Ujinga na kukosa exposure ni tatizo kubwa sana kwa wana CCM wengi

Hili ni funzo kwetu sote kutokuchagua mtu aliyekulia kwenye umasikini wa kutupwa na mshamba kuwa rais wa nchi
 
Wewe ni kielelezo cha wana Ccm waliokosa akili na exposure. Ni nchi gani duniani zimeendelea hapa duniani bila uwekesaji wa nje???

Unadhani Dubai walioinyanyua ni watu wa ndani?? Singapore walioinyanyua ni watu wa ndani? Malyasia walioinyanyua ni watu wa ndani? China walioinyanyua ni watu wa ndani????

Una elimu gani kwani?

umesoma nlichoandika ama umeruka?
 
Acha kujidhalilisha unadhani kuwa na malighafi ndo kuwa tajiri? Teknolojia unayo?? Pesa unazo???

Nani kakwambia kwenye Bandari ya Bagamoyo wafanyakazi wote watakuwa wachina??? Kawalishe ujinga wako waburundi wenzako huko chato!

Kwenye ndege kuna mtu aliwaambia wanunue ndege bila business plan?

😂 😂 😂 ehe ehe ehe, ndo maaana i said mko hopeless, infact kama upinzani ndo huu basi ukandamizwaji uendelee tu
 
Aliwakatalia wajenzi kuweka lift hospital ya Chamwino tena live kwenye camera. Mawazo yake elevator ni anasa kumbe kwa hospital ya ghorofa kuwepo kwa elevator ni compulsory
Hili nalikumbuka sana, akawa anabishana na civil engineer aliekuwa anajaribu kumwelewesha kwamba, jengo lolote la huduma za umma likiwa la ghorofa lazime liwe na lift ili liweze kuhudumia watu wenye ulemavu na wazee. Huu nao ni ushamba wa aina yake.
 
li Tanzania na CCM ipone kwenye hili ni lazima tujifunze na kuacha ujinga na ushamba na tuitazame dunia Kama sehemu ya ushindani wa kibiashara na kimaisha ili tuweze kutumia akili zetu na rasilimali zetu vizuri kwa maendeleo yetu ya kweli.
Mawakala wa mafisadi mnatapa tapa
Yaani wewe kwako Manji ndio umeona wa kutolea mfano?
Mbona Bakhresa,Mo,Zakaria,Rostam,Mengi na wengineo viwanda vyao havikufa?
Bakhresa ameongeza Bagamoyo sugar chini ya Magufuli huyu huyu,tena akapewa na 11,000ha alime miwa
Mo kafungua kiwanda cha nafaka cha kisasa,chini ya Magufuli huyu huyu
Rostam kafungua kiwanda cha ngozi cha kisasa chini ya Magufuli huyu huyu
Zakaria kafungua kiwanda cha kukoboa mpunga cha kisasa zaidi chini ya Magufuli huyu huyu
Manji alikua na janja janja nyingi sana
 
Amani iwe kwenu wadau!
Watanzania wote ni mashuhuda kwa jinsi gani Magufuli alivyoliharibu Taifa hili kwa miaka yake 5 na miezi 4 aliyokaa madarakani

Alama kuu ya uchumi kuwa vizuri kwenye nchi ni kwa jinsi gani hali ya maisha ya watu wa nchi iyo inavyoboreka na kuwa Nzuri siku hadi siku.
Alama nyingine ni kwa jinsi gani wananchi wa nchi iyo wanapata ajira na kuweza kuendesha maisha yao ya kila siku.

katika miaka 5 na miezi 4 ya uongozi wa Hayati Magufuli nchi ya Tanzania ilianguka vibaya sana kwenye hayo maeneo na vielelezo ni hivi.

1. Makampuni mengi makubwa yaliyokuwa yameajiri watu wengi, yalikufa kutokana na chuki tu za magufuli zilizopelekea kupewa madai ya kodi makubwa. Mfano ni Kampuni zote za Manji zilizokuwa Chini ya Jina Quality Group. Kampuni hizi zilikuwa zimeajiri watanzania wengi sana wasiopungua 5000 kwa ajira za moja Kwa moja na wengineo wasiopungua 10000 waliokuwa wanaingiza tu pesa kutokana na uwepo wa kampuni hizi za manji. Biashara ya soko la mbaazi na sehemu ya biashara ya korosho ilikuwa inapata nguvu kwenye soko Kwa sababu ya uwepo wa kampuni hizi. Baada ya Magufuli kummaliza Manji kiuchumi sote tukaona kwa jinsi gani wakulima wa Mbaazi na korosho walivyoathilika na maelfu ya watu wetu kukosa ajira. Huu ni mfano wa Manji tu, Kuna kampuni nyingine nyingi kama Rhino cement, Shoprite, Nakumat na nyingine nyingi. Kufa kwa hizi biashara kwa kiasi kikubwa kumesababisha hadi shopping malls nyingi kufa katika jiji la biashara Dar es Salaam kama Mkuki, Quality Centre na nyinginezo nyingi.kampuni hizi zikipokufa hii imefanya hata kampuni nyingine zilizotegemea hizi biashara kama AAR kufa kwa sababu wafanyakazi wa kampuni hizi ndo walikuwa wanalipa Bima ya Afya AAR na kwenye makampuni mengineyo.
Ili kukwepa aibu ya kufanya Tatizo la ajira kuwa kubwa Tanzania alijifanya yupo karibu na Wamachinga, mamalishe na bodaboda kwa kuwaruhusu kufanya biashara popote pale jambo lililoharibu usafi na mipango mizuri ya miji yetu na kuleta tatizo kubwa Zaid la kodi maana walipa kodi wengi walipungua sana!

2. Aliua miradi ya muda mrefu ambayo ingetengeza stability ya kiuchumi Tanzania na kutengeneza mamilioni ya ajira kwa Watanzania. Mfano Bandari ya Bagamoyo.
Katika mradi wa Bandari ya Bagamoyo, uwekezaji mkubwa ulikuwa ufanyike kwenye kujenga viwanda vingi katika eneo la viwanda na pia katika Bandari yenyewe. Uwekezaji huu ungehusisha pia ujenzi wa reli na miji ya kisasa maeneo ya kule Bagamoyo. Hela za mradi huu zote zilikuwa kutoka Kwa wawekezaji wa China na Oman. Hakuna hata senti ingetoka Tanzania, ila watanzania wangepata ajira za uhakika, mji ungeendelezwa na hatimaye Tanzania ndo ingekuja kuwa gateway ya East na Central Africa Kwa usafirishaji wa bidhaa. Mradi huu ungezalisha ajira za kudumu na uhakika za watanzania zaidi ya laki 5 kutokana na uwepo wa bandari husika na Viwanda. Aliacha kujenga bandari akaenda kujenga daraja la kigongo- Busisi ambalo kiuchumi halina faida kubwa kwa idadi kubwa ya watu na halitaingiza faida kubwa huko mbeleni.

3. Sera ya fedha imezifanya bank kuwa hoi kiuchumi. Kuua Kwa makampuni na sera yake ya kufreeze account za watu kulipelekea watu kutoa hela kwa kiwango kikubwa sana kwenye mabenki yetu na hata kampuni kufirisika na kufa kulipelekea bank nyingi kufa. Matokeo yake watu wengi wakapoteza ajira kama kwenye bank M, Exim Bank na pia mitaji ya Bank nyingi ikapungua. Ushahidi wa hili ni kwa jinsi gani mabenki yamekuwa yakichelewa kutoa mikopo kwa wateja wake Mf. CRDB na NMB. Na Pia kufeli kwa bank zingine kujiendesha Mf. Azania Bank ambayo kwa sasa ni kama nayo imekufa ipo ipo tu!

4. kutumia hela nyingi kununua ndege bila kuwa hata na business plan.
Kati ya biashara ambazo ni High risk duniani ni biashara ya ndege. Shirika la ndege la Rwanda liko hoi kifedha, imebidi waliunganishe na Qatar airways, Same wa South African Airways na Kenya Airways bila kusahau Air Uganda. Kitendo cha yeye kwenda kununua ndege nyingi tena kwa cash bila kuzingatia kuwa hakuwa na business plan ya kuliendesha hili Shirika ni kielelezo tosha kuwa alikuwa akikurupuka ili tu kutaka sifa kutokana na ujinga wake na kukosa kwake exposure / ushamba.

Mambo yote haya ya kafanya akope zaidi ili aweze kuendesha nchi na kufanya miradi mingine ambayo kiukweli nayo kamwe haiwezi kuja kuleta faida Kwa sababu mradi mdogo tu wa Mwendokasi uliotengenezwa ili kuwa mradi wa kisasa na ulete faida kwa nchi aliuharibu vibaya na kwa sasa hauna tofauti na mfumo wa awali wa daladala.

Ili Tanzania na CCM ipone kwenye hili ni lazima tujifunze na kuacha ujinga na ushamba na tuitazame dunia Kama sehemu ya ushindani wa kibiashara na kimaisha ili tuweze kutumia akili zetu na rasilimali zetu vizuri kwa maendeleo yetu ya kweli.
Suala la Bandari ya Bagamoyo ni controversial na umelieleza kwa jiko la makengeza. Hatujaona pia Mkataba na feasibility study. Wazo ni nzuri kuwa na bandari lakini je masharti mbona yalikuwa ya hovyo na mtoa mada huzungumzii jinsi ambavyo yamgeumiza nchi. Tenda itangazwe upya. Zingaita case ya Sri lanka na Zambia.Magufuli ameacha legacy bayo itaishi milele. Miradi aliyojenga inafunika udhaifu mchache.
Kuhusu ndege ni biashara inayohitaji kujitosa kama nchi too much academic analysis on business plans wakati mwingine hupotosha. Hivu watu wote huanza biashara na business plan kwani tulikuwa tunaenda kukopa.
Kuhusu sekta binafsi bado wafanya biashara wanaendelea na biashara zao wachache wakwepa kodi na waliozoea na ubadhirifu iliwaathiri sana. Lakini pia ugonjwa wa Korona duniani hususani kwenye source market iliathiri biashara nyingi na siyo Magufuri as an individual. Uchambuzi wako umegubikwa na chuki binafsi na hivyo kukosa majibu yaliyosimama yenyewe na yenye utafiti wa kisayansi. Mengi uliyosema yana speculations. Jioni njema
 
Kwa iyo unslinganisha maelfu ya biashara na viwanda vilivyofungwa na hivyo Viwanda 3 vilivyoanzishwa??? Unaposema Manji alikuwa janja janja, wewe umeajiri watu wangapi kumzidi Manji alieajiri maelfu ya watanzania?
Mawakala wa mafisadi mnatapa tapa
Yaani wewe kwako Manji ndio umeona wa kutolea mfano?
Mbona Bakhresa,Mo,Zakaria,Rostam,Mengi na wengineo viwanda vyao havikufa?
Bakhresa ameongeza Bagamoyo sugar chini ya Magufuli huyu huyu,tena akapewa na 11,000ha alime miwa
Mo kafungua kiwanda cha nafaka cha kisasa,chini ya Magufuli huyu huyu
Rostam kafungua kiwanda cha ngozi cha kisasa chini ya Magufuli huyu huyu
Zakaria kafungua kiwanda cha kukoboa mpunga cha kisasa zaidi chini ya Magufuli huyu huyu
Manji alikua na janja janja nyingi sana
 
My friend Lord denning. Longtime-no see. Hapo tu kwenye bandari ya Bagamoyo tafadhali tuonyeshane kwanza mkataba. Usiingie kwenye band wagon ya wasimuliaji ya “kusimulia “ faida au hasara ya mradi lakini mkataba hauonyeshwi.
Hizo lugha za sisi hatutatoa senti hata moja ni Wachina wameamua kuwekeza, msije mkatupelekea ya Sri Lanka, Mombasa, Zambia na kwingineko.
Kwanza Bandari ya Bagamoyo ni mkopo kwetu au uwekezaji wao kwa fedha zao? Nijibu hapo
 
Yule mzee bora Mungu kamchukua tu!
Hili nalikumbuka sana, akawa anabishana na civil engineer aliekuwa anajaribu kumwelewesha kwamba, jengo lolote la huduma za umma likiwa la ghorofa lazime liwe na lift ili liweze kuhudumia watu wenye ulemavu na wazee. Huu nao ni ushamba wa aina yake.
 
Kwanza Bandari ya Bagamoyo ni mkopo kwetu au uwekezaji wao kwa fedha zao? Nijibu hapo
Mimi sijui aisee ndio maana nasema uletwe kwanza mkataba na uonekane pale bungeni. Hatuhitaji mambo ya kusimuliana faida wala hasara bila kuona mikataba.
 
Kwa iyo unslinganisha maelfu ya biashara na viwanda vilivyofungwa na hivyo Viwanda 3 vilivyoanzishwa??? Unaposema Manji alikuwa janja janja, wewe umeajiri watu wangapi kumzidi Manji alieajiri maelfu ya watanzania?
weka ushahidi wa hayo maelfu ya viwandfa yaliofungwa
 
Kwa roho yako ya kiburundi lazima uone ukandamizaji ni sawa
upinzani umekandamizwa maisha yamekua mazuri, miradi inasogea, raisi anafanya maamuzi yenye akili dunia nzima wanashangaa kwann tusiendelee na ukandamizaji, tena ni bora hata magu yaaani ingekua ni mm mfano najenga flyovevr kuanzia riverside mpaka sam mujoma kupunguza foleni alafu mseme haina kazi, mngekua mnavuka mkiwa na kadi ya uanachama wa ccm tu, hatuwezi kuentatain upumbavu kama huo wenu
 
Back
Top Bottom