Uhamiaji Tanzania: Bila dhumuni la safari hakuna kupewa pasi ya kusafiria (Passport)

Yaani Tz na siasa za kikomunisti, ni pasua kichwa na zitaendelea kutuchelewesha sana .......
utaambiwa shule tunazo tele hapa kwetu secondary za kumwaga vyuo vyote tunavyo hapa akasome huko.
Siyo nje!! Unalo????

Hata akipewa hiyo passport ataulizwa anaenda kufanya nini?? km siyo kuzurura tu???

halafu akikwama huko gharama za serikali kumrudisha. Jipange kwa hayo maswali...
 
Wabongo wazamiaji kuliko Wnaigeri? Wao wanapata pass nje nje tu.
Wanigeria hadi raha kule kwao passport chap chap lengo sababu nchi wanaona ajira hamna wanatoa kirahisi watu wakatafute fursa mbele kwa mbele nchi za watu

Halafu kuna kichekesho kingine mfano mnigeria kasafiri mfano akakaa nchi ya watu akapitiliza muda wa visa aliyopewa akafungashwa virago kuruidishwa kwao na kwa kawaida mtu kama huyo hugongewa muhuri wa PI kwenye passport kwa wale msiojua PI ni nini ni PROHIBITED IMMIGRANT Kuwa hurusiwi kukanyaga nchi yao tena .Muhuri huo hugongewa wahalifu waliofanya uhalifu nchi za watu kwenye passport zao

Sasa ukienda nchi nyingine yeyote afisa uhamiaji mpakani au airport akipitia hiyo passport akikuta kuna mhuri wa PI hakuruhusu kuingia nchini kwake wala hakuulizi swali hata ukiernda ubalozi wowote ukiomba visa wakiona PI hawakupi VIZA

Sasa wanigeria mabalozi wao nchi zao huwa na taarifa zote za wanigeria wao walioko nchi husika.Wanigeria wakifika nchi yeyote cha kwanza hujitahidi kuripoti ubalozi wao kwa hiyo anajua huyo mnigeria karudishwa kwa kosa la ku over stay.Taarifa zinatumwa haraka ofisi ya makao makuu ya uhamiaji Nigeria kuwa kuna mtu wetu anarudishwa huko kagongewa PI kwenye passport hajafanya uhalifu wowote zaidi ya ku overstay!!.Akitua tu NIGERIA ANAENDA OFISI YA UHAMIAJI nIGERIA ANAPEWA Pole na kupewa passport ingine safi mpya aendelee na safari yake ya kuhangaika kutafuta riziki nchi zingine nje ya ile waliyomgongea PI

Sisi hapa kwetu mtu anarudishwa kisa passport hana alishindwa kuipata akazamia mfano Afrika ya kusini akifika hapa anakamatwa anaswekwa mndani na kuburuzwa mahakamani!!! Utakuta maafisa uhamiaji wanachekelea kuwaafikisha mahakani kisutu Dar es salaam.
Mfano ni hawa wazamiaji 100

"WATANZANIA 100 wamepewa adhabu ya kutofanya kosa ndani ya miezi sita baada ya kupatikana na hatia ya kutenda kosa la kutoka ndani ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na kwenda Afrika Kusini bila kufata utaratibu wa uhamiaji.

Raia hao ni Laurence Omary, Sultani Ditutu, Nassoro Lingumbulu, Abdul Masoud, Waziri Waziri, Dotto Abdallah na wenzao 94 ambao walipewa adhabu hiyo leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba.

Katika kesi hiyo, wakili wa serikali Godfrey Ngwijo, akisaidiana na Sitta Shija, wamedai kuwa, washitakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo Julai 3 mwaka 2020 katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.

Ilidaliwa kwamba, wakiwa raia wa Tanzania walibainika kutoka nje ya Tanzania katika tarehe zisizofahamika bila kufata utaratibu wa kiuhamiaji na kuelekea Afrika Kusini."

Cheki Afisa uhamiaji anavyosikia raha kuwakimbiza kama wanyama pori mahakamani kisutu Da es salaam

Wanatia hadi huruma

1621141319541.png

Source ya habari yenyewe: Magazeti mbalimbali na jamii forums
 
Cheki Afisa uhamiaji anavyosikia raha kuwakimbiza kama wanyama pori mahakamani kisutu

Wanatia hadi huruma

View attachment 1786634

Source ya habari yenyewe: Magazeti mbalimbali na jamii forums
Watanzania tunakwamishana wenyewe kwa wenyewe bila sababu. Angalia mtiti wa TRA, ni shida hadi kufanya biashara inakuwa kero. Serikali ni lazima iweke sheria taratibu na kanuni wezeshi kwa wananchi wake ili kufanya kazi zao za kila siku kwa urahisi.
 
Uko sahihi inatakiwa ku facilitate sio kukwamisha
Mfano unakuta soko mla kahawa Uganda bei nzuri mno kuliko Tanzania lakini ukitaka kupeleka unakwamishwa na watazania wenzetu hawataki uuze huko upate bei nzuri kwa roho mbaya tu
 
Aah! Sijui kama nitakosea nikisema tatizo ni baadhi ya viongozi kuwa na "mawazo mgando?" Kuna shida gani kama mtu si muhalifu akikabidhiwa passport yake akae nayo ili hata ikitokea safari asisumbuke kuishughulikia?

Serikali haioni kuwa kuwawekea watu wake vigingi kwenye suala la passport inawakosesha fursa?

Haioni kuwa hata yenyewe inakosa pesa? Kwani passport inatolewa Bure? Si inaweza kuwa Moja ya vyanzo vya kipato?

Aaah! Inakera sana.
 
Ash! Sijui kama nitakosea nikisema tatizo ni baadhi ya viongozi kuwa na "mawazo mgando?" Kuna shida gani kama mtu si muhalifu akikabidhiwa passport yake akae nayo ili hata ikitokea safari asisumbuke kuishughulikia?

Uko sahihi mia kwa mia hujakosea chochote

You are right hundred percent
 
Yaani serikali ndo ingekuwa inahamasisha watu wengi kujipatia passports, kwenda nje kusaka fursa na ajira manake Kwa Sasa ajira nchini hakuna badala ya kuweka vikwazo chungu nzima....na Kwa mfano chukulia wastani wa wananchi milioni 10 wapata passport kwa mwaka, mbona serikali ingepata kipato kizuri tu@150,000...tatizo bado Tz hang' over za siasa za ujamaa na kikomunisti bado zipo kwenye institution nyingi za utawala.....mifumo mingi ya utawala,etc kupenda kudhibiti nyendo na maisha ya kila siku ya watu wake, mara sijui unaenda kufanya nini nje????? Wakati wanapoenda nje wanapunguzia mzigo serikali...... Yaani kaazi kwelikweli.. mambo hayo yamepitwa na wakati bana....hata waanzilishi China na Urusi wamebadilika siku hizi na wana mikakatiya makusudu Kwa kuhakikisha watu wake, kusambaa duniani...
 
Yaani serikali ndo ingekuwa inahamasisha watu wengi kujipatia passports, kwenda nje kusaka fursa na ajira manake Kwa Sasa ajira nchini hakuna badala ya kuweka vikwazo chungu nzima....na Kwa mfano chukulia wastani wa wananchi milioni 10 wapata passport kwa mwaka, mbona serikali ingepata kipato kizuri tu.....tatizo Tz hang' over za siasa za ujamaa na kikomunisti bado zipo kwenye institution nyingi za utawala.....mifumo mingi ya utawala,etc kupenda kudhibiti nyendo na maisha ya kila siku ya watu wake, mara sijui unaenda kufanya nini nje????? Wakati wanapoenda wanakunguzia mzigo ....Kaazi kwelikweli.. mambo hayo yamepitwa na wakati....hata China na Urusi wamebadilika siku hizi...
Sahihi

Passport moja Shs 150,000

Passport milioni 10 ni sawa na
Na matrilioni ya pesa mtu mwenye Passport Asafiri au asisafiri serikali imeingiza chake
 
  • Kwa mujibu wa historia, wafalme walikuwa wakiruhisu vijana wao kwenda nje ya himaya kuiba ili walete mali.
  • Ajabu na nusu kuna taifa karne hii watu wake wakionekana 'kuukaribia' mpaka wa jirani wanatendewa kama wahalifu wa kimataifa
 
Ash! Sijui kama nitakosea nikisema tatizo ni baadhi ya viongozi kuwa na "mawazo mgando?" Kuna shida gani kama mtu si muhalifu akikabidhiwa passport yake akae nayo ili hata ikitokea safari asisumbuke kuishughulikia?

Serikali haioni kuwa kuwawekea watu wake vigingi kwenye suala la passport inawakosesha fursa?

Haioni kuwa hata yenyewe inakosa pesa? Kwani passport inatolewa Bure? Si inaweza kuwa Moja ya vyanzo vya kipato?

Aaah! Inakera sana.
Nchi ya hovyo Sana hii! Ni haki ya kila raia kupata pass, na sio bure! Maccm ni ya hovyo!
 
  • Kwa mujibu wa historia, wafalme walikuwa wakiruhisu vijana wao kwenda nje ya himaya kuiba ili walete mali.
  • Ajabu na nusu kuna taifa karne hii watu wake wakionekana 'kuukaribia' mpaka wa jirani wanatendewa kama wahalifu wa kimataifa
Watanzania tunakwamishana wenyewe kwa wenyewe bila sababu. Angalia mtiti wa TRA, ni shida hadi kufanya biashara inakuwa kero. Serikali ni lazima iweke sheria taratibu na kanuni wezeshi kwa wananchi wake ili kufanya kazi zao za kila siku kwa urahisi.
Kule Mutukula upande wa Uganda, kuna Watanzania wengi wana Maduka upande wa Uganda, kwa sababu tu mazingira ya kufanya biashara ni rafiki kuliko Tanzania. Mtu anaamka Asubuhi anaenda kufungua biashara yake Uganda, na Usiku anarejea kwake Tanzania.

Ujamaa ni sumu ya maendeleo ya biashara.
 
Uko sahihi inatakiwa ku facilitate sio kukwamisha
Mfano unakuta soko mla kahawa Uganda bei nzuri mno kuliko Tanzania lakini ukitaka kupeleka unakwamishwa na watazania wenzetu hawataki uuze huko upate bei nzuri kwa roho mbaya tu
Labda, hawataki Watanzania wawe matajiri.

Mawazo ya kijamaa nayo, mhhh!!! Yanahuzunisha na kuchekesha kwa pamoja
 
Yaani serikali ndo ingekuwa inahamasisha watu wengi kujipatia passports, kwenda nje kusaka fursa na ajira manake Kwa Sasa ajira nchini hakuna badala ya kuweka vikwazo chungu nzima....na Kwa mfano chukulia wastani wa wananchi milioni 10 wapata passport kwa mwaka, mbona serikali ingepata kipato kizuri tu@150,000...tatizo bado Tz hang' over za siasa za ujamaa na kikomunisti bado zipo kwenye institution nyingi za utawala.....mifumo mingi ya utawala,etc kupenda kudhibiti nyendo na maisha ya kila siku ya watu wake, mara sijui unaenda kufanya nini nje????? Wakati wanapoenda wanakunguzia mzigo ....Kaazi kwelikweli.. mambo hayo yamepitwa na wakati bana....hata waanzilishi China na Urusi wamebadilika siku hizi...
China na Urusi? Mkuu, siyo kwamba tu wamebadilika, Kuna mtu mwingine ukimwambia kuwa China ilishawahi kuwa na Sera kama za "Tanganyika" ( sijui kama na Wazanzibar nao wanapitia kadhia kama ya Watanganyika) anaweza asikuekewe. Wewe huoni Wachina walivyojazana Afrika Mashariki? Wanafanya mpaka biashara za "umachinga"

Unafikiri wamekuja kwa kutoroka? Dhubutu!

Machina siyo mjinga. Anajua anachokihitaji. Viongozi wao wanajitambua. Lazima wamewezeshwa kuja Afrika kihalali.
 
Sahihi

Passport moja Shs 150,000

Passport milioni 10 ni sawa na
Na matrilioni ya pesa mtu mwenye Passport Asafiri au asisafiri serikali imeingiza chake
Na hiyo ni mbali na pesa ambazo wangeziingiza nchini watakapofanikiwa huko nje.

Wana ndugu zao Tanzania, wakiwatumia pesa haitaadhiri kwa namna chanya mzunguko wa pesa nchini?

Kuna watakaohitaji kujenga. Huoni huko nako ni faida kwa Watanzania na Tanzania kwa ujumla.

Je kwa wale watakaorejea nchini kuwekeza baada ya kukusanya mtaji huko nje, hawatakuwa wamesaidia kukuza uchumi wa nchi?
Biashara zao hazitatoa ajira kwa Watanzania na pia Serikali kupata mapato kupitia kodi?

Wakati mwingine nawaza na kuishia kusema, TANZANIA HAINA UPUNGUFU WA WATU, LAKINI INA UPUNGUFU WA WATU WANAOFIKIRIA.

Hata kama PASSPORT zingetolewa bure, bado faida ambayo ingepatikana ingeizidi gharama ya kuziandaa.

Angalia nchi ya watu WANAOFIKIRIA.
Nigeria HAINA dini. Lakini kipindi fulani, mmoja wa wahubiri maarufu nchini humo alitaka kuhamishia huduma yake nchi nyingine. Ilibidi Serikali imbembeleze asiondoke.

Serikali ya Nigeria ilikuwa inahitaji mahubiri yake? Noo! Lakini ilipopiga hesabu ya watu mbali mbali kutoka mataifa mengine yanayoenda kanisani kwa huyo muhubiri, ilibaini kuwa ingepoteza mapato makubwa sana.

Wageni waliokuwa wakienda kwa huyo muhubiri walikuwa wakiingizia Nigeria fedha nyingi za Kigeni.
 
  • Kwa mujibu wa historia, wafalme walikuwa wakiruhisu vijana wao kwenda nje ya himaya kuiba ili walete mali.
  • Ajabu na nusu kuna taifa karne hii watu wake wakionekana 'kuukaribia' mpaka wa jirani wanatendewa kama wahalifu wa kimataifa
Na wengine "wakaligundua " ziwa kubwa barani Afrika wakaliita Lake Victoria, japo kwa Wasukuma haikuwa "news", "wakagundua" mlima mrefu Afrika, ingawa Wachaga walikuwa wakiuona tokea wanazaliwa. Wakaenda mbali zaidi, wakawagundua na watu weusi.

Lakini kwa Tanzania, wanabanwa wasiende nchi zingine, labda, ili na wao wasije wakagundua kuwa wana akili kama wengine wenye akili.

Labda, Serikali haitaki watu wake wagundue...
 
Hii ndio taarifa mpya kutoka Uhamiaji iliyotolewa leo na Msemaji wake Paul Mselle.

Paul Mselle amesema haya...

Pasi ya kusafiria ni 'document' ya kiusalama na ni haki ya kiusalama na ni mali ya Serikali, pale ambapo mtu ataitumia vibaya basi anaweza akanyang’anywa

Pasi ya kusafiria sio kitambulisho kusema mtu achukue abaki nayo ndani ni lazima kuwe na dhumuni la safari, kama hauna safari hatuwezi kukupa pasi ya kusafiria

Mtu atakayepoteza Pasi yake ya kusafiria (Passport), itamlazimu kutoa taarifa Polisi pamoja na kutangaza kwenye gazeti na kwamba ni lazima atoe kiasi cha shilingi Laki tano kwa kupoteza Passport hiyo, na ili aweze kupata nyingine.

Kumekuwa na changamoto ya kuchelewa kwa pasi ya kusafiria sababu unakuta mtu hajakamilisha vigezo vya kupata pasi ya kusafiria. Kuna wengine wanawasilisha vyeti vya kuzaliwa ambavyo haviko kwenye mfumo wa RITA na ukimuuliza alikipataje anasema alimtuma mtu kwa maana ya vishoka na hawa unakuta wengine ni raia wa Tanzania na wengine sio raia wa Tanzania

Wengine nao unakuta taarifa za cheti cha kuzaliwa zinatofautiana na taarifa za vitambulisho vya Taifa, unakuta kwenye Kitambulisho cha TAIFA(NIDA) kazaliwa Temeke kwenye cheti kazaliwa Morogoro.

Mbona hii imeanza 2020.
 
Back
Top Bottom