Ujasusi wa Kifamilia: Stadi za kazi (Maisha) kwa Watoto

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,895
UJASUSI WA KIFAMILIA; STADI ZA KAZI(MAISHA) KWA WATOTO

Anaandika, Robert Heriel
Jasusi

Wapi tulipotoka, wapi tupo, na wapi tuendako?
Tulikuwa wangapi, tupo wangapi, na tunatarajia tuwe wangapi?
Tulikuwa na nini, tunanini na tunahitaji kuwa na nini hapo baadaye?
Tulifanya nini, tunafanya nini, na yapi tutafanya siku zijazo?
Nini tulitarajia, nini kimetokea, na kipi kitatokea Wakati ujao?

ujasusi pia unahusu Utabiri na ubashiri Kutokana na taarifa zilizokuwepo na zilizopo.
Hesabu ya Kijajusi hazikamiliki Kwa taarifa ya Jana na leo tuu Bali na taarifa ya kesho.
A+B≥C or
A+B≤C

Ikiwa A= Jana(Past),. B= Leo(Present) C=Kesho(Future).
Tunaweza sema Ujasusi wa kifamilia ni kama hesabu za pembetatu ∆ABC ambapo kuna pembe ^A, ^B, na ^C
Line AB~line AB~ line AC kama itakuwa ni pembetatu Pacha. Hii ni kumaanisha ikiwa mtu ataoa au kuolewa katika familia zinazofanana. Mfano familia ya MKE na Mume wote wanahali Sawa za kiuchumi aidha kiutajiri au kiumaskini. Ikiwa Familia hazifanani basi uwezekano wa kutoa matokeo yasiyofanana ni hakika.

A= Wazazi {Past}
B= wanandoa(MKE na Mume) { Presence}
C= Watoto {Future}
Hesabu hiyo ya ujasusi WA kifamilia Ipo Kwa kizazi cha Kwanza mpaka cha tatu.

Ili familia iundwe ambayo kimsingi inabeba muundo wa umbo la pembetatu, lazima Kanuni ya mfanano izingatiwe, mfanano huu unaratibiwa na nguvu ya iitwayo mapenzi. Hisia za mapenzi huwavuta pamoja Watu wanaofanana ili kuunda familia. Hata hivyo kuna familia za Aina mbili kulingana na chanzo chake.

1. Familia yenye asili ya Mapenzi, upendo.
2. Familia yenye Asili ya Sheria (ubinafsi)
Hii ni mada nyingine.

Familia inaundwa Baada ya kila mmoja kutosheka na taarifa za mwenzake. Hapo mmoja ataitwa Mune mwenye majukumu ya utawala na wajibu mkubwa, huku wapili akiitww Mke mwenye majukumu mepesi ya Usaidizi Kwa Mtawala.

1. Ni jukumu la wazazi (MKE na Mume) kujua wanazaa Watoto wangapi, Watoto wa Aina gani,
Kabla Watoto hawajazaliwa lazima Mume na Mke wajiulize Kwa nini wanazaa, wanazaa wakina Nani na idadi Yao.

2. Ni jukumu la Mzazi (mume na Mke) Kufanya Ukusanyaji katika mambo yafuatayo:

I) Ukusanyaji wa taarifa sahihi za muhimu na zitolewe maelezo yenye mantiki. Taarifa za Elimu sahihi, Imani sahihi
Ii) Ukusanyaji wa Mali kama viwanja, mashamba, migodi, misitu, n.k
iii) Taarifa za Historia zilizopita zinazohusu asili Yao, wapi walipo na upi mwelekeo wa Ulimwengu Kwa kizazi kinachokuja. Hii itawasaidia Watoto kujua nini chakufanya, sio Kwa vile Baba alisoma na mtoto asome ilhali mzazi ameshaona Ulimwengu unaokuja hakutakuwa na application ya Elimu ya darasani(huu ni mfano)
iv) Ukusanyaji wa taarifa za kijiografia yenye potential Kwa kizazi kinachokuja.

3. Ni jukumu la Mzazi (Mume na Mke) kujenga jina bora litakalowasaidia Watoto kuheshimiwa. Hivyo mzazi unapaswa ufanye mambo mazuri yenye tija Kwa jamii ili kuipa familia na ukoo utakaouzalisha heshima katika eneo ulilopo.

4. Ni jukumu la Mzazi (Mume na Mke) kuwafundisha Watoto Elimu, maarifa, Imani na kila Aina ya Jambo lenye manufaa linalolenga kumfanya mtoto awe Bora. Unapochagua mwalimu WA kumfundisha mtoto wako Elimu iwe ya kidunia au ya Kiroho lazima huyo Mwalimu umthibitishe kuwa anaviwango na anasifa za kumfundisha mwanao. Sio Kwa vile anapigiwa au kujipa promo mtandaoni au kwenye vyombo vya habari basi unaona huyu ndiye. Na ili umthibitishe mwalimu huyo lazima nawe uwe na uelewa Fulani. Sio unapeleka mtoto shule na unalipia hela nyingi alafu unadhani umemaliza. Nop! Hili ni somo la siku nyingine

5. Ni jukumu la Mzazi (Mume na Mke) kumfundisha mtoto Stadi za Maisha(kazi)
Tayari unataarifa za kutosha, tayari wewe ni mzazi, sasa ni lazima umfundishe mtoto na kumuandaa na Maisha yake kulingana na Jana, Leo na kesho.

Iangalie miaka 20-30 ijayo je nini kitatokea Wakati mtoto wako akiwa na umri huo kutakuwa na Hali gani ya Maisha, vipi Tabia ya nchi, vipi idadi ya Watu, vipi Rasilimali zitakazokuwepo, je mtoto wako anatakiwa afikiri Kwa namna ipi na atende Kwa namna ipi Kwa kiwango gani. Hayo ni mambo ya kuyafikiria sana.

Mambo ambayo ni muhimu ni lazima uhakikishe mtoto wako Akili yake Ipo Flexible na anaweza ku-copy katika mazingira Mbalimbali. Ni lazima umfundishe mtoto wako Kutumia silaha zaidi ya moja, umfundishe mtoto kuishi baharini, angani, na ardhini.

Mambo yafuatayo ni muhimu kumfundisha mwanao:

1. Mfundishe Kujipenda na kupenda wengine.
Na ili MTU awe anaupendo ni lazima awe anapenda Haki na Ukweli. Mwambie apende ukweli na Haki na apende kuutafuta ukweli, na asiamini ukweli unaokuja kirahisi. Ukweli unaokuja kirahisi asiutolee maamuzi.

2. Mfundishe Kujilinda
Alinde Afya yake, Roho yake, Akili yake, hisia zake, na Mwili wake. Hapo lazima umpe Elimu Bora ya kujilinda.
Kisha umfundishe mapigano ya kujilinda ikiwemo Martial arts bila kujali jinsia yake. Mfundishe pia kuogelea.

3. Mfundishe Saikolojia ya jinsi ya kuchangamana na watu pamoja na viumbe wengine.

4. Mfundishe kazi za Mikono, kushona nguo, kujenga mabanda ya kuku, kulima, Kutengeneza Gari, kufuga kuku au mifugo mingine. Ni vizuri mtoto asisomee shule za Boarding ili uweze kuwa naye karibu. Huwezi muandaa mtoto wako Kwa kumkabidhi MTU mwingine zaidi ya miezi na miezi bila ya kumuona. Ni vizuri awe anaenda Asubuhi jioni upo naye.

5. Mfundishe Saikolojia ya Mahusiano ya mapenzi tangu akiwa mchanga. Akiwa mdogo atajifunza kupitia wewe na Mkeo/Mumeo jinsi mnavyoishi. Hivyo ni vizuri kuishi vizuri na Mwenza wako ili Watoto wajifunze, kila mmoja abaki kwenye nafasi yake. Akikua zaidi na umri wa utambuzi ndipo uanze kumfundisha kwa kumwambia namna ya kuishi na Mwenza wake siku atakapoanzisha familia yake. Ni vizuri mafundisho yaende Kwa vitendo Kwa yeye kuona Kutoka kwenu, kuona katika jamii kisha wewe kama mzazi unayatolea uchambuzi.

Hakikisha wewe ndio Reference kuu ya mtoto wako Kwa mambo mengi 90%. Mtoto asijifunze mapenzi mitandaoni au Kwa Watu wa nje, labda kama umeamua kuratibu mchakato huo.

6. Mfundishe mtoto kufanya uchaguzi na maamuzi sahihi. Hiyo atajifunza Kutoka Kwako Wakati akiwa mdogo. Pia utamfundisha Kwa kumpa baadhi ya machaguo yeye kama yeye ili kupima uwezo wake wa kuchagua. Katika uchaguzi lazima umfundishe mtoto mambo ya kuzingatia:

a) Kujiuliza matokeo ya uchaguzi Kabla hajafanya maamuzi.
b) Tija ya uchaguzi je ni Kwa muda mfupi au mrefu?
c) Wakati. Je, Wakati na mazingira yanaruhusu kuchagua chaguo Hilo
d) Urahisi na uwezekano. Je uchaguzi aliouchagua unatekelezeka Kwa Njia rahisi au hautekelezeki?
e) Kuvunja mahusiano na mipango.

Je, uchaguzi wa chaguo Hilo utavunja mipango na hatma yangu, na kuvunja mahusiano niliyonayo na watu wangu muhimu kama wazazi, MKE, Mume na watoto?

Taikon Acha nipumzike SASA. Ikiwa kuna swali Leo mpaka jumapili Ruhusa kuuliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Ntumie no yako nkurushie elf 10 ununue hata bundle leo
 
Back
Top Bottom