Uhusiano kati ya kiu ya maji na mauti

Uhusiano kati ya kiu ya maji na mauti

KIIMANI:
Roho ya mtu inapoacha mwili huwa Mara nyingi haitaki mtu ashuhudie hivyo anapokutuma kalete hiki au kile(Mara nyingi huwa maji) ni njia/janja ya kukutoa ili uhai umtoke. Ndo maana mara nyingi unapokuwa unarud ndio utakuta anamalizikia kukata roho!.
ILA KWELI!
 
Tunataka ushahidi wa kusayansi.achana na mambo ya dini, ni mambo ya kudumaza ubongo kupokea bila kuhoji wala kuthibitisha ukweli wa jambo.
Sijakushikia fimbo wala bunduki ili uamini, na wala mleta mada hakutaka proof za kisayansi, mimi nimesema vile imani yangu inavyoamini, wewe baki na sayansi yako mimi nabaki na imani yangu.. Very simple kiongozi.

Kudumaa akili huo ni ubwege mtozeni wa mtu, mimi naamin katika quraan na mtume kwa maana vimeongelewa vitu vya kweli kabla sayansi haijathibitisha na baadae ikaja kuthibitisha ukweli juu ya hayo, sasa ni vipi nisiamini!?

Ni kawaida hatuwezi kuwa upande mmoja lazima tutofautiane, kifikra, kimawazo, kimaono n.k, ila si kulazimishana tu awe kule ulipo,

Siku njema kiongozi.
 
Kwa elimu ndogo niliyonayo wacha nishare nanyi.

Tuanze na umauti, mtu alimuuliza mtume muhammad(s.a.w) kuhusu uchungu wa umauti unakoje ama unafananaje.. Jibu alisema ni sawa na mtu uchunwe ngozi kuanzia unyayo mpaka utosini, na machungu haya aliyafananisha kwa mbali hakusema ni sawa sawa ila kwa mbali, yanausogelea uchungu wa umauti kwa mbali, kwahyo maana yake ni zaidi ya hapo.
Sasa kama ukijikwaa ukachunika ngozi ikabaki kidogo wakati unaimalizia ukakosea ukaichuna mpaka ile ambayo haijafa ganzi, au kuna vile vigozi viotavyo katika kidole ukikosea kuvichuna nadhani sote tunajua balaa lake, sasa maumivu hayo ndio uyapate kuanzia unyayoni mpaka utosini na hapo ni maumivu ya mbali sio halisi..

Katika umauti imeelezwa mtu anapata kiu isiyoelezeka, hata akapewa maji ya ulimwengu mzima hayawezi kukata kiu hiyo.
Aiseee
 
Aisee Dada Jirani yangu alifanyiwa operation Kujifungua ... Akahitaji Maji Kasema kiu Sana aisee ... Akapewa Hali ikabadilika ....R.I.P

Mtoto wake now days anatimiza 1 year [emoji31][emoji31]
Masikini rip huyo mdada Mungu azidi kumkuza huyo mtoto
 
Sijakushikia fimbo wala bunduki ili uamini, na wala mleta mada hakutaka proof za kisayansi, mimi nimesema vile imani yangu inavyoamini, wewe baki na sayansi yako mimi nabaki na imani yangu.. Very simple kiongozi.

Kudumaa akili huo ni ubwege mtozeni wa mtu, mimi naamin katika quraan na mtume kwa maana vimeongelewa vitu vya kweli kabla sayansi haijathibitisha na baadae ikaja kuthibitisha ukweli juu ya hayo, sasa ni vipi nisiamini!?

Ni kawaida hatuwezi kuwa upande mmoja lazima tutofautiane, kifikra, kimawazo, kimaono n.k, ila si kulazimishana tu awe kule ulipo,

Siku njema kiongozi.
Mbona km umehemka.Unaamini au umekaririshwa na hivyo vitabu? Mtu mvivu wa kufikiri siku zote yeye majibu yake ni biblia na kuran.
 
Mbona km umehemka.Unaamini au umekaririshwa na hivyo vitabu? Mtu mvivu wa kufikiri siku zote yeye majibu yake ni biblia na kuran.
Mimi na wewe nani aliyehemka sasa, nioneshe sehemu nimehemka, nimekushauri tu kama huamini ninachokiamini huwezi kunifanya nikuaminishe kwa njia unayoamin wewe, simple n clear, baki unapoona salama nami nabaki ninapoona sahihi.. Mengine yatajulikana mbele ya safari..

Siku njema kiongozi.
 
Mungu atupe mwisho mwema jamani ninavyoogopa kufa mm yaani nikifikilia kufa nawaza sipati jibu
Amin rabilallamin shunie akee!!

Haina haja ya kuogopa kifo hali ya kuwa hakikwepeki, muhimiu ni maandalizi kwa kufanya amali njema, tujitahidi mnoo kutenda mema shunie akee.
 
Lakin mmeongelea kiimani suala la kuomba maji kabla ya kifo .......je ki biologia chanzo ni nini hasa ...kwa wataalamu wa mambo haya ebu watuelekeze kidg
 
yaan huyo ndie mtenda mema.. sas hao watenda madhambi.. sijui inakuwaje.. TUOMBE mwisho mwema INSHAALLAH...
Al' insaan ni hili jumba la mwili ni mwili wenyewe yaani. Roho elimu yake ipo kwa Mungu ila kuvishwa ndani ya mwili wa binadamu elimu hiyo tumepewa. Katika haya matabaka ya ngozi ya mwili wa binadamu ndipo roho ilipovikwa. Leta taswira katika hilo utokaji wake( roho) utakuaje?! Inavutwa kwa kunyofolewa, inachunwa katika hizo tabaka za ngozi hali ya kuwa upo hai katika hali ya kukielekea kifo.

Kwa mja mwema, bila shaka ni suratul nnaziati aya ya i na ii inaelezea jinsi Malaika wanaotoa roho za waja wema na Malaika wanaotoa roho za waja wasiyo wema. Ila sakaratul maut ni haki kwa kila mtu kuionja licha ya watu kufa kwa vifo vya namna tofauti tofauti na kuchunwa roho ni kwa kila mtu aliye mwema na asiye mwema utofauti unakuja katika hali ile ya uchunwaji na utolewaji wake.

Waallahu Aalam.
 
Mimi na wewe nani . aliyehemka sasa, nioneshe sehemu nimehemka, nimekushauri tu kama huamini ninachokiamini huwezi kunifanya nikuaminishe kwa njia unayoamin wewe, simple n clear, baki unapoona salama nami nabaki ninapoona sahihi.. Mengine yatajulikana mbele ya safari..

Siku njema kiongozi.
Hakuna mahali wala mstari au neno nimelitumia kukulazimisha hoja yangu.nilichoandika ni mtazamo wangu. Hoja za kidini siyo measurable, siyo testable, hazina logical consistent, zina self contradictions na siyo repeatable
 
Though hatuwezi kuwa na jibu kulingana na experience but we can think about it kufwatana na uelewa, imani n.k, kama kichwa kinavyoeleza si kitu kigeni masikioni mwako au pengine umewahi kushuhudia mwenyewe baadhi ya wagonjwa dakika za mwisho kabla ya umauti kuwafika huwatuma watu wanaowauguza kuwachukulia maji ya kunywa though wengi wao huwa hata hawafanikiwi kuyanywa yale maji, process ya mpaka mtu kutokwa na roho inaambatana na energy kubwa ambayo pengine hupelekea hadi mtu kuhisi kiu; najaribu tu kuwaza je mwenzangu unawaza nini??
Sijui sababu ila inashauriwa mgonjwa(ambae anadalili za kuzidiwa) au majeruhi yoyote ambae amejeruhiwa vibaya akiomba chakula chochote au kinywaji chochote usimpe kabisa.kuna jamaa mmoja alipgwa na kitu kizito kifuani akaomba soda ya coca alipomaliza tu kuinywa akakata roho.Mwili ulipopelekwa hospitali ukafanyiwe uchunguzi ikagundulika kua alipatwa tatzo ndani ya mwili ila soda ndo iliopelekea yeye kukata roho.polisi walikuja wakambeba aliempa soda tulimuona baada ya miaka miwili.
 
Wanatuachia alama muhimu kuwa maji ni uhai,no life without water.heshimu maji na hali zake,MUNGU alitupendelea maji ya kila aina yakachukua sehem kubwa ya dunia na mwili wa mwanadamu pia
 
Sijui sababu ila inashauriwa mgonjwa(ambae anadalili za kuzidiwa) au majeruhi yoyote ambae amejeruhiwa vibaya akiomba chakula chochote au kinywaji chochote usimpe kabisa.kuna jamaa mmoja alipgwa na kitu kizito kifuani akaomba soda ya coca alipomaliza tu kuinywa akakata roho.Mwili ulipopelekwa hospitali ukafanyiwe uchunguzi ikagundulika kua alipatwa tatzo ndani ya mwili ila soda ndo iliopelekea yeye kukata roho.polisi walikuja wakambeba aliempa soda tulimuona baada ya miaka miwili.
Du
 
Hakuna mahali wala mstari au neno nimelitumia kukulazimisha hoja yangu.nilichoandika ni mtazamo wangu. Hoja za kidini siyo measurable, siyo testable, hazina logical consistent, zina self contradictions na siyo repeatable
Ni sawa na mbishi anaebisha yeye sio mbishi!!

Umeona sasa kama hunilazimishi katika sayansi why ulalame juu ya mimi kusema kile ninachokiamini katika dini, wewe umelazimisha mimi nitoe ushuhuda wa kisayansi hali mimi nipo kwenye dini. Kama ungekuwa hulazimishi usingelalama mimi kutumia dini na kunitaka nilete proof za sayansi, hapo tayar umeonesha umelazimisha..

Siku njema kiongozi.
 
Back
Top Bottom