Ujumbe mzito kutoka kwa Ex's

Ujumbe mzito kutoka kwa Ex's

Namwambia hivi "kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mchukuzi"afadhali ameenda, achape lapa na asigeuke nyuma
 
Anisamehe sana kwa kumuumiza vile, huku nilipo ni mateso tuu..natamani nirudishe muda nyuma nisimkosee tena lakini nd ivo haiwezekani. You're so missed Baby J
Lazima ntakua ni mimi ninaeongelewa[emoji23][emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
"Mi ndio maji usiponinywa utanioga, usiponioga hata chooni utanitumia, usipontumia chooni utanifulia nguo zako nenda mwanakwenda", hapa still unampenda but unajifanya mwache aendee [emoji28] [emoji28] [emoji28]
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] yani nmecheeeeka kifala
 
Namshukuru kwa kunifundisha maisha halisi hasa ya kuwa mume bora, huku nilipo naishi kwa raha kwa kutumia yale mafunzo yake, Mungu akawe upande wake ili aliyempata akapate kukaa naye maisha yake yote..
 
Duh bitter to be swallowed, Mungu akupe wepesi, mungu anasikiliza nafsi yenye majuto, but its better ukamwomba msamaha personally then urafiki kati yenu uendelee
Alinipenda sana, alifanya kila alichoweza ili nione thaman ya upendo wake kwangu. Alinibeea zawadi kila alipopata nafasi kwenda town. Alikuja geto akafua, alipika, akaosha vyombo, akatandika kitanda na kila kazi. Weekend alipokua haendi kazin tulishinda ndani kwangu kutwa nzima.

Sijui nilikua na akili gani aisee...Alinifumania akalia sana..nilimbembeleza anisamehe na kum promise sitorudia tena, ilibaki kidogo aniache kipindi kile lakini baada ya dada angu mmoja kumbembeleza sana akakubal kurudisha moyo wake nyuma. Nilimhakikishia sitofanya ujinga tena, akarudisha imani yake kwangu na mapenzi yakaendelea...

Lakini bado sikuacha ule mchezo japo wakat huu nliufanya kwa siri na umakin zaidi japo walikuja kuharibu wahenga tuu pale waliposema kila lenye mwanzo lina mwisho wake, wiki mbili tuu baadae akaja kunifumania tena na mwanamke yuleyule...ooh why did i hurt that innocent heart kwa kiasi kile.

Now anaonekana ana furaha na hanichukii, she calls kuuliza naendekea vipi na hali na vitu kama ivo..ameamua ku move on.,

Shida nnayopata huku sijui hata nielezeeje..janamke babe babe tuu likija hata lilale siku mbili halijishughulishi na kazi yoyote, chakula halipiki eti tukale mtaani, tukipita sehem anachagua vitu na kuweka kwene mkoba kisha ananitumbulia macho hapo anasubiri nilipe.
 
Ex naahukuru sana kwa vituko, uhuni uliokuwa ukinifanyia huku ukijua wazi wazi nilikuwa nakupenda. Nilijotela kwa vingi katika maisha, hata wewe mwenyewe ni shahidi. Lakini Uliniona poyoyo kwako sihemi, ukaamua kuniacha kwa dharau ,kejeli na matusi ukaenda kuolewa.
Nashukuru kwa yote kwani kupitia mateso hayo nimekuwa mwanaume bora kuliko na Mungu kanibariki nina mafanikio na nimepata aliyebora kuliko wewe.

Sijui ndoa yako inaendeleaje, lakin nakutakia maisha mema huko uliko.
 
M
Alinipenda sana, alifanya kila alichoweza ili nione thaman ya upendo wake kwangu. Alinibeea zawadi kila alipopata nafasi kwenda town. Alikuja geto akafua, alipika, akaosha vyombo, akatandika kitanda na kila kazi. Weekend alipokua haendi kazin tulishinda ndani kwangu kutwa nzima.

Sijui nilikua na akili gani aisee...Alinifumania akalia sana..nilimbembeleza anisamehe na kum promise sitorudia tena, ilibaki kidogo aniache kipindi kile lakini baada ya dada angu mmoja kumbembeleza sana akakubal kurudisha moyo wake nyuma. Nilimhakikishia sitofanya ujinga tena, akarudisha imani yake kwangu na mapenzi yakaendelea...

Lakini bado sikuacha ule mchezo japo wakat huu nliufanya kwa siri na umakin zaidi japo walikuja kuharibu wahenga tuu pale waliposema kila lenye mwanzo lina mwisho wake, wiki mbili tuu baadae akaja kunifumania tena na mwanamke yuleyule...ooh why did i hurt that innocent heart kwa kiasi kile.

Now anaonekana ana furaha na hanichukii, she calls kuuliza naendekea vipi na hali na vitu kama ivo..ameamua ku move on.,

Shida nnayopata huku sijui hata nielezeeje..janamke babe babe tuu likija hata lilale siku mbili halijishughulishi na kazi yoyote, chakula halipiki eti tukale mtaani, tukipita sehem anachagua vitu na kuweka kwene mkoba kisha ananitumbulia macho hapo anasubiri nilipe.
Mtendwa hutendwa mkuu, what's go around comes around, karma is working mkuu
 
Sijui hata niseme mimi yan... Wacha nipite tu [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124]

Cc Smart911
 
My dear X,
Naamini haukuwa mpango wa Mungu tuishi pamoja, yote yanayotokea kwenye maisha yetu yana sababu.
Sisi ni binadamu, tuna mapungufu pia. Kuishi na binadamu yahitaji uvumilivu, busara na hekima pia. Hayo tulikuwa nayo kwa kiwango kikubwa lakini niseme haikuwa imepangwa tuwe wa kufa na kuzikana.
Mimi nina amani pamoja na yote yalotekea, naanimi nawe una aamani pia.

Mungu akupe wa kufanana nawe my dear X!!!
Aaamin.
 
Back
Top Bottom