Ujana ni kama Moshi, ukitoka haurudi; Maendeleo ya taifa letu yanahitaji watu na watu wenyewe ni vijana

Sifael Mpollo

Member
Jan 20, 2018
24
34
Na. Sifael Essau Mpollo.

Rais wa 32 wa Marekani Franklin Delano Roosevelt aliwahi kusema “We cannot always build a future for our youth, but we can always build our youth for the future.” Kwa tafsiri isiyo rasmi katika Kiswahili ni kwamba "Siku zote hatuwezi kujenga mustakabali wa vijana wetu lakini tunaweza kuwajenga vijana wetu kwa siku zijazo."

Vijana ni watu wenye ufahamu, vipaji, nguvu, uthubutu na wenye kutambua jema na baya. Katika karne ya ishirini na moja vijana ni rasilimali kubwa zaidi kwa sababu wanatoa msukumo wa kuleta mageuzi ya kijamii, kiuchumi na kisiasa. Taifa lolote duniani linajengwa na nguvu kubwa ya vijana kwa sababu ndiyo kundi kubwa na pana katika shughuli za kila siku za binadamu.

Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 1996 imetoa fasili ya vijana kuwa ni kundi la watu wenye umri kati ya miaka 15 – 35 na kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kupitia Sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012 asilimia ya vijana wenye umri wa 15 hadi 35 ni 35.1%. Mbali na kuwa kundi hili ni nguvu kazi ya taifa limekuwa likutupiwa lawama nyingi kuwa vijana wengi hawajitambui, wakorofi, hawaaminiki, wanagombana wao kwa wao na wakipewa nafasi za uongozi hawazitendei haki hivyo kuendelea kukosa imani.

Ukiangalia shughuli ndogondogo za uchumi, masuala ya siasa, sheria, utawala na kadhalika utaona idadi kubwa ya watu waliopo huko ni vijana. Ukweli vijana hawa wanaweza na wanajituma kwa hali na mali ijapokuwa kundi hili linakabiliwa na changamoto kadhaa zikiwamo ukosefu wa malezi, ajira, mitaji, maarifa/taarifa sahihi na ujuzi stahiki; vijana hawa wanapokosa hayo ni dhahiri taifa linakuwa la kuyumbayumba kwa sababu linaweka mategemeo makubwa ya kupata maendeleo yake katika kundi ambalo halijaandaliwa.

Vijana wanatakiwa kupewa misingi mizuri ya malezi, uongozi, elimu na ukakamavu ili wawe wachapakazi, wenye weledi na uwezo mkubwa wa kufanya kazi bila kusukumwa. Ni muhimu kuwaandaa vijana kuwa viongozi, watoa maamuzi, wajasiriamali, wazazi na walezi kwa sababu wana nafasi muhimu ya kuchukua katika maendeleo ya jamii na uchumi wa taifa letu na malezi ya vijana yanaanzia nyumbani ndani ya familia.

Wazazi, Serikali na asasi za kiraia fanyeni kila linalowezekana kuwawezesha vijana wa Tanzania kwa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili ili waweze kushiriki kwa vitendo katika maendeleo ya taifa kwa sababu vijana ndiyo walioshika hatamu ya kujenga elimu bora, uchumi imara, uongozi na utawala makini. Lakini vijana ili kuweza kufikia malengo ni lazima kushirikiana kwa sababu Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.

Vijana ndiyo nguvu kazi ya taifa unapokuwa kijana unapaswa kutumia nguvu ulizonazo ili kujiletea maendeleo yako binafsi, jamii inayokuzunguka na taifa kwa sababu ujana huenda haraka na hutokomea kama moshi pasipo na kuridhia na ukitoka kamwe haurudi.

Maendeleo ya taifa letu yanahitaji watu na watu wenyewe ni vijana.

IMG_1568-min.JPG
 
UCHAWA ndio mpango mzima
 
Safi Sana👍
 
Back
Top Bottom