Ujue ukubwa wa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume

Papa Mobimba

JF-Expert Member
Dec 6, 2018
1,153
1,359
Kuna matatizo mengi ya tendo la ndoa ambayo yanaathiri wanawake kwa wanaume. Kwa wanaume inawezekana ikawa ni kukosa hamu ya tendo, upungufu wa nguvu za kiume au kuwahi kufika kileleni. Leo nataka kuzungumzia ukubwa wa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume matatizo mengine nitazungumza katika makala zingine katika siku sijazo.

Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume wakati mwingine inaitwa uhanithi (impotence), japo neno hilo uhanithi hatupendi kulitumia kwa wagonjwa kwa sababu linaambatana na unyanyapaa wa kiasi fulani.

Wakati gani mwanaume anatajwa kuwa na tatizo la Upungufu wa Nguvu za Kiume, ni pale ambapo hata baada ya kukaa na mwanamke kwa muda mrefu anakuwa hawezi kusimamisha na hata akisimamisha haitadumu kwa muda mrefu. Wenyewe wanaita mtarimbo umelala doro.

Watu wengi wanaathirika na tatizo hili. Wengine kuanzia utoto wao, wengine wakati wa ujana na wengine ukubwani.

Katika utafiti mmoja uliohusisha nchi nane, ulionyesha kwamba tatizo hili la upungufu wa nguvu za kiume linaathiri asilimia 16 ya wanaume kwenye jamii. Kwa umri, watu umri kuanzia miaka 70 - 75, asilimia 37 yaani wanaume (37 kwa kila wanaume 100) walikuwa na tatizo hili wakati watu wenye umri wa kuanzia miaka 20 - 30, asilimia 8 (yaani wanaume 8 kwa kila wanaume 100) wana tatizo.

Hapa Tanzania, katika utafiti mmoja uliofanyika katika wilaya ya Kinondoni, miongoni mwa watu waliohojiwa asilimia 24% walikuwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Tatizo hili ni sababu mojawapo ya ndoa nyingi kuvurugika. Lakini bado wanaume wamekuwa wakimya na wagumu wa kutafuta tiba. Wamekuwa wakiungua kuanzia kitandani, kwenye mioyo yao, akili zao. Wanaungua kwa sababu ya aibu.

Takwimu zinaonyesha kwamba tatizo hili linaongezeka kwa kasi. Kufikia mwaka 2025, inakadiriwa zaidi ya watu milioni 332 watakuwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Ni muhimu sana, sana kutafuta tiba!
 
Tupambane kupata nguvu za kiuchumi hizo nguvu za kiume zikikosekana zitasaidia kupunguza maambukizi ya magonjwa ya ngono
 
Back
Top Bottom