Uingereza: Waziri Mkuu Boris Johnson ajiuzulu rasmi

Watanzania wengi lugha ya kiingereza inawatesa sana mpaka wanafikiria sababu zilizopelekea Boris Johnson kujiuzulu ni vita vya Russia na Ukraine wakati Uingereza haipigani hivyo vita.
Kama huna uwezo wa kufikiria lazima useme hivyo huoni uchumi umetikisika,mfumuko wa bei,gesi imepanda bei.uingereza haipigani hiyo Vita lakini inatumia resources zake nyingi mpaka nchi inafilisika proNato mnafikiria Kwa nini?

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Ni upuuzi na uphaller wa kiwango cha juu kumpa Urusi credit katika hili.
Huyu Boris ameanza kupitia misuko suko kuanzia kipindi cha korona hili ni hitimisho tu.

Kwa taarifa yako toka mwaka 1750 ni waziziri mkui mmoja pekee ameongoza kwa miaka 20 akifuatiwa na Thatcher kwa miaka 11, Blair kwa 10 na waliosalia ni miaka 6, 5, 4, 3, 2, 1 na wengine ni siku chache tu.

Tangu cheo cha waziri mkuu kianze Uingereza imrkuwa na zaidi ya Ma waziri wakuu zaidi ya 77 na huwa wanakaa kwa muda mfupi.

Hii tabia ya kusifia kila ujinga na kumhusisha Putin ni akili ndogo za ccm ambazo mtu hata akila nyama anamsifia Samia.
Sie hatuangalii alikojikwalia, tunaangalia alikojibwaga. Mshikwa na ngozi...
 
Litaathir alikuwa mstari wa mbele Sana kumkabili kibabu Putin
Asisahau kwamba ndiye kiongozi pekee mkubwa aliyeitembelea Ukraine kwenye mstari wa mbele vitani. Ikumbukwe kwamba Boris Johnson ana cheo kingine cha Waziri Mkuu, au tuseme Kiranja Mkuu, wa NATO. Rais JB, PM ni BJ.
 
Uk sio Tanzania, hata ajaye lazima atafuata sera za nchi yake na za kimataifa kama kawaida.
Wajibu wa uk kwa NATO sio matakwa ya mtu mmoja wala chama bali nchi.
Amebadilishwa mtu na sio sera.

Tuhuma nyungi na mbaya zilizomgharimu ni tabia yake binafsi.
Usichokijua ni kwamba UK raia wengi sana wanavichukia vita vya Ukraine. Na msukumo mkubwa wa kuhamasisha vita hivi ulitokana na ushawishi wa Boris Johnson--bila kutaja unufaikaji mkubwa ambao amejipatia yeye binafsi.

Wasichotaka kukwambia Waingereza ni kwamba hawapendi Marekani na dunia ijue sababu halisi (kuitumbikiza UK katika vita proxy vya Ukraine na kupoteza fedha, mali, silaha, na uchumi kuporomoka)--kwa sababu wanaamini ikiwekwa public, ni sawa na kumpatia Putin ushindi wa mezani.

In short, Putin ndiye sababu kubwa ya kung'olewa kwa Boris Johnson. Mengine yaliyobaki ni nyongeza tu.
 
Kuwa challenged na maoni ya mihemko ni jambo la kawaida ila kuna wakati inafika mahala ushabiki unaenda overboard. Kujiudhulu kwa viongozi wakuu inchini uingereza ni jambo la kawaida sana na imetokea mara nyingi. Issue za ukraine sio personal wenzetu hawana huo ujinga lazima bunge likae kujadili kuona kama inafaa. Nenda kupitie maoni ya wahusika wenyewe utajionea utofauti na Sisi tunaojifanya wajuaji.
Mbona unateseka unajieleza saana kubali mwamba Putin ndo mume wenu

Sent from my TECNO K9 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom