Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,226
- 26,048
Enzi za Mao, China ilikuwa nchi ya kikomunisisti iliyoamini katika Sera za Ukomunisti.
Pamoja na Ukomunisti wa China, Rais wa kwanza wa China, Mao aliamini kuwa ni lazima apeleke vijana nje ya China wakajifunze Dunia inaendaje na ikoje ili warudi kufanya mabadiliko China.
Moja ya vijana hao alikuwepo Den Xiapoing ambaye alikuja kuwa Rais wa China baada ya Mao. Den alipelekwa Ulaya na akajifunza sana namna uchumi wa Ulaya ulivyokuwa unaenda.
Alipokuja kurudi China, Den alianzisha mfumo wa Private Property na Uwekezaji wa Sekta binafsi katika mfumo wa Uchumi wa China. Kipindi chake ndo makampuni mengi ya Marekani yalienda kufungua viwanda na kufanya uwekezaji China.
Kwa wachina wengi walimuona Deng ni msaliti wa Mao kwa kuwa wengi walikuwa wanaamini kila kitu ni cha wachina na mwekezaji kutoka nje ni mwizi. Den aliwajibu haijalishi kama paka ni mweupe au ni mweusi ili mradi anakamata panya basi huyo anatufaa
Pamoja na wachina kupata shida kuelewa Sera za Den Xiapoing ila leo ndo wachina wanamsujudu kama The Father of Modern China.
Ukiacha China kuna nchi za Singapore na Umoja wa Falme za Kiarabu ambao Dubai ni nchi mojawapo za umoja huo.
Hizi nchi nazo miaka ya 1960 ilikuwa kama sisi! Ila watawala wao walipata akili kuwa kwa akili za kuwaza sisi ndo sisi hatutafika popote. Kupitia rasilimali ya mafuta Dubai walibadilisha Sera zao kuhamasisha uwekezaji wa sekta binafsi. Leo hii kila mtu Duniani anakwenda kutalii Dubai na si kwa sababu ya mafuta tu ila kutokana na namna ikivyojengwa , inavyopendeza na ilivyo na uchumi mkubwa na maendeleo makubwa.
Ukija Tanzania. Hapa ndo shida ilipo. Nchi hii ilianzishwa katika misingi ya kijamaa. Misingi hii iliwaaminisha watu kuwa kila kitu ni Serikali na Serikali ni kila kitu. Mfumo huu ambao unaamini katika state capture umedumaza akili za Watanzania wengi sana kiasi ambacho kuna Watanzania leo hawajifunzi hata dunia ikoje, inaenda wapi na itakuwa wapi miaka hata 50 mbele.
Akili hizi zinaamini kuwa Sera ya uwekezaji ni kuuza nchi, Uwekezaji ni uuzaji wa nchi. Sera hii imewafanya Watanzania kuwa nyuma sana. Nchi yetu kuwa nyuma sana, mifumo yetu ya huduma kuwa nyuma sana.
Leo hii Tanzania, unatoka Dar hadi Kigoma kwa masaa zaidi ya 15 kwenye treni ambayo muda wowote unaweza kuambiwa leo hakuna usafiri. Ndani ya hiyo treni vyoo vichafu, huduma ni mbovu ila mtanzania hana shida ili mradi tu inamilikiwa na Serikali
Leo hii nchi yetu ina bandari zinayoweza kuhudumia ipasavyo nchi hadi 8 zinazotuzunguka, ila meli zinakaa wiki 2 hadi 3 kushusha mizigo, wafanyabiashara wanapoteza mizigo yao, hakuna mapato makubwa nchi inaweza kupata na kufanya maendeleo makubwa ila watu wanaona sawa tu ili mradi iwe chini ya Serikali. Hawajali hata wakiambiwa meli zinakimbia zinaenda Bandari za nchi jirani ili mradi waone au wasikie Serikali ndo mmiliki. Huu ni ujinga uliotukuka sana.
Kibaya zaidi pamoja na ujinga huu wa Watanzania, nchi jirani zinazotuzunguka zinakimbia sana ili kukamata fursa za kiuchumi sisi tusiwe na kitu. Rwanda amejenga Bandari kavu kubwa sana ili mizigo ya Congo Mashariki ipite kwake . Bandari hii kawapa wawekezaji. Sasa Rwanda anajenga uwanja wa Ndege mkubwa zaidi Afrika Mashariki ambao utaendeshwa pia na Sekta binafsi.
Huku Kenya amejenga Bandari ya Lamu ambayo ataiendesha kwa sehemu kubwa kupitia sekta binafsi, Msumbiji kaomba vikosi vya Rwanda vilinde Bandari zake ili wawekezaji waweze kuwekeza na zifanye biashara. Hawa wakifanya haya Serikali ikichukua hatua kuboresha utendaji wa Bandari kuna watu wanaaza kusema nchi inauzwa.
Serikali ikiwasikiliiza hawa watu kuna hatari kubwa sana huko mbeleni nchi yetu kuja kuwa kituko cha mwisho zaidi kuliko hata sasa, kutokana na kusikiliza wajinga huku nchi ikitakuwa ikimbie iendane na mabadiliko ya Dunia ya sasa.
Kwa Dunia inavyokwenda sasa, Tanzania haipaswi kurudi nyuma tena! Ujinga usipewe tena nafasi Tanzania!