WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 956
Naanza na kutoa Pole kwa watanzania wote, hasa ndugu jamaa na marafiki wa karibu wa Kanumba The Great (R.I.P) kabla sijatoa mchango wangu kuhusu hili jambo zito na nyeti ambalo limetawala maongezi katika kipindi hiki cha Sikukuu ya Pasaka. Mengi yamesemwa na pia kuna mengi pia hayajasemwa, moja wapo likiwa "ujinai" wa Lulu katika kifo cha Kanumba.
Katika mukatadha wa sheria, tunaona kwamba Tanzania ni moja ya nchi zenye kuuweka uwajibikaji kijinai kuwa chini ya UMRI wa miaka 18 kwa kuweka miaka 10 kama umri ambapo mtu anaweza kushtakiwa kwa kosa la jinai. (Linganisha na Kenya miaka 8, Zimbabwe -7,Zambia 8,Africa Kusini 10) n.k. Ina maana kwamba mtu (mtoto) aliye chini ya umri huu hawezi kushtakiwa labda ithibitishwe kuwa alikua anajua kabisa anachokifanya. Lulu hafit kwenye kundi hili hata kama ana umri wa miaka 17 kama ambavyo Mh Halima Mdee ame tweet leo baada ya kumtembelea LuLU Oysterbay Polisi.
Tukiacha sheria na matakwa yake, kwa kuzingatia yale yanayosemwa kuhusu mkasa huu wa kifo cha Kanumba (R.I.P), inatupasa tuone kuwa kila hadithi ina pande mbili. Hadithi ya Kanumba ambaye kwa sasa hayupo kuelezea, na hadithi ya Lulu aliye mahabusu. Inasikitisha sana kwamba kifo kimetokea katika mazingira ya kutatanisha. Kifo hiki kimesikitisha watu wengi na kufanya udadisi wa kutaka kujua ukweli ulio objective iwe vigumu. Watu wamebakia kushusha lawama ZOTE kwa Lulu tu bila kutaka kujua haswa ilitokea nini hadi kifo hicho kikatokea.
Kama watanzania wengine napenda niseme kwamba , nahuzunika kama wengine kumpoteza Kanumba na pia kuona ndoto zake kama msanii zikizimwa ghafla. Aidha wapenzi wake wamekatishwa ile raha ya kuendelea kuburidika na filamu zake. Pamoja kuwa na huzuni kuu, pia najaribu kuangalia upande wa pili – Lulu! Huyu binti wa miaka 17/18 kijamii bado ni msichana mdogo japo kisheria hasamehewi kuwajibishwa kijinai. Lakini uwajibishwaji huo utakuja pale upelelezi utakapokamilika. Kufuatana na waliobahatika kumuona huyu binti, ana majeraha kuashiria kuwa alipigwa na kuumizwa na marehemu. Ingekuwa marehemu hakufa, basi nadhani kesi hii ingekuwa ya aina yake kama ingefika kunakohusika. Wote walijeruhiana. Lakini mazingira ya kujeruhi huko ni yepi?
Tumeambiwa na hata kusoma kwamba:
1. Lulu alienda kwa Kanumba usiku mkali mishale ya saa 6, kusudi watoke kwenda kucheza muziki kwa msanii Chaz baba – Mashujaa band ( Kanumba alishapiga simu kutaka andaliwe viti na sehemu maalum ya kukaa yeye na marafiki zake na pia akiomba hata wimbo maalum atakapofika)
2. Lulu alitoka nje kusikiliza simu – Kanumba akamfuata na kumrudisha ndani ili aeleze anaongea na nani.( Hapa tunaona kabisa Kanumba akianzisha shari yeye mwenyewe badala ya kuepuka shari)
3. Kanumba alimfungia Lulu ndani wakawa wanagombana. Aggressor hapa ni Kanumba na siyo Lulu.Kelele za ugomvi ziliashiria vurugu na kwa vile mlango ulifungwa na ufunguo, ilikuwa vigumu Lulu kukimbia tena au hata watu nje kuja kutoa msaada.
4. Lulu alitoka nje kwenda kumwita Seth na kumwambia Kanumba kaanguka.Lulu alikimbia akiwa na majeraha.Hii haionyeshi kuwa Lulu aliua vinginevyo angetoka kimya kimya akatokomea.
Sasa ndugu zanguni, kwanini Lulu anaonekana alifanya mauaji ya kukusudia? Ikiwa Kanumba alianguka katika purukushani na kuponda kichwa na kufa, Lulu kaua vipi? Kukamatwa na polisi na kushikiliwa ili kusaidia uchunguzi ni utaratibu wa kawaida sana. Nimewahi kushuhudia mtu kajiua, ndugu yake na mkewe waliomgundua kajining'iniza walikamatwa wakakaa ndani ili wasaidie uchunguzi Ilahali mtu kajiua mwenyewe. Ilisikitisha sana kwa maana wafiwa walitiwa misukosuko kwa kifo ambacho marehemu alijiletea kwa kujitundika. Walikaa masaa kadhaa kabla ya ndugu kwenda kuwatetea na kushinikiza waachiwe!
Kwenye hii kesi ya Lulu, bahati mbaya sana Lulu ana sifa mbaya kwenye jamii kiasi kwamba hakuna mtu anathubutu kumtetea na kumsaidia angalau aweze kujipanga kukabiliana na siku za kusubiri hatma baada ya upelelezi. Kibaya zaidi kuna statements za watu wazito ndani ya jamii, statements ambazo zenyewe tu zimeshapasisha kwamba Lulu ndio muuaji. Kibaya zaidi, unyeti wa hali inayozunguka msanii maarufu kipenzi cha wengi utaathiri hata mwenendo mzima wa upelelezi na kitakachojiri to the detriment of Lulu.
Nadhani kwa vile hii haijawa kesi ya kimahakama, na kwa vile jamii inazungumzia hiki kifo, hakuna ubaya tukawa na scenario zote.
Sijaandika haya kwa vile nataka kumsemea Lulu asiwajibike kama anahusika kijinai bali najaribu kupanua mjadala.
Nawasilisha.
WoS.