Ujenzi wa nyumba za kuficha paa/contemporary/ hidden roof

Ukisoma changamoto ambazo wengi wanasema hapa ni uwezekano wa kuvuja kwa paa! Binafsi ningependa kufahamishwa ni kwanini hii ni changamoto ya aina hii ya ujenzi, na Kwa namna gani inatatulika? Kwa wajuzi/wataalam wa ujenzi, naomba msaada.
 
Kwa utafiti wangu mdogo nimeufanya, wengi wanaosema hazifai wapo na maneno ya kuambiwa. Hawajawahi hata kujenga hizo nyumba. Ni kama wale wanaokwambia usinunue Nissan haifai kabisa, ukiuliza kama amewahi hata kumiliki utagundua ni maneno ya kijiweni.

Nakubaliana na wanaosema tatizo ni mafundi. Nyumba hizi zinahitaji fundi anayezijua. Tatizo lipo kwa wenye nyumba, unamuamini fundi aliyekufanyia kazi za tofali akuezekee na bati tu kwa sababu gharama amefanya ndogo.

Contemporary ni zaidi ya kuezeka na mafundi wazuri wapo.
 
Unamawazo kama yangu mkuu nilikuwa najiuliza hapa
Inawezekana pia lakini bado utahitaji kui treat juu ya hiyo slab, utahitaji membrane cloth na bitumen nyeupe ili kuzuia unyevu hasa kipindi cha mvua za muda mrefu
Na vipi ukiamua kupiga zege badala ya kuweka bati dizain kama zile nyumba za wagogo ambazo zinajengwa kwa tope mwanzo mwisho hadi kuezeka?
 
Bro umeongea yote;
Iko hivi: nyumba hii inahitaji myaalam ambaye anajua namna ya kuanza hadi kumaliza.
Wengi anampa fundi wa kujenga tofali then analeta mwingine wa kuezeka....

Hii nyumba inajengwa na mtaalam mmoja mwanzo hadi mwisho.

Chukua haya yafuatayo;
1. Msingi uinuke
2. Boma liwe na tofali laini 11
3. Baada ya lenta hakikisha unatengeneza sehemu ya kupokelea maji
4. Pawepo na ducts za kupitishia maji na sio bomba
5. Upake bitumen pamoja na mebrane cloth maeneo ya wazi ya kupokelea maji.

6. Epuka slop ndefu za paa bali livunje vunje vipande vipande ili maji yashukie sehemu tofauti

Ukizingatia haya nyumba hii hsivuji na utaifurahia na haina gharama kubwa
 
Hakikisha kwenye mdingi unaanda matoleo ya maji mkuu
 
Uko sahihi, nimeandika hapo juu pia
 
Asante kwa ufafanuzi... binafsi nazipenda sana ila sioni unafuu wake
 
Asante kwa ufafanuzi... binafsi nazipenda sana ila sioni unafuu wake
Nyumba hizi ni nafuu sana kwa upande wa paa...bati na mbao.
Kitu kinachoongeza gharama ni urembo tu.

Kimsingi mtu mwenye uelewa sahihi urembo mwingi huharibu mwonekano wa nyumba hizi.

Jambo muhimu ni;
1. Msingi mrefu...nyumba iinuke
2. Madirisha makubwa
3. Urembo kiasi/ plain design inapendeza zaidi
 
Ukisoma changamoto ambazo wengi wanasema hapa ni uwezekano wa kuvuja kwa paa! Binafsi ningependa kufahamishwa ni kwanini hii ni changamoto ya aina hii ya ujenzi, na Kwa namna gani inatatulika? Kwa wajuzi/wataalam wa ujenzi, naomba msaada.
Soma hapa mkuu
 
Umelenga mulemule mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…