Uhusiano wa namba hizi na majini,Shetani ....

Uhusiano wa namba hizi na majini,Shetani ....

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
28,259
Reaction score
20,919
Wakuu,

Sina kawaida ya kudharau jambo hata kama linaonekana ni la kijinga na nimeshapata faida kubwa kutokana na mtazamo wangu huu,nimeshafanikiwa kwenye mambo mengi ambayo watu waliyaona ni ya kijinga na wengine walijifunza kupitia hili

Leo naomba niwashirikishe jambo hili ambalo ni mewauliza watu kadhaa na wameonekana kunishangaa mtu kama mimi ni kwanini hasa nimeamua kulifuatilia hili,lakini najua kupitia hili naweza kujifunza kitu ambac ho sikua nakijua au nikajikuta napoteza muda wangu,yote haya ni matokeo na nimejiandaa kwa yote

Kuna namba watu wamekuwa wakidai kuwa kama unataka kuzungumza na Shetani au majini basi unaweza kuzipiga,kuna jamaa yangu aliwahi kuzipiga nikiwa nae na simu iliita na ikapokelewa halafu aliulizwa shida yake na alisema lakini aliepokea simu alimuambia kuwa "huwezi wewe na usitusumbue"

Kuna jamaa yangu mwingine alipiga nae simu ilipokelewa na aliambiwa kuwa wapo busy hivyo hawahitaji usumbufu

Ukiangalia namba hizi hazina namba kiunganishi ili ujue hata location ya namba hizi,kitu hiki kimenifanya nijiulize sana kama hii inakubalila kwa mamlaka husika za mawasiliano

Sina ufahamu hasa wa mambo ya mawasiliano na nadhani hapa kuna watu wengi wanaweza kunipa maelezo ya kutosha na nikaridhika kuhusiana na dhana hii kuwa namba hizi ukipiga unazungumza na shetani au majini,sidhani kama jambo hili halina maelezo kwa wale ambao wanajua kuhusu mawasiliano na ndio maana nikaamua kuja kuuliza hapa ili jambo hili niachane nalo

Namba zenyewe ni 11111111111 na 999999999 nadhani zipo na zingine,hebu wakuu nisaidieni hapo ili niweze kujua

Nikwanini hakuna namba kiunganishi lakini simu inaita?
Je ni akina nani wanaopokea simu hizi?

Karibuni ....

Mkuu juve2012 hebu sogea pan de hizi tuendelee kujifunza mambo haya,karibuni na wengine pia .....!!
 
Last edited by a moderator:
nikae makoa wa kujua... mbona namba ipo bussy hiyo ya 1111111111 ial ya 99999999 hawaijui
 
Katika Stori za mtaani nishawahi kusikia kitu kama hicho, ila sijawahi kujipa muda kufatilia.
 
Mmmh aisee jaman hao viumbe achananeni nao wanajua wanachokifanya hebu subiri nipige
 
Mkuu Eiyer kwa uelewa wangu izo ni namba za polis na si shetan mkuu
 
Last edited by a moderator:
Mi nlishawahi kupiga ikaita hadi ikakata

Sasa jamaa yangu alipiga wakapokea na aliweka laudi spika na walimuambia kama nilivyosema hapo juu

Ngoja tusubiri wajuzi waje watupe maelekezo maana inawezekana ikawa kutokujua kwetu ndio kunatufanya tuhusishe na masuala haya ya mashetani na majini!
 
Mkuu Eiyer kwa uelewa wangu izo ni namba za polis na si shetan mkuu

Polisi wa nchi gani?

Umesoma hicho kisa cha jamaa yangu hapo juu?

Kama ni polisi iweje wamjibu vile?
 
Sasa jamaa yangu alipiga wakapokea na aliweka laudi spika na walimuambia kama nilivyosema hapo juu

Ngoja tusubiri wajuzi waje watupe maelekezo maana inawezekana ikawa kutokujua kwetu ndio kunatufanya tuhusishe na masuala haya ya mashetani na majini!

Mi siku yenyewe nliyopiga nlikuwa natetemeka nashukuru hawakupokea maana nlikuwa naogopa kujiingiza kwenye maagano ambayo ntashindwa kutoka
 
Back
Top Bottom