Moshi: Ulevi umekithiri, vijana washindwa kuwapa mimba wenza wao

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,753
15,227
Mkuu wa wilaya ya Moshi, Zephania Sumaye amesema atatangaza operesheni maalumu ya siku 21 kupambana na unywaji wa pombe ovyo uliopelekea vijana wengi waliofikia umri wa kuoa kushindwa kuoa na hata walioa kushindwa kuwapa mimba wake zao maana hawajiwezi kabisa kitandani kutokana na ulevi uliopitiliza!

Naye Padri wa kanisa Katoliki amesema ubatizaji watoto kwenye wilaya hiyo umeshuka kutoka watoto 100 hadi wanane kwa mwaka, na kuna muda mwingine wanakosa kabisa watoto wa kubatiza!.

Padri Vumilia amesema kuwa "Kumekuwepo na changamoto baada ya jamii kuporomoka katika malezi na maadili hata katika suala la uzao nalo limepungua sana, limeathiri sana hata katika wale watoto wanaoingia katika malezi ngazi za mafundisho kwa upande wa wakatoliki, mafundisho ya komunio ya kwanza na kipaimara idadi yao imeshuka sana.

"Jumatatu ya pasaka tunategemea kubatiza, imekuwa ni tofauti na siku za nyuma tulikuwa tuna batiza watoto 100 lakini kwa kipindi hiki tunabatiza watoto wanane pekee

Imefika mahali jamii imeshindwa kujitawala kwa sababu tunaishi katika ulimwengu ambao ni huru sana, pombe zimekuwa zikipatikana katika maeneo mbalimbali, jamii ijifunze kujijengea nidhamu, wale walioaminiwa na kupewa dhamana ya uongozi katika jamii, wajifunze kutekeleza wajibu wao, kama kuna taratibu za kutoa huduma ya pombe basi zitolea katika taratibu zile ambazo zinatakiw
a”
 
Mmh!

Kwa hiyo hawagongi?
Visungura vinakufanya uwe mkali, jasiri kwa sura na uonekane sura kavu ambayo unaweza kumpiga mtu mkwara au kumtishia mtu yeyote na akatishika, lakini ukweli ni kwamba ukipigwa kofi moja tu unaweza kata moto kabisaaaa, coz viongo vyote vya mwilini mpaka huko chini ni legevu na completely useless 🐒
 
visungura vinakufanya uwe mkali, jasiri kwa sura na uonekane sura kavu ambayo unaweza kumpiga mtu mkwara au kumtishia mtu yeyote na akatishika, lakini ukweli ni kwamba ukipigwa kofi moja tu unaweza kata moto kabisaaaa, coz viongo vyote vya mwilini mpaka huko chini ni legevu na completely useless
Hapa umenena kweli kabisaa. Watumiaji wa hicho kinywaji wanatisha kwa muonekano wallah.
 
Back
Top Bottom