KERO Ujenzi wa Barabara hii ya Bukoba Manispaa ulitakiwa kukamilika Oktoba 2024, haujakamilika hadi Februari 2026

KERO Ujenzi wa Barabara hii ya Bukoba Manispaa ulitakiwa kukamilika Oktoba 2024, haujakamilika hadi Februari 2026

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Ujenzi wa kipande cha Barabara ya Kilomita 1.6 kinachopita maeneo kadhaa ndani ya Manispaa ya Bukoba ambacho ujenzi wake ulianza Oktoba 9, 2023 ilipaswa kukamilika tangu October 8, 2024 mpaka leo Feb 16 2026 hakijakamilika na kuta zinazidi poromoka.

Kinachosikitisha zaidi ni kuwa kuta za mawe za barabara hiyo zimeshaporomoka zaidi ya mara moja kwa nyakati tofauti, jambo linalotia wasiwasi juu ya uwezo wa mkandarasi husika na usalama wa barabaraba hiyo hasa itakapokamilika

Kuna nini kinaendelea kati ya mamlaka na mkandarasi huyo aliyejizolea umaarufu mkoa hapa hata anashindwa kuwajibishwa licha ya kuwa nje ya mkataba kwa miezi zaidi ya 15 sasa?

Bukoba road.jpeg
Bukoba roada.jpeg
Bukoba.jpeg
 
Samahani itabidi mvute subira mpaka kipindi cha uchaguzi ujao. Labda kama 2028 hivi.
 
Bukoba huku Kuna shida sana ,halmashauri ya bukoba ufuatiliaji hakuna Kuna Miradi Mingi inazorota sana
 
Back
Top Bottom