Uingereza Soka Sasa Mtandaoni.

Junius

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
3,181
139
Pambano la kutafuta nafasi ya kucheza fainali za kombe la dunia siku ya Jumamosi England itakapocheza nchini Ukraine litaoneshwa kupitia mtandaoni kwa watakaolipia tu angalo paundi 4.99.
Awali michezo yote ya England ilikuwa ikioneshwa kupitia Televisheni.
Kentaro ambalo ni shirika la wakala la kimataifa lililoteuliwa na Shirikisho la soka la Ukraine, awali liliuza haki za kuonesha mechi kwa kampuni Uingereza Setanta.
Lakini baada ya Setanta kilichokuwa kituo cha televisheni cha kulipia kufilisika, wakateuliwa wataalam wengine wa kuonesha michezo kwenye mtandao.
Mchezo huo utaoneshwa katika mtandao wa www.ukrainevengland.com na watazamaji watanunua haki ya kuona wakitumia PayPal, mtandao wa malipo kwa njia ya kisasa.
SOURCE:IDHAA YA KISW. BBC LONDON
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom