Habari MMU
Naomba niwape ujumbe nilioutafakari kwa kipindi kirefu,mimi sijaolewa kwa maana hio sijui ndoa ila ntawashauri wanaume mliooa wenye ndoa zenu.
Wanaume mna hii mentality kuwa huwezi kukaa na mwanamke mmoja, lazima uchepuke !
Umeanza kuchepuka mtoto wa watu anakupenda anaamini utatulia anakufanyia kila kitu chako kama kakuzaa,anakuzalia na watoto anawalea kama unamlipa. Wewe kazi yako kubwa ulioiona ni kujilisha upepo wa kucheat!
Haya basi mtoto watu kakaa kaona isiwe tabu mme wangu labda ndo nature yenu kucheat "my hubby Cheat in peace" basi unajiona ndo umeshinda kombe unabadili wadada kila siku dharau nyumbani.
Ngoja niwaambie kitu wanaume ,mwanamke akishakuacha u cheat in peace kwanza kashakuona wewe ni mpumbavu. Hata kama una miaka 50 wewe utabaki kuwa mpumbavu mbele yake!usijidanganye "mwanamke wangu ata hanifatilii yanii nna raha kweli"
Mynigga hakufatilii kwasababu hawezi kuhangaisha akili yake kwa ajili ya "mpumbavu"
Na wewe kuacha hawara zako wampande mkeo kichwani ni Upumbavu XXL.
Haicost kitu kuambia mpango wa kando nna mke mapenzi yetu yawe na mipaka, usinipigie masimu ovyo ovyo usinitumie masms huwezi kushindana na mtu anaenilea kwa kila kitu!
Ukiona unachepuka na mwanamke anaeshindwa kuyaelewa hayo muache tu mbona wamejaa sana ambao watakubaliana na term zako ili mjilishe upepo vizuri.
Lingine my nigga's wanawake wa sikuizi wanaroga,mtarogwa msahau future zenu na wake zenu/watoto/familia zenu!
Wewe chekelea kujilisha upepo na akina mwajuma wa buza kumbe unarogwa na wewe unachekelea.
Hakuna mwanamke kama mke wako,wewe jilishe upepo weeeh kwa mama fulani utarudi siku moja,jifunzeni kutofautisha kati ya An empress na concubine,Weka mpaka kati ya Hawara na Mke wa ndoa.
NB: Hii ni kwa wanaume waliooa wanawake wanaojielewa,wanaotimiza wajibu wote.
Wanawake mlioolewa na tabia zenu mbofu mbofu sina la kuwatetea.