Jumlisha
JF-Expert Member
- Jul 10, 2022
- 2,140
- 4,279
Ila Zambia bhana, hawa migration wa Zambia ni habari nyingine linapokuja suala la raia wa kigeni.
Watz wanaofanya biashara Zambia wanaelewa muziki wa migration wa Zambia. Jamaa wanakufata mpaka getto ulilopanga, na wakikukosa unafuatwa mpaka kwa restaurant.
Nakumbuka wamewahi kutunasa toka Lusaka, wakaturudisha mpaka border ya Tunduma kwa gharama zao. Hawa jamaa ni moto.
Sasa, siku moja nipo Zambia ndani kabisa, nilikuwa na passport ndogo ile ya dharura. Nakumbuka jamaa alikuwa ananigongea nikae Zambia wiki mbili tu, wakati mimi naenda kukaa zaidi ya mwezi.
Ile kuongea nae vizuri na ongo kidogo, jamaa akaniandikia mwezi mmoja. Nikasema fresh. Ile nimefika Zambia, nimepiga mishe nikaona mambo hayaendi, nikasema ngoja nifosi chaka vijijini nikiwa na mzigo.
Nikajisemea, bora niende migration niongeze siku kabisa, ili ikitokea nimezidisha siku isiwe shida. Wakati huo nilikuwa nimekaa wiki mbili tu Zambia na nimebakiza wiki mbili kwenye ile emergency passport yangu.
Oyaaah, moto niliokutana nao hapo haukuwa wa mchezo. Jamaa waliwaka, “Naendaje kuongeza siku wakati umebakiza wiki mbili kwenye passport?” Wanaongea kiwemba, najifanya siwaelewi. Nimekaa kimya, nimetia huruma kama mtu aliyekamatwa kwa fumanizi. Aisee, nimetulia pale.
Wakiniuliza kitu, najibu, “I’m sorry, I didn’t know if it’s a problem. I’m sorry officer.” Naongea pale, yale majamaa marefu yamepanda hewani, meusi yamenikazia, nasikia “lockup! lockup!” Maskini mimi, jumlisha na kigugumizi changu, niko hoi, najisemea kimoyomoyo.
Wakanitoa pale, wakanipeleka kwenye chumba kimoja. Nimekaa pale ndani kama masaa matatu, ndio wakaja kunitoa. Wakanipa warnings kibao, alafu wakaniongezea na wiki moja wakaniacha niende. Aisee, sikuamini.
Ndio kuja kugundua pale ndani kulikuwa na officer mmoja amesoma Bongo, akanionea huruma tu. Juu ya kwamba sisi Watz ni wakarimu sana kwa wageni, alinisaidia. Akanipa lift kwenye gari yake wakati natoka pale migration, tukabonga Kiswahili muda huo.