greater than
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 1,759
- 3,222
SEHEMU YA PILI
Namna ya kuzuia maji katika jengo
1.Mfumo wa kuchepusha maji mbali na jengo
2.Uwepo wa gutter
3.Matilio zenye kuzuia maji
1.MFUMO WA KUCHEPUSHA MAJI KATIKA KIWANJA
Njia hii inatakiwa kutumika katika kukabiliana na maji yanayogusa sehemu za chini katika jengo lako,sehemu hizo ni kama Msingi,Plinth,vibaraza na kuta (usawa wa chini).
Hii ndiyo namna nyepesi na gharama nafuu zaidi katika kupambana na maji
Namna kufanikisha hivi ni
i). Kutoweka Bustani (maua/nyasi) sambamba na ukuta
ii). Kuweka kibaraza katika mzunguko wote wa kuta/eneo la jengo
iii). Kuweka mitaro inayo chepusha maji mbali na jengo
iv). Kuweka mambomba yanayo chepusha maji ardhini mbali na Msingi
v). Kuweka vizuizi vya maji katika njia ambapo maji yanatokea kabla hayajafika kwenye msingi
2.UWEPO WA GUTTER
Gutter ni kifaa kinachowekwa/fungwa kwenye ukingo wa paa kwa dhumuni la kukusanya maji ya mvua.
Katika paa za mgongo Tembo,hizi huwa na muundo wa cylinder nyembamba na huwa ya plastick au bati
Katika paa za zege huwa kuna mistari inawoekwa mwishoni mwa kibaraza,ambapo huwa kama gutter
Uweo wa gutter huambatana na Uwepo wa pipe za chini, ambazo hukusanya maji ya kwenye gutter na kupeleka chini.
3. WATER PROOFING MATERIALS
Kuna Matilio ya aina nyingi ambazo huwa zinafanya kazi ya kuzuia maji.ambazo ni
i). Matilio zenye asili ya saruji
•Hizi huundwa kwa mchanganyiko wa saruji+Mchanga+Kaolin na polymers
•Hutumika kulinda sehemu za ndani za jengo i.e vyooni,jikoni
•Mfano; Sikacemflex na sikalastic 510
•Badala ya saruji ya kawaida,tumia matilio hizi kujengea marumaru ya chooni au jikoni
ii). Acyrilic coating
•Hutokna na acrylic polymers na hupatikana katika Mfumo wa kimiminika au spray.
•Hufungashwa kwenye ndoo,huwa katika rangi tofauti
•Hupakwa katika paa za zege,hupakwa kwenye kuta za handaki/basement
•Gharama yake ni kubwa
iii). Polyuretherane
•Nayo ni ina asili ya kimiminika na huwekwa kwa kupakwa kama rangia kupulizwa
•Ina dumu zaidi,ila inahitaji utaalam zaidi katika kuwekwa
•Nzuri kwenye nyufa
•XYPEX FCM
iii) Crystalline
Kwenye hii,chemicals huingia ndani ya ukuta au zege na kutengeneza crystals zenye kuzuia maji kupita
•XYPEX PATCH N PLUG
•XYPEX MEGAMIX
iv). Bitumen/Rami
•Ile rami ya kawaida ,ni kizuizi kizuri sana cha maji na majengo mengi ya zamani yametumia hii katika paa zao za zege.
Ukuta wa basement ukifunikwa na MEMBRANE YA RAMI
Baada ya mkanda wa Zege,membrane ya Rami imewekwa ili kuzuia maji yasije kupanda kwenye ukuta
Vitako vya misingi ya nguzo vikiwa vimepakwa Rami
Upakaji wa Acrylic katika paa
Mfumo wa kukusanya maji chini ya ardhi,kukwepesha yasiende kwenye msingi
Nakaribisha Maswali na maoni...
Unachangamoto inayotokana na maji,,tuma picha ili uweze kupata ushauri bila gharama

- Plasta ya ndani unaweza changanya matilio hizi na mortar ya kawaida

- Kuna tambala (membrane ) ya Rami ambapo sikuhizi zinatumika sana kwenye ujenzi
- Huchomwa kwenye paa za zege
- Lakini pia huchomwa kwenye kuta za Basment/handaki
- Kuna Rangi za Bitumen,nazo zipo karibia kila duka la ujenzi,hupakwa kwenye misingi au kuta za parapet za kwenye paa
- Hizi ni maalum kwa ajili ya kuzipa mianya iliyopo kwenye makutano ya fremu za madirisha na ukuta,au fremu na kioo
- asili ya kitu kinachotakiwa kulindwa,kama ni chuma,mbao,tofali
- Gharama : kuna matilio ni gharama sana ,ambapo kwa mjenzi wa kipato kidogo anaweza asimudu
- Upatikanaji : Nje ya Dar,matilio nyingi za ujenzi zinakuwa ngumu kupatikana
- Uwezo wa Fundi/Mjenzi wako
- Kwa Dar,nenda maduka yaliyopo Gerezani
- Maduka ambao ni mawakala wa bidhaa za Sika na Xypex
- Ofisi za nabaki Afrika