Ujasiriamali ndani ya Mabasi ya Abiria!

Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
48,281
53,247
Salaam wana JF wote. Jana nilikuwa safarini toka Kahama kuja Dar ndani ya basi,akapanda kijana na kunadi biashara zake ambazo ni sabuni yakuogea Dalin,dawa ya meno ya Alovera,sabuni ya Kaisiki maluum kwa wanawake. Hoja yangu wakuu hapa naomba kujuza kuhusu sabuni Dalin eti inaleta hamu ya kuoga maana mjasiriamali aliinadi akadai lazima usiiache bafuni bilakufunga. Pili kuhusu sabuni Kaisiki maalum kwa wanawake eti inasafisha sehemu nyeti, Sasa hapo kuna ukweli wowote au ni swaga za ujasiriamali ili mteja anunue tu?
 
mfumo wetu wa biashara unaharibika kadri siku zinavyokwenda, wengi wamamua kuwa wezi/matapeli na serikali inakaa kimya kwa kuwa na viongozi wetu nao ni wa jinsi hiyo. Huwa nachukizwa sana na tabia ya hawa wanaojiita wajasiriamali kufanya biashara ndani ya vyombo vya usafiri, hivi hii ipo duniani kote au ni bongo tu, nisijekuwa nashangaa mambo ambayo ndio mfumo unaotumika duniani kote. Isitoshe hawa wanaofanya biashara hizi hawapatiwi mafunzo juu ya maelezo ya bidhaa husika, kigezo pale ni utaalamu wako wa kupiga soga. Huu ujasiriamali wa kuwa wachuuzi ninashindwa kuielewa sera hii, nilifikiri ujasiriamali ilikuwa ni ujasri katika kuzalisha mali, sasa ni ujasiri katika kufanya usanii......!!!????
 
Wanakwepa kulipa kodi. Sasahivi kila gari la mkoani lazima apande mmoja au wawili halafu wana ile namna yao ya kuongea huwa inanikera. Mi nakushauri ununue hizo products zao ndio utapata majibu kama ni za kweli au lah.
 
Ujasiriamali hata kwenye ndege unafanyika. Tatizo ni mode wanayotumia ya kupiga tumba. Usiombe mjasiria pesa akawa ana njaa afu kasimama pembeni yako! Utaoga harufu ya kinywa n mate, ukishushia na kajasho kake. Ingependeza wangegawa gazeti ama picha na bei ya bishaa watu wajichagulie kuliko data za uongo na stori kibao!
 
Wanakwepa kulipa kodi. Sasahivi kila gari la mkoani lazima apande mmoja au wawili halafu wana ile namna yao ya kuongea huwa inanikera. Mi nakushauri ununue hizo products zao ndio utapata majibu kama ni za kweli au lah.

Mmh hapo ndipo kwenye mtihani,kuna jamaa yangu Arusha ana meno ya dhahabu sasa miaka miwili ilipita aliuziwa dawa ya meno ili yawe meupe cha ajabu. Alitumia dawa lakini meno hayakuwa meupe kama matarajio yake.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom