"Ujinai" wa Lulu katika "mauaji" ya Kanumba (R.I.P)

Thread ndeefu hata haimtji Ray!

ehee... Paxman..hiyo "Ray factor" nimeiruka makusudi .Nilisikia unofficially kuwa Ray, JB na Sauda Mwilima walikuwa kule Mashujaa saa chache kabla ya kipindi alichotarajiwa Kanumba kuingia ukumbini.Kisha wakaondoka.
Inaelekea kuna kitu...... ngoja tutasikia.
Hata hivyo mimi nilitaka kuona ujinai wa Lulu hapo kulingana na facts tulizozipata rasmi kutoka vyombo rasmi.
 
ni ushahidi gani unaokufanya useme motive ya murder haikuwepo?unajuaje kwamba lulu alifika na kifaa(mfano chuma kizito) kwa ajili ya kumpiga kanumba?
Unajuaje simu aliyopokea lulu ilimpa maelekezo nini cha kufanya ili amuadhibu marehemu?

Maswali magumu hayo, siwezi sema chochote sababu sio mpelelezi wa hii kesi.
 
k upata haki Lulu,kupata haki marehemu au ndugu wa marehemu kwa utendaji wa jeshi letu la polisi ni kitendawili kwani mazingira mengi ya ushahidi yamevurugwa.
 
Umegusa penyewe kabisa!
Ukiangalia mazingira ya tukio, sijaona kiwango cha kuridhisha kutosha kukusanya ushahidi forensically.Eneo la tukio limeingiliwa na watu wa kila aina kiasi ambacho sijui kama kweli inawezekana kupata forensic evidence.Pia Kanumba alipofikishwa Muhimbili alipelekwa motuary moja kwa moja......

Tunao forensic investigators? Katika hali ya kawaida nilitegemea eneo ambalo mauaji yalitokea liwe 'out of bound' lakini imekuwa vinginevyo.
 
  • Thanks
Reactions: Aza
she must be the prime suspect!nasikia alitoka uchi na kumuita seth akamuone kanumba halafu yeye akatokomea(sina uhakika kama alitembea uchi)

Either way, tayari kuna kamanda wa polisi ameshai-prejudice kesi kwa kutoa tamko la kwamba eti uchunguzi ukikamilika watampeleka mahakamani kumfungulia mashitaki ya mauaji!

Should the case see the light of day it'd be a slam dunk for the defense. The police have provided so much ammunition for the defense (team) to use.
 
ni ushahidi gani unaokufanya useme motive ya murder haikuwepo?unajuaje kwamba lulu alifika na kifaa(mfano chuma kizito) kwa ajili ya kumpiga kanumba?
Unajuaje simu aliyopokea lulu ilimpa maelekezo nini cha kufanya ili amuadhibu marehemu?

And what makes you so sure of that??
Jamani eeeh, tusimuhukumu mtoto wa watu, the same incidence can happen to anybody., You, Me or anybody. So, tusiwe judgemental guyz
 
ehee... Paxman..hiyo "Ray factor" nimeiruka makusudi .Nilisikia unofficially kuwa Ray, JB na Sauda Mwilima walikuwa kule Mashujaa saa chache kabla ya kipindi alichotarajiwa Kanumba kuingia ukumbini.Kisha wakaondoka.
Inaelekea kuna kitu...... ngoja tutasikia.
Hata hivyo mimi nilitaka kuona ujinai wa Lulu hapo kulingana na facts tulizozipata rasmi kutoka vyombo rasmi.

Duh..! asee :car:
 
Hakuna kesi hapa, sheria ya Tanzania inaruhusu kumuua mtu katika self-defence ila mradi utumie reasonable force binti ataachiwa muda si mrefu.
 
Tunao forensic investigators? Katika hali ya kawaida nilitegemea eneo ambalo mauaji yalitokea liwe 'out of bound' lakini imekuwa vinginevyo.

That's another ammunition for the defense...to my knowledge the place wasn't even cordoned off by the cops to conduct a thorough investigation and to collect evidence if there was any.
 
Kanumba pia alikuwa akitumia kilevi! Yawezekana alipoteza stability baada ya pombe kuathiri stability yake
 
LULU HAKUPANGA KUMUUA KANUMBA!

1.katika mazungumzo yake na mkasi,hakupenda kugusia kama ana mahusiano na Kanumba.pia sikuona kama alishtushwa na swali hili.lakini tusisahau kuwa swali hili lingeweza kumkumbusha mabaya(ubakaji) aliokuwa akifanyiwa na marehemu labda kwa kisingizio cha kumtoa kimaisha.

2.kama lulu angepanga kumuua kanumba asingeweza kutumia ugomvi kwa sababu asingekuwa na uhakika wa kumshinda kanumba kimabavu.

3.kama lulu angepanga kumuua kanumba sitegemei angefanya hivyo nyumbani kwa kanumba tena kwa kutumia ugomvi.

4.pia kama lulu angepanga kumuua kanumba asingetoka na kumuambia seth kuwa kanumba kaanguka.angesubiri mpaka afe na baadaye kuondoka kimya kimya.

..........ngoja niendelee kufikiria!
 
Either way, tayari kuna kamanda wa polisi ameshai-prejudice kesi kwa kutoa tamko la kwamba eti uchunguzi ukikamilika watampeleka mahakamani kumfungulia mashitaki ya mauaji!

Should the case see the light of day it'd be a slam dunk for the defense. The police have provided so much ammunition for the defense (team) to use.
NN,
Unachosema nami nakiunga mkono maana kwa mtizamo objective ndicho hasa kilivyo.
Tatizo kama nilivyosema kwenye bandiko langu la mwanzo, hii kesi ina sensitivities ambazo zinazima objectivity.
Nimemskiliza Msemaji wa polisi muda huu anasema bado wanamhoji Elizabeth (Lulu) na pia wanachunguza mawasiliano ya simu.Nionavyo mimi, polisi wanafanya kile wanachoona kinafaa kwa wakati uliopo hata kama kesi itafia mahakamani.
 
Mimi naona maelezo yaliyopatikana ni ya pande mbili,yaani Lulu na Sethi.Lakini sikuona sababu ya lulu kuondoka eneo la tukio mapema kiasi hicho kwasababu mtu aliyokuwa anamuogopa tayari alikuwa hana fahamu.Angesubiri mpaka daktari aje waondoke na mwili mpaka hospitari.

Tatizo hapa ni kwanini alitoweka eneo la tukio mapema kiasi hiki,kitendo hicho ndicho kinapelekea wadau wahisi kama pengine alihusika.

Mdogo wa marehemu yaani Sethi,amenukuliwa akisema alisikia sauti za malumbano, lakini alishindwa kuingia ndani kwasababu mlango wa chumbani ulikuwa umefungwa.Kwa mujibu wa kauli hii inaonyesha kuwa sauti zilizokuwa zinasikika zilikuwa za kawaida kiasi kwamba hazikumfanya apige keleke kuomba msaada kutoka nje.

Mtazamo wangu ni kwamba kama Marehemu angekuwa hai angetoa maelezo ya makovu yaliyokutwa kwa lulu kuwa yametokana na kipigo kutoka kwake au alikuja nayo; Lakini kama Lulu ndiye aliyetoa taarifa kwa Sethi kuhusu kudondoka kwa Kanumba,Basi hata Sethi anaweza kutoa ushuda wake kwa namna alivyo muona Lulu pindi alipompa taarifa, kwamba alimuona ana makovu au laa.

Ushauri wangu ni kwamba, hakuna tukio lisilokosa sababu,na ajali haina kinga; Fundisho hapa tuwe na kiasi kwa kila jambo:Simu za mkononi ni nzuri kama zitatumika kwa uaangalifu mkubwa,lakini ni mbaya kama zitatumika vibaya. Mimi naamini hakuna mpenzi asiye na wivu kwa mwinzi wake hasa kama anampenda, cha msingi tuwe makini na hivi vilonga longa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom