Uhusiano wa namba hizi na majini,Shetani ....

Uhusiano wa namba hizi na majini,Shetani ....

Hahahaha.

Unachosema hapa ni swa na mtu kusema "kwa kuwa umesema kwamba hujui square root ya mbili ni nini, jibu lake ni nane".

Ukweli kwamba mimi sijui square root ya mbili ni nini haumaanishi jibu lako lolote lile ni sahihi.

Inabidi utuonyeshe jibu lako limepatikanaje.

Isitoshe, naweza kuwa sijui square root ya mbili ni nini, lakini nikajua kwamba jibu lazima liwe dogo kuliko mbili, na hivyo ukinipa jibu la namba nane, nitajua si jibu sahihi, hata kama sijui jibu sahihi ni lipi.

Sasa niambie, unajuaje kwamba mungu yupo?

Unaweza kuthibitisha?
Unataka vithibitisho vipi?
 
Okey....nimekupata, ila kumbuka sio suala la kuenda maabara na kurudi na majibu? Unakubaliana na hilo suala?
 
hizo nahisi kweli si zakawaida kwan tulishawahi kuzipiga tukiwa sec na tulijibiwa hivi ninyi wanafunzia acheni kutusumbua na tukiwafuata hapo mtakiona cha moto kwa kweli tulijiuliza maswali mengi sana kwan walijuaje sis ni wanafunzi
 
Wapi nimesema kwamba nataka mungu atuumbe kama maroboti?

Na unaweza vipi kunibishia nikikwambia kwamba, kama unaamini mungu yupo, ama kama unaamini mungu wa Biblia/Quran au mungu yeyote, na mungu huyu ndiye aliyeumba dunia na viumbe vyake, basi mungu huyu kaumba viumbe vyake viwe vinaenda kama ma robot yaliyokuwa programmed?

For starters, waamini wanasema mungu anajua yote. Alijua mambo yote yatakavyokuwa kabla hayajawa.

Maana yake, alijua mtu mwizi atakuwa mwizi kabla huyo mtu mwizi hajazaliwa.

Na kwa sababu mungu ujuzi wake hauna makosa, akishajua ni kama na kwamba kapanga.Ujuzi wake si kama utabiri wa hali ya hewa kwamba anaweza kujua itanyesha mvua halafu isinyeshe.

Sasa mungu akijua kwamba fulani atazaliwa na kuwa mwizi, huyo fulani anaweza kubadili hilo alilolijua mungu?

Zaidi ya hapo, wewe unaweza kurudi nyuma katika muda?

Kama huwezi, huoni kuwa tayari ushakuwa programmed kwamba uweze kwenda mbele tu katika muda na usiweze kurudi nyuma?

Kujua ni kupanga?
 
Soma nilichokiquote ambacho ni maandiko yako mwenyewe!

Kwa mjuzi wa yote na muweza yote hakuna tofauti ya kujua na kupanga.

Kama kuna tofauti, basi si mjuzi wa yote na muweza yote.

Mwanadamu ambaye maisha yake yashaonwa yatakavyokuwa na mungu kabla mwanadamu huyo hajazaliwa, na mungu huyu by definition hawezi kukosea, alichokiona lazima kiwe, kwa huyu mwanadamu, anawezaje kubadili kile kilichoonwa na mungu?

Akibadili atakuwa ana m prove mungu kuwa wrong.

Na mungu wako hawezi kuwa wrong, kwa sababu anajua yote.

Huqezi kuwa na mungu anayejua yote halafu ukabakia na mwanadamu mwenye uhuru wa kuchagua.
 
nyingine ni hii hapa 0758278962 iliwai kunipigia saa nane usku nikakuta misscall asubui kuipigia ikawa haipokelewi nilivyoichunguza kwenye mpesa nilitaka kuzimia

Nasikia mwenye hiyo namba ni KING FREEMASON! Vipi ndo jina lililotokea?
 
Kwa mjuzi wa yote na muweza yote hakuna tofauti ya kujua na kupanga.

Kama kuna tofauti, basi si mjuzi wa yote na muweza yote.

Mwanadamu ambaye maisha yake yashaonwa yatakavyokuwa na mungu kabla mwanadamu huyo hajazaliwa, na mungu huyu by definition hawezi kukosea, alichokiona lazima kiwe, kwa huyu mwanadamu, anawezaje kubadili kile kilichoonwa na mungu?

Akibadili atakuwa ana m prove mungu kuwa wrong.

Na mungu wako hawezi kuwa wrong, kwa sababu anajua yote.

Huqezi kuwa na mungu anayejua yote halafu ukabakia na mwanadamu mwenye uhuru wa kuchagua.

Umerudia maelezo yale yale ambayo yalizaa swali ambao nilikuuliza na kwasababu hiyo hujalijibu

Sijasema kuwa Mungu hajui bali nakubaliana na wewe kuwa iko hivyo,sasa ndio nakuuliza kuwa kujua ni kupanga?

Yaani kitendo cha kujua hatma ya kitu au jambo ndio utakuwa umepanga?
 
Kwa binadamu asiye na ujuzi wote na uwezo wote, kujua si kupanga.

Kwa mungu mwenye ujuzi wote na uwezo wote, kujua ni kupanga.

Think about it.

Mungu kajua mwizi ataiba siku ya mwaka mpya 2015. Kabla ulimwengu haujaumbwa.

Wizi hauwezi kutokea bila kupangwa.

Alichokijua mungu ni lazima kitokee, kwa sababu ujuzi wake hauna makosa.

Mwizi akiiba siku ya mwaka mpya 2015, nani kapanga wizi huu?
 
Mungu anauwezo wa kujua kama kuwa wewe utaenda kujisaidia haja kubwa baada ya masaa mawili,swali la msingi hapa ni kuwa amejuaje?

Mungu anajua kwasababu anaweza akasafiri hadi future kisha akarudi present muda huo huo yaani anaweza akaona mwisho kuanzia mwanzo,sasa basi kile ambacho Mungu anakijua ni kile ambacho kitatokea kiuhalisia lakini hii haina maana kuwa amepanga

Wewe ndio utapanga kuwa utajisaidia baada ya masaa mawili na sio Mungu,Mungu yeye amejua tu kile ambacho wewe utakifanya na ndio maana huwa anatoa taarifa kuwa kuna hiki na hiki kitatokea

Matukio ya maisha yetu anayajua lakini ni kwasababu tu ana uwezo wa kujua kabla hatujatenda na kwa maana hiyo anajua wewe utaishia kufanya nini kwenye maisha yako,hii ni kama vile unaangalia muvi ambayo tayari umeshaiona!
 
Back
Top Bottom