Ujasiriamali utotoni: watoto wamenifurahisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujasiriamali utotoni: watoto wamenifurahisha

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by kanyagio, Dec 20, 2011.

 1. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #1
  Dec 20, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  ndugu zangu mim naomba ku-share na ninyi story hii.

  watoto wangu (wana miaka 6 na 4) wamefunga shule . walienda kwa grandparents wakakaa kama wikil mbili. wamerudi Jumamosi. kesho yake jumapili baada ya juice ya Rosella kutengenezwa wakashinikiza watengeneze "Ice creams" kutokana na hiyo juice. waliona jirani wa grandparents wakitengeneza wakadevelop interest na walikuja na vifuko vya kuwekea hizo "ice cream".

  baada ya kutenegeneza na kugandisha kwenye fridge, next step wakaanza kudemand wanataka kwenda kuuza nje ya nyumba. kumbuka ni watoto wa age ya 6 na 4. sisi hatuna hili wana lile kumbe wameweka hizo ice creams kwenye ki-container na wametoka nje kuziuza (ila msichana wa kazi alikuwa anawa-monitor). baada ya muda walikuja wakaniambia kuwa wameuza mbili na nyingine zimeyeyuka. sisi wazazi tulijiuliza maswali na baadae tukagundua mambo yafuatayo:
  • mazingira yana-shape watoto. utegenezaji wa ice cream waliuona kwa bibi yao.
  • upande mmoja tuliona watoto kama wana makosa, lakini baadae tuka-conclude kwamba hawa watoto wakiendelezwa wanaweza kuwa wajasiriamali. hebu imagine kuwa unawekea utaratibu na mfumo mzuri wa biashara ndogo ya ice cream baada ya miaka 10 si wanaweza kuwa mbali (in fact hapa unazingatia kuwa isilete negative impact katika shule). mfano mzuri ni wenzetu wahindi wanavyofundisha watoto wao biashara wakiwa wadogo
  • Zile ice cream ambazo ziliyeyuka hawakuziuza - hii ikatufundisha kuwa wanaweza kutofautisha kitu chenye ubora na kitu kilichoharibika. na haikuishia hapo wali-demand tuwanunulie kifaa cha kuwekea ice-cream zisiyeyuke
  • fedha waliyopata (Tsh 200) walisema wanaitunza.. hii ikatuonyesha kuwa the little amount you get can be saved withought being used rampantly (maana wangeamua kununulia pipi
  kimsingi, sisi wazazi tulifurahi kuwa watoto wanaweza kubuni kitu na kukifanya biashara. ni watu wangapi wanashinda majumbani hata kuingiza Tsh 200 hawawezi.

  incidence hii imenikumbusha Robert Kiyosaki anavyosimulia katika kitabu chake cha Rich Dad , poor Dad jinsi walivyoanza kutengeneza vitu at very very early age
   
 2. Don Mangi

  Don Mangi JF-Expert Member

  #2
  Dec 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,206
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Nice one
   
 3. Vato

  Vato JF-Expert Member

  #3
  Dec 20, 2011
  Joined: Feb 15, 2009
  Messages: 230
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33
  Pongezi nyingi to ur "teen tycoon" would bes.

  Wamepotray quality nyingne ambayo nadhani inapaswa kuitwa "Sustainable Entrepreurship" practice in which ktk kutengeneza bidhaa yao wanajali afya ya mteja wao. Kwanini??

  Huko mitaani wanatengeza average ice cream kwaku2mia chemicals kwa 99%, wanatumia sukari artificial, artificial color na flavour. On the other hand ur little angels wao wametumia Rosella which is a natural product that has myriad of health benefits to a user. This is Innovation.

  On the other hand kwa ku2mia Rosella wame add value kwenye bidhaa yao, kwanini? As i said Rosela ina health benefits nyingi kwa m2miaji so its very obvious customer mwenye uelewa yupo tayari kuinunua at a higher than average ice cream price since atafaidika kwa vingi sio kwa ladha tu.

  Kudos. I wish ningewanunuza hata 1.

  Wakuze ktk moyo huo huo wa uelewa na mapenzi ya biashara.

  Ktk Rich Dad Poor Dad kwenye chapter za mwanzo unakumbuka kuna mahali jamaa alisema (ckumbuki exact words so nita paraphrase)..elimu kuhusu biashara na fedha ni muhmu mtoto kuijua toka udogo, but watoto wengi hawapati elimu hyo na wazazi hawakai chni na watoto wao na kuwapa hyo elimu.

  Watoto huipata elimu hyo kwa uchache sana kwa mfano wanapokuwa mezani wakila wakat wazazi wanajadiliana kuhusu mambo yanayohusiana na fedha nk. So wanaipata elimu hyo accidentaly/ by chance. Nilisoma muda mrefu so i dnt remember vizuri.
   
 4. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #4
  Dec 20, 2011
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  .....Kuza kipaji cha watoto, wanunulie vifaa vya kutengenezea ice cream na kutunzia, kwa sasa wanaweza kutengeneza na kutumia wenyewe sababu umri wao ni mdogo kwa kufanya biashara.

  Vile vile kama inawezekana wewe mwenyewe unaweza kuanza hii biashara, ili watoto waje kuwa wajasiliamali kama wewe.
   
 5. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #5
  Dec 20, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Inabidi uwaendeleze, unaweza wanunulia vitu vidogo vidogo kwa bei ya jumla then ukawakabidhi kama bidhaa zao za kuanzia biashara na wao wakawa wanawauzia hapo nyumbani. Endelea kuwafundisha kufanya saving hata kidogo kwa hela yao ya shule wanayoipata. Kama na wewe ni mjasiriamali wape nafasi watoto wajue biashara yako.
   
 6. M

  Malila JF-Expert Member

  #6
  Dec 20, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Nenda nao vizuri,unaweza ukashangaa wanajisomesha kwa hela zao huko mbeleni. Si ajabu miaka michache ijayo tukaona Kanyagio and sons bakery ltd.
   
 7. RGforever

  RGforever JF-Expert Member

  #7
  Dec 20, 2011
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 6,165
  Likes Received: 1,890
  Trophy Points: 280
  Hili ni Jambo la kawaida sana kwa watoto. Mfano
  -Wakati wa utoto wengi wetu tulikuw tunafanya mambo mengi sana mpaka unashangaa mda ulipata wapi?... Kuna waliofuga Sungura,kuku,njiwa,bata na wakawauza. Msupport tu mtoto wako nae atajisikia furaha sana.
   
 8. Boniface Evarist

  Boniface Evarist JF-Expert Member

  #8
  Dec 21, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 1,100
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Waendeleze kijasiriamali zaidi. Nimejifunza kuwa 2wachunguze watoto na kuwaendeleza kwa interest zao.
   
 9. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #9
  Dec 21, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Next step, how to manage their money!
  Ukianza hiyo kwa umri huo walio nao, litakuwa jambo la maana.
   
 10. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #10
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Familia nyingi za kiafrika zina mapokeo ya mtoto kutompa nafasi ya kujenga ubunifu, bali kumsikiliza mkubwa na kufanya anayoambiwa na wakubwa tu. Hata wanayojifunza mashuleni wakishavika nyumbani hasa vijijini wazazi wakiwaona wanacheza mpira wataambia hapa si shuleni, hayo ni mambo ya shuleni.

  Malezi mazuri na kuwaandaa watoto kwa maisha yao ni vema kusoma mwelekeo wa mtoto katika vipaji vyao, kwani talent zao mara nyingi hujitokeza wangali katika umri mdogo, na hivyo wazazi wanahitaji kukuza talent za watoto. Kutowaruhusu au kupuuzi ni kuua talent zao, na wakisha kua huku wamekosa msukomu na melezi ya kukuza talent zao huwa vigumu kuanza upya wakti wameshazingirwa na mengi yanayotifua na hivyo kukosa mwelekeo sahihi.

  Watu mashuhuri duniani kama hayati King Michael Jackson alianza muziki tangu utotoni, na kama wazazi wake wangempuuzi asingefikiwa uwa gwiji duniani.
   
 11. Tulizo

  Tulizo JF-Expert Member

  #11
  Dec 23, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 849
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Saafi sana..ila inaonekana mkuu unayo challenge ya kuendeleza vipaji na uwezo wa hao watoto.. Ni motisha tosha kwako ku-invest maisha yako kwa watoto na kuachana na porojo za siasa na starehe za kupita...All the best!
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Dec 23, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kanyagio........

  Usiachie hapo, waendeleze;
  1. namna ka kupata fedha kihalali
  2. mjeta anapenda nini
  3. nini faida na hasara za biashara (wasije wakaacha interest na shule)
  4. maana na faida za kuangalia ubora
  5. uaminifu
  6. faida ni nini katika biashara??
  7. hasara ni nini katika biashara
  faida za elimu ili wawe wafanyabiashara wazuri zaidi
   
 13. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #13
  Dec 27, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45

  ahsante sana kwa maoni . wazazi waliowengi hatujachukua muda kuendeleza interest za watoto. ushauri wangu ni kuwa karibu na watoto na kuwaendeleza.

  reading Robert's famous book "Rich Dad, Poor dad" chapter two.. you can compare and contrast ujasiriamali utotoni and Robert case. let me quote some sections:

  At age of 9 yrs:
  "Oh, my God!" my dad said. "You're casting nickels out of lead."
  "That's right," Mike said. "We are doing as you told us to do. We're making money." .......
  " You boys have shown great creativity and original thought. Keep going. I'm really proud of you!" my dad said gently.

  My father was just leaving as I said that. "Boys," he said. "You're only poor if you give up. The most important thing is that you did something. Most people only talk and dream of getting rich. You've done something. I'm very proud of the two of you. I will say it again. Keep going.
  Don't quit." Mike and I stood there in silence. They were nice words.

  jisomee kitabu hiki hapa
  http://www.bachaccountants.co.za/wp-content/uploads/2010/08/RichDadPoorDad.pdf

  haya ndugu, zidi kutafakari!
   
 14. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #14
  Dec 27, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Mkuu linapokuja swala la Entrepreneurship spirt kuna mchango mkubwa sana wa wazazi kufanikisha hilo.
  - Mchango wa wazazi katika kumuandaa mtoto kuja kuwa mjasirimali ni mkubwa sana kuliko hata mchango wa walimu na watu wengine.

  - Kuna msemo wa samaki mkunje angali mbichi, sasa huku kwetu tumekuwa tukifundishwa ujasiriamli uzeeni mtu ameisha fanya kazi amechoka sasa ndo anaanza kufundishwa ujasiriamli, hii ni kosa kubwa sana.

  - ILI MTOTO AJE KUWA MJASIRIMALI MZURI KUNA MCHANGO KUTOKA KWA MAKUNDI YAFUATAYO

  1. WAZAZI.
  - Wazazi wanatakiwa waandae mtoto kuja kuwa mfanya biashara mzuri sana, kivipi wamuandae? Watamuandaa kupitia mafundisho wanayo mpa mtoto, mara nyingi wazazi wamekuwa wakimsisitizia mtoto asome aje kuwa Dactari, Meneja, Mkurugenzi au asome aje kufanya kai nzuri.
  - Mtoto hukuwa akiamini kwamba anasoma aje kufanya kazi nzuri so aje kuwa na maisha mazuri na husoma akitageti kufanya kazi, benk, bandarini, TRA, na kwenye mashirika makubwa ya uma.
  - Hapa mtoto akija kukua mawazo yote yako kwenye kuajiriwa na si kujiajiri.

  2, WALIMU, MASHULENI NA VYUONI
  - Walimu nao wamekuwa mabingwa wa kusisitiza watoto wasome waje kufanya kazi kwenye mashirika na tasisi kubwa sana na ukifuatilia utaona hakuna mwalimu hata mmoja anae wasisitizia wanafunzi wasome waje kuanzisha miradi au wasome waje kuwa wajasiriamli na wawajiri watu wengine.
  - Walimu inatakiwa wawajenge watoto katika mfumo wa kujitegemea, wawasisitizie kwamba wanatakiwa wasome waje kuwa wafanya biashara na walipa kodo wakubwa nchi hii

  3. SERIKALI YETU,
  - Ina mchango mkubwa sana katika kuwaandaa watoto kuja kuwa wafanya biashara wakubwa hapa ni kupitia sera za Elimu pamoja na sera za kujiajiri kwa wano maliza shule na vyuo mbalimbali

  4. MARAFIKI MBALIMBALI
  - Marafiki nao wana mchango mkubwa sana, Hapa mtoto akiwa na marafiki wenye muelekeo wa kuwa wafanya kazi na yeye ni razima awe mfanya kazi au aajiriwe, Mtoto tangia akiwa shule ya msingi, sekondary na hata chuo, akiwa na marafiki ambao hata wao maswala ya kujiajiri ndo kipa umbele na yeye hapa ni razima awafuate.
   
 15. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #15
  Dec 29, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  I know a secret which, if fully understood by our government, business, and community leaders, could have enormous positive implications for the future of our society. Simply put, the secret is this: Youth born into poverty develop special gifts that prepare them for business formation and wealth creation. They are mentally strong, resilient, and full of chutzpah.

  They are sceptical of hierarchies and the status quo. They are long-suffering in the face of adversity. They are comfortable with risk and uncertainty. They know how to deal with stress and conflict. These are the attitudes and abilities that make them ideally suited for breaking out of the cycle of dependency that so often comes with poverty, ideally suited for getting ahead in the marketplace. In short, youth from low-income communities have "street smarts," or what we call "business smarts." Precisely because of their background - that is, because of their experience surviving in a challenging world - they are able to perceive and pursue short-lived opportunities that others, more content with their lot in life, can easily miss

  We need to equip today's aspiring entrepreneurs (like your childrens) with every tool possible to succeed. That means making sure they receive a strong financial education that prepares them for the unique challenges and opportunities of the 21st century. A solid background in finance and business skills will help the next generation to compete and succeed.
   
 16. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #16
  Dec 29, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Entrepreneur na KOMANDOO na MTM mmetoa michango imenifurahisha sana. we all agree that external inflluences has impact on the entrepreneurial successes at early age.
  i like your posts guys!!
   
 17. M

  Masikini mjanja Senior Member

  #17
  Nov 26, 2017
  Joined: Oct 13, 2017
  Messages: 152
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 60
  Very nice
   
Loading...