezani.
Mpaka sasa hakuna hoja iliyojibiwa mnambwela tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom