Ushauri huu ni wa upendo mkuu. Na upendo ndiyo amri kuu tuliyopewa na Mungu wetu. Tena tunaulizwa, utawezaje kusema unampenda Mungu usiyemwona wakati unamchukia ndugu yako?
Ninaamini Rais Samia ni muumini wa Mungu, mtu anayeamini katika maisha baada ya kifo, hukumu ya Mungu, na ufufuo wa wao waliolala. Hivyo ndivyo dini zote kuu 3 za Ibrahamic, ambazo chanzo chake ni Baba yetu wa imani Ibrahim, yaani Uyahudi, Ukristo, na Uislam, zinavyoamini.
Na kila mmoja atahukumiwa kwa kuangalia aliyoyanena na kutenda katika wajibu wake. Rais Samia utahukumiwa kwa wajibu aliopewa kama Rais, nami Hamattan kwa nafasi yangu ya katika ustawi wa Ulimwengu, na wengine wote ni hivyo hivyo.
Rais Samia, jukumu lako kubwa kama Rais ni kuhakikisha wananchi wote wanatendewa haki, wananchi wote wanapata ulinzi wa maisha yao na mali zao, tena bila ya ubaguzi.
Sasa Rais Samia, ukipimwa katika hayo, kweli pepo utaikaribia? Au jehanamu ndiyo itakuwa nyumba ya wazi kwako? Sitaki kuhukumu kwa sababu tumeaswa tusihukumu, tusije tykahukumiwa. Hivyo, nafsi yamo inalo jibu sahihi. Yafikirie mambo yafuatayo:
1. Ulitakiwa kuwalinda wananchi wote na mali zao, tena kwa haki, sasa mbona watu wanaokukosoa wanatekwa, wanashambuliwa, wanajeruhiwa na kuuawawa? Mbona wanaokukosoa wabambikiwa kesi za uhaini? Kwenye hili, huoni una hatia ya wazi? Hata ukisema siyo wewe unayewateka, huoni bado utawajibika kwa sababu hukujishughulisha kuhakikisha watanzania wanakuwa salama, wanatendewa haki, na siyo kubambikiwa kesi kama alivyofanyiwa Lisu?
2. Katika upendo wa kweli, unastahili kuwatendea watu wote haki iliyo wazi. Sasa wewe mbona kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa ulidhulumu haki za watu, mpaka baadhi ya wagombea kupitia CHADEMA kuuawa? Utasema nini mbele ya Mola wako? Kwamba ama uliua au uliridhia watu wauawe kwaajili tu ya upendeleo wa madaraka kwa chama chako? Yaani wagombea wa uongozi wa chini kabisa, kama uongozi wa kitongoji, mtu anauawa!! Neno la Mungu linasema, ole wake anayewatendea uovu hawa watu wadogo, huyo anastahili kuvalishwa jiwe la kusagia shingoni, na kuzamishwa majini. Unaweza kusema kuwa siyo wewe uliyeagiza wauawe, lakini bado utaulizwa ulifanya nini ili kuwalinda? Ulifanya nini kuhakikisha unadhihirisha upendo wa kweli kwa wote kwa kuwatendea watu wote haki bila ya ubaguzi?
3. Mungu alipoweka kitu fulani katika nchi fulani, ni zawadi kwao waliopo kwenye nchi hiyo. Zawadi hiyo kamwe isigeuzwe kuwa laana kwako. Ulistahili kulinda rasilimali za nchi hii kama ulivyokuwa na wajibu wa kuwalinda Watanzania. Kwenye hili utasema, ulitekeleza kikamilifu? Ni vipi kuhusu bandari, mbuga za wanyama, misitu, na viwanja vya ndege? Kwa kuwagawia wageni, ndiyo umelinda mali za Watanzania?
Wote wanaoamini juu ya uwepo wa Mungu, wanaamini maisha ya mwanadamu Duniani ni mafupi sana, ukilinganisha na maisha ya umilele baada ya kuuacha Ulimwengu, na kwamba mwenye hekima ya Mungu kamwe hatataka maisha mafupi ya Duniani yamharibie maisha yake ya umilele.
Hujachelewa, Mungu wetu ni Mungu wa huruma, ni Mungu wa haki, si mwepesi wa hasira, bali tajiri wa msamaha kwa wote wenye kumgeukia.
Ni vyema sasa ukaugeukia upendo wa kweli na haki ya kweli kwa watu wote, ukafanya toba ya dhati. Wakati ukifanya toba hiyo, yafanye yafuatayo mara moja kama sehemu ya kudhihirisha unamwacha shetani na kumgeukia Mungu wa Haki na Upendo:
1. Toa tangazo kali kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuwa hutapenda kusikia tena wakosoaji wako wanatekwa, wanauawa, wanapotezwa. Ushetani huo usipokoma, wakuu wa vya ulinzi na usalama watawajibika.
2. Toa tangazo kali kwa jaji mkuu kuwa unataka mahakama zitende haki iliyo dhahiri, na majaji wote watakaoonekana kupindisha haki, michakato ianzishwe ya kuwavua ujaji.
3. Kesi za kuwabambikia watu kwa sababu ya masuala ya siasa au mengine yoyote iwe mwisho, na Lisu aachiwe mara moja, kwa sababu mwendesha mashtaka ameshindwa kupeleka ushahidi wa uhaini wa Lisu mahakamani.
4. Toa tangazo la kumtaka mwanashetia mkuu wa Serikali kuandaa utaratibu wa kuwapata watu huru kwaajili ya kuunda Tume huru ya uchaguzi, na kwamba Tume itakayoundwa itengeneze kanuni zinazolenga kusimamia uchaguzi utakaokuwa huru, wa haki na wa wazi, na kwamba hutataka kusikia kuna kanuni zile za kishenzi za mawakala kutopewa nakala za matokeo, mawakala kutoruhusiwa kuingia na simu au camera, na au wananchi kulazimishwa kutoonekana vituoni baada ya kupiga kura.
NB:
Mbele ta mamlaka ya Mungu tunayemwamini, hakuna utetezi wa eti nilishauriwa vibaya. Kama kushauriwa vibaya ingekuwa ni utetezi kwa Mungu unaokubalika, Hawa/Eva asingeadhibiwa maana alijitetea kuwa alidanganywa na nyoka. Na hata Adam asingeadhibiwa, kwani alijitetea kuwa alidanganywa na Eva. Ndivyo nawe utakavyosimama mwenyewe bila ya kusingizia chochote kwani mamlaka na wajibu ulipewa wewe. Umepewa pakubwa, ndivyo kwayo hukumu itakavyokuwa.
Ujaliwe hekima, bila toba, ujue daima damu za waliotekwa na kuuawa zitakulilia milele kwani ulishindwa kuzilinda.