Ujumbe kwa wanaume

Ujumbe kwa wanaume

Nani kakwambia kwamba Mungu karuhusu kusaliti ndoa au kuoa wake wengi eti kwa sababu tu hao uliowataja walifanya hivyo? Kwa taarifa yako Suleiman aliua baadhi ya ndugu zake ili apate ufalme na Mungu akambariki akawa mfalme kwahiyo unataka kusema kwamba baada ya hapo Mungu aliruhusu kuua na kuua siyo dhambi tena kwa sababu Suleiman aliua si ndiyo? Nijibu hili
Lameki katika Mwanzo 4:19 "Lameki alioa wanawake wawili" , Ibrahimu, Yakobo, Daudi, Sulemani, na wengine, wote walikuwa na wake wengi.
Katika 2 Samweli 12:8, Mungu, akizungumza kupitia ya nabii Nathani, alisema kwamba kama wake na mahawara wa Daudi hawakuwa wa kutosha, naye angempa Daudi zaidi. Sulemani alikuwa na wake 700 na masuria 300 (kimsingi wake wa hali ya chini). Kwa hiyo, inaonekana kwamba Mungu aliweza kuruhusiwa mitala kulinda na kukimu wanawake ambao hawakuweza kupata mume kwa vyovyote vile. mitala iliwezesha upanuzi wa jamii kwa kasi zaidi, kutimiza amri ya Mungu ya "Nanyi zaeni, mkaongezeke; zaeni sana katika nchi, mkaongezeke ndani yake" (Mwanzo 9:7). Wanaume wana uwezo wa kuwatia mimba wanawake wengi katika kipindi kimoja, na kusababisha ubinadamu kukua kwa kasi zaidi kuliko kama kila mume alikuwa tu anazalisha mtoto mmoja kila mwaka.
 
Nani kakwambia kwamba Mungu karuhusu kusaliti ndoa au kuoa wake wengi eti kwa sababu tu hao uliowataja walifanya hivyo? Kwa taarifa yako Suleiman aliua baadhi ya ndugu zake ili apate ufalme na Mungu akambariki akawa mfalme kwahiyo unataka kusema kwamba baada ya hapo Mungu aliruhusu kuua na kuua siyo dhambi tena kwa sababu Suleiman aliua si ndiyo? Nijibu hili
Wewe unafikiri bila kanisa kuua ungekuwa unajivunia ukrsto? Soma historia ya kanisa utajua zaidi
 
Kwa hiyo unataka kuniambia vitabu kwenye Agano la Kale tusivisome?
Hapana haujaambiwa usivisome ila nimekuambia nipe andiko linalosimama peke yake ambalo linaruhusu mwanaume kusaliti ndoa au kuoa mke zaidi ya mmoja usinitolee mifano ya kina Solomon na David sababu hao ni binadamu kama sisi

Tukisema kwenye biblia tufuate maandiko yanayoelezea historia za watu tutajikuta kila kitu siyo dhambi na hata hivyo baada ya wao kufanya hayo kuna adhabu walipewa na walipozeeka walikuja kutubu

Tena mfano mzuri ni huyo Suleiman alipozeeka aliandika vitabu viwili Mithali na Wimbo Ulio Bora kitabu cha Mithali kinaelezea jinsi anavyojutia ujana wake kwa yote aliyofanya na akagundua kuwa yote aliyofanya zilikuwa ni starehe na anasa hivyo akatubu na alisamehewa

Na katika kitabu cha Wimbo Ulio Bora anaelezea jinsi wanandoa wanavyotakiwa kusifiana na ukikisoma utagundua kuwa wanaosifiana ni mwanamume mmoja na mwanamke mmoja na wala siyo mwanamume mmoja na wake wengi au mwanamke mmoja na waume wengi
 
Acha ubishi ndugu yangu mimi nimekwambia nipe mifano inayoruhusu kusaliti ndoa au kuoa mke zaidi ya mmoja unanipa mifano kaa ukijua sheria za Mungu zipo pale pale na Mungu hawezi kuhalalisha kitu ambacho ni dhambi haijalishi nani kakifanya au watu wengi kiasi gani wamekifanya

Yeye alishaweka amri zake yaani kama ambavyo alimuumba Adam na akatumia ubavu wake kumuumbia mwanamke mmoja tu Evah ndivyo alitaka ndoa zote ziwe hivyo kama kweli lengo la Mungu lingekuwa mwanaume mmoja aoe mke zaidi ya mmoja si angeonyesha msisitizo akamuumbia Adam mke zaidi ya mmoja? Amri ya sita inasema Usizini

Na kumbuka pia maandiko yanasema mwanamume atawaacha baba yake na mama yake ataambatana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja (mkewe na siyo wakeze) andiko jingine linasema mwanaume ampende mkewe na mwanamke amtii mumewe (mwanaume ampende mkewe na siyo wakeze) andiko jingine linasema kila mwanaume awe na mke wake mwenyewe (mmoja) na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe (mmoja) andiko jingine linasema ndoa na iheshimiwe na watu wote na malazi yawe safi wazinzi na waasherati Mungu atawahukumia adhabu na hizo nilizokupa ndo sheria na amri za Mungu kupitia mitume na manabii wake

Sasa unaona mimi maandiko niliyokupa sijatolea mifano historia za watu nimekupa maandiko yamesimama yenyewe na mimi nipe andiko hata moja tu kama hayo ambalo linaruhusu mwanaume kusaliti ndoa au kuoa mke zaidi ya mmoja narudia tena usinipe mifano ya watu ambao na wao wenyewe walikuja kutubu hizo dhambi nipe andiko kama andiko yaani lililosimama kama sheria nasubiri
Wewe unafikiri bila kanisa kuua ungekuwa unajivunia ukrsto? Soma historia ya kanisa utajua zaidi
 
Na vipi ikitokea mwanamke ndo akaanza kulifanya kabla ya mwanaume huyo mwanaume anatakiwa afanyaje?
Devorce hakuna discussion hapoo... unarudi kwenuuuuu

Dada unapenda usawa hadi kwenye kuchepuka ehee?

Swali la kizushi, unaweza ukaolewa na wanume wawili kwa wakati mmoja?
 
Devorce hakuna discussion hapoo... unarudi kwenuuuuu

Dada unapenda usawa hadi kwenye kuchepuka ehee?

Swali la kizushi, unaweza ukaolewa na wanume wawili kwa wakati mmoja?
Mbona wapo wanawake wengi tu walioolewa na wanaume zaidi ya mmoja? Swala hapo siyo kushindana bali swala hapo ni "to every action there is an equal and opposite reaction".
 
Mbona wapo wanawake wengi tu walioolewa na wanaume zaidi ya mmoja? Swala hapo siyo kushindana bali swala hapo ni "to every action there is an equal and opposite reaction".
Wapi huko ambako mwanamke ameolewa na wanaume wawili kwa wakati mmoja na wakifahamiana kbisa wote watatu?

Kwa hiyo mpaka hapo unadhiirisha kabisa kwamba hata wewe uko tayari kuolewa na wanaume wawili na wakawa wanapokezana kupata huduma zote za kindoa?

Yote hii ni sababu tu ya "demand for gender equality in all aspects of life"?

Mpaka hapo tayari wewe ni mshindani wa kijinsia na ushindani wako unachekesha sana.

Dada kwa ninavyokuona mentality uliyonayo ipo siku utahamasisha wanawake wenzio mfanye maandamano ya kuwataka wanaume nao waanze kubeba mimba miezi tisa kama walivyo wanawake.... ukimaliza hilo utadai "na sisi wanawake tuwekewe vyoo vya kukojoa tukiwa tumesimama tumechoka kuchuchuma"....... Ukimaliza hilo utadai "na wanaume nao waaanze kumeza contraceptive pills kuzuia mimba sio kila siku wanawake tu"....

Lakini kamwe hutakuja kudai "na wanawake nao waanze kuingia frontline hata kama hawana military training pale inapotokea vita, sio kila mara wanaume tu"....kamwe hutakuja kudai "na wanawake nao waanze kuwalipia mahari wanaume wanapotaka kuoana sio kila siku wanaume tu."

Wanawake kama wewe huwa mnanufurahisha sana.
 
Nimetafuta nilipoandika kuwa "na mimi nitakuja kuolewa na wanaume zaidi ya mmoja" ila sijapaona yaani mtu akitetea vilema basi na yeye kashakuwa kilema?

Hapo umeniambia kuwa mwanamke hawezi kuolewa na wanaume zaidi ya mmoja mimi nikakwambia wapo na nimekwambia ukweli kuwa wapo kwani mbona wengine tunawaona mitandaoni wamepiga picha wameolewa na wanaume wawili na hao wanaume wanajuana na wanaelewana

Ila mimi kusema hivyo haimaanishi kwamba napenda iwe hivyo binafsi kwangu mimi mwanaume mwenye wake wengi na mwanamke mwenye waume wengi wote ni malaya tu na hakuna mwanamke anayetaka kushindana wala kuwa sawa na mwanaume

Ila ninachojaribu kusema hapa ni kwamba kwanini wanaume hata mnapokosea hamtaki wanawake tuwaambie ukweli mnataka tukae kimya tu? Mwanamke anayelipizia maovu ya mumewe ndo anayetafuta ushindani na usawa ila hapa tunaongelea mume unapokosea kwanini hautaki hata mkeo akurekebishe unataka akuvumilie tu?

Kwenye replies zangu mbili zilizopita nimekuuliza "wewe huko tayari kuolewa na wanaume wawili"? wewe jibu lako likawa "mbona wapo wengi tu" sasa unaposema mbona wapo wakati huo wewe hujasema kwamba "mimi sipo tayari", tayari moja kwa moja mimi hapo jibu ninaloliona ni kwamba na wewe ni mmoja wa hao ambao wanaona sawa tu kuolewa na wanaume wawili.

BTW, kitendo cha wewe kukataa kuolewa na wanawaume wawili, tayari umekubali kuwa hauko sawa na mwanaume kwenye suala zima la marital affair ambalo ndio msingi wa malumbano yangu mimi na wewe tangu tulipoanza mpaka hapa tulipofika.

Mwanaume mwenye wake wengi si malaya ikiwa kama atakuwa na wake hao kwenye mazingira ya uwazi, lakini wewe mwanamke mwenye wanaume wengi ni malaya haijalishi hata kama umeweka wazi mahusiano yako na wanaume hao.

Wewe mwanamke njia pekee ya kiakili ya ku deal na mwaume mzinzi/usiopendezwa na mahusiano yake kwako wewe ni kumkimbia kama huwezi kuishi nae, lakini kuingia kwenye multiple relations kama anavyofanya yeye ikiwa sehemu ya revenge ni UPUMBAVUU.
 
Samahani kama nitakachosema kitakuwa kimeonwa na wenzangu maana message nimeiona leo? Swali je ukiwa hujaolewa umeshaplan nani atakuoa? Hivi unajua ratio ya idadi ya watu namba ya wanawake iko juu kuliko ya wanaume. Tukishajua kwamba wanaume ni wachache kuliko wanaume na wewe hujaolewa na chukulia kila mwanaume achukue mwanamke mmoja, je ukikosa mwanaume utajisikiaje? Je ni halali ukae bila mwanaume, uzeeke bila mtoto maana wanaume wote wameoa mke mmoja niambie utajisikiaje? Ukishajibu ilo uone kwamba wanaume kuwa na nyumba ndogo ni msaada kubalance wiano ulipo

Si kila mwanamke anatakiwa kuolewa na si kila mwanamme anatakiwa kuoa. Things balance out.

By the same theory wanawake waolewe zaidi ya mara moja sababu tunaishi muda mrefu kuliko wanaume.
 
Si kila mwanamke anatakiwa kuolewa na si kila mwanamme anatakiwa kuoa. Things balance out.

By the same theory wanawake waolewe zaidi ya mara moja sababu tunaishi muda mrefu kuliko wanaume.
Mumeo akifa unaruhusiwa.
Hata kwenye biblia ipo.
 
1 Wakorintho 7 : 2 "Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe"
Haya Ni maoni binafsi ya Paul.
Yawezekana kwa mapungufu yake aliamua kutooa ndio akaona Ni bora.
Haikuwa amri ya Mungu au neno alilotumwa na Mungu.
Na alisema hivyo baada ya kuona watu wanahangaishwa na wanawake badala ya kuhangaika kumtafuta Mungu.
 
Kwenye replies zangu mbili zilizopita nimekuuliza "wewe huko tayari kuolewa na wanaume wawili"? wewe jibu lako likawa "mbona wapo wengi tu" sasa unaposema mbona wapo wakati huo wewe hujasema kwamba "mimi sipo tayari", tayari moja kwa moja mimi hapo jibu ninaloliona ni kwamba na wewe ni mmoja wa hao ambao wanaona sawa tu kuolewa na wanaume wawili.

BTW, kitendo cha wewe kukataa kuolewa na wanawaume wawili, tayari umekubali kuwa hauko sawa na mwanaume kwenye suala zima la marital affair ambalo ndio msingi wa malumbano yangu mimi na wewe tangu tulipoanza mpaka hapa tulipofika.

Mwanaume mwenye wake wengi si malaya ikiwa kama atakuwa na wake hao kwenye mazingira ya uwazi, lakini wewe mwanamke mwenye wanaume wengi ni malaya haijalishi hata kama umeweka wazi mahusiano yako na wanaume hao.

Wewe mwanamke njia pekee ya kiakili ya ku deal na mwaume mzinzi/usiopendezwa na mahusiano yake kwako wewe ni kumkimbia kama huwezi kuishi nae, lakini kuingia kwenye multiple relations kama anavyofanya yeye ikiwa sehemu ya revenge ni UPUMBAVUU.
Mkuu mimi ni mkristo na biblia inakataza mwanaume au mwanamke kusaliti ndoa na mwanaume kuoa mke zaidi ya mmoja au mwanamke kuolewa na mume zaidi ya mmoja ndiyo maana nasema kwangu mimo wote ni malaya na wote wana dhambi na hiyo ni kulingana na mafundisho ya imani yangu
 
Mother con
Ukilitafakari neno la upumbavu utapata jibu,kwanza ile siku anayoamua kukupa cheo cha upumbavu ndio siku anayoacha kukupenda. Sasa anakuchukulia kama mtu dhaifu anaehitaji msaada
Kwahiyo ww hata ukienda cambodia ukarudi kama mbwa wa kienyeji atakupokea tu atakulisha ukaendelee na mambo yako uko'
Let asshole be asshole u'll sleep better
Hapo kwenye dhaifu tuombe msamaha dhaifu wapo Bungeni umetukosea heshima
 
Haya Ni maoni binafsi ya Paul.
Yawezekana kwa mapungufu yake aliamua kutooa ndio akaona Ni bora.
Haikuwa amri ya Mungu au neno alilotumwa na Mungu.
Na alisema hivyo baada ya kuona watu wanahangaishwa na wanawake badala ya kuhangaika kumtafuta Mungu.
Vizuri kwahiyo kumbe hata Solomon naye kuoa wake wengi ilikuwa ni maamuzi yake binafsi na hayakupaswa kuigwa kwa sababu pia hata yeye mwenyewe kwenye vitabu vyake alivyoandika vya Mithali na Wimbo Ulio Bora hakuna sehemu aliyowashauri na wanaume wengine nao waoe wake wengi

Zaidi kitabu cha Mithali kinaonyesha jinsi alivyokuwa anajutia mambo aliyoyafanya kwenye ujana wake na alitubu baada ya kugundua kuwa zile zilikuwa ni starehe na anasa na kitabu cha Wimbo Ulio Bora kinaonyesha jinsi mume na mke wanavyotakiwa kusifiana na ukisoma vizuri unagundua kabisa kuwa yale mashairi ni mume mmoja na mke mmoja ndo wanaosifiana

Haya nimekwambia nipe andiko hata moja tu linalosimama peke yake kama sheria ambalo linaruhusu mwanaume kusaliti ndoa au kuoa mke zaidi ya mmoja usinitolee mifano ya kina David ambao walifanya kwa mapungufu yao binafsi mimi nilishakupa maandiko ambayo angalau yanaonyesha Mungu anataka ndoa iwe ya mume mmoja na mke mmoja

Moja kuna andiko linasema Mungu akaona ya kuwa si vyema mtu huyu awe peke yake nitamfanyia msaidizi (kumbuka ni msaidizi na siyo wasaidizi na ubavu wake ulitumika kuumba mwanamke mmoja tu Evah sasa kama Mungu alitaka wanaume muoe mke zaidi ya mmoja kwanini asingeonyesha msisitizo akamuongezea Adam wake wengine?)

Mbili kuna andiko linasema mwanaume atawaacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja (kumbuka ni mkewe na siyo wakeze)

Tatu kuna andiko linasema mwanaume ampende mkewe kama ambavyo Yesu analipenda kanisa lake (kumbuka ni mkewe na siyo wakeze)

Nne kuna andiko linasema mwanaume ampende mkewe na mwanamke amtii mumewe (kumbuka ni mkewe na siyo wakeze)

Haya mimi nimekupa maandiko ambayo yamesimama yenyewe kama sheria na siyo mifano ya watu tena hayo yote yanapatikana kwenye agano la kale na wewe nipe andiko japo moja tu ambalo linaruhusu mwanaume kusaliti ndoa au kuoa mke zaidi ya mmoja bila kunitolea mifano ya manabii maana yale yalikuwa ni maisha yao binafsi
 
Back
Top Bottom