Uhamiaji Tanzania: Bila dhumuni la safari hakuna kupewa pasi ya kusafiria (Passport)

Hakuna safari ya ghafla, ndo maana kuna temporary passport. Ukiwa na emergency ya kweli Kama vile ugonjwa Kuna procedures zake siku 1 tu unapewa passport. Punguzeni ujuaji. Ninahisi hujawahi kuomba passport kwasababu miaka yote ukiomba passport lazima uonyeshe sababu ya kuomba passport.Acha blabla za passport ni haki ya kila mtu.
Mkuu naomba kufahamu ni kipi kinahitajika (documents) ili kupata passport
 
Dunia imebadilika, kutafuta fursa vitu vingi vinaanzia online before hata hujawaza kusafiri na passport number inahitajika.
Uko sahihi lakini uhamiaji kwao pass ya kusafiria ndicho wanachowaza vichwani sasa sijui unapoomba uwaambie mnipe nataka kusafiri online ndio waelewe sijui.Wana vichwa vigumu balaa
 
kwani ukimpa mtu passport akakaa nayo unapungukiwa na nini? Kwani unampa bure?

tanzania pekee ndo tunaona passport NI MALI. Nchi nyingi haya mambo hayapo.
Nimecheka sana Mkuu..Jf raha sana.
Jamaa wanajikuta Passport kama wanakulipia wao vile.
 
Hii ndio taarifa mpya kutoka Uhamiaji iliyotolewa leo na Msemaji wake Paul Mselle.

Paul Mselle amesema haya...

Pasi ya kusafiria ni 'document' ya kiusalama na ni haki ya kiusalama na ni mali ya Serikali, pale ambapo mtu ataitumia vibaya basi anaweza akanyang’anywa

Pasi ya kusafiria sio kitambulisho kusema mtu achukue abaki nayo ndani ni lazima kuwe na dhumuni la safari, kama hauna safari hatuwezi kukupa pasi ya kusafiria

Mtu atakayepoteza Pasi yake ya kusafiria (Passport), itamlazimu kutoa taarifa Polisi pamoja na kutangaza kwenye gazeti na kwamba ni lazima atoe kiasi cha shilingi Laki tano kwa kupoteza Passport hiyo, na ili aweze kupata nyingine.

Kumekuwa na changamoto ya kuchelewa kwa pasi ya kusafiria sababu unakuta mtu hajakamilisha vigezo vya kupata pasi ya kusafiria. Kuna wengine wanawasilisha vyeti vya kuzaliwa ambavyo haviko kwenye mfumo wa RITA na ukimuuliza alikipataje anasema alimtuma mtu kwa maana ya vishoka na hawa unakuta wengine ni raia wa Tanzania na wengine sio raia wa Tanzania

Wengine nao unakuta taarifa za cheti cha kuzaliwa zinatofautiana na taarifa za vitambulisho vya Taifa, unakuta kwenye Kitambulisho cha TAIFA(NIDA) kazaliwa Temeke kwenye cheti kazaliwa Morogoro.

Pamoja na mengine makosa ktk document yanatokea tatizo ni kurekebisha hizo taarifa inakua ngumu
 
Hii ndiyo inaitwa kufanya kazi kwa mazoea au kiroboti kuwa ohhh miaka yote tangu wakati wa Nyerere sisi huwa tunafanya hivi hivi
Hujitambui wewe na yeyote mwenye mawazo kama yako.

Hata ukiingia Chooni lazima uwe na sababu na si lazima kwenda ku-puu,
Sasa wewe unataka upewe Nyaraka ya Serikali bila kuwa na sababu?
 
Nimecheka sana Mkuu..Jf raha sana.
Jamaa wanajikuta Passport kama wanakulipia wao vile.
Umeona eeh. Ni shida sana. Paspoti ni document ambayo kila Mtanzania mwenye nia ya kusaka maisha angepewa bila MASHARTI magumu, ili aende kokote akasake maisha na kurejesha kipato nyumbani (remittance). Sasa serikali imefanya maisha ya kupata pas yawe magumu sana. Inakera mno
 
Hii ndio taarifa mpya kutoka Uhamiaji iliyotolewa leo na Msemaji wake Paul Mselle.

Paul Mselle amesema haya...

Pasi ya kusafiria ni 'document' ya kiusalama na ni haki ya kiusalama na ni mali ya Serikali, pale ambapo mtu ataitumia vibaya basi anaweza akanyang’anywa

Pasi ya kusafiria sio kitambulisho kusema mtu achukue abaki nayo ndani ni lazima kuwe na dhumuni la safari, kama hauna safari hatuwezi kukupa pasi ya kusafiria

Mtu atakayepoteza Pasi yake ya kusafiria (Passport), itamlazimu kutoa taarifa Polisi pamoja na kutangaza kwenye gazeti na kwamba ni lazima atoe kiasi cha shilingi Laki tano kwa kupoteza Passport hiyo, na ili aweze kupata nyingine.

Kumekuwa na changamoto ya kuchelewa kwa pasi ya kusafiria sababu unakuta mtu hajakamilisha vigezo vya kupata pasi ya kusafiria. Kuna wengine wanawasilisha vyeti vya kuzaliwa ambavyo haviko kwenye mfumo wa RITA na ukimuuliza alikipataje anasema alimtuma mtu kwa maana ya vishoka na hawa unakuta wengine ni raia wa Tanzania na wengine sio raia wa Tanzania

Wengine nao unakuta taarifa za cheti cha kuzaliwa zinatofautiana na taarifa za vitambulisho vya Taifa, unakuta kwenye Kitambulisho cha TAIFA(NIDA) kazaliwa Temeke kwenye cheti kazaliwa Morogoro.

Ukiwa Askari au mwana CCM nchi hii hutakiwi kutumia akili kabisa, yaani dumisha fikra za mwenyekiti au tii amri za walio juu yako tu.
Yaani jamaa hata wakati anaongea alikiwa ajisikii anaongea Nini, hata wale wa NIDA nao wanaamini Kama Hawa. Nchi hii ni viongozi tu ndio wenye haki na ndio maana wao ndio Wana haki ya kutunzwa tu, nyie wengine tunawaombea. Mmenunua ndege watu wapande na hamtaki kutoa pass watapanda viongozi tu
 
Ujue HUU NI UPUMBAVU.

Passport ni haki ya kila raia kuwa nayo.haijalishi una safari au hauna. Passport sio mali ya uhamiaji.

Acheni UKOLONI.

Yaani siku nikipata safari ndo nianze kuhangaika kutafuta passport?
Cha kushangaza ukishasafiri au safari ikiahirishwa sio kwamba unairudisha unabaki nayo

Sasa bado sioni mantiki si ni bora umpe mtu atakaapoomba ili kupunguzia mtu kadhia ya zimamoto kuhangaika kupata pass wakati wa safari
 
Ili mradi uweke mazingira ya hela
Cha kushangaza ukishasafiri au safari ikiahirishwa sio kwamba unairudisha unabaki nayo

Sasa bado sioni mantiki si ni bora umpe mtu atakaapoomba ili kupunguzia mtu kadhia ya zimamoto kuhangaika kupata pass wakati wa safari
 
Duuh Polen Ndugu zangu; Ndugu mtoa mada hawajazungumzia Kuhusu expire kwa tulioko Ughaibuni? wamebadilisha Utaratibu? maana nchi yetu hiyo ishakuwa Problemaa, too many changes zisizo na Tija.

Warioba Mashaka,

St. George, Bermuda
Kuna fursa gani huko ulipo mkuu... tufumbue macho..!
 
Nilishaacha kufuata habari za uhamiaji tanzania, nikitaka natumia shortcut mchezo umeisha. Hao uhamiaji ni taasisi naichukia kuliko zote tanzania, wanaendesha kizamani sana. One day hao wazee wataondok kitakuja kizazi kingine hapo uhamiaji na milango itafunguka.

Uhamiaji wanaongeza umasikini tanzania kwa kuwanyima raia wake passport. Yaani kama unataka kwenda kufundisha kiswahili afrika kusini unaanza kuhangaika nao tena badala ya wao kuweka mazingira mazuri kwa kila mtanzania.
Mambo ya ajabu sana.. imagine mwalimua anataka wenda kutafuta ajira nje, PASSPORT kupata ni mtihani..

Haya na sasa hiv zaidi ya wahitimu laki +wa ualimu wapo mitahani.. nafasi zikitangazwa za ajira ya ualimu nyingi sana ni 6000.

Mwisho wa siku unakuta wakenya ndio wanafunshi kiswahili kwenye nchi za watu..

Hata mataifa mengine wanajua kiswahili ..ni cha Wakenya
 
Ndio. Passport ya mwanangu under 18 anaenda shule. Nini kitahitajika
utaambiwa shule tunazo tele hapa kwetu secondary za kumwaga vyuo vyote tunavyo hapa akasome huko.
Siyo nje!! Unalo????

Hata akipewa hiyo passport ataulizwa anaenda kufanya nini?? km siyo kuzurura tu???

halafu akikwama huko gharama za serikali kumrudisha. Jipange kwa hayo maswali...
 
Relax, kila kitu kipo vizuri.
 
Back
Top Bottom